Swahili subtitles

← Nguvu inayoponya katika kusoma

Get Embed Code
35 Languages

Showing Revision 15 created 07/22/2019 by Nelson Simfukwe.

 1. Ninataka kuzungumza namna kusoma
  kunavyoweza kubadilisha maisha yetu
 2. na kuhusu mipaka ya mabadiliko hayo
 3. Ninataka kuzungumza na wewe namna kusoma
  kunavyoweza kutupa ulimwengu wa ushirika
 4. wa muunganiko wenye nguvu wa kibinadamu
 5. pia namna ambavyo muunganiko huo
  ni sehemu tu mara zote
 6. Kusoma mwisho wa siku ni kitendo cha
  upweke na kisicho cha kawaida.
 7. Muandishi aliyebadilisha maisha yangu

 8. Ni mmarekani mweusi na mwandishi
  wa riwaya James Baldwin
 9. Wakati ninakuwa katika eneo la
  Magharibi mwa Michigan miaka ya 1980,
 10. hakukuwa na wamarekani wenye asili ya asia
  wengi wanaoandika kuhusu mabadiliko ya kijamii
 11. Na ndio maana nilimgeukia James Baldwin
 12. kama namna ya kuliziba hili ombwe,
  kama namna ya kuwamakini na rangi
 13. lakini haswa kwa sababu nilifahamu
  mimi sikuwa mmarekani mweusi,
 14. Pia nilisikia kupata changamoto na
  kuthibitishwa na maneno yake.
 15. Hasusani maneno haya:
 16. "Ni watu huria walio na mitazamo sahihi,
 17. lakini hawana misimamo halisi.
 18. pale ambapo vipande vipo chini
  na unawategemea kuleta matokeo,
 19. na huenda hawako hapo kwa namna fulani".
 20. Hawako hapo kwa namna fulani.
 21. Nikayachukua hayo maneno nikitafakari.
 22. Nijiweke wapi?
 23. Nilikwenda kwenye delta ya Mississippi,

 24. mojawapo ya maeneo masikini sana ya
  Marekani.
 25. Hii ni sehemu ambayo imejengwa
  na historia yenye nguvu.
 26. Katika mwaka wa 1960, Wamarekani weusi
  walijitoa maisha yao kupigania Elimu,
 27. kupigania haki ya kupiga kura.
 28. Nilitaka kuwa sehemu ya badiliko hilo,
 29. kuwasaidia vijana wadogo wamalize shule
  na kujiunga na vyuo.
 30. Nilipoenda kwenye Delta ya Mississipi,
 31. Palikuwa ni mahali duni bado,
 32. bado pametengwa,
 33. Bado panahitaji mabadiliko ya kasi.
 34. Shule yangu, pale nilipokuwa nasoma,

 35. haikuwa na maktaba, hakuna mshauri,
 36. lakini ilikuwa na afisa wa polisi.
 37. Nusu ya walimu walikuwa ni mbadala
 38. na wanafunzi walipoingia kwenye ugomvi,
 39. Shule iliwapeleka kwenye jela ya
  mahali hapo.
 40. Hii ndiyo shule nilipokutana na Patrick.

 41. Alikuwa na miaka 15 na alikamatwa mara
  mbili, alikuwa darasa la nane.
 42. Alikuwa ni mkimya na mndani,
 43. ni kama kila wakati alikuwa mwenye mawazo.
 44. Na alichukia kuona wengine wakipigana.
 45. Nilimuona mara moja akiruka kati ya
  mabinti wawili walipokuwa wakipigana
 46. Na akajikuta akidondoka na kuanguka chini.
 47. Patrick alikuwa na tatizo moja.
 48. Hakuwa akifika shuleni.
 49. Alisema kuwa shule wakati mwingine humfanya kuwa na msongo
 50. Sababu wanafunzi hupigana mara zote na
  walimu wanaondoka.
 51. Lakini pia, mama yake anafanya kazi mbili
  na huwa anachoka kuweza kumfanya aje shule.
 52. Hivyo nikafanya iwe kazi yangu
  kumfanya awe anakuja shule.
 53. Na sababu nilikuwa na wazimu na miaka 22
  na mwenye bidii ya matumaini
 54. Njia yangu ilikuwa ni
  kwenda nyumbani kwao
 55. na kusema "Eti, kwanini hauji
  shuleni?"
 56. Na njia hii ilifanya kazi,
 57. akaanza kuja shuleni kila siku.
 58. Na akaanza kufanikiwa katika darasa langu.
 59. Aliandika mashairi,
  alisoma vitabu.
 60. Alikuja shuleni kila siku.
 61. takriban muda ule ule

 62. Nilipogundua namna ya kushirikiana
  na Patrick,
 63. Nilikwenda shule ya sheria Harvard.
 64. Nilikutana tena na swali hili,
  nijiweke wapi,
 65. niuweke wapi mwili wangu?
 66. Na nikawaza mwenyewe
 67. Kuwa Mississipi Delta
  ni mahali ambapo watu wenye fedha,
 68. watu wenye fursa,
 69. watu hao huondoka.
 70. Na watu wanaobakia
 71. ni watu ambao hawana fursa ya kuondoka.
 72. Sikutaka kuwa mtu anayeondoka.
 73. Nilitaka kuwa mtu anayebakia.
 74. Kwa upande mwingine, nilikuwa mpweke
  na mchovu.
 75. Na hivyo nilijishawishi mwenyewe
  kuwa ninaweza kufanya mabadiliko
 76. Kwa kiasi kikubwa kama ningekuwa
  na shahada yenye heshima ya sheria.
 77. Hivyo nikaondoka.
 78. Miaka mitatu baadaye,

 79. Nilipokaribia kuhitimu
  shule ya sheria,
 80. rafiki yangu alinipigia simu
 81. na kuniambia kuwa Patrick
  amepigana na kuua mtu.
 82. Nilitaharuki.
 83. Sehemu ya mimi haikuamini,
 84. na sehemu ya mimi pia iliamini kuwa
  ni kweli.
 85. Nilisafiri kwenda kumuona Patrick.
 86. Nilimtembelea gerezani.
 87. Na aliniambia kuwa ilikuwa kweli.
 88. Ya kwamba ameua mtu.
 89. Na asingependa kuzungumzia suala hilo.
 90. Nilimuuliza nini kiliendelea kuhusu shule
 91. na akasema aliacha shule mwaka mooja
  baada ya mimi kuondoka.
 92. Na alitaka kuniambia kuhusu kitu kingine
 93. Alitazama chini akasema
  ya kwamba amepata mtoto wa kike
 94. ambaye ndiye kwanza amezaliwa.
 95. Na anahisi kuwa amemuangusha binti yake.
 96. Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mazungumzo yetu
  yalikuwa ya haraka na mabaya.
 97. Nilipotoka nje ya gereza,
  sauti ndani yangu iliniambia,

 98. "Rudi.
 99. Usiporudi sasa, hutarudi kamwe".
 100. Hivyo nikahitimu shule ya sheria na
  nikarudi.
 101. Nikarudi kumuona Patrick,
 102. Nikarudi kuona kama ninaweza kumsaidia
  na kesi yake ya sheria.
 103. Muda huu,
  nilipomuona kwa mara ya pili,
 104. Nilidhani nina hili wazo zuri,
  nikamwambia,
 105. "Hey, Patrick, kwanini usiandike barua
  kwa binti yako,
 106. ili uweze kumuweka katika
  fikra zako?"
 107. Nikampatia kalamu na
  kipande cha karatasi,
 108. na akaanza kuandika.
 109. Lakini nilipoiona karatasi aliyonipatia,

 110. Nilipigwa na butwaa.
 111. Sikuutambua mwandiko wake,
 112. alikuwa amefanya makosa
  machache ya matamshi.
 113. na nikawaza mwenyewe kama mwalimu,
 114. Ninafahamu ya kuwa mwanafunzi
  anaweza kufanya vizuri kwa kasi
 115. Kwa muda mfupi sana,
 116. lakini sikuwahi kuwaza kuwa mwanafunzi
  anaweza kurudi nyuma kwa kasi.
 117. kilichoniumiza zaidi,
 118. ni kuona kile alichokiandika
  kwa binti yake.
 119. aliandika,
 120. "Ninasikitika kwa makosa yangu,
  ninasikitika kutokuwa pamoja nawe."
 121. Na hiki ndicho alichojisikia
  anataka kusema naye.
 122. Nikajiuliza ni namna gani ninaweza
  kumshawishi kuwa anaweza kumwambia zaidi,
 123. ile sehemu yake ambayo
  hahitaji kuomba radhi kwayo.
 124. Nilitaka yeye ajisikie
 125. kuwa anakitu cha thamani
  kumshirikisha binti yake.
 126. Kwa kila siku kwa miezi saba iliyofuatia,

 127. Nilimtembelea na kumpelekea vitabu.
 128. Mkoba wangu uligeuka kuwa maktaba ndogo.
 129. Nilimpelekea James Baldwin,
 130. Nilipeleka Walt Whitman, C.S.Lewis.
 131. Nilileta vitabu vya mwongozo wa miti,
  wa ndege,
 132. na kitabu alichotokea kukipenda zaidi,
  kamusi.
 133. Kwa baadhi ya siku,
 134. tulikaa kimya kwa masaa,
  wote wawili tukisoma.
 135. Na siku nyingine,
 136. tulisoma pamoja,
  tulisoma mashairi.
 137. tulianza kwa kusoma haikus,
  mamia ya haikus,

 138. ni kito rahisi na danganyifu.
 139. Na ningemuuliza,
  "Nishirikishe haiku zako unazozipenda".
 140. Na baadhi yake ni za kufurahisha sana.
 141. Kuna hii ya Issa:
 142. "Usijali, buibui,
  ninaweka nyumba kikawaida."
 143. Na hii: "Nimelala nusu ya siku,
  na hakuna aliyeniadhibu!"
 144. Na hii nyingine ya kuvutia, inayohusu
  siku ya kwanza barafu ilipodondoka,
 145. "Kulungu wakilamba baridi ya kwanza
  kutoka kwenye koti la kila mmoja wao."
 146. Kuna kitu cha ajabu na cha kuvutia
 147. kuhusu namna shairi linavyoonekana.
 148. Nafasi ya shairi ni muhimu
  kama maneno yenyewe.
 149. Tunasoma shairi hili lililoandikwa na
  W.S.Merwin,

 150. ambalo aliliandika baada ya kumuona
  mkewe akifanya kazi kwenye bustani
 151. na akakumbuka kuwa wataishi maisha
  yao yote yaliyobaki wakiwa pamoja.
 152. "Wacha nifikiri kuwa tutakuja tena
 153. tutakapotaka na itakuwa wakati wa masika
 154. hatutakuwa na umri mkubwa
  kuliko tulivyowahi kuwa
 155. na majonzi yatakuwa mepesi kama
  mawingu ya mapema
 156. ambayo kwayo asubuhi
  huja yenyewe taratibu"
 157. Nikamuuliza Patrick mstari alioupenda
  zaidi ni upi, na akasema
 158. "Hatutakuwa na umri mkubwa
  kuliko tulivyokuwa."
 159. Alisema inamkumbusha
  mahali ambapo muda husimama,
 160. pale ambapo muda haumaanishi
  kitu chochote.
 161. Na nikamuuliza kama amewahi kuwa
  na mahali pa jinsi hiyo.
 162. pale ambapo muda hudumu milele.
 163. Na akasema, "Mama yangu".
 164. Na pale unaposoma shairi
  pamoja na mtu mwingine,
 165. shairi hubadilika katika maana.
 166. Kwa sababu huwa la kibinafsi kwa mtu huyo,
  huwa la kibinafsi kwako.
 167. Halafu tulisoma vitabu,
  tulisoma vitabu vingi sana,

 168. tulisoma kumbukumbu za Frederick Douglass,
 169. Mtumwa wa Marekani aliyejifunza mwenyewe
  kusoma na kuandika
 170. na aliyetoroka na kuwa huru
  sababu ya kuelimika kwake.
 171. Nimekua nikimfikiria Frederick Douglass
  kama shujaa
 172. na niliiona hii simulizi kama
  iliyojaa matumaini na yenye kuinua
 173. Lakini kitabu hiki kilimuweka Patrick
  katika hofu.
 174. Alibakia katika simulizi aliyoielezea
  Douglass jinsi ambavyo, katika Christmas,
 175. Mabwana waliwapa watumwa jini(pombe kali)
 176. kama namna ya kuwaaminisha kuwa
  hawawezi kuumudu uhuru.
 177. Kwa sababu watumwa waliweweseka
  katika mashamba.
 178. Patrick alisema anajifananisha na hili.
 179. Alisema kuwa kuna watu gerezani ambao,
  kama watumwa,
 180. hawataki kuwaza juu ya hali zao,
 181. kwa sababu inawaumiza sana.
 182. Inaumiza sana kuwaza mambo ya nyuma,
 183. inaumiza sana kuwaza
  kuhusu umbali gani tunapaswa kwenda.
 184. Mstari alioupenda sana ulikuwa huu:

 185. "Chochote kile, bila kujali chochote,
  kujiondoa katika kuwaza!
 186. Ilikuwa ni huku kuwaza kusiko koma kuhusu
  hali yangu ndiko kunako kipa mateso."
 187. Patrick alisema Douglass alikuwa jasiri
  kuandika, ili aendelee kuwaza.
 188. Lakini Patrick hakufahamu kuwa alionekana
  kufanana sana na Douglass kwangu.
 189. Namna alivyoendelea kusoma,
  ijapokuwa ilimuweka katika hofu.
 190. Alimaliza kitabu kabla yangu,
 191. akisoma katika ngazi za
  zege zisizo na taa.
 192. Halafu tukaendelea kusoma mojawapo
  ya vitabu ninavyovipenda,

 193. Cha Marilynne Robinson's "Gilead,"
 194. ambayo ni barua endelevu kutoka
  kwa baba kwenda kwa mwanae.
 195. Alipenda mstari huu:
 196. "Ninaandika hii kwa sehemu kukuambia
 197. ya kwamba kama umewahi kujiuliza
  kile umekifanya katika maisha yako...
 198. umekuwa neema ya Mungu kwangu,
 199. muujiza, kitu ambacho ni zaidi
  ya muujiza."
 200. Kitu kimoja kuhusu hii lugha,
  upendo wake, subira yake, sauti yake,

 201. iliamsha shauku ya Patrick katika kuandika.
 202. Na alijaza daftari kwa daftari
 203. na barua kwenda kwa binti yake.
 204. katika barua hizi nzuri na imara,
 205. alijiwazia yeye na binti yake
  wakipanda mtumbwi katika mto Mississipi
 206. Alijiwazia yeye na binti yake
  wakipata vijito vya milimani
 207. vikiwa na maji masafi bila kasoro.
 208. Nilipomtazama Patrick akiandika,
 209. Nilijiwazia mwenyewe,
 210. na sasa ninawaulizeni nyote,
 211. ni wangapi wenu mmewahi kuandika barua
  kwa mtu unayehisi umemwangusha?
 212. Ni rahisi sana
  kuwaweka hao watu nje ya fikra zako.
 213. Lakini Patrick alijitokeza kila siku,
  akimkabili binti yake,
 214. akijiwajibisha kwake,
 215. neno kwa neno kwa umakini wa hali ya juu.
 216. Ningependa katika maisha yangu binafsi

 217. kujiweka katika hatari kwa namna hiyo.
 218. Kwa sababu hatari hiyo inadhihirisha
  nguvu za moyo wa mtu.
 219. Ngoja nirudi hatua moja nyuma na niulize
  swali ambalo linaleta wasiwasi.
 220. Mimi ni nani kusimulia simulizi hii,
  hii simulizi ya Patrick?
 221. Patrick ndiye aliyeishi kwenye
  maumivu haya
 222. na mimi sijawahi kukaa na njaa hata
  kwa siku moja kwenye maisha yangu
 223. Ninawaza sana kuhusu swali hili,
 224. lakini ninachotaka kusema ni kuwa hii
  simulizi sio tu kuhusu Patrick.
 225. Inatuhusu sisi,
 226. ni kuhusu tofauti kati yetu.
 227. Ulimwengu wa vingi
 228. ambao Patrick na wazazi wake
  na mababu zake
 229. hawajawahi kuuona.
 230. Katika simulizi hii, mimi ninawakilisha
  huo ulimwengu wa vingi.
 231. Na katika kueleza simulizi hii
  sikutaka kujificha mwenyewe.
 232. Kuficha nguvu ambazo ninazo.
 233. Katika kueleza simulizi hii,
  ninataka kuifichua nguvu hiyo

 234. halafu kuuliza,
 235. tunawezaje kuipunguza
  umbali kati yetu?
 236. Kusoma ni njia mojawapo ya kuipunguza
  hiyo nafasi.
 237. Kunatuma ulimwengu wa ukimya
  ambao tunaweza kuushiriki pamoja,
 238. ambao tunaweza kuushiriki kwa usawa.
 239. Inawezekana unajiuliza sasa kuwa
  ni nini kilitokea kwa Patrick.

 240. Je kusoma kuliokoa maisha yake?
 241. Kuliyaokoa na hakukuyaokoa.
 242. Patrick alipotoka gerezani,
 243. safari yake ilikuwa ya maumivu.
 244. Waajiri hawakumkubali kwa sababu
  ya historia yake,
 245. rafiki yake mpenzi, mama yake,
  alifariki katika umri wa miaka 43
 246. kwa ugonjwa wa moyo na kisukari.
 247. Alikuwa hana pa kuishi,
  amekuwa hana chakula.
 248. Kwa hiyo watu wanasema mengi kuhusu kusoma
  ambayo kwangu ninahisi wanazidisha chumvi.

 249. Uwezo wa kusoma haukumzuia yeye
  asitengwe na jamii.
 250. Hakukumzuia mama yake asifariki.
 251. Kwa hiyo kusoma kunaweza kufanya nini?
 252. Nina majibu machache ninapomalizia leo.
 253. Kusoma kulibadili utu wake wa ndani

 254. kwa mambo yaliyofichika na uwezo wa
  kuwaza kwa picha.
 255. kwa uzuri.
 256. Kusoma kulimpa taswira zilizompa furaha:
 257. milima, bahari, kulungu, theluji.
 258. Maneno yenye ladha ya ulimwengu huru
  na halisi.
 259. Kusoma kulimpa lugha kwa yale aliyopoteza.
 260. Ni jinsi gani yalivyo mazuri haya maneno
  kutoka kwa mshairi Derek Walcott?
 261. Patrick alilikariri hili shairi.
 262. "Siku ambazo nilizishikilia,
 263. siku ambazo nilizipoteza,
 264. siku ambazo zinakuwa kupitiliza,
  kama mabinti,
 265. mikono yangu inayoshikilia."
 266. Kusoma kulimfundisha ujasiri wake
  mwenyewe.

 267. Kumbuka kwamba aliendelea kusoma
  Frederick Douglass,
 268. ijapokuwa ilikuwa ya kuumiza.
 269. Aliendelea kuwa makini,
  ijapokuwa kuwa makini kunauma.
 270. Kusoma ni aina ya kutafakari,
 271. ndio maana ni vigumu sana kusoma
  kwa sababu tunataka kutafakari.
 272. Na Patrick alichagua kutafakari,
  badala ya kutokutafakari.
 273. Na mwishoni, kusoma kulimpa lugha
  ya kuongea na binti yake.
 274. Kusoma kulimpa shauku ya kutaka kuandika.
 275. Muunganiko kati ya kusoma na
  kuandika ni wenye nguvu sana.
 276. Tunapoanza kusoma,
 277. tunaanza kupata maneno.
 278. Na alipata maneno ya kutafakari
  wao wawili wakiwa pamoja.
 279. Alipata maneno
 280. ya kumwelezea ni namna gani anampenda.
 281. Kusoma pia kulibadilisha
  mahusiano baina yetu.

 282. Kunatupa nyakati za kuwa karibu,
 283. kuweza kuona zaidi ya mitazamo yetu.
 284. Na kusoma kulichukua mahusiano ya
  kutokuwa sawa
 285. na kulitupa usawa wa muda mfupi.
 286. Ukikutana na mtu kama msomaji,
 287. unakutana naye kwa mara ya kwanza,
 288. kwa upya kabisa.
 289. Hakuna namna unaweza kufahamu mstari
  anaoupenda sana ni upi.
 290. Ni kumbukumbu zipi na huzuni zipi za
  siri alizonazo.
 291. Na unakutana na sitara ya hali ya juu
  ya utu wake wa ndani.
 292. Na halafu unaanza kushangaa,
  "Eti,utu wangu wa ndani umejengwa na nini?
 293. Ni kitu gani nilichonacho cha thamani
  cha kumshirikisha mwingine?"
 294. Ninataka kufunga

 295. kwa mistari yangu ninayoipenda
  kutoka kwa barua za Patrick kwa bintiye.
 296. "Mto una kivuli kwenye baadhi ya maeneo
 297. lakini mwanga unaangaza
  kupitia mianya ya miti...
 298. Kwenye baadhi ya matawi
  muliberi nyingi zimening'inia.
 299. Unanyoosha mkono wako
  ili uweze kuyachukua baadhi".
 300. Na barua hii ya upendo, anapoandika,
 301. "Fumba macho yako na usikilize
  sauti ya maneno.
 302. Ninafahamu shairi hili kwa moyo
 303. na ningependa pia wewe ulifahamu."
 304. Ninawashukuruni nyote.

 305. (Makofi)