Kutambua magonjwa mapema, tuongee lugha ya siri ya bakteria
-
0:02 - 0:03Hauwajui.
-
0:04 - 0:05Hauwaoni.
-
0:06 - 0:08Lakini daima wapo wanazunguka,
-
0:09 - 0:11wananong'oneza,
-
0:11 - 0:13wakitengeneza mipango ya siri,
-
0:14 - 0:17wakijenga jeshi la mamilioni ya wanajeshi.
-
0:19 - 0:21Na wanapoamua kushambulia,
-
0:21 - 0:24wanashambulia kwa wakati mmoja.
-
0:27 - 0:29Ninaongelea kuhusu bakteria.
-
0:29 - 0:30(Kicheko)
-
0:30 - 0:33Mlidhani ninaongelea kuhusu nani?
-
0:34 - 0:38Bakteria wanaishi kwenye jamii
kama tu binadamu. -
0:38 - 0:39Wana familia,
-
0:39 - 0:40wanaongea,
-
0:40 - 0:42na wanapanga shughuli zao.
-
0:42 - 0:45Na kama tu binadamu, wanahila, waongo,
-
0:45 - 0:47na wengine hata wanadanganyana wenyewe.
-
0:48 - 0:52Je kama nikikuambia kua tunaweza
kusikiliza mazungumzo ya bakteria -
0:52 - 0:56na kutafsiri taarifa zao za siri
kuwa lugha ya binadamu? -
0:56 - 1:01Na kama je nikiwaambia kuwa kutafsiri
mazungumzo ya bakteria kutaokoa maisha? -
1:03 - 1:04Nina PhD ya nanofizikia,
-
1:04 - 1:09na nimetumia teknolojia ya nano kuunda
chombo cha kutafsiri cha muda halisi -
1:09 - 1:11kinachoweza kupeleleza kwenye jamii
za bakteria -
1:11 - 1:14na kutupa rekodi za nini
bakteria wanafanya. -
1:16 - 1:18Bakteria wanaishi kila sehemu.
-
1:18 - 1:20Wako kwenye udongo, kwenye samani zetu
-
1:20 - 1:21na ndani ya miili yetu.
-
1:22 - 1:27Ki ukweli, asilimia 90 ya seli zote hai
kwenye huu ukumbi ni bakteria. -
1:28 - 1:30Baadhi ya bakteria ni wazuri
kwetu; -
1:30 - 1:33wanatusaidia kumeng'enya chakula
au kutengeneza dawa. -
1:33 - 1:35Na baadhi ya bakteria na wabaya kwetu:
-
1:35 - 1:37wanasababisha magonjwa na kifo.
-
1:38 - 1:40Kushirikisha kazi zote bakteria
walizonazo, -
1:40 - 1:42wanatakiwa wawe na uwezo wa
kupanga, -
1:42 - 1:44na wanafanya hivyo kama tu sisi
binadamu -- -
1:44 - 1:46kwa mawasiliano.
-
1:47 - 1:48Lakini badala ya kutumia
maneno, -
1:48 - 1:51wanatumia molekuli za ishara
kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe. -
1:52 - 1:53Bakteria wanapokuwa wachche,
-
1:53 - 1:56molekuli za ishara zinatiririka nje,
-
1:56 - 1:59kama kelele za mtu peke yake
jangwani. -
2:00 - 2:04Lakini kukiwa na bakteria wengi,
molekuli za ishara zinajikusanya, -
2:04 - 2:07na bakteria wanaanza kuhisi kuwa
hawapo peke yao. -
2:07 - 2:09Wanasikilizana wenyewe.
-
2:09 - 2:12Kwa njia hii, wanapima
wako wangapi -
2:12 - 2:16na wanapokuwa wengi wa kutosha
kuanzisha hatua mpya. -
2:17 - 2:20Na pale molekuli za ishara zinafika
kizingiti flani, -
2:20 - 2:24bakteria wote wanahisi kwa mara moja
kua wanahitaji kutenda -
2:24 - 2:25kwa tendo hilo hilo.
-
2:26 - 2:30Hivyo mazungumzo ya bakteria yanakuwa
na mwanzo na jibu, -
2:30 - 2:33uzalishaji wa molekuli
na majibu yake. -
2:35 - 2:38Kwenye utafiti wangu, nimelenga kupeleleza
kwenye jamii za bakteria -
2:38 - 2:40ndani ya mwili wa binadamu.
-
2:40 - 2:42Inafanyaje kazi?
-
2:42 - 2:44Tunasampuli kutoka kwa mgonjwa.
-
2:44 - 2:47Inaweza kuwa ni sampuli ya damu au mate.
-
2:47 - 2:50Tunapiga elektroni ndani ya sampuli,
-
2:50 - 2:54elektroni zitaingilia na molekuli
zozote za mazungumzo zilizopo, -
2:54 - 2:56na huu muingiliano utatupa
taarifa -
2:56 - 2:58ya aina ya bakteria,
-
2:58 - 3:00aina ya mawasiliano
-
3:00 - 3:02na kiasi gani bakteria wanazungumza.
-
3:04 - 3:07Lakini inakuaje pale
bakteria wakizungumza? -
3:08 - 3:12Kabla sijaunda chombo cha kutafsiri,
-
3:12 - 3:15dhana yangu ya kwanza ilikua bakteria
watakua na lugha ya halisi, -
3:15 - 3:19kama vichanga ambao bado hawajaunda
maneno na sentensi. -
3:19 - 3:22Wanapocheka, wanafuraha;
wanapolia, wanahuzuni. -
3:22 - 3:23Rahisi kama hivyo.
-
3:24 - 3:28Lakini bakteria walionekana kutokuwa
karibu na halisi kama nilivyodhani. -
3:29 - 3:31Molekuli sio tu molekuli.
-
3:31 - 3:34Inaweza kumaanisha vitu tofauti
kulingana na muktadha, -
3:34 - 3:37kama tu vilio vya watoto
vinavyomaanisha vitu tofauti: -
3:37 - 3:39saa nyingine mtoto ana njaa,
-
3:39 - 3:40saa nyingine amelowa,
-
3:40 - 3:42saa nyingine ameumia au anaogopa.
-
3:42 - 3:45Wazazi wanajua jinsi ya kusoma hivi vilio.
-
3:46 - 3:48Na kua chombo kizuri cha kutafsiri,
-
3:48 - 3:51kinatakiwa kiwe na uwezo wa kusoma
molekuli za ishara -
3:51 - 3:55na kuzitafsiri
kulingana na muktadha. -
3:55 - 3:57Na nani anajua?
-
3:57 - 3:59Labda Tafsiri ya Google inaweza
kuiptisha hii. -
3:59 - 4:01(Kicheko)
-
4:02 - 4:04Hebu niwape mfano.
-
4:04 - 4:08Nimeleta baadhi ya taarifa za bakteria
zinazoweza kuwa ngumu kuelewa -
4:08 - 4:09kama hauna mafunzo,
-
4:09 - 4:10lakini jaribu kuangalia.
-
4:12 - 4:13(Kicheko)
-
4:15 - 4:18Hii ni familia ya bakteria yeye furaha
ambayo imemshambulia mgonjwa. -
4:20 - 4:22Wacha tuwaite familia ya Montague.
-
4:24 - 4:27Wanatumia wote rasilimali,
wanazaliana, wanakua. -
4:28 - 4:30Siku moja, wanapata mgeni mpya,
-
4:33 - 4:35familia ya bakteria Capulet.
-
4:35 - 4:36(Kicheko)
-
4:36 - 4:39Kila kitu ni sawa,
alimradi wanafanya kazi kwa pamoja. -
4:40 - 4:43Lakini kitu kisichopangwa kinatokea.
-
4:44 - 4:49Romeo wa Montague anakua na mahusiano
na Juliet wa Capulet. -
4:49 - 4:50(Kicheko)
-
4:51 - 4:54Na ndio, wanagawiana chembe za urithi.
-
4:54 - 4:56(Kicheko)
-
4:58 - 5:01Sasa, uhamisho wa kinasaba unaweza
kuwa hatari kwa wakina Montague -
5:01 - 5:05waliokuwa na matarajio ya kuwa familia
pekee kwenye mgonjwa waliomshambulia, -
5:05 - 5:07kugawana chembe za urithi
kunachangia -
5:07 - 5:10kwa wakina Capulet kutengeneza
kinga kwa dawa. -
5:12 - 5:16Hivyo wakina Montague wanaanza kuongea
kwa ndani kuondoa hii familia nyingine -
5:16 - 5:18kwa kutoa molekuli hii.
-
5:19 - 5:20(Kicheko)
-
5:21 - 5:22Na kwa maelezo:
-
5:22 - 5:24[Hebu turatibu shambulizi.]
-
5:24 - 5:25(Kicheko)
-
5:26 - 5:27Hebu turatibu shambulizi.
-
5:29 - 5:32Na kila mtu mara moja akaitikia
-
5:32 - 5:37kwa kutoa sumu
itakayoua ile familia nyingine. -
5:37 - 5:38[Ondoa!]
-
5:40 - 5:42(Kicheko)
-
5:43 - 5:48Wakina Capulet wakajibu kwa
kuita shambulizi la kujibu. -
5:48 - 5:49[Shambulia!]
-
5:49 - 5:50Na wakawa na vita.
-
5:52 - 5:57Hii ni video ya bakteria wa ukweli
wakipigana na viumbe kama upanga, -
5:57 - 5:58ambapo wanajaribu kuuana
-
5:58 - 6:01kwa kuchomana kihalisi
na kupasuana wenyewe. -
6:03 - 6:07Familia ya yeyote atakayeshinda hii vita
anakuwa bakteria mkuu. -
6:08 - 6:12Hivyo ninachoweza kufanya ni kuchunguza
mazungumzo ya bakteria -
6:12 - 6:14yanayopelekea tabia
tofauti za kwa pamoja -
6:14 - 6:15kama ugomvi mliyouona.
-
6:16 - 6:19Na nilichofanya ni kupeleleza
kwenye jamii za bakteria -
6:19 - 6:21ndani ya mwili wa binadamu
-
6:21 - 6:22kwenye wagonjwa hospitalini.
-
6:23 - 6:25Nilifuatilia wagonjwa 62 kwenye jaribio,
-
6:25 - 6:29ambapo nilipima sampuli ya mgonjwa
kwa aina moja ya shambulizi, -
6:29 - 6:32bila kujua majibu ya
vipimo vya kawaida. -
6:32 - 6:37Basi, kwenye upimaji wa bakteria,
-
6:37 - 6:39sampuli inasambazwa kwenye kisahani,
-
6:39 - 6:42na kama bakteria watakua ndani ya siku
tano, -
6:42 - 6:44mgonjwa anagunduliwa kama ameathirika.
-
6:46 - 6:49Nilipomaliza utafiti na
kulinganisha majibu ya chombo -
6:49 - 6:52na vipimo vya kawaida
na vipimo vya kuhakikisha, -
6:52 - 6:53nilishtuka.
-
6:53 - 6:57Ilikua inashangaza zaidi
kuliko nilivyowahi kutarajia. -
6:58 - 7:00Ila kabla sijawaambia
nini chombo kilionyesha, -
7:00 - 7:03ningependa kuwaambia kuhusu
mgonjwa mahsusi niliomfuatilia, -
7:03 - 7:04binti mdogo.
-
7:05 - 7:06Alikua na cystic fibrosis,
-
7:06 - 7:10ugonjwa wa kurithi uliofanya mapafu yake
kuathiriwa kirahisi na bakteria. -
7:11 - 7:13Huyu binti hakua sehemu ya
majaribio. -
7:13 - 7:16Nilimfuatilia kwa sababu nilijua
kutoka kwenye taarifa zake -
7:16 - 7:18kua hakuwahi kupata mashambulizi
kabla. -
7:19 - 7:22Mara moja kwa mwezi, huyu binti
alienda hospitali -
7:22 - 7:24kuweka sampuli ya kohozi
ambayo alitemea kwenye kikombe. -
7:25 - 7:28Hii sampuli ilisafirishwa kwa
uchunguzi wa bakteria -
7:28 - 7:30huko maabara kuu
-
7:30 - 7:33ili madaktari watende haraka
iwapi wangekuta shambulizi. -
7:34 - 7:37Iliniruhusu mimi kupima chombo
changu kwa sampuli zake pia. -
7:37 - 7:41Miezi miwili ya mwanzo nilipima
sampuli zake, hakukua na kitu. -
7:42 - 7:43Lakini mwezi wa tatu,
-
7:43 - 7:46Niligundua mazungumzo ya
bakteria kwenye sampuli yake. -
7:46 - 7:50Bakteria walikua wanashirikiana
kuharibu tishu ya pafu lake. -
7:51 - 7:55Lakini vipimo vya kawaida
havikuonyesha bakteria kabisa. -
7:56 - 7:58Nilipima tena mwezi ujao,
-
7:58 - 8:01na niliona kua yale mazungumzo ya
bakteria yamekua makali zaidi. -
8:02 - 8:05Bado, vipimo vya kawaida
havikuonyesha chochote. -
8:06 - 8:10Utafiti wangu ukaisha, lakini nusu mwaka
baadae, nikafuatilia hali yake -
8:10 - 8:13kuona kama bakteria niliowajua
pekee walipotea -
8:13 - 8:15bila muingilio wa tiba.
-
8:16 - 8:18Hawakupotea.
-
8:18 - 8:21Yule binti sasa alikua amegundulika
na mashambulio makali -
8:21 - 8:22ya bakteria wabaya.
-
8:24 - 8:28Walikua ni wale wale bakteria
chombo changu kiligundua kabla. -
8:29 - 8:31Na licha ya ukali wa
dawa za kutibu, -
8:31 - 8:34ilikua inashindikana
kuondoa mashambulizi. -
8:35 - 8:38Madaktari waliona kua asingeweza
kufikia miaka ya 20. -
8:40 - 8:43Nilipopima kwenye sampuli ya binti huyu,
-
8:43 - 8:45kifaa changu kilikua kwenye
hatua za mwanzo. -
8:45 - 8:47Sikujua hata
kama njia yangu ilifanya kazi kabisa, -
8:47 - 8:50hivyo nikawa na makubaliano
na madaktari -
8:50 - 8:52kutowaambia chombo changu
kilichoonyesha -
8:52 - 8:54ili kutokuharibu matibabu yao.
-
8:54 - 8:57Hivyo nilipoona haya majibu
ambayo hata hayakuwa yamehakikishwa, -
8:57 - 8:58sikudhubutu kusema
-
8:58 - 9:01ka sababu kutibu mgonjwa
bila mashambulizi halisi -
9:01 - 9:04pia ina matokeo mabaya
kwa mgonjwa. -
9:05 - 9:07Lakini sasa tunajua bora,
-
9:07 - 9:10na kuna wavulana na wasichana wadogo
wengi bado wanaweza kuokolewa -
9:11 - 9:15kwa sababu, bahati mbaya,
hii hali inatokea mara nyingi. -
9:15 - 9:16Wagonjwa wanaathirika,
-
9:16 - 9:20bakteria kwa namna flani hawaonekani
kwenye vipimo vya kawaida, -
9:20 - 9:24na ghafla, maambukizi yanatokea
ndani ya mgojwa na dalili kali. -
9:24 - 9:26Na kwenye mda huo, tayari tumechelewa.
-
9:27 - 9:31Majibu ya kushangaza ya
wagonjwa 62 niliowafuatilia -
9:31 - 9:33yalikua chombo changu kilishika
mazungumzo ya bakteria -
9:33 - 9:36kwa zaidi ya nusu ya sampuli za wagonjwa
-
9:36 - 9:39ambao walikua wamegundulika bila kitu
kwa njia za upimaji za kawaida. -
9:39 - 9:43Kwa maneno mengine, zaidi ya nusu ya
hawa wagonjwa walirudi nyumbani wakiwaza -
9:43 - 9:45kua wako huru na maambukizi,
-
9:45 - 9:48japokuwa kihalisi walibeba
bakteria hatari. -
9:49 - 9:52Ndani ya wagonjwa waliopimwa vibaya,
-
9:52 - 9:55bakteria walikuwa wanaandaa shambulizi
la kuambatanishwa. -
9:56 - 9:57Walikua wananong'onezana.
-
9:58 - 10:00Ninachoita "mnong'ono wa bakteria"
-
10:00 - 10:03ni bakteria ambao njia za kawaida
za upimjai haziwezi kuona. -
10:03 - 10:07Mpaka sasa, ni chombo cha kutafsiri tu
kinachoweza kudaka hao wanong'onezaji. -
10:08 - 10:12Ninaamini kua mda uliopo ambao
bakteria bado wananong'onezana -
10:12 - 10:15ni nafasi nzuri ya matibabu
ya malengo. -
10:16 - 10:19Kama yule binti angekua ametibiwwa
kwenye kuu mda wenye nafasi, -
10:19 - 10:21ingekua inawezekana kuua
bakteria -
10:21 - 10:23kwenye hatua yao ya mwanzo,
-
10:23 - 10:25kabla maambukizi kuwa nje ya uwezo.
-
10:27 - 10:31Nilichopitia na huyu binti mdogo
kumenifanya niamue kufanya ninachoweza -
10:31 - 10:33kusukuma hii teknolojia kwenye hospitali.
-
10:34 - 10:35Pamoja na madaktari,
-
10:35 - 10:38tayari ninafanya kazi kutumia
hiki kifaa kwenye kliniki -
10:38 - 10:40kutambua maambukizi ya kwanza.
-
10:41 - 10:45Japo bado haijajulikana jinsi
madaktari watatibu wagonjwa -
10:45 - 10:46kwenye kipindi cha mnong'ono,
-
10:46 - 10:50hiki kifaa kinaweza kusaidia madaktari
kuwa makini na wagonjwa kwenye hatari. -
10:51 - 10:54Kinaweza kuwasaidia kuhakikisha
kama tiba imefanya kazi au la, -
10:54 - 10:57na inaweza kusaidia kujibu maswali rahisi:
-
10:57 - 10:58Mgonjwa ana mashambulizi?
-
10:58 - 11:00Na bakteria wako wanapanga nini?
-
11:01 - 11:03Bakteria wanaongea,
-
11:03 - 11:05wanatengeneza mipango ya siri,
-
11:05 - 11:08na wanatumiana taarifa za siri.
-
11:08 - 11:11Lakini sio tu kuawaangalia wenyewe
wakinong'onezana, -
11:11 - 11:13sisi sote tunaweza kujifunza lugha ya siri
-
11:13 - 11:16na kua wenyewe wanong'onezi wa bakteria.
-
11:17 - 11:19Na, kama bakteria wangesema,
-
11:20 - 11:23"3-oxo-C12-aniline."
-
11:24 - 11:25(Kicheko)
-
11:25 - 11:26(Makofi)
-
11:26 - 11:27Asanteni.
- Title:
- Kutambua magonjwa mapema, tuongee lugha ya siri ya bakteria
- Speaker:
- Fatima AlZahra'a Alatraktchi
- Description:
-
Bakteria "wanaongea" pamoja, wakituma taarifa za kemikali kuunda mashambulizi. Je kama tungesikiliza wanachosema? Mnanofizikia Fatima AlZahra's Alatraktchi ameunda kifaa cha kupeleleza mazungumzo ya bakteria na kutafsiri mazungumzo yao ya siri kwenda lugha ya binadamu. Kazi yake inaweza kuandaa njia ya ugunduzi wa mapema wa ugonjwa -- kabla hata hatujaumwa.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 11:41
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language | ||
Julieth Mbeyella accepted Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for To detect diseases earlier, let's speak bacteria's secret language |