WEBVTT 00:00:00.000 --> 00:00:01.976 Mimi ni msimuliaji wa hadithi 00:00:02.000 --> 00:00:04.976 Ningependa kuwasimulia kidogo maisha yangu 00:00:05.000 --> 00:00:09.976 juu ya kile ninachopenda kuita "hatari ya simulizi moja" 00:00:10.746 --> 00:00:13.976 Nilikulia mazingira ya chuo kikuu magharibi mwa Nigeria 00:00:14.158 --> 00:00:17.467 Mama yangu anasema nilianza kusoma nikiwa na miaka miwili 00:00:17.491 --> 00:00:20.507 japo nadhani miaka minne ni sahihi zaidi 00:00:21.753 --> 00:00:23.564 Niliwahi sana kuanza kusoma 00:00:23.588 --> 00:00:26.976 Nilisoma vitabu vya watoto vya Uingereza na Marekani NOTE Paragraph 00:00:27.706 --> 00:00:29.976 Pia nilianza kuandika katika umri mdogo 00:00:30.000 --> 00:00:33.976 Na nilipoanza kuandika, nikiwa na takriban miaka saba, 00:00:34.000 --> 00:00:36.048 hadithi za penseli na michoro ya rangi 00:00:36.072 --> 00:00:39.604 ambazo mama yangu alilazimika kuzisoma, 00:00:39.628 --> 00:00:43.196 niliandika hadithi sawa na zile nilizokuwa nazisoma: 00:00:43.220 --> 00:00:47.976 Wahusika wangu wote walikuwa wazungu na wenye macho ya bluu. 00:00:48.000 --> 00:00:50.307 Walicheza katika theluji. 00:00:50.331 --> 00:00:52.418 Walikula matofaa NOTE Paragraph 00:00:52.442 --> 00:00:53.839 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:00:54.013 --> 00:00:56.024 Na walizungumza sana kuhusu hali ya hewa, 00:00:56.048 --> 00:00:58.176 jinsi ilivyo vizuri kuona jua limechomoza. NOTE Paragraph 00:00:58.409 --> 00:01:00.373 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:01:00.397 --> 00:01:03.531 Yote haya,ingawa niliishi Nigeria. 00:01:03.555 --> 00:01:05.333 Nilikuwa sijawahi kwenda nje ya Nigeria. 00:01:07.143 --> 00:01:10.404 Hatukuwa na theluji, tulikula maembe. 00:01:10.428 --> 00:01:12.276 Na hatukuzungumza kuhusu hali ya hewa, 00:01:12.300 --> 00:01:13.976 sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo. NOTE Paragraph 00:01:14.269 --> 00:01:16.976 Wahusika wangu pia walikunywa sana bia ya tangawizi 00:01:17.000 --> 00:01:19.381 kwa sababu wahusika katika vitabu vya Uingereza 00:01:19.405 --> 00:01:20.976 walikunywa bia ya tangawizi. 00:01:21.301 --> 00:01:23.976 Ijapokuwa sikuifahamu bia ya tangawizi NOTE Paragraph 00:01:24.000 --> 00:01:25.531 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:01:25.555 --> 00:01:27.005 Na kwa miaka mingi baadaye 00:01:27.029 --> 00:01:29.976 nilikuwa na shauku ya kuonja bia ya tangawizi. 00:01:30.476 --> 00:01:31.976 Lakini hiyo ni hadithi nyingine. NOTE Paragraph 00:01:32.000 --> 00:01:34.483 Ambacho hii inaonyesha,nafikiri 00:01:34.507 --> 00:01:37.361 Ni namna tulivyo wajinga na wanyonge 00:01:37.385 --> 00:01:38.976 Tunapokabiliana na simulizi 00:01:39.000 --> 00:01:40.385 hasa hasa kama watoto 00:01:41.639 --> 00:01:45.409 Sababu nilisoma vitabu vyenye wahusika wa kigeni 00:01:45.433 --> 00:01:47.552 Nilikuwa nimeaminishwa kwamba vitabu 00:01:47.576 --> 00:01:50.746 kwa asili lazima viwe na wahusika wageni 00:01:50.770 --> 00:01:54.489 Na vielezo kuhusu mambo ambayo binafsi siyafahamu 00:01:55.600 --> 00:01:58.219 Mambo yalibadilika Nilipopata vitabu vya Afrika 00:01:59.000 --> 00:02:00.976 havikuwepo kwa wingi 00:02:01.000 --> 00:02:03.869 Na haikuwa rahisi kuvipata kama vya kigeni NOTE Paragraph 00:02:03.893 --> 00:02:06.976 Lakini sababu ya waandishi kama Chinua Achebe na Camara Laye 00:02:07.000 --> 00:02:10.976 Nilipata badiliko la akili ninavyoiona fasihi 00:02:11.000 --> 00:02:13.214 Niligundua kwamba watu kama mimi, 00:02:13.238 --> 00:02:15.245 wasichana weusi 00:02:15.269 --> 00:02:18.531 wenye nywele ngumu 00:02:18.555 --> 00:02:20.365 pia wapo katika fasihi. 00:02:20.682 --> 00:02:23.976 Nilianza kuandika vitu nilivyovifahamu NOTE Paragraph 00:02:24.737 --> 00:02:27.976 Nilikuwa navipenda hivyo vitabu vya Marekani na Uingereza 00:02:28.000 --> 00:02:31.976 Viliamsha fikra zangu Vilifunua vitu vipya. 00:02:32.000 --> 00:02:33.976 Lakini matokeo yasiyokusudiwa 00:02:34.000 --> 00:02:36.048 yalikuwa; sikufahamu kuwa watu kama mimi 00:02:36.072 --> 00:02:37.498 waweza kuwepo katika fasihi. 00:02:38.451 --> 00:02:41.976 hivyo ufumbuzi wa waandishi Waafrika: 00:02:42.000 --> 00:02:45.877 Uliniokoa na mtazamo mmoja juu ya vitabu NOTE Paragraph 00:02:47.000 --> 00:02:49.976 Ninatoka kwenye familia ya kawaida 00:02:50.000 --> 00:02:51.976 Baba yangu alikuwa mhadhiri 00:02:52.385 --> 00:02:54.068 Mama yangu ni afisa wa utawala 00:02:55.369 --> 00:02:58.171 Kwa hiyo kama kawaida, tulikuwa na, 00:02:58.195 --> 00:03:02.544 mtumishi wa nyumbani anayetoka vijiji vya jirani 00:03:03.182 --> 00:03:06.468 Nilipokuwa na miaka nane tulipata mtumishi wa kiume 00:03:07.102 --> 00:03:08.356 Jina lake aliitwa Fide 00:03:09.658 --> 00:03:13.959 Mama alituambia kuwa familia yake ni masikini sana 00:03:15.000 --> 00:03:19.976 Mama alituma magimbi na mchele na nguo zetu za zamani kwa familia yao 00:03:20.000 --> 00:03:22.620 Na niliposhindwa kumaliza chakula mama alisema, 00:03:22.644 --> 00:03:26.976 "Maliza chakula! kuna watu ambao hawana chochote 00:03:27.000 --> 00:03:30.976 Niliwahurumia sana familia ya Fide NOTE Paragraph 00:03:31.576 --> 00:03:34.473 Jumamosi moja tukaenda kijijini kwao kutembelea 00:03:34.497 --> 00:03:37.976 na mama yake akatuonyesha kikapu kizuri 00:03:38.000 --> 00:03:40.976 kilichosukwa kwa ukili uliopakwa rangi na kaka yake Fide 00:03:41.000 --> 00:03:42.976 Nilishangaa 00:03:43.000 --> 00:03:45.976 Sikudhani kuwa yeyote katika familia yake 00:03:46.000 --> 00:03:48.976 angeweza kutengeneza chochote 00:03:49.000 --> 00:03:51.976 yote niliyowahi kusikia kuhusu wao ni namna walivyo masikini 00:03:52.000 --> 00:03:56.467 Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwangu kuwaona tofauti na umasikini wao 00:03:57.143 --> 00:03:59.514 umasikini wao ilikuwa ni simulizi moja kwangu NOTE Paragraph 00:04:01.000 --> 00:04:03.524 baadaye niliwaza hili nilipotoka Nigeria 00:04:03.548 --> 00:04:06.230 Kwenda Marekani kusoma chuo kikuu 00:04:06.341 --> 00:04:07.674 Nilikuwa na miaka 19 00:04:08.421 --> 00:04:11.198 Mmarekani niliyekuwa naishi naye chumba kimoja alinishangaa 00:04:12.000 --> 00:04:15.586 Aliuliza wapi nimefunza kuzungumza kiingereza vizuri 00:04:15.610 --> 00:04:17.698 Alishangaa nilipomwambia kuwa Nigeria 00:04:17.722 --> 00:04:20.436 wanatumia kiingereza kama lugha ya taifa 00:04:21.753 --> 00:04:25.976 Aliomba kusikiliza "nyimbo za kikabila" 00:04:26.000 --> 00:04:27.976 na alipigwa butwaa vile vile 00:04:28.000 --> 00:04:29.976 Nilipompa kanda yangu ya Mariah Carey NOTE Paragraph 00:04:30.000 --> 00:04:32.976 (kicheko) NOTE Paragraph 00:04:33.000 --> 00:04:36.693 Alidhani kuwa sifahamu kutumia jiko la umeme NOTE Paragraph 00:04:37.782 --> 00:04:39.038 Kilichonishangaza mimi ni hiki 00:04:39.062 --> 00:04:42.137 Alikuwa ananihurimia hata kabla ya kuniona 00:04:42.528 --> 00:04:45.976 Mtazamo wake mbovu, kunihusu, kama Mwafrika, 00:04:46.000 --> 00:04:49.036 Ulikuwa wa huruma ya kudhalilisha, yenye kujali 00:04:50.000 --> 00:04:53.496 Alikuwa na simulizi moja kuhusu Afrika: 00:04:53.623 --> 00:04:55.977 Simulizi ya majanga. 00:04:56.412 --> 00:04:57.698 Kwenye simulizi hii moja, 00:04:57.722 --> 00:05:01.976 Hakukuwa na uwezekano wa Mwafrika kufanana naye kwa namna yeyote, 00:05:02.000 --> 00:05:04.976 Hakukuwa na uwezekano wa hisia ngumu zaidi ya huruma, 00:05:05.000 --> 00:05:08.976 Hakukuwa na uwezekano wa ushirikiano kama binadamu walio sawa. NOTE Paragraph 00:05:09.000 --> 00:05:11.123 Lazima niseme kuwa kabla ya kwenda Marekani, 00:05:11.147 --> 00:05:13.428 Sikuwa nikijitambua kwa undani kama Mwafrika. 00:05:14.000 --> 00:05:16.976 Lakini Marekani, popote Afrika ilipotajwa, watu walinigeukia. 00:05:17.000 --> 00:05:19.746 Bila kujali kuwa sifahamu chochote kuhusu nchi kama Namibia. 00:05:21.000 --> 00:05:23.096 Lakini nilikuja kuupokea huu utambulisho mpya, 00:05:23.120 --> 00:05:25.976 Na kwa namna nyingi sasa ninajitazama kama Mwafrika. 00:05:26.000 --> 00:05:29.976 Ijapokuwa bado ninakasirishwa sana pale Afrika inapoelezewa kama ni nchi 00:05:30.000 --> 00:05:33.976 Mfano wa karibu, ni safari yangu ya ndege 00:05:34.000 --> 00:05:35.285 Kutoka Lagos hivi juzi, 00:05:35.309 --> 00:05:38.191 Ambapo kulikuwa na tangazo 00:05:38.215 --> 00:05:42.976 Kuhusu kazi ya kujitolea kule "India, Afika na nchi nyingine" NOTE Paragraph 00:05:43.000 --> 00:05:44.317 Kicheko NOTE Paragraph 00:05:44.476 --> 00:05:47.976 Baada ya kuishi Marekani kama Mwafrica 00:05:48.000 --> 00:05:51.174 Nikaanza kuelewa mwitikio wa niliyekuwa naishi naye chumba kimoja 00:05:52.000 --> 00:05:54.025 kama sikukulia Nigeria 00:05:54.049 --> 00:05:57.190 Na kama kila nilichofahamu kuhusu Afrika kilitokana na picha maarufu 00:05:57.214 --> 00:06:02.386 Mimi pia ningedhani kuwa Africa ni mahali penye mandhari nzuri, 00:06:02.410 --> 00:06:03.976 Wanyama wa kupendeza, 00:06:04.000 --> 00:06:05.976 na watu wasioeleweka, 00:06:06.000 --> 00:06:09.631 wapiganao vita visivyo na maana, wanaokufa na umasikini na UKIMWI 00:06:09.655 --> 00:06:11.976 wasioweza kujisemea 00:06:12.000 --> 00:06:16.155 wanaosubiri kusaidiwa na mtu mweupe, mgeni mwenye ukarimu 00:06:16.928 --> 00:06:19.097 Ningewaona waafrika kwa namna ile ambayo mimi, 00:06:19.121 --> 00:06:21.824 nilipokuwa mtoto, niliiona familia ya Fide NOTE Paragraph 00:06:23.000 --> 00:06:26.976 Hii simulizi moja kuhusu Afrika nadhani inatokana na fasihi za magharibi 00:06:27.000 --> 00:06:31.976 Sasa, huu ni msemo kutoka katika uandishi wa mfanyabiashara wa London aitwaye John Lok, 00:06:32.000 --> 00:06:34.976 aliyesafiri kwa maji kuelekea Afrika magharibi mwaka 1561 00:06:35.000 --> 00:06:38.663 na aliweka hazina ya kuvutia kutokana na safari yake. 00:06:40.203 --> 00:06:43.976 Baada ya kuwaita Waafrika weusi kama " hayawani wasio na nyumba," 00:06:44.000 --> 00:06:47.976 aliandika,"Pia kuna watu wasio na vichwa, 00:06:48.000 --> 00:06:51.968 midomo na macho yao yapo katika vifua vyao." NOTE Paragraph 00:06:53.000 --> 00:06:55.096 Sasa, nilicheka kila nikisoma haya maneno. 00:06:55.120 --> 00:06:58.500 Na lazima mtu atakubaliana na fikira za John Lok. 00:06:59.373 --> 00:07:01.239 Lakini kipi ni muhimu kuhusu uandishi wake 00:07:01.263 --> 00:07:02.976 ni kwamba inawakilisha mwanzo 00:07:03.000 --> 00:07:05.976 wa utamaduni wa kuelezea hadithi za Afrika kwa Magharibi: 00:07:06.000 --> 00:07:09.367 Utamaduni wa kusini mwa jangwa la Sahara kama sehemu isiyofaa, 00:07:09.479 --> 00:07:11.634 yenye utofauti, yenye kiza, 00:07:11.658 --> 00:07:16.976 ya watu ambao, kutokana na maneno ya mshairi bora aitwaye Rudyard Kipling, 00:07:17.000 --> 00:07:18.941 ni "nusu shetani, nusu watoto." NOTE Paragraph 00:07:20.211 --> 00:07:22.976 Hivyo, nilianza kuelewa kwamba mwanafunzi Mmarekani ninayeshirikiana nae chumba 00:07:23.000 --> 00:07:24.976 lazima katika maisha yake 00:07:25.000 --> 00:07:28.976 atakuwa ameona na kusikia namna mbalimbali za hii hadithi moja, 00:07:29.000 --> 00:07:30.976 kama ilivyo kwa profesa, 00:07:31.000 --> 00:07:34.766 ambaye aliwahi niambia kuwa riwaya yangu haikuwa "na uhalisia wa Kiafrika," 00:07:35.869 --> 00:07:37.560 Sasa, nilikubaliana na kuchanganua 00:07:37.584 --> 00:07:40.679 kwamba kulikuwa na baadhi ya vitu ambavyo si sawa katika riwaya hii, 00:07:40.703 --> 00:07:43.976 na kuwa nilifeli katika maeneo mbalimbali, 00:07:44.000 --> 00:07:46.239 lakini sikufiria kwamba ilifeli 00:07:46.263 --> 00:07:48.976 katika kutekeleza uhalisia wake wa Kiafrika. 00:07:49.000 --> 00:07:52.706 Kiukweli, sikufahamu uhalisia wa Kiafrika ni upi. 00:07:54.000 --> 00:07:58.396 Profesa alinielezza kwamba wahusika kwenye riwaya walikuwa wanafanana mno kama yeye, 00:07:58.420 --> 00:08:00.396 msomi aliye katika maisha ya kati. 00:08:00.420 --> 00:08:02.522 Wahusika wangu waliendesha magari. 00:08:02.546 --> 00:08:04.976 Hawakuwa wanashinda na njaa. 00:08:05.000 --> 00:08:07.927 Kwa hiyo hawakuwa Waafrika halisi. NOTE Paragraph 00:08:09.000 --> 00:08:11.976 Lakini niongeze haraka-haraka kwamba najisikia hatia 00:08:12.000 --> 00:08:14.070 katika swali la la hadithi iliyo moja. 00:08:15.000 --> 00:08:17.991 Miaka michache iliyopita, nilitembelea Mexico nikitokea Marekani. 00:08:19.000 --> 00:08:21.667 Hali ya kisiasa nchini Marekani wakati huo ilikuwa tete, 00:08:21.691 --> 00:08:24.976 kulikuwa na majadiliano yanayoendelea kuhusu uhamiaji. 00:08:25.000 --> 00:08:26.976 Na, mara kwa mara hutokea Marekani, 00:08:27.000 --> 00:08:29.976 neno uhamiaji likaja kuwa linahusishwa na watu wenye asili ya Mexico. 00:08:30.698 --> 00:08:32.631 Kulikuwa na hadithi ndefu kuhusu Wamexico 00:08:32.655 --> 00:08:35.976 kama watu wanaonyonya mfumo wa afya, 00:08:36.000 --> 00:08:37.976 wanajipenyeza kwenye mipaka, 00:08:38.000 --> 00:08:40.465 wanakamatwa kwenye mipaka, vitu kama hivyo. NOTE Paragraph 00:08:42.163 --> 00:08:45.976 Nakumbuka siku ya kwanza nilipokuwa natembea eneo liitwalo Guadalajara, 00:08:46.000 --> 00:08:47.976 nikiwaangalia watu wakielekea makazini, 00:08:48.000 --> 00:08:49.976 wakitengeneza tortilla maeneo ya sokoni, 00:08:50.000 --> 00:08:51.973 wakivuta sigara, wakicheka. 00:08:53.195 --> 00:08:55.976 Nakumbuka kwa mara ya kwanza nilipatwa na mshangao kidogo. 00:08:56.000 --> 00:08:58.976 Kisha, nikagubikwa na aibu. 00:08:59.341 --> 00:09:03.976 Nikatambua ya kwamba nimezama sana katika habari zinazoelezea watu wa Mexico 00:09:04.000 --> 00:09:06.000 ambao wamekuwa jambo katika akili yangu, 00:09:06.024 --> 00:09:07.849 wahamiaji duni, 00:09:08.769 --> 00:09:11.191 nilidanganyika katika hadithi moja ya watu wa Mexico 00:09:11.215 --> 00:09:13.722 na sikuweza kujisikia aibu zaidi. NOTE Paragraph 00:09:14.071 --> 00:09:16.618 Kwa hiyo hiyo ndiyo namna ya kutengeneza hadithi moja. 00:09:16.642 --> 00:09:18.976 kuwaeleza watu kama jambo moja, 00:09:19.000 --> 00:09:20.976 kama jambo moja tu, 00:09:21.000 --> 00:09:22.976 tena na tena, 00:09:23.000 --> 00:09:24.515 na hivyo ndivyo watakavyokuwa. NOTE Paragraph 00:09:25.793 --> 00:09:28.239 Haiwezekani kuongelea kuhusu hadithi moja 00:09:28.263 --> 00:09:29.952 bila kuongelea kuhusu uwezo ya mamlaka. 00:09:31.496 --> 00:09:33.244 Kuna neno, neno la lugha ya Igbo, 00:09:33.268 --> 00:09:36.919 ambalo huwa naliwaza kila nikifikiria mfumo wa mamlaka wa dunia, 00:09:36.943 --> 00:09:38.133 na hili "nkali". 00:09:38.332 --> 00:09:42.976 Ni nomino ambayo inatafsiriwa kama "kuwa juu zaidi ya mwigine." 00:09:43.554 --> 00:09:46.482 Kama ulivyo ulimwengu wa kiuchumi na kisiasa, 00:09:46.506 --> 00:09:50.976 hadithi pia huelezwa kwa kanuni ya nkali: 00:09:51.000 --> 00:09:52.976 Zinaelezwaje, nani anaelezea, 00:09:53.000 --> 00:09:56.237 wakati gani zilielezwa, hadithi ngapi zinaelezwa, 00:09:56.261 --> 00:09:58.468 haya yote yanategemea sana nguvu ya mamlaka. NOTE Paragraph 00:10:00.000 --> 00:10:03.143 Mamlaka ni uwezo sio tu wa kueleza hadithi ya kuhusu mtu mwingine, 00:10:03.167 --> 00:10:06.976 lakini kuifanya iwe hadithi mahususi kuhusu mtu huyo. 00:10:07.000 --> 00:10:09.096 Mshairi wa Kipalestina Mourid Barghouti aliandika 00:10:09.120 --> 00:10:11.976 kwamba kama unataka kuwaondoa watu, 00:10:12.000 --> 00:10:14.976 njia rahisi ya kufanya hivyo ni kuelezea hadithi yao 00:10:15.000 --> 00:10:17.230 na kuanza na, "pili." 00:10:18.484 --> 00:10:22.382 Anza hadithi na mishale ya waliokuwa wakazi halisi wa Amerika, 00:10:22.406 --> 00:10:24.976 na sio baada ya kufika kwa Waingereza, 00:10:25.000 --> 00:10:27.977 na utakuwa na hadithi tofauti nyingine kabisa. 00:10:28.001 --> 00:10:32.433 Anza na hadithi kuhusu kuanguka kwa dola za Kiafrika, 00:10:32.457 --> 00:10:35.976 na sio dola za Kiafrika zilizotokana na ukoloni, 00:10:36.000 --> 00:10:38.742 na utakuwa na hadithi tofauti kabisa. NOTE Paragraph 00:10:40.000 --> 00:10:41.976 Hivi karibun nilitoa hotuba katika chuo 00:10:42.000 --> 00:10:45.785 ambapo mwanafunzi aliniambia kwamba ilikuwa ni aibu 00:10:45.809 --> 00:10:48.928 kwamba wanaume wa Kinigeria walikuwa wanyanyasaji 00:10:48.952 --> 00:10:50.896 kama alivyo muhusika ambaye ni baba katika riwaya yangu. 00:10:52.000 --> 00:10:55.976 Nikamwambia nimesoma riwaya iitwayo "Mwendawazimu wa Kiamerika" -- NOTE Paragraph 00:10:56.000 --> 00:10:57.976 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:10:58.000 --> 00:10:59.976 -- na kwamba ilikuwa aibu 00:11:00.000 --> 00:11:02.976 kwamba vijana wadogo wa Kiamerika walikuwa wauaji waliokubuhu. NOTE Paragraph 00:11:03.000 --> 00:11:06.976 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:11:07.000 --> 00:11:12.976 (Makofi) NOTE Paragraph 00:11:13.000 --> 00:11:15.976 Sasa, kiukweli nilisema hili kutokana na kukerwa. NOTE Paragraph 00:11:16.000 --> 00:11:17.976 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:11:18.000 --> 00:11:20.191 Lakini isingeweza kutokea kwangu kuwaza 00:11:20.215 --> 00:11:23.976 kwamba kwa sababu nimesoma riwaya ambayo muhusika ni muuaji wa kufululiza 00:11:24.000 --> 00:11:27.976 kwamba kwa kiasi fulani wanawakilisha Wamarekani wote. 00:11:28.000 --> 00:11:30.976 Hii si kwamba mimi ni mtu bora kuliko yule mwanafunzi, 00:11:31.000 --> 00:11:33.976 lakini kwa sababu ya utamaduni na nguvu ya uchumi wa Marekani, 00:11:34.000 --> 00:11:35.976 Nilikuwa nina hadithi nyingi za Marekani. 00:11:36.000 --> 00:11:39.976 Nilisoma Tyler na Updike na Steinbeck na Gaitskill. 00:11:40.000 --> 00:11:42.560 Sikuwa na hadithi moja ya Marekani. NOTE Paragraph 00:11:43.671 --> 00:11:45.377 Nilipojifunza, miaka kadhaa iliyopita, 00:11:45.401 --> 00:11:49.742 kwamba waandishi wanategemewa kuwa na maisha ya utotoni ambayo siyo ya furaha 00:11:49.766 --> 00:11:51.976 ili kuja kufanikiwa baadaye, 00:11:52.000 --> 00:11:56.000 Nilianza kuwaza ni namna gani naweza buni vitu vibaya ambavyo wazazi wangu walinifanyia. NOTE Paragraph 00:11:56.024 --> 00:11:57.976 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:11:58.000 --> 00:12:01.976 Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na maisha ya utoto ambayo yalikuwa ya furaha sana, 00:12:02.000 --> 00:12:04.976 yaliyojaa vicheko na upendo, katika familia iliyo na ukaribu sana. NOTE Paragraph 00:12:05.000 --> 00:12:08.211 Lakini pia nilikuwa na mababu waliofia kwenye kambi za wakimbizi. 00:12:08.750 --> 00:12:12.976 Binamu yangu Polle alifariki sababu hakupata matibabu yanayostahili. 00:12:13.000 --> 00:12:15.976 Mmoja wa rafiki zangu,Okoloma, alifariki kwenye ajali ya ndege 00:12:16.000 --> 00:12:18.976 kwa sababu gari zetu za zimamoto hazikuwa na maji. 00:12:19.000 --> 00:12:21.976 Nimekulia katika serikali ya kijeshi ambayo ni kandamizi 00:12:22.000 --> 00:12:23.976 ambayo haikujali elimu, 00:12:24.000 --> 00:12:26.976 kwa muda mwingine, wazazi walikuwa hawalipwi mishahara. 00:12:27.000 --> 00:12:30.977 Hivyo, kama mtoto, nilianza kuona jamu hakuna mezani wakati wa kupata kifungua kinywa, 00:12:31.001 --> 00:12:33.498 kisha siagi nayo ikakosekana, 00:12:33.522 --> 00:12:35.976 kisha mkate ukawa ghali sana, 00:12:36.000 --> 00:12:37.871 kisha maziwa yakapungua. 00:12:39.000 --> 00:12:42.657 Na katika yote, hali ya hofu ya kisiasa 00:12:42.681 --> 00:12:44.363 ikaingilia maisha yetu, NOTE Paragraph 00:12:45.823 --> 00:12:47.960 Na hadithi zote hizi zimenitengeneza mimi wa leo. 00:12:48.457 --> 00:12:51.976 Lakini kusisitiza katika hizi hadithi hasi 00:12:52.000 --> 00:12:54.976 ni kuongeza uzoefu wangu 00:12:55.000 --> 00:12:58.664 na kuachana na hadithi nyinginezo nyingi ambazo zimenitengeneza mimi. 00:12:59.394 --> 00:13:01.976 Hadithi moja hutengeneza tabaka, 00:13:02.000 --> 00:13:06.976 na tatizo la tabaka si kwamba hazina kweli, 00:13:07.000 --> 00:13:08.976 lakini hazijakamilika. 00:13:09.357 --> 00:13:11.960 Hufanya hadithi moja kuwa hadithi pekee. NOTE Paragraph 00:13:13.000 --> 00:13:15.572 Hakika, Afrika ni bara ambalo limejaa majanga: 00:13:15.596 --> 00:13:18.976 Kuna majanga yaliyo makubwa, kama ubakaji wa kutisha nchini Congo 00:13:19.000 --> 00:13:20.626 na wa kudidimiza, 00:13:20.650 --> 00:13:25.150 kama ukweli kwamba watu 5000 wanaomba nafasi moja ya kazi nchini Nigeria. 00:13:26.000 --> 00:13:29.563 Lakini kuna hadithi nyingine ambazo hazihusiani na majanga, 00:13:29.587 --> 00:13:32.976 na ni muhimu sana, ni namna kuziongelea. NOTE Paragraph 00:13:33.000 --> 00:13:34.976 Wakati wote nimekuwa nikihisi haiwezekani 00:13:35.000 --> 00:13:37.976 kujiunga kwa utaratibu na sehemu au mtu 00:13:38.000 --> 00:13:41.976 bila kuhusiana na hadithi zote za mahala pale au mtu huyo. 00:13:42.000 --> 00:13:45.580 Madhara ya hadithi moja ni kwamba: 00:13:45.604 --> 00:13:47.561 Hunyang'anya watu wa heshima. 00:13:48.332 --> 00:13:51.976 Hufanya utambuzi wetu wa usawa wa kibinadamu kuwa mgumu. 00:13:52.000 --> 00:13:56.164 Husisitiza ni jinsi gani tulivyo tofauti kuliko vile tulivyo sawa. NOTE Paragraph 00:13:57.000 --> 00:13:59.489 Inakuwaje wakati kabla ya safari yangu ya Mexico, 00:13:59.513 --> 00:14:02.976 Ningefatilia majadiliano ya uhamiaji kutoka pande zote, 00:14:03.000 --> 00:14:04.976 upande wa Marekani na wa Mexico? 00:14:05.000 --> 00:14:08.976 Ingekuwaje kama mama yangu angeniambia familia ya Fide ilikuwa masikini 00:14:09.000 --> 00:14:10.976 na ya wachapakazi? 00:14:11.000 --> 00:14:13.096 Inakuwaje kama tungekuwa na mtandao wa televisheni wa Kiafrika 00:14:13.120 --> 00:14:16.976 ambao unarusha vipindi vya hadithi za Afrika duniani kote? 00:14:17.000 --> 00:14:21.331 Kitu ambacho muandishi wa Kinigeria Chinua Achebe anaita "usawa wa hadithi." NOTE Paragraph 00:14:21.355 --> 00:14:25.331 Inakuweaje kama mwanafunzi niliyeishi naye chumba kimoja angefahamu kuhusu mchapishaji wangu wa Kinigeria, 00:14:25.355 --> 00:14:26.976 Muhtar Bakare, 00:14:27.000 --> 00:14:29.048 mtu wa kipekee ambaye aliacha kazi ya benki 00:14:29.072 --> 00:14:31.977 na kufuata ndoto zake na kuanzisha nyumba ya uchapishaji 00:14:32.001 --> 00:14:35.688 Sasa, hekima iliyozoeleka ilikuwa kwamba Wanigeria huwa hawasomi fasihi. 00:14:35.712 --> 00:14:36.966 Yeye alikataa. 00:14:36.990 --> 00:14:40.076 Alihisi kwamba watu ambao wanaweza kusoma, wangesoma, 00:14:40.100 --> 00:14:43.976 kama ungefanya kazi ya fasihi iwe katika bei nafuu na kupatikana kiurahisi. NOTE Paragraph 00:14:44.666 --> 00:14:46.976 Muda mfupi baada ya kuchapisha riwaya yangu ya kwanza, 00:14:47.000 --> 00:14:49.976 Nilikwenda kwenye kituo cha televisheni kilichopo Lagos kwa ajili ya mahojiano, 00:14:50.000 --> 00:14:53.191 na mwanamke ambaye anafanya kazi pale kama karani alinifata na kusema, 00:14:53.215 --> 00:14:55.976 "Nimependa sana riwaya yako. Sijapenda mwishoni mwake. 00:14:56.000 --> 00:14:59.239 Sasa, ni lazima uandike muendelezo na hiki ndicho kitatokea ..." NOTE Paragraph 00:14:59.263 --> 00:15:01.977 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:15:02.001 --> 00:15:04.977 Na alipoendelea kunielezea kipi cha kuandika kwenye muendelezo. 00:15:05.564 --> 00:15:07.976 Si kwamba nilivutiwa tu, lakini pia nilisisimka. 00:15:08.000 --> 00:15:10.976 Huyu ni mwanamke, mmoja wa watu wengi wa kawaida waliopo Nigeria, 00:15:11.000 --> 00:15:13.003 ambao hawakutakiwa kuwa wasomaji. 00:15:13.901 --> 00:15:15.525 Si kwamba alisoma tu kitabu, 00:15:15.549 --> 00:15:17.358 lakini pia alikimiliki 00:15:17.382 --> 00:15:20.485 na aliona ana haki kuaniambia kitu cha kuandika katika muendelezo. NOTE Paragraph 00:15:21.580 --> 00:15:24.976 Sasa, ingekuwaje kama mwanafunzi niishiye nae chumba kimoja angejua kuhusu rafiki yangu Funmi Lyanda, 00:15:25.000 --> 00:15:27.976 mwanamke jasiri ambaye anaongoza kipindi cha televisheni Lagos, 00:15:28.000 --> 00:15:31.000 na anadhamiria kuelezea hadithi ambazo tunapendelea kuzisahau? 00:15:31.695 --> 00:15:34.976 Inakuwaje kama mwenzangu angetambua kuhusu upasuaji wa moyo 00:15:35.000 --> 00:15:37.976 ambao ulifanyika wiki iliyopita jijini Lagos? 00:15:38.000 --> 00:15:41.976 Inakuwaje angefahamu kuhusu muziki wa kisasa kwa Kinigeria, 00:15:42.000 --> 00:15:44.976 watu wenye vipaji wanaoimba katika lugha za Kiingereza na pijini, 00:15:45.000 --> 00:15:46.976 na Kiigbo na Kiyoruba na Kiijo, 00:15:47.000 --> 00:15:50.976 wakichanganya ushawishi kutoka kwa Jay Z hadi kwa Fela 00:15:51.000 --> 00:15:53.182 kwenda kwa Bob Marley na babu zao. NOTE Paragraph 00:15:54.000 --> 00:15:56.239 Inakuwaje kama angejua kuhusu wakili mwanamke 00:15:56.263 --> 00:15:59.976 ambaye hivi karibuni alienda mahakamani nchini Nigeria kuipa changamoto sheria isiyo na maana 00:16:00.000 --> 00:16:02.976 ambayo inawataka wanawake kupewa ruhusa na waume zao 00:16:03.000 --> 00:16:05.976 kabla ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria? 00:16:06.000 --> 00:16:08.976 Inakuwaje kama angefahamu kuhusu Nollywood, 00:16:09.000 --> 00:16:13.380 iliyojawa na watu wabunifu wanaotengeneza filamu ingawaje kuna changamoto nyingi za kiufundi, 00:16:13.404 --> 00:16:14.976 filamu ambazo ni maarufu sana 00:16:15.000 --> 00:16:19.976 ambazo ni mfano mzuri unaoonyesha Wanigeria wanatumia kile wanachotengeneza? 00:16:20.000 --> 00:16:23.286 Inakuwaje kama angefahamu kuhusu msusi wangu bora kabisa, 00:16:23.310 --> 00:16:26.976 ambaye ameanza biashara yake mwenyewe akiuza nywele za kuongezea? 00:16:27.000 --> 00:16:30.976 Au kuhusu mamilioni ya Wanigeria wengine ambao huanza biashara na muda mwingine kuanguka, 00:16:31.000 --> 00:16:33.938 lakini huendelea kukuza azma yao? NOTE Paragraph 00:16:35.000 --> 00:16:36.976 Muda wote nikiwa nyumbani hukutana 00:16:37.000 --> 00:16:39.976 na vyanzo vya kila wakati vya kukwaza kwa Wanigeria wengi: 00:16:40.000 --> 00:16:43.444 miundombinu yetu mibovu, serikali iliyoanguka, 00:16:43.468 --> 00:16:45.523 lakini pia kwa ustahimilivu mkubwa 00:16:45.547 --> 00:16:48.976 wa watu ambao hufanikiwa, bila ya kutegemea serikali, 00:16:49.000 --> 00:16:50.261 bila yenyewe kabisa. 00:16:51.373 --> 00:16:53.976 Huwa natoa mafunzo ya uandishi kila kipindi cha joto jijini Lagos, 00:16:54.000 --> 00:16:56.976 na huwa inanishangaza kwa namna gani watu wengi hujiunga, 00:16:57.000 --> 00:16:59.976 namna ambavyo watu wengi wana shauku ya kuandika, 00:17:00.000 --> 00:17:01.386 ili kueleza hadithi. NOTE Paragraph 00:17:02.275 --> 00:17:05.298 Mimi na mchapishaji wa kitabu changu tumeanzisha taasisi isiyo ya kibiashara 00:17:05.322 --> 00:17:06.976 inayofahamika kama Farafina Trust, 00:17:07.000 --> 00:17:09.976 na tuna ndoto kubwa ya kujenga maktaba 00:17:10.000 --> 00:17:12.143 na kukarabati maktaba ambazo tayari zipo 00:17:12.167 --> 00:17:14.976 na kutoa vitabu kwa shule za majimboni 00:17:15.000 --> 00:17:17.096 ambazo hazina vitabu katika maktaba zao, 00:17:17.120 --> 00:17:19.501 na kuandaa mafunzo mengi mno, 00:17:19.525 --> 00:17:20.976 katika kuandika na kusoma, 00:17:21.000 --> 00:17:24.199 kwa watu wote ambao wana shauku ya kuelezea hadithi zetu nyingi. NOTE Paragraph 00:17:24.326 --> 00:17:25.976 Hadithi zina maana. 00:17:26.000 --> 00:17:27.976 Hadithi nyingi zina maana. 00:17:28.000 --> 00:17:31.976 Haidithi zimekuwa zikitumika kupokonya na kukejeli, 00:17:32.000 --> 00:17:35.976 lakini hadithi zinaweza tumika kuhamasisha na kuleta ubinadamu. 00:17:36.642 --> 00:17:38.976 Hadithi zinaweza kuvunja heshima ya watu, 00:17:39.000 --> 00:17:42.703 lakini hadithi zinaweza kurudisha heshima iliyopotea. NOTE Paragraph 00:17:44.000 --> 00:17:46.048 Mwandishi wa Kimarekani Alice Walker aliandika 00:17:46.072 --> 00:17:49.976 kuhusu ndugu zake wanaotokea Kusini ambao walihamia Kaskazini. 00:17:50.000 --> 00:17:51.976 Aliwaonyesha kitabu kuhusu 00:17:52.000 --> 00:17:54.068 maisha ya Kusini ambayo wameyaacha nyuma. 00:17:55.592 --> 00:17:58.976 "Walikaa, na wakakisoma kitabu, 00:17:59.000 --> 00:18:04.528 nisikilize mimi soma kitabu, na raha ya dunia utaipata tena." NOTE Paragraph 00:18:05.579 --> 00:18:08.441 Ningependelea kumalizia na hili wazo: 00:18:08.465 --> 00:18:10.976 Kwamba pale tunapokataa hadithi moja, 00:18:11.000 --> 00:18:13.976 tunapogundua kwamba hakuna hadithi moja 00:18:14.000 --> 00:18:16.441 kuhusu sehemu yoyote, 00:18:16.465 --> 00:18:17.976 huwa tunarejesha Furaha. NOTE Paragraph 00:18:18.695 --> 00:18:19.817 Asante. NOTE Paragraph 00:18:19.841 --> 00:18:22.841 (Makofi)