Swahili subtitles

← Kwanini unapaswa kusoma Flannery O'Connor? - Iseult Gillespie

Get Embed Code
23 Languages

Showing Revision 7 created 03/04/2019 by Nelson Simfukwe.

 1. Bibi muongeaji na mhalifu anayezurura
  wakizozana katika barabara chafu.
 2. Muuza Biblia anampeleka mwanafalsafa
  mwenye mguu mmoja bandani.
 3. Fundi anaesafiri anamfundisha mwanamke
  kiziwi neno lake la kwanza shambani.
 4. Kutoka shambani kwake vijijini Georgia,
 5. akizungukwa na kundi la ndege wa kufugwa,

 6. Flannery O'Connor aliandika simulizi
  za waliotengwa,
 7. wavamizi na wasioleweka waliunda
  dunia aliyoifahamu vizuri:
 8. Marekani Kusini.
 9. Alichapisha riwaya mbili,
 10. lakini anajulikana zaidi
  kwa simulizi zake fupi,
 11. ambazo zilichunguza maisha ya mji mdogo kwa
  lugha kali, na ucheshi usio wa kawaida,
 12. na mazingira ya kufurahisha yenye karaha.
 13. Kwenye muda wake wa ziada O'Connor
  alichora katuni,
 14. na uandishi wake pia
  umejaa masihara.

 15. Kwenye simulizi zake, mama na sura
  "pana na ya upole kama kabichi",
 16. mwanaume ana nguvu sana kama "dekio la
  sakafuni",
 17. na mwili wa mwanamke mmoja
  una umbo kama "chombo cha kuzika".
 18. Majina ya wahusika wake yamejawa ujanja.
 19. Chukulia simulizi "Maisha Unayoyaokoa
  Yanaweza Kuwa ya Kwako",

 20. ambapo mtembezi mwenye mkono mmoja
  Tom Shiftlet anaenda kwenye maisha
 21. ya ajuza mmoja aitwae Lucynell Crater
 22. na binti yake ambaye ni kiziwi na bubu.
 23. Japo mama Carter anajiamini,
 24. nyumba yake iliyojitenga inaanguka.

 25. Mwanzoni, tunaweza kushuku nia za Shiflet
 26. alipojitolea kusaidia kwenye nyumba,
 27. lakini O'Connor anaenda kuonyesha
  kuwa yule ajuza ni
 28. mjanja kama mgeni wake asiotarajiwa-
 29. na kutikisa mategemeo ya msomaji
  kuhusu nani ana faida zaidi.
 30. Kwa O'Connor, hamna somo lililokuwa
  na kizuizi.
 31. Japo alikuwa ni Mkatoliki aliyejitoa,

 32. hakuogopa kufuatilia uwezekano
 33. wa mawazo mema na tabia isiyo njema,
 34. inayokuwepo kwa mtu mmoja.
 35. Kwenye riwaya yake ya Wajeuri
  Wanaiondolea Mbali,
 36. mhusika mkuu anatingwa na mawazo
  ya kuwa mtu wa Mungu -
 37. lakini pia anawasha moto na kuua.
 38. Kitabu kinaanza na nabii amaesita
  akiwa kwenye nafasi yenye utata:
 39. "Mjomba wa Francis Marion Tarwater
  alikua amekufa kwa nusu siku tu
 40. pale huyo mvulana alipolewa sana akashindwa
  kumalizia kuchimba kaburi lake".
 41. Hii inamuacha mpita njia "kuvuta
  mwili kutoka kwenye meza ya chai
 42. ambapo ulikuwa umekaa bado na
  kuuzika [...]
 43. na udongo wa kutosha kwa juu
  kuzuia mbwa kuufukua".
 44. Japokuwa siasa zake bado ni za kulumbana,
 45. bunilizi ya O'Connor inaweza pia
  kulinganishwa na ubaguzi wa Kusini.

 46. Kwenye "Kila Kinachopanda Lazima
  Kikutane",
 47. anaelezea mvulana anayechukizwa
  na upendeleo wa mama yake.
 48. Lakini simulizi inaelezea kuwa
  ana mapungufu yake
 49. na inasema kwamba kuyagundua mabaya tu
 50. haitetei tabia yake kutokuthibitiwa.
 51. Hata O'Connor anavyochunguza
  mambo potofu ya ubinadamu,
 52. anaacha mlango wa ukombozi wazi kidogo.

 53. Kwenye "Mwanaume Mzuri ni Mgumu Kupata",
 54. anamkomboa ajuza anayeteseka kwa
  kumsamehe mshitakiwa aliyekubuhu,
 55. hata anavyoikaribia familia yake.
 56. Japo tunaweza kushtushwa na malipo
  anayolipa huyu mama kusamehewa,

 57. tunalazimika kukabiliana na
  yanayoendelea kwenye mda
 58. tunapoweza kuzingatia kuwa
  ukatili au ubaya.
 59. Uwezo wa O'Connor wa ajabu
 60. na tafiti zake za kujitenga na
  ushirikina wa Kusini

 61. ulimpelekea kutambuliwa kama
  mwandishi wa Kigothi wa Kusini.
 62. Lakini kazi yake ilisogea kupita
  tabia za kijinga kabisa
 63. na za kutisha zilizohusishwa
  na huo mtindo
 64. kuvumbua tofauti na mchanganyiko
  wa tabia za binadamu.
 65. Alijua baadhi ya hii tofauti
  ilileta karaha,
 66. na kuwa hadithi zake zingekuwa
  na ladha inayohitajika -
 67. lakini alisikia raha kuwachanganya
  wasomaji wake,
 68. O'Connor alikufa kwa lupus akiwa
  na miaka 39,
 69. baada ya ugonjwa kumweka shambani mwake
  Georgia kwa miaka kumi na mbili.

 70. Kwenye miaka hiyo,
 71. aliandika kazi zake nyingi
  alizokuwa akiwaza.
 72. Uwezo wake wa kuhama kati ya
  maudhi na uvumbuzi
 73. unaendelea kuvutia wasomaji kwenye
  dunia yake ya kufikirika isiyoisha.
 74. Kama mhusika Tom Shirlet anavyosema,
 75. mwili ni "kama nyumba:
 76. haiendi popote,
 77. lakini roho, mwanamke,
  ni kama gari moto:
 78. daima lipo kwenye mwendo".