Return to Video

Mapinduzi ya kilimo mapya ya dunia

  • 0:02 - 0:06
    Mwaka 2019, ubinadamu ulipata tahadhari:
  • 0:06 - 0:08
    30 ya wanasayansi mashuhuri duniani
    walipeana majibu
  • 0:08 - 0:12
    ya utafiti wa miaka mitatu ya
    kilimo cha kimataifa
  • 0:12 - 0:16
    na kutangaza kuwa uzalishaji wa nyama
    unaathiri sayari yetu
  • 0:16 - 0:17
    na kuhatarisha afya ya dunia.
  • 0:18 - 0:20
    Mwandishi mmoja wa utafiti alinena
  • 0:20 - 0:23
    ya kuwa "ubinadamu ni hatarisho
    kwa utulivu wa sayari ...
  • 0:23 - 0:28
    [Hii inahitaji] sio chini ya
    uvumbuzi mpya wa kilimo wa kimataifa."
  • 0:29 - 0:31
    Kama mtu ambaye ametumia miongo miwili
  • 0:31 - 0:34
    kutetea kuhama uzalishaji wa nyama
    kwa viwanda,
  • 0:34 - 0:38
    nilitaka kuamini kuwa wito huu
    ulikuwa unaenda kuleta mabadiliko.
  • 0:38 - 0:43
    Jambo ni kuwa nimeona hili
    mara kwa mara kwa miongo.
  • 0:44 - 0:47
    Hii hapa 2018 kutoka kwa jarida "Nature,"
  • 0:47 - 0:50
    2017 kutoka "Bioscience Journal,"
  • 0:50 - 0:54
    2016 kutoka Chuo cha Taifa cha Sayansi.
  • 0:54 - 0:58
    Lengo kuu la utafiti hizi
    huwa ni mabadiliko ya hewa.
  • 0:58 - 1:02
    Lakini upinzani wa kiuavijasumu
    ni tishio kubwa.
  • 1:03 - 1:06
    Tunawapa mifugo vipimo
    kubwa vya viuavijasumu.
  • 1:06 - 1:10
    Viuavijasumu kisha hubadilika
    na kuwa wadudu wenye nguvu
  • 1:10 - 1:13
    wanaotishia kufanya kiuavijasumu
    kuwa bila kazi
  • 1:13 - 1:16
    katika maisha yetu.
  • 1:16 - 1:17
    Unataka kitisho?
  • 1:17 - 1:20
    Tafuta: "mwisho wa kazi wa kiuavijasumu."
  • 1:21 - 1:23
    Naenda kuweka bayana jambo moja:
  • 1:23 - 1:25
    Siko hapa kueleza mtu anachopaswa kula.
  • 1:26 - 1:27
    Hatua ya kibinafsi ni sawa,
  • 1:27 - 1:30
    lakini upinzani wa kiuavijasumu
    na mabadiliko ya hewa --
  • 1:30 - 1:32
    yanahitaji zaidi.
  • 1:32 - 1:36
    Kando na hayo, kusadikisha ulimwengu
    kupunguza kula nyama haijafaulu.
  • 1:37 - 1:42
    Kwa miaka 50, wanaharakati wa mazingira,
    wataalamu wa afya wa duniani
  • 1:42 - 1:45
    na wanaharakati wa wanyama, wamesihi umma
    kula nyama kiasi.
  • 1:45 - 1:47
    Na bado, wastani wa ulaji nyama
  • 1:47 - 1:51
    umekuwa juu kihistoria.
  • 1:51 - 1:55
    Mkazi wastani wa Amerika Kaskazini
    alikula pauni 200 ya nyama mwaka jana.
  • 1:56 - 1:57
    Na sikula ata.
  • 1:57 - 1:58
    (Kicheko)
  • 1:59 - 2:02
    Inamaanisha kuna mtu huko nje
    alikula pauni 400 ya nyama.
  • 2:02 - 2:04
    (Kicheko)
  • 2:04 - 2:05
    Kwa njia tunayoelekea,
  • 2:05 - 2:10
    tunaenda kuhitaji kuzalisha asilimia
    70 hadi 100 zaidi ya nyama ifikapo 2050.
  • 2:10 - 2:13
    Hili linahitaji suluhisho la duniani pote.
  • 2:13 - 2:17
    Tunachohitaji ni kuzalisha nyama
    ambayo watu watapenda,
  • 2:17 - 2:20
    lakini tuizalishe kwa njia mpya.
  • 2:20 - 2:22
    Nina mawazo kadhaa.
  • 2:22 - 2:26
    Wazo la kwanza:
    tukuze nyama kutoka kwa mimea.
  • 2:26 - 2:28
    Badala ya kukuza mimea,
    kuyalisha kwa wanyama,
  • 2:28 - 2:30
    na hayo yote yasiyofaa,
  • 2:30 - 2:33
    tukuze mimea hiyo,
    tuikuze na nyama,
  • 2:33 - 2:34
    tuifanye iwe na nyama.
  • 2:35 - 2:38
    Wazo la pili: kwa nyama halisi ya wanyama,
  • 2:38 - 2:40
    tuikuze kwa chembe moja kwa moja.
  • 2:40 - 2:43
    Badala ya kukuza wanyama waliohai,
    tukuze chembe moja kwa moja,
  • 2:44 - 2:47
    Inachukua wiki sita kulea kuku
    afike kimo cha kuchinjwa.
  • 2:47 - 2:49
    Kuza chembe moja kwa moja,
    na utapata matokea sawia
  • 2:49 - 2:51
    kwa siku sita.
  • 2:52 - 2:54
    Hivi ndivyo itakuwa katika skeli.
  • 2:55 - 2:58
    Ni ujirani wa kirafiki wa kiwanda
    cha nyama.
  • 2:58 - 3:01
    (Kicheko)
  • 3:01 - 3:03
    Nitataja mambo mawili kuhusu hili.
  • 3:03 - 3:05
    Jambo la kwanza, tunasadiki tunaweza.
  • 3:05 - 3:09
    Miaka iliyopita, makampuni mengine
    yamekuwa yakikuza nyama kutoka kwa mimea
  • 3:09 - 3:13
    na walaji hawawezi tofautisha
    na nyama halisi,
  • 3:13 - 3:17
    na sasa kuna makampuni mbalimbali
    yanayokuza nyama halisi ya wanyama
  • 3:17 - 3:19
    moja kwa moja kutoka kwa chembe.
  • 3:19 - 3:21
    Nyama hii ya mimea na ya chembe
  • 3:21 - 3:23
    inawapa walaji vyote
    wanavyopenda kuhusu nyama --
  • 3:23 - 3:25
    ladha, umbile na kadhalika --
  • 3:25 - 3:28
    lakini bila hitaji ya viuavijasumu
  • 3:28 - 3:31
    na sehemu ya madhara kwa hali ya hewa.
  • 3:31 - 3:35
    Na kwa sababu teknolojia
    hizi mbili ni bora zaidi,
  • 3:35 - 3:36
    kwa ukuzaji
  • 3:36 - 3:38
    bidhaa hizi zitakuwa za bei ya chini.
  • 3:39 - 3:41
    Jambo moja kuhusu hilo --
  • 3:41 - 3:43
    haitakuwa rahisi.
  • 3:43 - 3:47
    Makampuni haya yanayotumia mimea
    yametumia misandali kidogo kwa baga zao,
  • 3:47 - 3:50
    na chembe ya nyama bado
    haijazinduliwa kibiashara.
  • 3:51 - 3:53
    Kwa hivyo tutahitaji ushirikiano wa wote
  • 3:53 - 3:55
    ili kufanya hili liwe kiwanda
    cha nyama duniani.
  • 3:56 - 3:59
    Mwanzo, tunahiaji sekta ya nyama
    ya sasa.
  • 3:59 - 4:01
    Hatutaki kuvuruga sekta ya nyama,
  • 4:01 - 4:03
    tunataka kuibadilisha.
  • 4:03 - 4:05
    Tunahitaji dhana yake ya uchumi,
  • 4:05 - 4:08
    msururu wake wa ugavi,
    utaalam wake wa uuzaji
  • 4:08 - 4:10
    na wateja wake.
  • 4:11 - 4:13
    Tunahitaji pia serikali.
  • 4:13 - 4:16
    Serikali hutumia mabilioni ya madola
    kila mwaka
  • 4:16 - 4:18
    kwa utafiti na maendeleo
  • 4:18 - 4:21
    unaozingatia afya duniani
    na mazingira.
  • 4:21 - 4:25
    Yanafaa kuwekeza sehemu ya fedha hizo
    katika sadifisha na kuboresha
  • 4:25 - 4:29
    uzalishaji wa mimea na
    nyama iliyokuzwa na chembe ya mimea.
  • 4:30 - 4:35
    Tazama, kumi ya maelfu ya watu walikufa
    kutoka kwa usugu wa viuavijasumu
  • 4:35 - 4:37
    Amerika Kaskazini mwaka jana.
  • 4:38 - 4:43
    Ifikapo 2050, tarakimu hiyo itakuwa
    milioni 10 kwa mwaka duniani.
  • 4:44 - 4:48
    Mabadiliko ya hewa pia
    ni athari iliyopo
  • 4:48 - 4:51
    kwa sehemu kubwa ya familia yetu duniani,
  • 4:51 - 4:55
    wakiwemo watu maskini zaidi
    hapa duniani.
  • 4:55 - 5:00
    Mabadiliko ya hewa, kinga ya
    viuavijasumu-- hizi ni dharura duniani.
  • 5:00 - 5:05
    Uzalishaji wa nyama unazidi
    dharura hizi kwa kipimo duniani.
  • 5:05 - 5:08
    Lakini hatuendi kupunduza
    ulaji nyama
  • 5:08 - 5:11
    hadi tuwape walaji bidhaa mbadala
  • 5:11 - 5:15
    zitakazo gharimu sawa au chini
    na ladha iwe sawia au bora.
  • 5:16 - 5:17
    Tuko na jawabu.
  • 5:17 - 5:21
    Tutengeneze nyama kutoka kwa mimea.
    Tuikuze moja kwa moja kutoka kwa chembe.
  • 5:21 - 5:25
    Tayari tumechelewa kutumia
    raslimali tulizonazo
  • 5:25 - 5:30
    kutengeneza mapinduzi ya kilimo mapya.
  • 5:30 - 5:31
    Asanteni.
  • 5:31 - 5:35
    (Makofi)
Title:
Mapinduzi ya kilimo mapya ya dunia
Speaker:
Bruce Friedrich
Description:

Njia ya uzalishaji nyama ya kawaida inaathiri mazingira yetu na ni athari kwa afya ya ulimwengu, lakini watu hawaendi kupunguza ulaji nyama hadi tuwape chaguo mbadala yanye bei sawia (au ya chini) na ladha sawia (au bora). Kwa hotuba ya kufungua macho, mvumbuzi wa vyakula na mwana TED Bruce Friedrich anaonyesha bidhaa za mimea na chembe ambazo zinaweza kubadilisha sekta ya nyama duniani -- na sahani yako ya chajio.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
05:48

Swahili subtitles

Revisions