-
Title:
Jinsi tunaweza fundisha miili yetu kupona haraka
-
Description:
Itakuaje kama tutaweza saidia miili yetu kupona haraka bila makovu, kama Wolverine kwenye X-Men? Mshiriki wa TED Kaitlyn Sadtler anafanya kazi ili ndoto hii iwe kweli kwa kutengeneza vifaa vya biolojia vipya vinavyoweza kubadili jinsi mfumo wetu wa kinga unavyojibu majeraha. Kwenye mazungumzo haya mafupi, anaonyesha njia tofauti ambazo bidhaa hizi zinaweza kusaidia mwili ukajijenga upya.
-
Speaker:
Kaitlyn Sadtler
-
Je kama unaweza kuchukua kidonge
au chanjo
-
na kama ukawa unapona mafua,
-
unaweza kuponya jeraha kwa urahisi?
-
Leo, kama tukiwa na upasuaji au ajali,
-
tunakaa hospitalini kwa wiki,
-
na mara nyingi tunabaki na makovu
na madhara ya uchungu
-
kwa uwezo wetu wa kutengeneza au
kukuza afya, na viungo visivyo na jeraha.
-
Nafanya kazi kujenga vifaa
-
vinavyofundisha mfumo wetu wa kinga ili
utupe alama za kukuza tishu mpya.
-
Kama tu chanjo inavyofundisha
mwili wetu kupigana na magonjwa,
-
badala yake tunaweza fundisha
mfumo wetu wa kinga
-
kujenga tishu
na kuponya majeraha kwa urahisi.
-
Sasa, kukuza sehemu za mwili kutoka
popote inaweza kuonekana kama uchawi,
¶
-
lakini kuna viumbe kadhaa
vinavyoweza kutimiza mafanikio haya.
-
Baadhi ya mijusi inaweza kukuza mikia yao,
-
yule salamanda mnyenyekevu
anaweza kukuza kabisa mkono wake,
-
na hata binadamu tu
wanaweza kukuza ini lao
-
baada ya kupoteza zaidi ya nusu
ya uzito wao wa awali.
-
Ili kufanya uchawi huu
kuwa karibu zaidi na ukweli,
¶
-
nina fanya uchunguzi wa jinsi mwili wetu
unaweza kuponya majeraha na kujenga tishu
-
kupitia maelekezo kutoka mfumo
wa kinga.
-
Kutoka kwenye mkato wa goti lako
mpaka maambukizi ya sinus yanayoboa,
-
mfumo wetu wa kinga unalinda
mwili wetu na hatari.
-
Mimi ni immunolojisti
-
na kwa kutumia ninachojua
kuhusu mfumo wa ulinzi wa mwili wetu,
-
niliweza kutambua wachezaji wakuu
-
kwenye mapambano ya kujenga
mikato na michubuko yetu.
-
Tunapoangalia vifaa
vinavyojaribiwa kwa sasa
¶
-
kwa uwezo wao wa kusaidia kukuza misuli,
-
timu yetu imeona kua baada ya kutibu
msuli uliojeruhiwa na vifaa hivi,
-
kulikua na idadi kubwa ya seli za kinga
-
ndani ya kifaa
na inayozunguka msuli.
-
Hivyo kwa sababu hii,
-
badala ya seli za kinga kukimbilia
kwenye maambukizi kupigana na bakteria,
-
zinakimbilia kuelekea kwenye jeraha.
-
Nimegundua aina maalum
ya seli za kinga,
-
ni msaidizi T kiini,
-
ilikua inapatikana ndani ya
kile kifaa nilichokipanda
-
na ni muhimu kabisa kwa ajili ya uponyaji
jeraha.
-
Sasa, kama tu ulivyokua mdogo na
ukavunja penseli yako
¶
-
na kujaribu kugundisha kwa pamoja tena,
-
tunaweza kupona,
-
lakini inaweza isiwe
njia inayofanya kazi zaidi,
-
na tutapata kovu.
-
Hivyo kama hatuna hizi msaidizi T kiini,
-
badala ya misuli yenye afya,
-
misuli yetu inatengeneza
seli za mafuta ndani yake,
-
na kama kuna mafuta kwenye misuli yetu,
haina nguvu.
-
Sasa, kutumia mfumo wetu wa kinga,
-
miili yetu inaweza kukua tena
bila haya makovu
-
na kuonekana kama ilivyokua
kabla hata hatujajeruhiwa.
-
Nina fanya kazi kutengeneza vifaa
¶
-
vinavyotuma alama
za kujenga tishu mpya
-
kwa kubadilisha mwitikio wa kinga.
-
Tunajua kua muda wowote
kifaa kinapopandwa mwilini mwetu,
-
mfumo wa kinga utaitikia kwake.
-
Hii hutofautiana kwanzia kipima mapigo ya
moyo mpaka pampu za insulini
-
mpaka vifaa ambavyo wanatumia wahandisi
ili kujaribu kujenga tishu mpya.
-
Hivyo ninapoweka hicho kifaa,
au kiguzo, ndani ya mwili,
-
mfumo wa kinga hutengeneza
mazingira madogo ya seli na protini
-
ambazo zinaweza badili jinsi
seli shina zetu zinavyoishi.
-
Sasa, kama hali ya hewa
inavyoathiri shughuli zetu za siku,
-
kama kwenda kukimbia
-
au kukaa ndani na kutazama
kipindi kizima cha TV kwenye Netflix,
-
mazingira ya kinga ya kiguzo
-
inaathiri jinsi seli shina zetu
zinavyokua na kuendelea.
-
Kama tunakua na ishara za mbovu,
-
tuseme kama ishara za Netflix,
-
tunapata seli za mafuta badala ya misuli.
-
Viguzo hivi vimetengenezwa na
aina nyingi tofauti ya vitu,
-
kwanzia plastiki mpaka vitu
vinavyopatikana kiasili,
-
nyuzi ndogo zinazotofautiana unene,
-
sifongo ambazo zina matundu makubwa
au madogo,
-
jeli zenye ugumu unaotofautiana.
-
Na watafiti wanaweza hata
kutengeneza vifaa
-
kutoa ishara tofauti na mda.
-
Hivyo kwa maneno mengine, tunaweza kupanga
maonyesho hayaya Broadway ya seli
-
kwa kuzipa jukwaa, sehemu
na heshima sahihi
-
inayoweza kubadilishwa kwa tishu tofauti,
-
kama tu mtengenezaji anavyobadilisha
jukwaa
-
kwa "Les Mis" dhidi ya
"Little Shop of Horrors."
-
Nina changanya aina maalum za ishara
-
ambazo zinaiga jinsi miili yetu inavyojibu
maumivu kutusaidia kua wapya.
-
Huko mbeleni, tutaona bandi ya misaada
ambayo ni kizuia kovu,
-
kijazo cha msuli kinachofinyangika
au hata chanjo inayoponya jeraha.
-
Sasa, hatutaweza kuamka kesho na
kuweza kuponywa kama Wolverine.
¶
-
Pengine hata sio Jumanne ijayo pia.
-
Ila na haya maednelelo,
-
na kufanya kazi na mfumo wetu wa kinga
kusaidia kuunda tishu na kutibu majeraha,
-
tunaweza kuanza kuona
bidhaa kwenye soko
-
zinazofanya kazi na mfumo wa ulinzi
mwilini kusaidia kutengeneza upya,
-
na labda siku moja tutaweza
kua sambamba na salamander.
-
-