-
[Ujumuishaji ni nini?]
-
[Kuhusisha]
-
Sielewi ni
kwa nini nimeketi nyuma ya darasa.
-
Natamani ingekuwa kama kila mtu.
-
Ningependa kufanya wanachofanya.
-
Lakini nipo hapa,
-
nikifanya shughuli za nambari sawa za
zamani,
-
nikitazama wanafunzi wenza
wakijifunza kitu kingine.
-
Wanajua kuwa wananiweka
katika hali ya kushindwa?
-
Hawajui kuwa mustakabali wangu
upo mikononi mwao?
-
Ningependa kufanya kazi darasani mwangu,
-
kujifunza wanachojifunza
na kufanya shughuli wanazofanya.
-
Lakini nipo hapa, nimekwama upande
wa nyuma, nikiwa na matarajio madogo,
-
Kuwa na msaidizi wa ana kwa ana wa
mwalimu hunifunza tu kumtegemea
-
na inamaanisha mwalimu
hamakiniki zaidi nami.
-
Sijumuishwi darasani.
-
Niko katika chumba kimoja
lakini nimetengwa na wenzangu,
-
nikiwa nimeketi upande au nyuma, nikifanya
mambo tofauti na kukosa mafunzo.
-
Ningependa kuwa huru
kujifunza na wenzangu,
-
kufikia uwezo wangu kamili na
kuonekana kama watu wengine.
-
Nahitaji mambo yabadilike.
-
[Ujumuishaji unaokisiwa]
-
Huenda unashangaa ni
nini kibaya na picha hii?
-
Nipo darasani na wenzangu,
nimeketi katika kitu changu,
-
nikijifunza mambo sawa kama wengine.
-
Huenda unafikiri huu ni ujumuishaji,
-
lakini sivyo.
-
Nimesongwa, kuwekewa vikwazo
na kuzuiliwa kufikia uwezo wangu kamili.
-
Ingawa nampenda mwalimu wangu msaidizi,
mara nyingi sifikiri mwenyewe.
-
Ukweli ni kwamba, mara nyingi mwalimu
wangu msaidizi hufikiri kwa niaba yangu,
-
hata anganong'oneza jibu
katika sikio langu wakati tayari nalijua.
-
Kadri anapokua nami,
-
ndivyo nagundua kuwa hakuna haja
ya mimi binafsi kufikiri
-
kwa sababu bado tu atanipa jibu.
-
Nina hakika pia kuna watoto wengine
wanaohitaji usaidizi wake.
-
Je, anahitaji kuwa nami?
-
Hawezi kuwasaidia wengine?
-
Ninapohitaji usaidizi,
-
naweza kuinua mkono na kumuuliza
mwalimu kama wanavyofanya marafiki zangu.
-
Marafiki na wenzangu wangependa kunisaidia
-
lakini kwa kuwa na mtu
karibu nami, hawawezi.
-
Nahitaji kujifunza kutoka kwa wenzangu
-
niweze kufanya kazi za kikundi
na kupewa changamoto.
-
Ningependa kuruhusiwa kushindwa
au kufaulu na kujifunza kutokana nayo.
-
Jambo linahitaji kubadilika
-
[Ujumuishaji]
-
Je, unaweza kunipata katika umati?
-
Ujumuishaji ni zaidi ya neno tu,
-
ni utamaduni, mwenendo
-
na matarajio kuwa kila mtu anaweza
na atajifunza na kufaulu
-
pamoja na wenzake wa umri unaofaa.
-
Naweza inaweza kuwa vigumu
kunijumuisha katika mafunzo
-
kwa kuwa wakati mwingine huenda nikahitaji
nyenzo na maelezo ya ziada,
-
lakini kunipa nafasi ya kujifunza
kutoka kwa malimu na wenzangu
-
ni njia bora ya kunipa changamoto
na kuniruhusu kukua.
-
Ningependa kujifunza mambo sawa
na wenzangu,
-
na ningependa walimu wawe na matarajio
sawa kwangu kama kwa marafiki zangu.
-
Huenda mafunzo yangu yakahitaji
kubadilishwa,
-
lakini bado ningependa fursa ya
kuonyesha ninachoweza kufanya,
-
na si kulenga kwa nisichoweza.
-
Nichukuliwe kama mwanafunzi mwingine
yeyote na unitazame nikifaulu,
-
Nitazidi matarajio mnayoniwekea.
-
Je, mko tayari kunijumuisha kihalisia?
-
Manukuu yaliandikwa na Juliana Ponesi
Ukaguzi umefanywa na Carol Wang