Return to Video

Njia isiyo na mwiko kuongelea kuhusu siku za hedhi

  • 0:01 - 0:02
    Siku.
  • 0:02 - 0:03
    Damu.
  • 0:04 - 0:05
    Hedhi.
  • 0:05 - 0:07
    Uchafu.
  • 0:07 - 0:09
    Siri.
  • 0:09 - 0:10
    Kuficha.
  • 0:10 - 0:12
    Kwanini?
  • 0:13 - 0:15
    Utaratibu asilia kibaolojia
  • 0:15 - 0:18
    ambao kila msichana na mwanamke
    anapitia kila mwezi
  • 0:19 - 0:21
    kwa karibia nusu ya maisha yake.
  • 0:21 - 0:23
    Jambo ambalo ni la umuhimu mkubwa sana
  • 0:23 - 0:28
    kiasi kwamba kupona na uenezwaji
    wa spishi zetu unautegemea.
  • 0:28 - 0:30
    Bado tunauchukulia kama mwiko.
  • 0:31 - 0:34
    Tunajisikia ugumu
    na fedheha kuliongelea.
  • 0:36 - 0:38
    Nilipopata siku zangu mara ya kwanza,
  • 0:38 - 0:40
    Niliambiwa nifanye iwe
    siri nisiwaambie wengine--
  • 0:41 - 0:43
    hata kwa baba yangu au kaka.
  • 0:44 - 0:46
    Baadaye wakati hili somo
    limejitokeza vitabuni mwetu,
  • 0:46 - 0:49
    mwalimu wetu wa baolojia aliiruka mada.
  • 0:49 - 0:51
    (Kicheko)
  • 0:52 - 0:54
    Nilijifunza nini kutokana na hili?
  • 0:54 - 0:58
    Nilijifunza kwamba
    ni fedheha mno kuongelea jambo hili.
  • 0:58 - 1:01
    Nilijifunza kufedheshwa na mwili wangu.
  • 1:01 - 1:04
    Nilijifunza kutokufahamu siku zangu
  • 1:04 - 1:06
    ili kuweza kubaki na heshima.
  • 1:06 - 1:08
    Utafiti katika sehemu mbalimbali India
  • 1:08 - 1:13
    waonyesha wasichana watatu kati ya kumi
    hawafahamu kuhusu hedhi
  • 1:13 - 1:15
    wakati wa siku zao za kwanza.
  • 1:15 - 1:17
    Na baadhi ya sehemu za Rajasthan
  • 1:17 - 1:22
    hii namba ni kubwa kama wasichana tisa
    kati ya kumi kutokufahamu
  • 1:23 - 1:24
    Unaweza kushangazwa kujua
  • 1:24 - 1:27
    kwamba wasichana wengi
    nilioongea nao,
  • 1:27 - 1:31
    waliokuwa hawajui kuhusu siku zao
    wakati wa hedhi zao za kwanza
  • 1:31 - 1:33
    walifikiria kuwa wana saratani ya damu
  • 1:33 - 1:35
    na watakufa muda sio mrefu.
  • 1:37 - 1:40
    Usafi wa hedhi
    ni kipengele muhimu cha hatari
  • 1:40 - 1:42
    kwa maambukizi wa mfumo wa via vya uzazi.
  • 1:43 - 1:46
    Lakini India, ni asilimia 12 tu
    ya wasichana na wanawake
  • 1:46 - 1:50
    wanaweza kupata njia za usafi
    wa kumudu siku zao.
  • 1:51 - 1:52
    Ukifanya mahesabu,
  • 1:52 - 1:57
    asilimia 88 ya wasichana na wanawake
    hutumia njia zisizo salama kwa siku zao.
  • 1:57 - 1:59
    Nilikuwa mmoja wao.
  • 2:00 - 2:03
    Nilikulia kwenye mji mdogo
    uitwao Garhwa, jimbo la Jharkhand,
  • 2:03 - 2:06
    ambako hata kununua pedi
    ilichukuliwa kama fedheha.
  • 2:07 - 2:09
    Sasa nilipoanza kupata siku zangu,
  • 2:09 - 2:11
    Nilianza kutumia matambara.
  • 2:13 - 2:15
    Baada ya kila matumizi
    niliyafua na kuyatumia tena.
  • 2:15 - 2:16
    Lakini kuyahifadhi,
  • 2:17 - 2:19
    Niliyaficha na kuyaweka
    sehemu yenye giza na unyevu
  • 2:19 - 2:22
    ilikwamba mtu asijue
    kuwa niko kwenye hedhi.
  • 2:23 - 2:25
    Kwa kuyarudia kufua
    matambara yalikuja kuwa magumu,
  • 2:25 - 2:28
    na mara nyingi nilipata upele
    na maambukizi kwa kuyatumia.
  • 2:29 - 2:33
    Niliyavaa kwa muda wa miaka mitano
    hadi nilipohama ule mji.
  • 2:36 - 2:38
    Suala lingine
    ambalo siku zilileta maishani mwangu
  • 2:38 - 2:40
    lile la kuwekewa mipaka kijamii
  • 2:40 - 2:45
    iliyowekwa kwa wasichana wetu
    na wanawake wakiwa kwenye siku zao.
  • 2:45 - 2:47
    Nafikiri wote lazma mtakuwa mnajua,
  • 2:47 - 2:50
    lakini bado nitaelezea
    kwa wale wachache wasiojua.
  • 2:51 - 2:53
    Sikuruhusiwa kula au kugusa vitu vichachu.
  • 2:54 - 2:59
    Sikuruhusiwa kukaa kwenye sofa
    au kitandani mwa ndugu wa familia.
  • 2:59 - 3:01
    Nilitakiwa kufua mashuka
    kila baada ya siku zangu,
  • 3:01 - 3:03
    hata kama hazikuchafuka kwa madoa.
  • 3:03 - 3:05
    Nilichukuliwa kama najisi
  • 3:05 - 3:10
    na kukatazwa kuabudu au kugusa
    kitu chochote chenye umuhimu kidini.
  • 3:11 - 3:13
    Ulikutana na matangazo nje ya misikiti
  • 3:13 - 3:16
    kukataza wasichana
    na wanawake walio kwenye hedhi.
  • 3:17 - 3:18
    Chakuchekesha,
  • 3:18 - 3:21
    wakati wote ni wanawake watu wazima
  • 3:21 - 3:26
    ndio walioweka vizuizi hivyo
    kwa wasichana wadogo katika familia.
  • 3:26 - 3:31
    hata hivyo, wamekua
    wakikubali vizuizi hivyo kama desturi.
  • 3:31 - 3:34
    Na katika kukosekana kwa kuingiliwa,
  • 3:34 - 3:36
    ni imani potofu na kutoeleweka
  • 3:36 - 3:38
    kunakoenezwa
    kizazi hata kizazi.
  • 3:39 - 3:41
    Kwa miaka nilyofanyia kazi
    taaluma hii,
  • 3:41 - 3:43
    Nimeshakutana na hadithi
  • 3:43 - 3:46
    ambapo wasichana walitakiwa kula
    na kuosha vyombo vyao kwa kutengwa.
  • 3:46 - 3:49
    Hawakuruhusiwa
    kuoga wakati wa siku zao,
  • 3:49 - 3:53
    na katika nyumba nyingine walitengwa
    hata na ndugu wengine wa familia.
  • 3:54 - 3:57
    Kiasi cha asilimia 85 za wasichana
    na wanawake India
  • 3:57 - 4:03
    walifuata moja au zaidi ya masharti
    ya mila kwenye siku zao kila mwezi.
  • 4:03 - 4:05
    Unafikiria hii inafanya nini
  • 4:05 - 4:08
    katika kujithamini
    na kujiamini kwa msichana mdogo?
  • 4:09 - 4:11
    Kiwewe cha kisaikolojia
    ambacho hili huumiza,
  • 4:11 - 4:14
    kuathiri haiba yake,
  • 4:14 - 4:16
    utendaji wake kimasomo
  • 4:16 - 4:20
    na kila kipengele cha ukuaji
    katika miaka ya awali ya uumbaji wake?
  • 4:22 - 4:26
    Nilifuata kwa bidii masharti haya yote
    ya kimila kwa miaka 13,
  • 4:26 - 4:29
    hadi mjadala na mshirika mwenzangu, Tuhin,
  • 4:29 - 4:31
    ulipobadilisha mtazamo wangu
    kuhusu hedhi milele.
  • 4:32 - 4:38
    Mwaka 2009, mimi na Tuhin tulikuwa
    tunasoma stashada katika ubunifu.
  • 4:38 - 4:39
    Tukapendana
  • 4:39 - 4:42
    na nilikuwa huru
    kujadiliana naye kuhusu siku zangu.
  • 4:43 - 4:45
    Tuhin alijua kidogo kuhusu siku.
  • 4:46 - 4:48
    (Kicheko)
  • 4:52 - 4:55
    Alishangazwa kujua kwamba
    wasichana hupata maumivu makali
  • 4:55 - 4:57
    na hutokwa damu kila mwezi.
  • 4:57 - 4:59
    (Kicheko)
  • 4:59 - 5:00
    Ndio.
  • 5:01 - 5:02
    Alishtushwa kabisa kujua
  • 5:02 - 5:07
    kuhusu vizuizi vinavyowekwa kwa
    wasichana na wanawake walio kwenye hedhi
  • 5:08 - 5:10
    na familia pamoja na jamii zao wenyewe.
  • 5:10 - 5:12
    Ili kuweza kunisaidia na maumivu yangu,
  • 5:12 - 5:16
    alikwenda kwenye mtandao wa intaneti
    kujifunza kuhusu hedhi.
  • 5:17 - 5:18
    Aliponielezea alichojifunza,
  • 5:18 - 5:21
    Niligundua ufahamu mdogo
    nilionao kuhusu hedhi,
  • 5:22 - 5:25
    na vitu vingi nilivyoamini
    vilikuja kuwa ni imani potofu,
  • 5:26 - 5:28
    Ndipo nilipojiuliza:
  • 5:28 - 5:30
    kama sisi, tumesoma vizuri hivi,
  • 5:30 - 5:32
    tumefundishwa vibaya kuhusu hedhi,
  • 5:32 - 5:36
    kutakuwa na mamilioni ya wasichana huko
    nje waliofundishwa vibaya, pia.
  • 5:38 - 5:39
    Kusoma--
  • 5:39 - 5:41
    kuelewa tatizo vizuri,
  • 5:41 - 5:45
    Nilifanya utafiti wa mwaka mmoja kujifunza
    ukosefu wa ufahamu kuhusu hedhi
  • 5:45 - 5:47
    na chanzo chake nyuma yake.
  • 5:48 - 5:50
    Wakati kiujumla inaaminika
  • 5:50 - 5:56
    kwamba kutokufahamu hedhi na
    kuelewa vibaya ni tatizo la vijijini,
  • 5:56 - 5:57
    katika utafiti wangu,
  • 5:57 - 6:00
    Niligundua kwamba
    ni tatizo la mijini pia.
  • 6:00 - 6:04
    Na lipo kwa daraja la walioelimika
    mijini, pia.
  • 6:05 - 6:08
    Wakati naongea na wazazi wengi
    pamoja na waalimu,
  • 6:08 - 6:13
    Niligundua kuwa wengi wao walitaka
    kuelimisha wasichana kuhusu siku zao
  • 6:13 - 6:16
    kabla hawajaanza
    kupata mzunguko wao wa hedhi.
  • 6:17 - 6:18
    Na--
  • 6:18 - 6:22
    lakini wenyewe walikosa
    njia stahiki.
  • 6:22 - 6:23
    Na kwavile ni mwiko,
  • 6:23 - 6:26
    wanajisikia kusita
    na fedheha kuongelea jambo hilo.
  • 6:27 - 6:31
    Wasichana siku hizi hupata siku zao
    wakiwa darasa la sita na la saba,
  • 6:31 - 6:33
    lakini mtaala wetu wa elimu
  • 6:33 - 6:37
    hufundisha wasichana kuhusu siku zao
    darasa la nane na la tisa tu.
  • 6:38 - 6:39
    na kwa vile ni mwiko,
  • 6:40 - 6:43
    waalimu bado
    wanairuka mada.
  • 6:45 - 6:49
    Hivyo shule haziwafundishi
    wasichana kuhusu siku zao,
  • 6:49 - 6:51
    wazazi hawazungumzii jambo hilo.
  • 6:51 - 6:53
    Wasichana wanaenda wapi?
  • 6:54 - 6:57
    Miongo miwili iliyopita na sasa--
  • 6:57 - 6:58
    hakuna kilichobadilika.
  • 7:00 - 7:03
    Nilimshirikisha Tuhin matokeo yangu
    na tulijiuliza
  • 7:03 - 7:05
    Itakuwaje tukianzisha kitu
  • 7:05 - 7:09
    ambacho kitasaidia wasichana kuelewa
    kuhusu hedhi wao wenyewe --
  • 7:09 - 7:13
    Kitu ambacho kitawasaidia
    wazazi na waalimu
  • 7:13 - 7:16
    kuongelea kuhusu siku za hedhi
    kwa raha kwa wasichana wadogo?
  • 7:18 - 7:19
    Wakati wa utafiti wangu,
  • 7:19 - 7:21
    Nilikuwa nakusanya hadithi nyingi.
  • 7:21 - 7:26
    Hizi ni hadithi za mambo waliyopitia
    wasichana kipindi cha siku zao.
  • 7:27 - 7:30
    Hadithi hizi zitawafanya wasichana
    wawe wadadisi na kuvutiwa
  • 7:30 - 7:34
    katika kuongea kuhusu hedhi
    ndani ya watu wao wa karibu.
  • 7:34 - 7:35
    Hicho ndio tulichotaka.
  • 7:36 - 7:39
    Tulitaka kitu ambacho
    kingewafanya wasichana wawe wadadisi
  • 7:39 - 7:41
    na kuwasukuma kujifunza.
  • 7:41 - 7:44
    Tulitaka kutumia hadithi hizi
    kufundisha wasichana kuhusu siku zao.
  • 7:45 - 7:48
    Hivyo tukaamua kutengeneza kitabu
    cha vikatuni
  • 7:48 - 7:52
    ambapo wahusika wa katuni
    wataigiza hadithi hizi
  • 7:52 - 7:56
    na kuwaelimisha wasichana kuhusu hedhi
    kwa njia ya kufurahisha na kuwashirikisha.
  • 7:56 - 7:59
    Kuwasilisha wasichana
    katika hatua zao tofauti za kubalehe,
  • 7:59 - 8:01
    tunao wahusika watatu.
  • 8:02 - 8:05
    Pinki, ambaye hajapata siku zake bado,
  • 8:05 - 8:08
    Jiya anayepata siku zake
    wakati wa simulizi za kitabu
  • 8:08 - 8:12
    na Mira ambaye tayari
    amekuwa akipata siku zake.
  • 8:12 - 8:14
    Kuna mhusika wa nne, Priya Didi.
  • 8:14 - 8:18
    Kupitia yeye, wasichana wanakuja kujua
    kuhusu vipengele kadhaa vya ukuaji
  • 8:18 - 8:19
    na kusimamia usafi wa hedhi.
  • 8:20 - 8:22
    Utengenezaji kitabu,
    ulitumia umakini
  • 8:22 - 8:26
    hakuna katika vielelezo ambavyo
    vilikuwa na pingamizi lolote
  • 8:26 - 8:28
    na hiyo ni nyeti kitamaduni.
  • 8:29 - 8:33
    Wakati wa majaribio ya sampuli ya awali
    tuligundua wasichana wakilipenda kitabu.
  • 8:33 - 8:34
    Walikuwa na hamu ya kukisoma
  • 8:34 - 8:37
    na kujua zaidi na zaidi
    kuhusu siku zao wao wenyewe.
  • 8:38 - 8:41
    Wazazi na waalimu walikuwa
    hawaoni shida kuongea kuhusu siku
  • 8:41 - 8:43
    kwa wasichana wadogo kutumia kitabu
  • 8:43 - 8:46
    na wakati mwingine hata wavulana
    walivutiwa kukisoma.
  • 8:46 - 8:48
    (Kicheko)
  • 8:48 - 8:50
    (Makofi)
  • 8:52 - 8:56
    Kitabu cha vikatu kilisaidia
    katika kujenga mazingira
  • 8:56 - 8:58
    ambapo itasimamisha hedhi kuwa mwiko.
  • 8:59 - 9:03
    Wengi wa waliojitolea walichukua hii
    sampuli ya awali kuelimisha wasichana
  • 9:03 - 9:07
    na kufanya warsha za kuelimisha hedhi
    katika majimbo matano tofauti India.
  • 9:07 - 9:10
    na mmoja wa waliojitolea alitumia
    sampuli hii kuelimisha watawa vijana
  • 9:10 - 9:12
    na aliipeleka kwenye nyumba ya utawa
    Ladakh.
  • 9:12 - 9:16
    Tulitengeneza toleo la mwisho la kitabu,
    tukakiita "Menstrupedia Comic"
  • 9:16 - 9:19
    na kukizindua Septemba mwaka jana.
  • 9:19 - 9:20
    Na mpaka sasa,
  • 9:21 - 9:25
    zaidi ya wasichana 4,000 wameelimika
    kwa kutumia kitabu India na --
  • 9:25 - 9:28
    (Makofi)
  • 9:28 - 9:29
    Asanteni.
  • 9:29 - 9:31
    (Makofi)
  • 9:34 - 9:36
    na nchi nyingine 10.
  • 9:37 - 9:40
    Mara kwa mara tunakitafsiri kitabu
    katika lugha tofauti
  • 9:40 - 9:43
    Na kushirikiana na mashirika ya ndani
    nchi
  • 9:43 - 9:46
    na kufanya hiki kitabu kipatikane
    katika nchi tofauti.
  • 9:46 - 9:49
    Mashule 15 katika sehemu tofauti India
  • 9:49 - 9:52
    yamekifanya kitabu hiki
    kuwa sehemu ya mtaala wa shule zao
  • 9:52 - 9:54
    kufundisha wasichana kuhusu hedhi.
  • 9:54 - 9:56
    (Makofi)
  • 10:00 - 10:06
    Nafurahishwa kuona jinsi wanaojitolea,
  • 10:06 - 10:10
    watu binafsi, wazazi
    waalimu, wakuu wa mashule
  • 10:10 - 10:11
    wamekutana pamoja
  • 10:11 - 10:16
    na kufanya msukumo huu wa ufahamishaji
    wa hedhi kwa jamii zao,
  • 10:16 - 10:19
    wamehakikisha wasichana wanajifunza
    kuhusu siku zao katika umri sahihi
  • 10:19 - 10:22
    na kusaidia katika kuvunja mwiko huu
  • 10:23 - 10:27
    Ninaota maisha ya mbele
    ambapo hedhi sio laana,
  • 10:27 - 10:29
    sio ugonjwa,
  • 10:29 - 10:31
    ila ni mabadiliko katika
    maisha ya msichana.
  • 10:32 - 10:33
    Na ninge --
  • 10:33 - 10:35
    (Makofi)
  • 10:38 - 10:39
    Na ningependa kumalizia hii
  • 10:39 - 10:43
    kwa ombi dogo
    kwa wazazi wote hapa.
  • 10:43 - 10:44
    Wapendwa wazazi,
  • 10:45 - 10:47
    kama mtakuwa mnafedheheshwa na hedhi
  • 10:47 - 10:50
    na mabinti zenu watafedheheshwa, pia.
  • 10:50 - 10:52
    Hivyo tafadhali muwe na mtazamo chanya
    katika siku.
  • 10:52 - 10:53
    (Kicheko)
  • 10:53 - 10:55
    Asanteni.
  • 10:55 - 10:57
    (Makofi)
Title:
Njia isiyo na mwiko kuongelea kuhusu siku za hedhi
Speaker:
Aditi Gupta
Description:

Ni kweli: kuongelea kuhusu hedhi kunafanya watu wengi wakose raha. Na mwiko huo una matokeo yake: nchini India, wasichana watatu kati ya 10 hawajui hata hedhi ni nini wakati wa siku zao za kwanza, na masharti ya mila yanayohusiana na siku za hedhi yanaleta uharibifu kisaikolojia kwa wasichana. Kukua katika mwiko huu mwenyewe, Aditi Gupta alijua anataka kusaidia wasichana, wazazi, waalimu kuzungumzia kuhusu siku za hedhi kwa raha bila aibu. Anatushirikisha alivyofanya.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
11:10

Swahili subtitles

Revisions