Namna ipi ya kuhamasisha watu kutenda mema kwa wengine
-
0:01 - 0:04Namna gani tunaweza wafanya watu kutenda
mema zaidi, -
0:05 - 0:09kwenda katika uchaguzi, kujitolea msaada,
kutunza rasilimali, -
0:09 - 0:12au hata kufanya kitu rahisi kama kuosha
vikombe vyao wakiwa kazini -
0:12 - 0:15ili sinki lisiwe muda wote limejaa
vyombo vichafu? -
0:15 - 0:17(Kicheko)
-
0:17 - 0:21(Makofi)
-
0:21 - 0:23Nilipoanza kushughulikia hili tatizo,
-
0:23 - 0:25Nilishirikiana na kampuni ya nishati
-
0:25 - 0:29kuwapa mafunzo wateja kuhusu programu
inayozuia kukatika kwa umeme -
0:29 - 0:31kwa kupunguza mahitaji ya nishati
kipindi cha juu. -
0:32 - 0:35Programu imetengenezwa na teknolojia
iliyojaribiwa na ya ukweli. -
0:35 - 0:37Ni ambayo hata utawala wa Obama uliita
-
0:37 - 0:40"jiwe la msingi la kuleta ukisasa katika
mfumo wa umeme Amerika." -
0:41 - 0:44Lakini, kama ilivyo mifumo mingi
mikubwa ya teknlolojia, -
0:44 - 0:46huwa na udhaifu:
-
0:48 - 0:49watu.
-
0:50 - 0:51Watu wanahitaji kujisajili.
-
0:52 - 0:56Ili kufanya watu wajisajili,
kampuni iliwatumia wateja barua nzuri, -
0:56 - 0:58kuwaambia kuhusu faida
zote za programu, -
0:58 - 1:01na kuwaambia wapige huduma kwa wateja
kama wangependa. -
1:01 - 1:02Barua zilitumwa,
-
1:02 - 1:05lakini simu, zilikuwa kimya.
-
1:06 - 1:09Hivyo tulivyohusishwa, tulipendekeza
badiliko moja dogo. -
1:09 - 1:11Badala ya simu ya huduma kwa wateja,
-
1:11 - 1:16tulipendekeza watumie karatasi za kujisajili zitakazotumwa
kwenye sanduku za barua zilizokaribu -
1:16 - 1:17katika majengo ya watu.
-
1:18 - 1:21Hii iliongeza walioshiriki kwa mara tatu.
-
1:23 - 1:24Kwanini?
-
1:26 - 1:30Sasa, wote tunajua watu wanajali sana
kuhusu kile wengine wanachofikiri juu yao, -
1:30 - 1:33kua tunajaribu kuonekana kama
tuna heshima na tunaojali, -
1:33 - 1:36na tunajaribu kuepuka kuonekana kama
wabinafsi au mabaradhuli. -
1:36 - 1:41Iwe tunatambua au la, hii ni nafasi kubwa
ya kwanini watu wanatenda mema, -
1:41 - 1:46hivyo mabadiliko madogo ambayo huwapa
watu sifa kwa kutenda mema, -
1:46 - 1:48hayo mabadiliko yanaweza
leta utofauti mkubwa. -
1:48 - 1:51Mabadiliko madogo kama kubadili kutoka
simu ya huduma kwa wateja, -
1:51 - 1:54ambapo hamna mtu atayeweza tambua
kuhusu mwenendo wako mwema, -
1:54 - 1:56hadi kwenye karatasi ya kujisajili
-
1:56 - 1:59ambapo kila mtu anayepita
anaweza kuona jina lako. -
2:01 - 2:04Katika ushirikiano na serikali, mashirika
ya kujitolea, makampuni, -
2:04 - 2:07tunajaribu kuwafanya watu
kufanya mema zaidi, -
2:07 - 2:09tunavuna nguvu ya sifa.
-
2:10 - 2:12Na tuna karatasi rahisi ya
kuangalia hili. -
2:12 - 2:16Kwa uwazi, tayari unatambua kitu
cha kwanza katika listi hiyo. -
2:17 - 2:19Ni katika kuongeza uangalizi,
-
2:19 - 2:22kuhakikisha watu wanatambua
kuhusu matendo mema. -
2:23 - 2:26Sasa, subiri kidogo, najua baadhi
yenu pengine mnawaza, -
2:26 - 2:28hakuna namna watu hapa wangefikiri,
-
2:28 - 2:31"Oh, kwa vile sasa ninapata sifa kwa matendo mema,
-
2:31 - 2:32matendo yangu yana thamani."
-
2:32 - 2:34Upo sahihi.
-
2:34 - 2:35Kawaida, watu hawadhani hivyo.
-
2:36 - 2:39Bali, pale wanapofanya
maamuzi wakiwa peke yao, -
2:39 - 2:41huwa na hofu kuhusu matatizo yao,
-
2:41 - 2:45kuhusu nini cha kuweka mezani mda wa kula
au jinsi ya kulipa ankara zao kwa wakati. -
2:45 - 2:48Lakini, pale tunapofanya maamuzi
yao kuwa wazi zaidi, -
2:48 - 2:51wanaanza kutumia nafasi ya
kufanya mema zaidi. -
2:52 - 2:55Kwa maneno mengine, kilicho na nguvu
sana kuhusu njia yetu -
2:55 - 2:59ni kwamba inaweza ongeza mshawasha
wa kutenda mema, -
2:59 - 3:02kwa suala hili, kuzuia kukatika
kwa umeme. -
3:03 - 3:05Turudi katika uangalizi.
-
3:05 - 3:07Nataka niwape mfano mwingine.
-
3:07 - 3:08Huu unatoka katika ushirikiano
-
3:08 - 3:11na taasisi isiyo ya kibiashara
inayohamasisha upigaji kura, -
3:11 - 3:14na inafanya hivi kwa kutuma mamia ya
maelfu ya barua kila uchaguzi -
3:14 - 3:18ili kuwakumbusha watu na kujaribu
kuwashawishi kwenda katika uchaguzi. -
3:19 - 3:21Tulishauri kuongezwa kwa hii sentensi:
-
3:22 - 3:26"Unaweza pigiwa simu na mtu na kuulizwa
ni namna gani uliuona uchaguzi." -
3:27 - 3:30Sentensi hii inafanya uangalizi
zaidi unapoenda katika uchaguzi, -
3:31 - 3:34na inaongeza matokeo ya
barua kwa asilimia 50. -
3:37 - 3:40Kufanya barua kuwa fanisi zaidi kuli-
punguza gharama za kupata kura ya nyongeza -
3:40 - 3:43kutoka dola 70 hadi takribani dola 40.
-
3:43 - 3:45Uangalizi umetumika kufanya vitu
-
3:45 - 3:48kama kufanya watu kuchangia
damu mara kwa mara -
3:48 - 3:51kwa kuorodhesha majina ya
wachangiaji katika vijarida, -
3:51 - 3:52au kulipa kodi kwa wakati
-
3:53 - 3:56kwa kuorodhesha majina ya
wakwepaji katika tovuti ya umma. -
3:56 - 3:58(Kicheko)
-
4:00 - 4:01Vipi kuhusu huu mfano?
-
4:03 - 4:07Toyota ina mamia ya maelfu ya watu wa
kununua magari yatumiayo mafuta vizuri -
4:07 - 4:10kwa kufanya gari la Prius kuwa tofauti ...
-
4:10 - 4:12(Kicheko)
-
4:13 - 4:15kua matendo yao mema yalionekana
kutokea umbali wa maili. -
4:16 - 4:19(Kicheko)
-
4:19 - 4:21Sawa, kwa hivyo uangalizi ni bora,
-
4:21 - 4:25lakini wote tunajua, wote tumejionea
-
4:25 - 4:27watu huipitiliza nafasi ya kufanya mema.
-
4:28 - 4:31Watamuona mtu akiomba hela pembeni ya njia
-
4:31 - 4:34na watatoa simu zao na kuonekana
wapo bize sana, -
4:34 - 4:38au watakwenda makumbusho na watachakacha
pembeni ya boksi la mchango. -
4:38 - 4:40Fikiria kwamba ni muda wa mapumziko
-
4:40 - 4:44na unakwenda supamaketi, na kuna mtu
anayejitolea katika jeshi la wokovu, -
4:44 - 4:45na anapiga kengele yake.
-
4:45 - 4:47Miaka kadhaa iliyopita, watafiti wa
San Diego -
4:47 - 4:51waliungana na tawi la wenyeji
kutoka jeshi la wokovu -
4:51 - 4:53kutafuta njia za kuongeza michango.
-
4:54 - 4:56Walichogundua kilikuwa kinafurahisha.
-
4:57 - 4:59Wanaojitolea waliposimama
mbele ya mlango mmoja, -
5:00 - 5:03watu walikwepa kuchangia kwa
kutokea mlango mwingine. -
5:05 - 5:06Kwanini?
-
5:07 - 5:11Kwa sababu muda wote walidai,
"Oh, sijamuona mtu wa kujitolea," -
5:11 - 5:13au, "Nilikuwa nafata kitu fulani kule,"
-
5:13 - 5:14au, "Gari langu lipo huko."
-
5:16 - 5:17Kwa maneno mengine, kuna sababu nyingi.
-
5:19 - 5:22Na hilo linatupeleka katika kitu cha
pili katika listi yetu: -
5:22 - 5:23kuondoa visingizio.
-
5:25 - 5:26Katika suala la jeshi la wokovu,
-
5:26 - 5:30kuondoa visingizio ina maana
kusimama katika milango yote, -
5:30 - 5:32na hakika, walipofanya hivi,
-
5:32 - 5:33michango iliongezeka.
-
5:35 - 5:37Lakini ndipo ambapo vitu vilianza
kuchekesha, -
5:37 - 5:39kuchekesha zaidi.
-
5:40 - 5:42Watafiti walikuwa nje katika eneo
la kuegesha magari, -
5:43 - 5:46na walikuwa wakihesabu watu walipoingia
na kutoka katika duka, -
5:46 - 5:50na waligundua kua pale wanaojitolea
waliposimama mbele ya milango yote, -
5:50 - 5:52watu waliacha kutoka nje ya duka kabisa.
-
5:52 - 5:55(Kicheko)
-
5:55 - 5:59Kihalisia, walishangazwa na hili,
hivyo waliamua kuangalia kwa undani, -
5:59 - 6:04na ndipo waligundua kwamba kulikuwa
na mlango mdogo wa wafanyakazi -
6:04 - 6:06kawaida hutoa bidhaa za kutengeneza upya --
-
6:06 - 6:08(Kicheko)
-
6:08 - 6:11na sasa watu walikuwa wanatokea mlango
huo ili kukwepa wanaojitolea. -
6:11 - 6:14(Kicheko)
-
6:14 - 6:17Hii inatufundisha somo muhimu.
-
6:18 - 6:22Pale tunapojaribu kuondoa visingizio,
tunatakiwa kuwa makini, -
6:22 - 6:24kwa sababu watu ni wabunifu kweli
kuvitengeneza. -
6:24 - 6:27(Kicheko)
-
6:30 - 6:32Sawa, nataka kuhamia katika mpangilio
-
6:32 - 6:34ambapo visingizio vinakuwa na
madhara ya mauti. -
6:36 - 6:40Inakuwaje kama ningekuambia kwamba ugonjwa
wa kuambukiza unaoua sana una tiba, -
6:41 - 6:44kiuwazi, ilikuwa na tiba moja kwa
miaka 70, -
6:44 - 6:46iliyo bora, ifanyayo kazi karibia
kila wakati? -
6:48 - 6:49Ni ajabu, lakini ni kweli.
-
6:50 - 6:52Ugonjwa huu ni kifua kikuu.
-
6:52 - 6:55Huambukiza watu milioni 10 kwa mwaka,
-
6:55 - 6:57na huua takribani watu milioni mbili yao.
-
6:58 - 7:02Kama ilivyo programu ya kuzuia kukatika
kwa umeme, tumepata suluhisho. -
7:02 - 7:03Tatizo ni watu.
-
7:04 - 7:06Watu wanatakiwa kunywa dawa
-
7:06 - 7:08ili waweze kupona,
-
7:08 - 7:10na pia wasiweze ambukiza watu wengine.
-
7:12 - 7:14Miaka michache sasa,
tumekuwa tukishirikiana -
7:14 - 7:16na taasisi mpya ya afya iitwayo Keheala
-
7:16 - 7:19kusaidia wagonjwa wa kifua kikuu
wakipata matibabu. -
7:19 - 7:22Sasa, unatakiwa kuelewa, matibabu ya
kifua kikuu, ni magumu sana. -
7:22 - 7:25Tunaongelea kuhusu kunywa dawa kali sana
-
7:25 - 7:27kila siku kwa miezi sita au zaidi.
-
7:27 - 7:30Dawa hiyo ni kali sana mpaka itakufanya
ujisikie mgonjwa. -
7:30 - 7:32Itakufanya ujisikie kichefuchefu na homa.
-
7:32 - 7:34Itafanya mkojo kuwa na rangi za ajabu.
-
7:35 - 7:38Ni tatizo pia kwa sababu unatakiwa
kurudi tena kliniki -
7:38 - 7:40karibuni kila wiki ili kupata dawa zaidi,
-
7:40 - 7:44na Afrika ya kusini mwa Sahara au sehemu
ambapo kifua kikuu ni janga, -
7:44 - 7:46sasa unaongelea kuhusu kwenda
sehemu ya mbali kweli, -
7:46 - 7:49na kupanda usafiri wa jumuiya ambao
upo taratibu, -
7:49 - 7:51pengine kliniki haina ufanisi.
-
7:51 - 7:54Sasa unaongelea kuhusu kuchukua
nusu siku kazini kila wiki -
7:54 - 7:57kwenye kazi usiyoweza kumudu kuipoteza.
-
7:58 - 8:01Ni mbaya zaidi ukizingatia ukweli kwamba
kuna unyanyapaa wa kutisha, -
8:01 - 8:05na kwa namna yoyote hutaki watu
watambue kwamba una ugonjwa. -
8:05 - 8:08Baadhi ya simulizi tunazosikia huwa
zinasimuliwa na wanawake -
8:08 - 8:11ambao, katika sehemu hizi ambapo ukatil
wa kijinsia ni suala la kawaida, -
8:11 - 8:14wanatuambia kwamba wanahitajika
kuficha kwa waume zao -
8:14 - 8:16kwamba wanakwenda kliniki.
-
8:18 - 8:21Hivyo siyo jambo la kushangaza
kua watu hawamalizi tiba. -
8:22 - 8:24Mikakati yetu inaweza kuwasaidia kweli?
-
8:24 - 8:26Tutawasaidia kweli kupona?
-
8:28 - 8:29Ndiyo.
-
8:30 - 8:34Kila siku, tunawatumia wagonjwa ujumbe
wa simu kuwakumbusha kunywa dawa, -
8:34 - 8:36lakini kama tungekwama pale,
-
8:36 - 8:38kungekuwa na visingizio vingi.
-
8:38 - 8:39"Basi, sikuona ujumbe."
-
8:39 - 8:42Au, "Unajua, niliona ujumbe,
ila nikasahau kabisa -
8:42 - 8:44niliweka simu chini na nikasahau."
-
8:44 - 8:46Au, "Nilimuazima mama yangu simu."
-
8:48 - 8:50Tunatakiwa kuondokana na hivi visingizio
-
8:50 - 8:52na tunafanya hivyo kwa kuwauliza wagonjwa
-
8:52 - 8:55kujiandikisha na kuthibitisha kwamba
wamekunywa dawa. -
8:56 - 8:58Kama wasipojisajili, tunawatumia
ujumbe tena. -
8:58 - 9:00Kama hawajisajili, tunawatumia
ujumbe tena. -
9:01 - 9:04Kama, baada ya mara tatu
bado hawajathibitisha, -
9:04 - 9:06tunawajulisha timu ya wahisani
-
9:06 - 9:08na timu hiyo itawapigia na kuwatumia
ujumbe -
9:08 - 9:10ili waweze kunywa dawa.
-
9:11 - 9:12Hamna visingizio.
-
9:14 - 9:17Mkakati wetu, ambao, kwa kukubali,
unatumia njia zote za kuelewa tabia, -
9:17 - 9:21ukijumuisha, kama ambavyo
umegundua, uangalizi, -
9:21 - 9:22ulikuwa na ufanisi sana.
-
9:23 - 9:25Wagonjwa wasiopata huduma yetu
-
9:25 - 9:28walikuwa na nafasi mara tatu
zaidi kutomaliza tiba yao. -
9:32 - 9:33Sawa,
-
9:33 - 9:34umeongeza uangalizi.
-
9:34 - 9:37umeondoa visingizio,
-
9:37 - 9:39lakini kuna jambo la tatu ambalo
unatakiwa litambua. -
9:41 - 9:44Kama umewahi fika Washington, DC
au Japan au London, -
9:44 - 9:46unajua kua waendesha treni kule
-
9:46 - 9:49huwa waangalifu kusimama kwenye
upande wa kulia wa kiinuzi -
9:49 - 9:52ili watu waweze kupita upande wa kushoto
-
9:52 - 9:55Lakini bahati mbaya,
si kote kuna huo utaratibu, -
9:55 - 9:58na kuna sehemu nyingi
ambapo unaweza kusimama pande zote -
9:58 - 9:59na kuzuia kiinuzi.
-
9:59 - 10:01Hakika, ni bora kwa wengine
-
10:01 - 10:03tunaposimama upande wa kulia
na kuwaacha wapite, -
10:03 - 10:06lakini tunategemewa kufanya
hivyo baadhi ya sehemu. -
10:07 - 10:08Hii ni suala la jumla.
-
10:08 - 10:10Wakati mwingine tunagemewa kufanya mema
-
10:10 - 10:12na wakati mwingine si hivyo,
-
10:12 - 10:15na inamaanisha kua watu wanachukulia
uzito sana suala la foleni -
10:15 - 10:18na wanategemewa kufanya mema
katika suala kama hilo, -
10:20 - 10:23ambapo inatupeleka katika jambo la tatu
na la mwisho katika listi yetu: -
10:23 - 10:25kufanya mawasiliano ya mategemeo,
-
10:25 - 10:27kuwaambia watu,
-
10:27 - 10:29"Fanya jambo jema sasa hivi."
-
10:31 - 10:33Hii ni njia rahisi ya
kuwasilisha mategemeo; -
10:33 - 10:36kwa urahisi waambie, "Jamani, kila mtu
anafanya matendo mema." -
10:36 - 10:40Kampuni ya Opower hutumia watu
katika ankara zao za umeme -
10:40 - 10:43maelezo madogo ambayo hulinganisha
matumizi yao ya nishati -
10:43 - 10:46na wale walio na nyumba ambazo
zinafanana ukubwa na wao. -
10:47 - 10:50Na pale watu wanapogundua kwamba
majirani zao wanatumia umeme kidogo, -
10:50 - 10:52wanaanza kutumia umeme kidogo pia.
-
10:52 - 10:56Mkakati huo, umetumika kuwafanya watu
kupiga kura au kutoa misaada -
10:56 - 10:58au kutumia tena mataulo katika hoteli.
-
11:00 - 11:01Vipi kuhusu hili?
-
11:02 - 11:05Hii ni namna nyingine ya
kuwasilisha mategemeo; -
11:05 - 11:09kwa urahisi fanya kwa kusema,
"Tenda yaliyo mema" kwa mda unaofaa. -
11:12 - 11:13Vipi kuhusu hii?
-
11:14 - 11:17Hii inatengeneza picha
-
11:17 - 11:20ya namna ya kidunia ya kuzima taa
-
11:20 - 11:23na kuwasha katika mchango wa kimazingira.
-
11:24 - 11:27Hitimisho ni kwamba,
njia nyingi za kufanya hili, -
11:27 - 11:29namna nyingi za kuwasilisha mategemeo.
-
11:29 - 11:31Usisahau kufanya.
-
11:31 - 11:33Hivyo tu.
-
11:33 - 11:34Hiyo ndiyo listi yetu.
-
11:36 - 11:41Wengi wenu mnashughulikia matatizo
muhimu yaliyo na madhara kwa jamii, -
11:41 - 11:44na muda mwingine mnaweza hitaji
kuwahamasisha watu kutenda mema. -
11:46 - 11:49Somo la leo linaweza kukusaidia kwa hilo.
-
11:49 - 11:52Na somo hili, haliihitaji kufanya
harambee ya kuongeza fungu -
11:52 - 11:55au kuunda teknolojia iliyo na nakshi.
-
11:55 - 11:57Inahitaji kuweza kupata sifa
-
11:57 - 12:01kwa kuongeza uangalizi, kuondoa visingizio
-
12:01 - 12:03na kuwasilisha mategemeo.
-
12:04 - 12:05Asante.
-
12:05 - 12:10(Makofi)
- Title:
- Namna ipi ya kuhamasisha watu kutenda mema kwa wengine
- Speaker:
- Erez Yoeli
- Description:
-
Namna gani tunaweza wafanya watu kutenda mema: kwenda kwenye uchaguzi, kutoa misaada, kutumia rasilimali au kwa ujumla kuwa wastaarabu kwa wengine? Mtafiti na mwanasayansi wa MIT anashirikisha listi ndogo ya mambo ya kufanya ya namna ya kupata nguvu ya sifa -- tamaa yetu kama binadamu kuonekana kama wastaarabu na wema badala ya wabinafsi -- kuhamasisha watu kufanya vitu kwa manufaa ya wengine. Jifunze zaidi kuhusu namna ambavyo mabadiliko madogo katika mikakati yako ya kuwafanya watu kufanya mema na pia kupata matokeo bora ya kushangaza.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 12:22
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for How to motivate people to do good for others | ||
Doris Mangalu accepted Swahili subtitles for How to motivate people to do good for others | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for How to motivate people to do good for others | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for How to motivate people to do good for others | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for How to motivate people to do good for others | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How to motivate people to do good for others | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How to motivate people to do good for others |