Swahili subtitles

← Kufanya yasiyowezekana, kuishinda hofu| Dan Meyer | TEDxMaastricht

Get Embed Code
85 Languages

Showing Revision 19 created 10/14/2017 by Nelson Simfukwe.

 1. Asante
 2. Palikuwa na mfalme nchini India, Maharaja
  na siku yake ya kuzaliwa ilitolewa amri
 3. kwamba machifu wote walete
  zawadi kwa mfalme.
 4. Wengine wakaleta hariri bora,
  wengine wakaleta panga maridadi,
 5. wengine dhahabu
 6. mwisho wa mstari alikuja akitembea
  mzee mdogo mwenye makunyanzi
 7. ambaye alitembea kutoka kijijini kwake
  kwa safari ya siku nyingi kando ya bahari.
 8. alipokuwa akisogea mwana mfalme akauliza,
  'Umemletea zawadi gani Mfalme?'
 9. Na mzee yule taratibu sana
  akakunjua mkono wake kuonyesha
 10. kombe la baharini zuri sana, lenye makoa
  ya zambarau na njano,nyekundu na bluu.
 11. Na mwana Mfalme akasema,
 12. "Hiyo si zawadi kwa Mfalme!
  Ni zawadi gani hiyo?"
 13. Mzee yule akamwangalia taratibu
  na kusema
 14. "Kutembea mwendo mrefu.. ni sehemu
  ya zawadi"
 15. (Kicheko)
 16. Baada ya muda mfupi,
  Nitawapa zawadi,
 17. zawadi niaminiyo
  ni zawadi inayostahili kuenezwa.
 18. Ila kabla ya hayo, ngoja niwachukue
 19. kwenye mwendo wangu mrefu.
 20. Kama wengi wenu,
 21. Nilianza maisha kama mtoto mdogo.
 22. Wangapi kati yenu
  mlianza maisha kama mtoto ?
 23. Aliyezaliwa mchanga?
 24. Karibia nusu yenu.. Sawa
 25. (Kicheko)
 26. Na mliobakia, vipi?
  Mlizaliwa mkiwa watu wazima?
 27. Ama kweli, nataka kukutana na mama zenu!
 28. Ongelea yasiyowezekana!
 29. Nikiwa mtoto mdogo, siku zote nilipendezwa
  kufanya mambo yasiyowezekana
 30. Leo ni siku ambayo nimekuwa nikiitarajia
  kwa miaka mingi,
 31. kwa sababu leo ni siku ambayo
  nitajaribu
 32. kufanya yasiyowezekana
  mbele ya macho yenu
 33. Hapahapa TEDxMaastrich
 34. Nitaanza
 35. Kwa kuonyesha mwisho wake:
 36. Na nitawathibitishia kwamba
 37. yasiyowezekana siyo hayawezekani
 38. Na nitamalizia kwa kuwapa
  zawadi yenye kustahili kuieneza:
 39. Nitawaonyesha kwamba unaweza
  kufanya yasiyowezekana maishani mwako.
 40. katika kutafuta kufanya yasiyowezekana,
  nimegundua kuna
 41. mambo mawili yanayofanana
  kati ya watu duniani.
 42. Kila mtu ana hofu,
 43. na kila mtu ana ndoto.
 44. Katika kutafuta kufanya yasiyowezekana
  nimegundua kuna vitu vitatu
 45. ambavyo nimevifanya miaka mingi ambavyo
 46. vimenisababishia kufanya yasiyowezekana:
 47. Mchezo wa mpira wa kuchenga au "Trefball"
 48. Superman,
 49. na Mbu
 50. Hayo ni maneno yangu matatu makuu.
 51. Mmeshajua kwanini nafanya
  yasiyowezekana maishani mwangu
 52. Hivyo nitawachukua katika safari
  yangu, ya mwendo mrefu
 53. kutoka kwenye hofu hadi ndoto
 54. kutoka kwenye maneno hadi panga,
 55. Kutoka Mpira wa kuchenga
 56. hadi Superman
 57. hadi kwa Mbu
 58. Na ninatumaini kuwaonyesha
 59. unawezaje kufanya yasiyo
  wezekana maishani mwako
 60. Oktoba 4, mwaka 2007.
 61. Moyo wangu ulienda mbio,
  magoti yangu yalitetema
 62. nilipokuwa napanda jukwaani
 63. kwenye ukumbi wa Sanders
 64. Chuo cha Harvard kupokea
 65. Tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu
 66. kwa kushiriki kuandika ikisiri
  ya utafiti wa kitabibu
 67. ulioitwa "Kumeza Upanga...
 68. ...na Athari zake"
 69. (Kicheko)
 70. Ilichapishwa kwenye jarida dogo
  ambalo sikuwahi kulisoma kabla,
 71. Jarida la Kitabibu la Uingereza.
 72. Na kwangu, hiyo ilikuwa ndoto
  isiyowezekana kuwa kweli,
 73. ilikuwa ni mshangao usiotegemewa
  kwa mtu kama mimi,
 74. ilikuwa ni heshima ambayo sitaweza kusahau
 75. Lakini haikuwa sehemu ya kubwa ya
  kukumbuka maishani mwangu.
 76. Mnamo Oktoba 4, mwaka 1967
 77. kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba
 78. aliteseka na hofu kubwa kupita kiasi.
 79. Alipojiandaa kupanda jukwaani,
 80. moyo wake ulienda mbio,
 81. magoti yake yalikuwa yakitetemeka.
 82. Alikwenda kufungua kinywa chake kuongea,
 83. maneno hayakuweza kutoka.
 84. Alisimama akitetemeka na kutoa machozi.
 85. Alipooza kwa mshtuko wa ghafla,
 86. alipatwa fadhaa kwa hofu.
 87. huyu kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba
 88. alitesekana na hofu kubwa kupita kiasi.
 89. Alikuwa na hofu ya giza,
 90. hofu ya vimo virefu,
 91. hofu ya buibui na nyoka ...
 92. Kuna yeyote anayeogopa buibui na nyoka?
 93. Naam, wachache wenu ...
 94. Alikuwa na hofu ya maji na papa ...
 95. Hofu ya madaktari na manesi na madaktari
  wa meno,
 96. na sindano na kutobolewa na vitu vya
  ncha kali.
 97. Lakini zaidi ya chochote,
  alikuwa na hofu ya
 98. watu
 99. Huyo kijana mwoga,mwenye aibu na mwembamba
 100. alikuwa mimi.
 101. Nilikuwa na hofu ya kushindwa na
  kukataliwa,
 102. kutojithamini, kujiona duni,
 103. na kitu ambacho hata hatukujua
  unaweza kujiandikisha kwa siku hizo:
 104. ugonjwa wa hofu ya ukaribu na watu.
 105. Kwa sababu nilikuwa na hofu, waonevu
  walinitania na kunipiga.
 106. Walinicheka na kuniita majina,
  Hawakuniruhusu kucheza nao
 107. michezo ya aina yoyote.
 108. Ah, kulikuwa na mchezo mmoja
  walikuwa wakiruhusu kucheza kwenye ...
 109. Mpira wa kuchenga -
 110. na sikuwa mchengaji nzuri.
 111. Waonevu waliita jina langu,
 112. na nilipoangalia
  niliona mipira myekundu ya kukwepa
 113. ikivurumishwa usoni wangu kwa kasi kubwa
 114. bam, bam, bam!
 115. Ninakumbuka siku nyingi
  nikirudi nyumbani kutoka shule,
 116. uso wangu ulikuwa mwekundu ukichonyota,
  masikio yangu yalikuwa mekundu yakivuma.
 117. Macho yangu yalichoma kwa machozi,
 118. na maneno yao yalichoma masikioni mwangu.
 119. Na yeyote aliyesema,
 120. "Fimbo na mawe vyaweza kunivunja mifupa,
  bali maneno hayatoniumiza kamwe "...
 121. Ni uongo.
 122. Maneno huweza kukata kama kisu.
 123. Maneno huweza kupenya kama upanga.
 124. Maneno huwezafanya majeraha yenye kina
 125. yasiweze kuonekana.
 126. Hivyo nilikuwa na hofu.
  Na maneno yalikuwa adui yangu mkubwa.
 127. Bado ni adui yangu.
 128. Lakini pia nilikuwa na ndoto.
 129. Nilienda nyumbani
  na kutorokea kwenye futuhi za Superman
 130. na nilisoma futuhi za Superman
 131. na niliota kutaka kuwa shujaa mkubwa
  kama Superman.
 132. Nilitaka kupigania kweli na haki,
 133. Nilitaka kupambana dhidi ya
  wahalifu na mahasimu,
 134. Nilitaka kupaa duniani kote
  kufanya vitendo vya ujasiri kuokoa maisha.
 135. Nilikuwa pia navutiwa mno
  na vitu vilivyokuwa kweli.
 136. Nilisoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness
  na kitabu cha Ripley kiitwacho Amini au Usiamini.
 137. Yeyote kati yenu amewahi kusoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness au kitabu cha Ripley?
 138. Navipenda vitabu hivi!
 139. Niliona watu wafanyao ujasiri halisia.
 140. Nikasema, Nataka kufanya hivyo.
 141. Ikiwa waonevu hawataniruhusu
 142. kucheza katika michezo yao yoyote,
 143. Nataka kufanya maajabu, ujasiri halisi.
 144. Nataka kufanya kitu cha kusifika
  ambacho hao waonevu hawawezi kufanya.
 145. Nataka kupata kusudi langu na wito wangu,
 146. Nataka kujua kuwa maisha yangu yana maana,
 147. Nataka kufanya kitu cha kushangaza
  kubadili ulimwengu;
 148. Ninataka kuthibitisha
  yasiyowezekana sio hayawezekani.
 149. Kupeleka mbele miaka 10 -
 150. Ilikuwa wiki kabla ya kutimiza miaka 21.
 151. Mambo mawili yalitokea kwa siku moja
  ambayo yangebadilisha maisha yangu milele.
 152. Nilikuwa nikiishi Tamil Nadu, India Kusini
 153. Nilikuwa mmishonari huko,
 154. na mshauri wangu, rafiki yangu aliniuliza,
 155. "Je, una Thromu, Daniel?"
 156. Na nikasema, "Thromu?
  Thromu ni nini? "
 157. Alisema, "Thromu ni malengo makuu ya
  maisha.
 158. Ni muunganiko
  wa ndoto na malengo, kama ungeweza
 159. kufanya chochote unachotaka,
  kwenda popote unapotaka
 160. kuwa mtu yeyote unayetaka,
 161. ungekwenda wapi?
  Ungefanya nini?
 162. Ungekuwa nani?
 163. Nikasema, "Siwezi kufanya hivyo!
  Naogopa sana! Naogopa mengi mno! "
 164. Usiku huo nilichukua mkeka wangu wa mchele
  juu ya paa la ghorofa,
 165. nikautandika chini ya nyota,
 166. na kuangalia popo wakiwashambulia mbu.
 167. Na yote niliyofikiria ilikuwa thromu,
  na ndoto na malengo,
 168. na wale washujaaji wenye mipira ya kuchenga.
 169. Masaa machache baadaye niliamka.
 170. Moyo wangu ulienda mbio,
  magoti yangu yakitetemeka.
 171. Safari hii haikuwa na hofu.
 172. Mwili wangu wote ulitikisika.
 173. Na kwa siku tano zilizofuata
 174. Nilipoteza na kurudisha fahamu,
  kitandani nikipigania maisha yangu.
 175. Ubongo wangu ulikuwa unawaka
  na homa ya malaria yenye jotoridi la 105.
 176. Na kila fahamu ziliponirudia,
  nilichowaza ilikuwa kuhusu thromu.
 177. Niliwaza
  "Nataka kufanya nini na maisha yangu?"
 178. Hatimaye, usiku kabla
  sijafikisha miaka 21,
 179. katika wakati wa kuelewa,
 180. Nilikuja kutambua:
 181. Nilitambua kwamba yule mbu mdogo,
 182. Anofelesi Stefensi,
 183. yule mbu mdogo
 184. aliye na uzito chini ya mikrogramu 5
 185. chini ya punje ya chumvi,
 186. anaweza kuangusha
  mtu wa ratili 170, mtu wa kilo 80,
 187. Niligundua kwamba alikuwa hasimu wangu.
 188. Kisha nikagundua,
  hapana, hapana, sio mbu,
 189. Ni vimelea vidogo
  ndani ya mbu,
 190. Plasmodium Falciparum,
  ambao huua zaidi ya watu milioni kwa mwaka
 191. Kisha nikagundua
  Hapana, hapana, tena ni ndogo zaidi,
 192. lakini kwangu, ilionekana kubwa zaidi.
 193. Niligundua,
 194. hofu ilikuwa hasimu yangu,
 195. vimelea yangu,
 196. vilivyonitia ulemavu
  na kunipooza mimi maisha yangu yote.
 197. Unajua, kuna tofauti
  kati ya hatari na hofu.
 198. Hatari ni halisi.
 199. Hofu ni hiari.
 200. Na nikagundua kuwa nina hiari:
 201. Aidha niishi kwa hofu,
  na kufa katika kushindwa usiku ule,
 202. au ningeweza kuua hofu yangu,
  na ningeweza
 203. kufikia ndoto zangu,
  Ningeweza kuthubutu kuishi maisha.
 204. Na unajua, kuna kitu kuhusu
  kuwa kwenye kitanda cha mauti
 205. na kukabiliwa na kifo ambacho haswa
  kinakufanya utake kweli kuishi maisha.
 206. Nikagundua kuwa kila mtu hufa,
  si kila mtu huishi.
 207. Ni katika kufa ndio sisi tunaishi.
 208. Unajua, wakati unapojifunza kufa,
 209. unajifunza kweli kuishi.
 210. Kwa hiyo nikaamua nitaenda kubadilisha
 211. hadithi yangu usiku huo.
 212. Sikutaka kufa.
 213. Hivyo nikafanya sala ndogo, nikasema,
 214. "Mungu, ukiniruhusu niishi
  nifikishe miaka 21,
 215. Sitaruhusu hofu
  itawale maisha yangu tena.
 216. Nitaziweka hofu zangu kifoni,
 217. Nitaenda kuzifikia ndoto zangu,
 218. Ninataka kubadilisha mtazamo wangu,
 219. Nataka kufanya kitu cha ajabu
  na maisha yangu,
 220. Nataka kupata kusudi langu na wito wangu,
 221. Ninataka kujua kuwa yasiyowezekana
  si hayawezekani. "
 222. Sitawaambia kama nilinusurika usiku ule;
  Nitawaacha mfikirie.
 223. (Kicheko)
 224. Lakini usiku huo niliandika orodha
  ya Thromu zangu 10 za kwanza:
 225. Niliamua nilitaka
  kutembelea mabara makubwa
 226. kutembelea Maajabu 7 ya Dunia
 227. kujifunza lugha nyingi,
 228. kuishi kwenye kisiwa kitupu,
 229. kuishi kwenye meli baharini,
 230. kuishi na kabila la Wahindi
  katika Amazon,
 231. kupanda hadi juu
  ya mlima mrefu kuliko yote Sweden,
 232. Nilitaka kuona mawio Mlima Everest,
 233. kufanya kazi na biashara ya muziki
  Nashville,
 234. Nilitaka kufanya kazi ya sarakasi,
 235. na nilitaka kuruka nje ya ndege.
 236. Zaidi ya miaka ishirini iliyofuata,
  Nilitimiza thromu hizo kwa wingi.
 237. Kila wakati niliondoa
  thromu kwenye orodha yangu,
 238. Niliongeza 5 au 10 zaidi kwenye orodha
  na orodha yangu iliendelea kukua.
 239. Kwa miaka saba iliyofuata, niliishi
  kwenye kisiwa kidogo katika Bahamas
 240. kwa karibu miaka saba
 241. katika kibanda cha makuti,
 242. nikiwinda papa na taa wa kula,
  nikiwa mtu pekee kwenye kisiwa,
 243. nikiwa nimevaa msuli,
 244. na nikajifunza kuogelea na papa.
 245. Na kutoka huko, nikahamia Mexico,
 246. na kisha nikasafiri
  kwa bonde la Mto Amazon nchini Ecuador,
 247. Pujo Pongo Ecuador,
  niliishi na kabila moja huko,
 248. na kidogo kidogo nilianza kuongeza
  kujiamini kwa thromu zangu tu.
 249. Nilihamia biashara ya muziki Nashville,
  kisha Sweden,
 250. nikahamia Stockholm,
  kufanyakazi katika biashara ya muziki,
 251. ambapo nilipanda kilele cha Ml. Kebnekaise
  juu ya mzunguko wa Arctic.
 252. Nilijifunza udamisi,
 253. na viinimacho,
 254. na kutembea kama ngongoti,
 255. kuendesha baiskeli kwa tairi moja,
  kula moto, kula kioo.
 256. Mwaka 1997 nilisikia kuna
  wameza panga wasiozidi kumi na mbili
 257. na nikasema, "Inabidi kufanya hivyo!"
 258. Nilikutana na mmeza panga,
  na nikamwomba vidokezo.
 259. Akasema, "Naam, nitakupa vidokezo 2:
 260. Namba 1: Ni hatari sana,
 261. Watu wamekufa wakifanya hivi.
 262. Namba 2:
 263. Usijaribu! "
 264. (Kicheko)
 265. Basi nikaiongeza kwenye orodha ya thromu.
 266. Na nikafanya mazoezi
  mara 10 hadi 12 kwa siku, kila siku
 267. kwa miaka minne.
 268. Sasa nilipigia hesabu hizo...
 269. 4 x 365 [x 12]
 270. Ilikuwa karibu 13,000
  majaribio yasiyofanikiwa
 271. kabla sijatia panga langu wa kwanza
  chini koo mwaka 2001.
 272. Wakati huo nikaweka thromu
 273. kuwa mtaalamu wa ulimwengu
  kwa kumeza panga.
 274. Basi nilitafuta kila kitabu,
  gazeti, makala ya gazeti,
 275. kila ripoti ya kitabibu,
  Nilijifunza fiziolojia, anatomia,
 276. Niliongea na madaktari na manesi,
 277. niliwakutanisha wameza panga wote
  pamoja
 278. kwenye Shirikisho la Wameza Panga
  Kimataifa,
 279. nikafanya ikisiri miaka 2
  ya utafiti kitabibu
 280. kuhusu Umezaji wa Panga na athari zake
 281. iliyochapishwa
  katika Jarida la Kitabibu Uingereza.
 282. (Kicheko)
 283. Asanteni.
 284. (Makofi)
 285. Na nilijifunza mambo ya kuvutia sana
  kuhusu umezaji wa panga.
 286. Vitu vingine ambavyo haujawahi kufikiria
  kabla, hutasahau baada ya usiku huu.
 287. Wakati utakapoenda nyumbani, na unakata
  steki yako na kisu chako
 288. au panga, au "bestek" zako,
  utafikiri juu ya hili ...
 289. Nilijifunza kwamba umezaji panga
  ulianzia India -
 290. mahali nilipona kwa mara ya kwanza
  nikiwa kijana wa miaka 20 -
 291. karibu miaka 4000 ya kale, karibu 2000 BC.
 292. Zaidi ya miaka 150 iliyopita,
  wameza panga walitumika
 293. katika medani za sayansi na kitabibu
 294. ili kusaidia kuunda
  endoskopia imara mwaka 1868
 295. wakiwa na Dk. Adolf Kussmaul wa Freiburg, Ujerumani
 296. Mnamo 1906, elektrokadiogramu huko Wales,
 297. kujifunza matatizo ya kumeza,
  na mmeng'enyo wa chakula,
 298. aina ya bronkoskopia, .
 299. Lakini zaidi ya miaka 150 iliyopita,
 300. tunajua mamia ya madhara
  na vifo kadhaa ...
 301. Hii ni endoskopia imara
  iliyoanzishwa na Dk. Adolph Kussmaul.
 302. Lakini tuligundua kuwa kulikuwa na
  Vifo 29 zaidi ya miaka 150 iliyopita.
 303. pamoja na mmezaji panga huko London
  aliyetoboa moyo wake kwa panga
 304. Tulijifunza pia kuwa kuna kesi tatu hadi nane za
 305. madhara mkubwa ya umezaji panga
  kila mwaka.
 306. Najua kwa sababu mimi hupata simu.
 307. Nilikuwa na wawili,
 308. mmoja kutoka Sweden, na kutoka Orlando
  wiki chache zilizopita,
 309. wamezaji panga waliopo hospitalini
  kutokana na madhara.
 310. Kwa hiyo ni hatari sana.
 311. Jambo jingine nililojifunza ni kuwa
  kumeza panga huchukua
 312. miaka 2 hadi miaka 10
  kujifunza jinsi ya kumeza panga
 313. kwa watu wengi.
 314. Lakini ugunduzi unaovutia sana
  Nilijifunza ilikuwa
 315. jinsi wameza panga wanavyojifunza
  kufanya yasiyowezekana.
 316. Nami nitawapa siri ndogo:
 317. Usizingatie kwenye asilimia 99.9
  kuwa haiwezekani.
 318. Unazingatia hiyo 1% ambayo inawezekana,
  na fikiria jinsi ya kufanya iwezeikane
 319. Sasa napenda kukupeleka kwenye safari
  ndani ya akili ya mmeza panga.
 320. Ili kumeza panga,
  inahitaji akili itafakari jambo,
 321. uzingativu wa hali ya juu,
  kuonyesha ufasaha ili
 322. kutenganisha viungo vya ndani vya mwili
  na kushinda vitendo hiari mwilini
 323. kupitia njia ya ubongo iliyoimarishwa,
  kupitia marido ya kumbukumbu ya misuli
 324. kwa mazoezi ya makusudi
  zaidi ya mara 10,000.
 325. Sasa ngoja niwasafirishe kidogo
  ndani ya mwili wa mmeza panga
 326. Ili kumeza panga,
 327. Lazima niteleze panga juu ya ulimi wangu,
 328. nizuie kutaka kutapika
  kwenye shingo ya umio,
 329. zungusha mgeuko wa nyuzi 90
  chini ya gegedu ya ulimi,
 330. pitia kwenye msuli juu ya kilinda umio,
 331. zuia vitendohiari vya tumbo,
 332. telezea makali kwenye shimo la kifua
 333. kati ya mapafu.
 334. Katika hatua hii,
 335. Lazma kweli nisukume moyo wangu pembeni.
 336. Ikiwa utaangalia kwa makini,
 337. unawezaona moyo ukidunda kwa panga langu
 338. kwa sababu linaegemea moyo
 339. ikitenganishwa na karibu thumuni ya inchi
  ya tishu ya umio.
 340. Hicho sio kitu unaweza kudanganya.
 341. Kisha hutelezesha
  kupita mfupa wa kifua,
 342. kupita kilinda umio,
  chini ndani ya tumbo,
 343. zuia vitendohiari ndani ya tumbo
  njia yote hadi kwenye mbuti.
 344. Rahisi sana.
 345. (Kicheko)
 346. Kama ningetakiwa kwenda zaidi ya hapo,
 347. hadi kufikia mirija yangu ya mayai.
  mirija ya mayai! (Kidachi)
 348. Wanaume, mnaweza kuwauliza wake zenu
  kuhusu hiyo baadaye ...
 349. Watu huniuliza, wanasema,
 350. "lazima kuchukua ujasiri mwingi
  ili kuhatarisha maisha yako,
 351. kusogeza moyo wako,
  na kumeza panga ... "
 352. Hapana. Kinachofanya ujasiri halisi
 353. ni kwa yule kijana mwoga, mwenye aibu,
  mwembamba
 354. kwa kuhatarisha kushindwa na kukataliwa,
 355. kufungua moyo wake,
 356. na kumeza kiburi chake
 357. na kusimama hapa mbele
  ya kundi la watu asiowafahamu kabisa
 358. na kukuambia hadithi yake
  kuhusu hofu na ndoto zake,
 359. kwa hatarisha kumwaga habari zake,
  vyote kihalisia na kitamathali.
 360. Unaona - asante.
 361. (Makofi)
 362. Unaona, jambo la kustaajabisha sana ni
 363. Nimetaka kufanya mambo
  ya kusifika maishani mwangu
 364. na sasa nimesifika.
 365. Lakini jambo la kusifika haswa
  sio kwamba ninaweza kumeza
 366. panga 21 kwa mara moja,
 367. au futi 20 chini ya maji kwenye tanki
  la papa 88 na taa
 368. kwa kitabu cha Amini au Usiamini,
 369. au kuchowa hadi kuwa mwekundu nyuzi 1500
  kwa Watu jasiri wa Stan Lee
 370. kama "Mtu wa Chuma"
 371. na yule jamaa alikuwa moto!
 372. Au kuvuta gari kwa upanga kwa Ripley,
 373. au Guinness,
 374. au kufikia fainali za
  shindano la vipaji Marekani,
 375. au kushinda 2007
  tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu.
 376. La, hilo sio
  jambo la kusifika sana.
 377. Hivyo ndio watu wanafikiria.
  La, la, la. Sio hivyo.
 378. Jambo la kusifika sana
 379. ni Mungu angemchukua kijana,
  mwoga, mwenye aibu mwembamba
 380. aliyehofia vimo virefu,
 381. aliyehofia ya maji na papa,
 382. na madaktari na manesi
  na sindano na vyenye ncha kali
 383. na kuzungumza na watu
 384. na sasa ananifanya
  nipae duniani kote
 385. katika kina cha futi 30,000
 386. kumeza vitu vya ncha
  chini ya maji ya tanki ya papa,
 387. na kuzungumza na madaktari na wauguzi
  na hadhira kama ninyi duniani
 388. Hilo ni jambo la kustaajabu sana kwangu.
 389. Nimetaka kufanya mambo yasiyowezekana -
 390. Asante.
 391. (Makofi)
 392. Asante.
 393. (Makofi)
 394. Sikuzote nilitaka kufanya yasiyowezekana,
  na sasa nimeweza.
 395. Nilitaka kufanya kitu cha kusifika
  maishani na kubadilisha ulimwengu,
 396. na sasa nimeweza.
 397. Siku zote nilitaka kupaa duniani kote
  kufanya vitendo vigumu
 398. na kuokoa maisha, sasa nimeweza.
 399. Na unajua nini?
 400. Bado kuna sehemu ndogo
  ya ndoto kubwa ya yule mtoto mdogo
 401. ndani kabisa.
 402. (Kicheko) (Makofi)
 403. Na unajua, sikuzote nilitaka kupata
  kusudi langu na wito wangu,
 404. na sasa nimepata.
 405. Lakini nadhani nini?
 406. Si kwa panga,
  sio unavyofikiria, si kwa nguvu zangu.
 407. Ni kwa udhaifu wangu, maneno yangu.
 408. Kusudi langu na wito
  ni kubadili ulimwengu
 409. kwa kukata kupitia hofu,
 410. upanga mmoja kwa wakati, neno moja
  kwa wakati,
 411. kisu moja kwa wakati, maisha kwa wakati,
 412. kuhamasisha watu kuwa mashujaa
 413. na kufanya yasiyowezekana maishani mwao.
 414. Kusudi langu ni kusaidia wengine
  kupata yao.
 415. La kwako ni lipi?
 416. Nini kusudi lako?
 417. Uliwekwa kufanya nini hapa?
 418. Naamini sisi wote
  tumeitwa kuwa mashujaa.
 419. Nguvu yako kubwa ni nini?
 420. Kati ya idadi ya watu duniani
  ya watu zaidi ya bilioni 7,
 421. kuna wameza upanga
  wachache sana
 422. waliobakia duniani kote leo,
 423. lakini kuna wewe mmoja.
 424. Wewe ni wa pekee.
 425. Hadithi yako ni nini?
 426. Nini kinakufanya uwe tofauti?
 427. Simulia hadithi yako,
 428. hata kama sauti yako ni nyembamba
  na inatetemeka.
 429. Je, thromu zako ni nini?
 430. kama ungefanya chochote,
  kuwa yeyote, kwenda popote -
 431. Ungefanya nini?
  Ungekwenda wapi?
 432. Ungefanya nini?
 433. Unataka kufanya nini na maisha yako?
 434. Nini ndoto zako kubwa?
 435. Nini ndoto zako kubwa ulipokuwa mdogo?
  Fikiria tena
 436. Nina uhakika hii haikuwa hivyo, si ndiyo?
 437. Nini zilikuwa ndoto zako
  kuu
 438. ulizofikiri zilikuwa ajabu sana
  na zisizoeleweka?
 439. Hakika hii inafanya ndoto zako zisionekane
  za ajabu tena, sivyo?
 440. Upanga wako ni nini?
 441. Kila mmoja wenu ana upanga,
 442. upanga wa pande mbili wa hofu na ndoto.
 443. Meza upanga wako, chochote utachokuwa.
 444. Fuata ndoto zako, mabibi na mabwana,
 445. Hujachelewa sana kuwa
  chochote unataka kuwa.
 446. Kwa wale waonevu na mipira ya kukwepa,
  wale watoto waliodhani
 447. kuwa sitaweza kufanya yasiyowezekana,
 448. Nina kitu kimoja tu cha kuwaambia:
 449. Asanteni.
 450. Kwa sababu kama si kwa wahalifu,
  tusingekuwa kuwa na mashujaa.
 451. Nipo hapa kuthibitisha
  yasiyowezekana si hayawezekani.
 452. Hii ni hatari sana,
  Inaweza kuniua.
 453. Natumaini mtafurahia.
 454. (Kicheko)
 455. Nitahitaji msaada wenu kwenye hili.
 456. Hadhira:Mbili, tatu.
 457. Dan Meyer:La, la, la. Nahitaji msaada wenu
  kwenye kuhesabu, nyote, sawa?
 458. (Vicheko)
 459. Kama unajua maneno? Sawa?
  Hesabu na mimi. Tayari?
 460. Moja.
 461. Mbili.
 462. Tatu.
 463. La, hiyo ni 2, lakini mmeelewa
 464. Hadhira: Moja.
 465. Mbili.
 466. Tatu.
 467. (Vuta pumzi)
 468. (Makofi)
 469. DM: Ndiyo!
 470. (Makofi) (Kushangilia)
 471. Asanteni sana.
 472. Asante, asante, asante.
  Asante kutoka kina cha moyo wangu
 473. Kweli, asante
  kutoka chini ya tumbo langu.
 474. Niliwaambia nimekuja hapa kufanya
  yasiyowezekana, na sasa nimeweza.
 475. Ila hii haikuwa isiyowezekana.
  Ninafanya hivi kila siku.
 476. Kitu kisichowezekana ilikuwa yule mwoga,
  mwenye aibu mwembamba kukabili hofu zake
 477. kusimama hapa kwenye jukwaa la [TEDx],
 478. na kubadilisha dunia,
  neno moja kwa wakati,
 479. upanga kwa wakati, maisha kwa wakati.
 480. kama nimekufanya ufikiri kwa njia mpya,
  kama nimekufanya uamini
 481. yasiyowekana si hayawezekani,
 482. ikiwa nimekufanya uelewe kuwa waweza
  fanya yasiyowezekana maishani mwako,
 483. basi kazi yangu imekwisha,
  na yako ndiyo kwanza imeanza.
 484. Usiache kuwa na ndoto. Usiache kuamini.
 485. Asanteni kwa kuniamini
 486. na asanteni kuwa sehemu
  ya ndoto yangu.
 487. Hii ni zawadi kwenu:
 488. Yasiyowezekana si ...
 489. Hadhira: Hayawezekani.
 490. Mwendo mrefu ni sehemu ya zawadi.
 491. (Makofi)
 492. Asanteni.
 493. (Makofi)
 494. (Kushangilia)
 495. Mwenyeji: Asante, Dan Meyer, wow!