[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:00.00,0:00:01.98,Default,,0000,0000,0000,,Mimi ni msimuliaji wa hadithi Dialogue: 0,0:00:02.00,0:00:04.98,Default,,0000,0000,0000,,Ningependa kuwasimulia kidogo maisha yangu Dialogue: 0,0:00:05.00,0:00:09.98,Default,,0000,0000,0000,,juu ya kile ninachopenda kuita\N"hatari ya simulizi moja" Dialogue: 0,0:00:10.75,0:00:13.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilikulia mazingira ya chuo\Nkikuu magharibi mwa Nigeria Dialogue: 0,0:00:14.16,0:00:17.47,Default,,0000,0000,0000,,Mama yangu anasema nilianza kusoma\Nnikiwa na miaka miwili Dialogue: 0,0:00:17.49,0:00:20.51,Default,,0000,0000,0000,,japo nadhani miaka minne ni sahihi zaidi Dialogue: 0,0:00:21.75,0:00:23.56,Default,,0000,0000,0000,,Niliwahi sana kuanza kusoma Dialogue: 0,0:00:23.59,0:00:26.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilisoma vitabu vya watoto vya Uingereza\Nna Marekani Dialogue: 0,0:00:27.71,0:00:29.98,Default,,0000,0000,0000,,Pia nilianza kuandika katika umri mdogo Dialogue: 0,0:00:30.00,0:00:33.98,Default,,0000,0000,0000,,Na nilipoanza kuandika,\Nnikiwa na takriban miaka saba, Dialogue: 0,0:00:34.00,0:00:36.05,Default,,0000,0000,0000,,hadithi za penseli na michoro ya rangi Dialogue: 0,0:00:36.07,0:00:39.60,Default,,0000,0000,0000,,ambazo mama yangu alilazimika kuzisoma, Dialogue: 0,0:00:39.63,0:00:43.20,Default,,0000,0000,0000,,niliandika hadithi\Nsawa na zile nilizokuwa nazisoma: Dialogue: 0,0:00:43.22,0:00:47.98,Default,,0000,0000,0000,,Wahusika wangu wote \Nwalikuwa wazungu na wenye macho ya bluu. Dialogue: 0,0:00:48.00,0:00:50.31,Default,,0000,0000,0000,,Walicheza katika theluji. Dialogue: 0,0:00:50.33,0:00:52.42,Default,,0000,0000,0000,,Walikula matofaa Dialogue: 0,0:00:52.44,0:00:53.84,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:00:54.01,0:00:56.02,Default,,0000,0000,0000,,Na walizungumza sana kuhusu hali ya hewa, Dialogue: 0,0:00:56.05,0:00:58.18,Default,,0000,0000,0000,,jinsi ilivyo vizuri kuona jua limechomoza. Dialogue: 0,0:00:58.41,0:01:00.37,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:01:00.40,0:01:03.53,Default,,0000,0000,0000,,Yote haya,ingawa niliishi Nigeria. Dialogue: 0,0:01:03.56,0:01:05.33,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa sijawahi kwenda nje ya Nigeria. Dialogue: 0,0:01:07.14,0:01:10.40,Default,,0000,0000,0000,,Hatukuwa na theluji, tulikula maembe. Dialogue: 0,0:01:10.43,0:01:12.28,Default,,0000,0000,0000,,Na hatukuzungumza kuhusu hali ya hewa, Dialogue: 0,0:01:12.30,0:01:13.98,Default,,0000,0000,0000,,sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo. Dialogue: 0,0:01:14.27,0:01:16.98,Default,,0000,0000,0000,,Wahusika wangu pia\Nwalikunywa sana bia ya tangawizi Dialogue: 0,0:01:17.00,0:01:19.38,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu wahusika \Nkatika vitabu vya Uingereza Dialogue: 0,0:01:19.40,0:01:20.98,Default,,0000,0000,0000,,walikunywa bia ya tangawizi. Dialogue: 0,0:01:21.30,0:01:23.98,Default,,0000,0000,0000,,Ijapokuwa \Nsikuifahamu bia ya tangawizi Dialogue: 0,0:01:24.00,0:01:25.53,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:01:25.56,0:01:27.00,Default,,0000,0000,0000,,Na kwa miaka mingi baadaye Dialogue: 0,0:01:27.03,0:01:29.98,Default,,0000,0000,0000,,nilikuwa na shauku\Nya kuonja bia ya tangawizi. Dialogue: 0,0:01:30.48,0:01:31.98,Default,,0000,0000,0000,,Lakini hiyo ni hadithi nyingine. Dialogue: 0,0:01:32.00,0:01:34.48,Default,,0000,0000,0000,,Ambacho hii inaonyesha,nafikiri\N Dialogue: 0,0:01:34.51,0:01:37.36,Default,,0000,0000,0000,,Ni namna tulivyo wajinga na wanyonge Dialogue: 0,0:01:37.38,0:01:38.98,Default,,0000,0000,0000,,Tunapokabiliana na simulizi Dialogue: 0,0:01:39.00,0:01:40.38,Default,,0000,0000,0000,,hasa hasa kama watoto Dialogue: 0,0:01:41.64,0:01:45.41,Default,,0000,0000,0000,,Sababu nilisoma vitabu\Nvyenye wahusika wa kigeni Dialogue: 0,0:01:45.43,0:01:47.55,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa nimeaminishwa kwamba vitabu Dialogue: 0,0:01:47.58,0:01:50.75,Default,,0000,0000,0000,,kwa asili lazima \Nviwe na wahusika wageni Dialogue: 0,0:01:50.77,0:01:54.49,Default,,0000,0000,0000,,Na vielezo kuhusu mambo ambayo\Nbinafsi siyafahamu Dialogue: 0,0:01:55.60,0:01:58.22,Default,,0000,0000,0000,,Mambo yalibadilika\NNilipopata vitabu vya Afrika Dialogue: 0,0:01:59.00,0:02:00.98,Default,,0000,0000,0000,,havikuwepo kwa wingi Dialogue: 0,0:02:01.00,0:02:03.87,Default,,0000,0000,0000,,Na haikuwa rahisi kuvipata\Nkama vya kigeni\N Dialogue: 0,0:02:03.89,0:02:06.98,Default,,0000,0000,0000,,Lakini sababu ya waandishi\Nkama Chinua Achebe na Camara Laye Dialogue: 0,0:02:07.00,0:02:10.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilipata badiliko la akili\Nninavyoiona fasihi Dialogue: 0,0:02:11.00,0:02:13.21,Default,,0000,0000,0000,,Niligundua kwamba watu kama mimi, Dialogue: 0,0:02:13.24,0:02:15.24,Default,,0000,0000,0000,,wasichana weusi Dialogue: 0,0:02:15.27,0:02:18.53,Default,,0000,0000,0000,,wenye nywele ngumu Dialogue: 0,0:02:18.56,0:02:20.36,Default,,0000,0000,0000,,pia wapo katika fasihi. Dialogue: 0,0:02:20.68,0:02:23.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilianza kuandika \Nvitu nilivyovifahamu Dialogue: 0,0:02:24.74,0:02:27.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa navipenda hivyo vitabu\Nvya Marekani na Uingereza Dialogue: 0,0:02:28.00,0:02:31.98,Default,,0000,0000,0000,,Viliamsha fikra zangu\NVilifunua vitu vipya. Dialogue: 0,0:02:32.00,0:02:33.98,Default,,0000,0000,0000,,Lakini matokeo yasiyokusudiwa Dialogue: 0,0:02:34.00,0:02:36.05,Default,,0000,0000,0000,,yalikuwa; sikufahamu kuwa\Nwatu kama mimi Dialogue: 0,0:02:36.07,0:02:37.50,Default,,0000,0000,0000,,waweza kuwepo katika fasihi. Dialogue: 0,0:02:38.45,0:02:41.98,Default,,0000,0000,0000,,hivyo ufumbuzi wa waandishi Waafrika: Dialogue: 0,0:02:42.00,0:02:45.88,Default,,0000,0000,0000,,Uliniokoa na mtazamo mmoja\Njuu ya vitabu Dialogue: 0,0:02:47.00,0:02:49.98,Default,,0000,0000,0000,,Ninatoka kwenye familia\Nya kawaida Dialogue: 0,0:02:50.00,0:02:51.98,Default,,0000,0000,0000,,Baba yangu alikuwa mhadhiri Dialogue: 0,0:02:52.38,0:02:54.07,Default,,0000,0000,0000,,Mama yangu ni\Nafisa wa utawala Dialogue: 0,0:02:55.37,0:02:58.17,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo kama kawaida, tulikuwa na, Dialogue: 0,0:02:58.20,0:03:02.54,Default,,0000,0000,0000,,mtumishi wa nyumbani\Nanayetoka vijiji vya jirani Dialogue: 0,0:03:03.18,0:03:06.47,Default,,0000,0000,0000,,Nilipokuwa na miaka nane\Ntulipata mtumishi wa kiume Dialogue: 0,0:03:07.10,0:03:08.36,Default,,0000,0000,0000,,Jina lake aliitwa Fide Dialogue: 0,0:03:09.66,0:03:13.96,Default,,0000,0000,0000,,Mama alituambia kuwa familia\Nyake ni masikini sana Dialogue: 0,0:03:15.00,0:03:19.98,Default,,0000,0000,0000,,Mama alituma magimbi na mchele\Nna nguo zetu za zamani kwa familia yao Dialogue: 0,0:03:20.00,0:03:22.62,Default,,0000,0000,0000,,Na niliposhindwa kumaliza chakula\Nmama alisema, Dialogue: 0,0:03:22.64,0:03:26.98,Default,,0000,0000,0000,,"Maliza chakula! kuna watu\Nambao hawana chochote Dialogue: 0,0:03:27.00,0:03:30.98,Default,,0000,0000,0000,,Niliwahurumia sana\Nfamilia ya Fide Dialogue: 0,0:03:31.58,0:03:34.47,Default,,0000,0000,0000,,Jumamosi moja tukaenda\Nkijijini kwao kutembelea Dialogue: 0,0:03:34.50,0:03:37.98,Default,,0000,0000,0000,,na mama yake akatuonyesha\Nkikapu kizuri Dialogue: 0,0:03:38.00,0:03:40.98,Default,,0000,0000,0000,,kilichosukwa kwa ukili uliopakwa rangi\Nna kaka yake Fide Dialogue: 0,0:03:41.00,0:03:42.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilishangaa Dialogue: 0,0:03:43.00,0:03:45.98,Default,,0000,0000,0000,,Sikudhani kuwa yeyote katika familia yake Dialogue: 0,0:03:46.00,0:03:48.98,Default,,0000,0000,0000,,angeweza kutengeneza chochote Dialogue: 0,0:03:49.00,0:03:51.98,Default,,0000,0000,0000,,yote niliyowahi kusikia kuhusu wao\Nni namna walivyo masikini Dialogue: 0,0:03:52.00,0:03:56.47,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwangu\Nkuwaona tofauti na umasikini wao Dialogue: 0,0:03:57.14,0:03:59.51,Default,,0000,0000,0000,,umasikini wao ilikuwa\Nni simulizi moja kwangu Dialogue: 0,0:04:01.00,0:04:03.52,Default,,0000,0000,0000,,baadaye niliwaza hili \Nnilipotoka Nigeria Dialogue: 0,0:04:03.55,0:04:06.23,Default,,0000,0000,0000,,Kwenda Marekani kusoma\Nchuo kikuu Dialogue: 0,0:04:06.34,0:04:07.67,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa na miaka 19 Dialogue: 0,0:04:08.42,0:04:11.20,Default,,0000,0000,0000,,Mmarekani niliyekuwa\Nnaishi naye chumba kimoja alinishangaa Dialogue: 0,0:04:12.00,0:04:15.59,Default,,0000,0000,0000,,Aliuliza wapi nimefunza \Nkuzungumza kiingereza vizuri Dialogue: 0,0:04:15.61,0:04:17.70,Default,,0000,0000,0000,,Alishangaa nilipomwambia kuwa Nigeria Dialogue: 0,0:04:17.72,0:04:20.44,Default,,0000,0000,0000,,wanatumia kiingereza kama lugha ya taifa Dialogue: 0,0:04:21.75,0:04:25.98,Default,,0000,0000,0000,,Aliomba kusikiliza "nyimbo za kikabila" Dialogue: 0,0:04:26.00,0:04:27.98,Default,,0000,0000,0000,,na alipigwa butwaa vile vile Dialogue: 0,0:04:28.00,0:04:29.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilipompa kanda yangu ya Mariah Carey Dialogue: 0,0:04:30.00,0:04:32.98,Default,,0000,0000,0000,,(kicheko) Dialogue: 0,0:04:33.00,0:04:36.69,Default,,0000,0000,0000,,Alidhani kuwa sifahamu\Nkutumia jiko la umeme Dialogue: 0,0:04:37.78,0:04:39.04,Default,,0000,0000,0000,,Kilichonishangaza mimi ni hiki Dialogue: 0,0:04:39.06,0:04:42.14,Default,,0000,0000,0000,,Alikuwa ananihurimia\Nhata kabla ya kuniona Dialogue: 0,0:04:42.53,0:04:45.98,Default,,0000,0000,0000,,Mtazamo wake mbovu,\Nkunihusu, kama Mwafrika, Dialogue: 0,0:04:46.00,0:04:49.04,Default,,0000,0000,0000,,Ulikuwa wa huruma ya kudhalilisha,\Nyenye kujali Dialogue: 0,0:04:50.00,0:04:53.50,Default,,0000,0000,0000,,Alikuwa na simulizi moja\Nkuhusu Afrika: Dialogue: 0,0:04:53.62,0:04:55.98,Default,,0000,0000,0000,,Simulizi ya majanga. Dialogue: 0,0:04:56.41,0:04:57.70,Default,,0000,0000,0000,,Kwenye simulizi hii moja, Dialogue: 0,0:04:57.72,0:05:01.98,Default,,0000,0000,0000,,Hakukuwa na uwezekano wa Mwafrika\Nkufanana naye kwa namna yeyote, Dialogue: 0,0:05:02.00,0:05:04.98,Default,,0000,0000,0000,,Hakukuwa na uwezekano wa hisia\Nngumu zaidi ya huruma, Dialogue: 0,0:05:05.00,0:05:08.98,Default,,0000,0000,0000,,Hakukuwa na uwezekano wa ushirikiano\Nkama binadamu walio sawa. Dialogue: 0,0:05:09.00,0:05:11.12,Default,,0000,0000,0000,,Lazima niseme kuwa\Nkabla ya kwenda Marekani, Dialogue: 0,0:05:11.15,0:05:13.43,Default,,0000,0000,0000,,Sikuwa nikijitambua kwa undani\Nkama Mwafrika. Dialogue: 0,0:05:14.00,0:05:16.98,Default,,0000,0000,0000,,Lakini Marekani, popote Afrika ilipotajwa,\Nwatu walinigeukia. Dialogue: 0,0:05:17.00,0:05:19.75,Default,,0000,0000,0000,,Bila kujali kuwa sifahamu chochote\Nkuhusu nchi kama Namibia. Dialogue: 0,0:05:21.00,0:05:23.10,Default,,0000,0000,0000,,Lakini nilikuja kuupokea\Nhuu utambulisho mpya, Dialogue: 0,0:05:23.12,0:05:25.98,Default,,0000,0000,0000,,Na kwa namna nyingi sasa \Nninajitazama kama Mwafrika. Dialogue: 0,0:05:26.00,0:05:29.98,Default,,0000,0000,0000,,Ijapokuwa bado ninakasirishwa sana\Npale Afrika inapoelezewa kama ni nchi Dialogue: 0,0:05:30.00,0:05:33.98,Default,,0000,0000,0000,,Mfano wa karibu, ni safari yangu ya ndege Dialogue: 0,0:05:34.00,0:05:35.28,Default,,0000,0000,0000,,Kutoka Lagos hivi juzi, Dialogue: 0,0:05:35.31,0:05:38.19,Default,,0000,0000,0000,,Ambapo kulikuwa na tangazo Dialogue: 0,0:05:38.22,0:05:42.98,Default,,0000,0000,0000,,Kuhusu kazi ya kujitolea kule\N"India, Afika na nchi nyingine" Dialogue: 0,0:05:43.00,0:05:44.32,Default,,0000,0000,0000,,Kicheko Dialogue: 0,0:05:44.48,0:05:47.98,Default,,0000,0000,0000,,Baada ya kuishi Marekani kama Mwafrica Dialogue: 0,0:05:48.00,0:05:51.17,Default,,0000,0000,0000,,Nikaanza kuelewa mwitikio wa \Nniliyekuwa naishi naye chumba kimoja Dialogue: 0,0:05:52.00,0:05:54.02,Default,,0000,0000,0000,,kama sikukulia Nigeria Dialogue: 0,0:05:54.05,0:05:57.19,Default,,0000,0000,0000,,Na kama kila nilichofahamu kuhusu Afrika \Nkilitokana na picha maarufu Dialogue: 0,0:05:57.21,0:06:02.39,Default,,0000,0000,0000,,Mimi pia ningedhani kuwa Africa ni mahali\Npenye mandhari nzuri, Dialogue: 0,0:06:02.41,0:06:03.98,Default,,0000,0000,0000,,Wanyama wa kupendeza, Dialogue: 0,0:06:04.00,0:06:05.98,Default,,0000,0000,0000,,na watu wasioeleweka, Dialogue: 0,0:06:06.00,0:06:09.63,Default,,0000,0000,0000,,wapiganao vita visivyo na maana,\Nwanaokufa na umasikini na UKIMWI Dialogue: 0,0:06:09.66,0:06:11.98,Default,,0000,0000,0000,,wasioweza kujisemea Dialogue: 0,0:06:12.00,0:06:16.16,Default,,0000,0000,0000,,wanaosubiri kusaidiwa na\Nmtu mweupe, mgeni mwenye ukarimu Dialogue: 0,0:06:16.93,0:06:19.10,Default,,0000,0000,0000,,Ningewaona waafrika\Nkwa namna ile ambayo mimi, Dialogue: 0,0:06:19.12,0:06:21.82,Default,,0000,0000,0000,,nilipokuwa mtoto,\Nniliiona familia ya Fide Dialogue: 0,0:06:23.00,0:06:26.98,Default,,0000,0000,0000,,Hii simulizi moja kuhusu Afrika\Nnadhani inatokana na fasihi za magharibi Dialogue: 0,0:06:27.00,0:06:31.98,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, huu ni msemo kutoka katika uandishi\Nwa mfanyabiashara wa London aitwaye John Lok, Dialogue: 0,0:06:32.00,0:06:34.98,Default,,0000,0000,0000,,aliyesafiri kwa maji kuelekea \NAfrika magharibi mwaka 1561 Dialogue: 0,0:06:35.00,0:06:38.66,Default,,0000,0000,0000,,na aliweka hazina ya kuvutia \Nkutokana na safari yake. Dialogue: 0,0:06:40.20,0:06:43.98,Default,,0000,0000,0000,,Baada ya kuwaita Waafrika weusi kama\N" hayawani wasio na nyumba," Dialogue: 0,0:06:44.00,0:06:47.98,Default,,0000,0000,0000,,aliandika,"Pia kuna watu wasio na vichwa, Dialogue: 0,0:06:48.00,0:06:51.97,Default,,0000,0000,0000,,midomo na macho yao\Nyapo katika vifua vyao." Dialogue: 0,0:06:53.00,0:06:55.10,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, nilicheka kila \Nnikisoma haya maneno. Dialogue: 0,0:06:55.12,0:06:58.50,Default,,0000,0000,0000,,Na lazima mtu \Natakubaliana na fikira za John Lok. Dialogue: 0,0:06:59.37,0:07:01.24,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kipi ni muhimu \Nkuhusu uandishi wake Dialogue: 0,0:07:01.26,0:07:02.98,Default,,0000,0000,0000,,ni kwamba inawakilisha mwanzo Dialogue: 0,0:07:03.00,0:07:05.98,Default,,0000,0000,0000,,wa utamaduni wa kuelezea hadithi \Nza Afrika kwa Magharibi: Dialogue: 0,0:07:06.00,0:07:09.37,Default,,0000,0000,0000,,Utamaduni wa kusini mwa jangwa la Sahara\Nkama sehemu isiyofaa, Dialogue: 0,0:07:09.48,0:07:11.63,Default,,0000,0000,0000,,yenye utofauti, yenye kiza, Dialogue: 0,0:07:11.66,0:07:16.98,Default,,0000,0000,0000,,ya watu ambao, kutokana na maneno ya\Nmshairi bora aitwaye Rudyard Kipling, Dialogue: 0,0:07:17.00,0:07:18.94,Default,,0000,0000,0000,,ni "nusu shetani, nusu watoto." Dialogue: 0,0:07:20.21,0:07:22.98,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo, nilianza kuelewa kwamba mwanafunzi\NMmarekani ninayeshirikiana nae chumba Dialogue: 0,0:07:23.00,0:07:24.98,Default,,0000,0000,0000,,lazima katika maisha yake Dialogue: 0,0:07:25.00,0:07:28.98,Default,,0000,0000,0000,,atakuwa ameona na kusikia \Nnamna mbalimbali za hii hadithi moja, Dialogue: 0,0:07:29.00,0:07:30.98,Default,,0000,0000,0000,,kama ilivyo kwa profesa, Dialogue: 0,0:07:31.00,0:07:34.77,Default,,0000,0000,0000,,ambaye aliwahi niambia kuwa \Nriwaya yangu haikuwa "na uhalisia wa Kiafrika," Dialogue: 0,0:07:35.87,0:07:37.56,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, nilikubaliana na kuchanganua Dialogue: 0,0:07:37.58,0:07:40.68,Default,,0000,0000,0000,,kwamba kulikuwa na baadhi ya vitu \Nambavyo si sawa katika riwaya hii, Dialogue: 0,0:07:40.70,0:07:43.98,Default,,0000,0000,0000,,na kuwa nilifeli katika maeneo mbalimbali, Dialogue: 0,0:07:44.00,0:07:46.24,Default,,0000,0000,0000,,lakini sikufiria kwamba ilifeli Dialogue: 0,0:07:46.26,0:07:48.98,Default,,0000,0000,0000,,katika kutekeleza \Nuhalisia wake wa Kiafrika. Dialogue: 0,0:07:49.00,0:07:52.71,Default,,0000,0000,0000,,Kiukweli, sikufahamu \Nuhalisia wa Kiafrika ni upi. Dialogue: 0,0:07:54.00,0:07:58.40,Default,,0000,0000,0000,,Profesa alinielezza kwamba wahusika kwenye riwaya\Nwalikuwa wanafanana mno kama yeye, Dialogue: 0,0:07:58.42,0:08:00.40,Default,,0000,0000,0000,,msomi aliye katika maisha ya kati. Dialogue: 0,0:08:00.42,0:08:02.52,Default,,0000,0000,0000,,Wahusika wangu waliendesha magari. Dialogue: 0,0:08:02.55,0:08:04.98,Default,,0000,0000,0000,,Hawakuwa wanashinda na njaa. Dialogue: 0,0:08:05.00,0:08:07.93,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo hawakuwa Waafrika halisi. Dialogue: 0,0:08:09.00,0:08:11.98,Default,,0000,0000,0000,,Lakini niongeze haraka-haraka \Nkwamba najisikia hatia Dialogue: 0,0:08:12.00,0:08:14.07,Default,,0000,0000,0000,,katika swali la la hadithi iliyo moja. Dialogue: 0,0:08:15.00,0:08:17.99,Default,,0000,0000,0000,,Miaka michache iliyopita, \Nnilitembelea Mexico nikitokea Marekani. Dialogue: 0,0:08:19.00,0:08:21.67,Default,,0000,0000,0000,,Hali ya kisiasa nchini Marekani \Nwakati huo ilikuwa tete, Dialogue: 0,0:08:21.69,0:08:24.98,Default,,0000,0000,0000,,kulikuwa na majadiliano yanayoendelea \Nkuhusu uhamiaji. Dialogue: 0,0:08:25.00,0:08:26.98,Default,,0000,0000,0000,,Na, mara kwa mara hutokea Marekani, Dialogue: 0,0:08:27.00,0:08:29.98,Default,,0000,0000,0000,,neno uhamiaji likaja kuwa \Nlinahusishwa na watu wenye asili ya Mexico. Dialogue: 0,0:08:30.70,0:08:32.63,Default,,0000,0000,0000,,Kulikuwa na hadithi ndefu \Nkuhusu Wamexico Dialogue: 0,0:08:32.66,0:08:35.98,Default,,0000,0000,0000,,kama watu wanaonyonya mfumo wa afya, Dialogue: 0,0:08:36.00,0:08:37.98,Default,,0000,0000,0000,,wanajipenyeza kwenye mipaka, Dialogue: 0,0:08:38.00,0:08:40.46,Default,,0000,0000,0000,,wanakamatwa kwenye mipaka,\Nvitu kama hivyo. Dialogue: 0,0:08:42.16,0:08:45.98,Default,,0000,0000,0000,,Nakumbuka siku ya kwanza nilipokuwa natembea\Neneo liitwalo Guadalajara, Dialogue: 0,0:08:46.00,0:08:47.98,Default,,0000,0000,0000,,nikiwaangalia watu wakielekea makazini, Dialogue: 0,0:08:48.00,0:08:49.98,Default,,0000,0000,0000,,wakitengeneza tortilla maeneo ya sokoni, Dialogue: 0,0:08:50.00,0:08:51.97,Default,,0000,0000,0000,,wakivuta sigara, wakicheka. Dialogue: 0,0:08:53.20,0:08:55.98,Default,,0000,0000,0000,,Nakumbuka kwa mara ya kwanza \Nnilipatwa na mshangao kidogo. Dialogue: 0,0:08:56.00,0:08:58.98,Default,,0000,0000,0000,,Kisha, nikagubikwa na aibu. Dialogue: 0,0:08:59.34,0:09:03.98,Default,,0000,0000,0000,,Nikatambua ya kwamba nimezama sana katika habari zinazoelezea watu wa Mexico Dialogue: 0,0:09:04.00,0:09:06.00,Default,,0000,0000,0000,,ambao wamekuwa jambo katika akili yangu, Dialogue: 0,0:09:06.02,0:09:07.85,Default,,0000,0000,0000,,wahamiaji duni, Dialogue: 0,0:09:08.77,0:09:11.19,Default,,0000,0000,0000,,nilidanganyika katika hadithi moja\Nya watu wa Mexico Dialogue: 0,0:09:11.22,0:09:13.72,Default,,0000,0000,0000,,na sikuweza kujisikia aibu zaidi. Dialogue: 0,0:09:14.07,0:09:16.62,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo hiyo ndiyo\Nnamna ya kutengeneza hadithi moja. Dialogue: 0,0:09:16.64,0:09:18.98,Default,,0000,0000,0000,,kuwaeleza watu kama jambo moja, Dialogue: 0,0:09:19.00,0:09:20.98,Default,,0000,0000,0000,,kama jambo moja tu, Dialogue: 0,0:09:21.00,0:09:22.98,Default,,0000,0000,0000,,tena na tena, Dialogue: 0,0:09:23.00,0:09:24.52,Default,,0000,0000,0000,,na hivyo ndivyo watakavyokuwa. Dialogue: 0,0:09:25.79,0:09:28.24,Default,,0000,0000,0000,,Haiwezekani kuongelea kuhusu hadithi moja Dialogue: 0,0:09:28.26,0:09:29.95,Default,,0000,0000,0000,,bila kuongelea kuhusu uwezo ya mamlaka. Dialogue: 0,0:09:31.50,0:09:33.24,Default,,0000,0000,0000,,Kuna neno, neno la lugha ya Igbo, Dialogue: 0,0:09:33.27,0:09:36.92,Default,,0000,0000,0000,,ambalo huwa naliwaza kila nikifikiria \Nmfumo wa mamlaka wa dunia, Dialogue: 0,0:09:36.94,0:09:38.13,Default,,0000,0000,0000,,na hili "nkali". Dialogue: 0,0:09:38.33,0:09:42.98,Default,,0000,0000,0000,,Ni nomino ambayo inatafsiriwa kama \N"kuwa juu zaidi ya mwigine." Dialogue: 0,0:09:43.55,0:09:46.48,Default,,0000,0000,0000,,Kama ulivyo ulimwengu wa\Nkiuchumi na kisiasa, Dialogue: 0,0:09:46.51,0:09:50.98,Default,,0000,0000,0000,,hadithi pia huelezwa kwa kanuni ya nkali: Dialogue: 0,0:09:51.00,0:09:52.98,Default,,0000,0000,0000,,Zinaelezwaje, nani anaelezea, Dialogue: 0,0:09:53.00,0:09:56.24,Default,,0000,0000,0000,,wakati gani zilielezwa,\Nhadithi ngapi zinaelezwa, Dialogue: 0,0:09:56.26,0:09:58.47,Default,,0000,0000,0000,,haya yote yanategemea sana \Nnguvu ya mamlaka. Dialogue: 0,0:10:00.00,0:10:03.14,Default,,0000,0000,0000,,Mamlaka ni uwezo sio tu wa kueleza\Nhadithi ya kuhusu mtu mwingine, Dialogue: 0,0:10:03.17,0:10:06.98,Default,,0000,0000,0000,,lakini kuifanya iwe hadithi mahususi\Nkuhusu mtu huyo. Dialogue: 0,0:10:07.00,0:10:09.10,Default,,0000,0000,0000,,Mshairi wa Kipalestina\NMourid Barghouti aliandika Dialogue: 0,0:10:09.12,0:10:11.98,Default,,0000,0000,0000,,kwamba kama unataka kuwaondoa watu, Dialogue: 0,0:10:12.00,0:10:14.98,Default,,0000,0000,0000,,njia rahisi ya kufanya hivyo \Nni kuelezea hadithi yao Dialogue: 0,0:10:15.00,0:10:17.23,Default,,0000,0000,0000,,na kuanza na, "pili." Dialogue: 0,0:10:18.48,0:10:22.38,Default,,0000,0000,0000,,Anza hadithi na mishale\Nya waliokuwa wakazi halisi wa Amerika, Dialogue: 0,0:10:22.41,0:10:24.98,Default,,0000,0000,0000,,na sio baada ya kufika kwa Waingereza, Dialogue: 0,0:10:25.00,0:10:27.98,Default,,0000,0000,0000,,na utakuwa na hadithi tofauti nyingine kabisa. Dialogue: 0,0:10:28.00,0:10:32.43,Default,,0000,0000,0000,,Anza na hadithi kuhusu \Nkuanguka kwa dola za Kiafrika, Dialogue: 0,0:10:32.46,0:10:35.98,Default,,0000,0000,0000,,na sio dola za Kiafrika \Nzilizotokana na ukoloni, Dialogue: 0,0:10:36.00,0:10:38.74,Default,,0000,0000,0000,,na utakuwa na hadithi tofauti kabisa. Dialogue: 0,0:10:40.00,0:10:41.98,Default,,0000,0000,0000,,Hivi karibun nilitoa hotuba katika chuo Dialogue: 0,0:10:42.00,0:10:45.78,Default,,0000,0000,0000,,ambapo mwanafunzi aliniambia \Nkwamba ilikuwa ni aibu Dialogue: 0,0:10:45.81,0:10:48.93,Default,,0000,0000,0000,,kwamba wanaume wa Kinigeria \Nwalikuwa wanyanyasaji Dialogue: 0,0:10:48.95,0:10:50.90,Default,,0000,0000,0000,,kama alivyo muhusika \Nambaye ni baba katika riwaya yangu. Dialogue: 0,0:10:52.00,0:10:55.98,Default,,0000,0000,0000,,Nikamwambia nimesoma riwaya \Niitwayo "Mwendawazimu wa Kiamerika" -- Dialogue: 0,0:10:56.00,0:10:57.98,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:10:58.00,0:10:59.98,Default,,0000,0000,0000,,-- na kwamba ilikuwa aibu Dialogue: 0,0:11:00.00,0:11:02.98,Default,,0000,0000,0000,,kwamba vijana wadogo wa Kiamerika \Nwalikuwa wauaji waliokubuhu. Dialogue: 0,0:11:03.00,0:11:06.98,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:11:07.00,0:11:12.98,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi) Dialogue: 0,0:11:13.00,0:11:15.98,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, kiukweli nilisema hili \Nkutokana na kukerwa. Dialogue: 0,0:11:16.00,0:11:17.98,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:11:18.00,0:11:20.19,Default,,0000,0000,0000,,Lakini isingeweza kutokea kwangu kuwaza Dialogue: 0,0:11:20.22,0:11:23.98,Default,,0000,0000,0000,,kwamba kwa sababu nimesoma riwaya \Nambayo muhusika ni muuaji wa kufululiza Dialogue: 0,0:11:24.00,0:11:27.98,Default,,0000,0000,0000,,kwamba kwa kiasi fulani \Nwanawakilisha Wamarekani wote. Dialogue: 0,0:11:28.00,0:11:30.98,Default,,0000,0000,0000,,Hii si kwamba mimi \Nni mtu bora kuliko yule mwanafunzi, Dialogue: 0,0:11:31.00,0:11:33.98,Default,,0000,0000,0000,,lakini kwa sababu ya utamaduni \Nna nguvu ya uchumi wa Marekani, Dialogue: 0,0:11:34.00,0:11:35.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilikuwa nina hadithi nyingi za Marekani. Dialogue: 0,0:11:36.00,0:11:39.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilisoma Tyler na Updike \Nna Steinbeck na Gaitskill. Dialogue: 0,0:11:40.00,0:11:42.56,Default,,0000,0000,0000,,Sikuwa na hadithi moja ya Marekani. Dialogue: 0,0:11:43.67,0:11:45.38,Default,,0000,0000,0000,,Nilipojifunza, miaka kadhaa iliyopita, Dialogue: 0,0:11:45.40,0:11:49.74,Default,,0000,0000,0000,,kwamba waandishi wanategemewa kuwa na maisha ya utotoni ambayo siyo ya furaha Dialogue: 0,0:11:49.77,0:11:51.98,Default,,0000,0000,0000,,ili kuja kufanikiwa baadaye, Dialogue: 0,0:11:52.00,0:11:56.00,Default,,0000,0000,0000,,Nilianza kuwaza ni namna gani naweza buni \Nvitu vibaya ambavyo wazazi wangu walinifanyia. Dialogue: 0,0:11:56.02,0:11:57.98,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:11:58.00,0:12:01.98,Default,,0000,0000,0000,,Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na maisha ya utoto ambayo yalikuwa ya furaha sana, Dialogue: 0,0:12:02.00,0:12:04.98,Default,,0000,0000,0000,,yaliyojaa vicheko na upendo,\Nkatika familia iliyo na ukaribu sana. Dialogue: 0,0:12:05.00,0:12:08.21,Default,,0000,0000,0000,,Lakini pia nilikuwa na mababu \Nwaliofia kwenye kambi za wakimbizi. Dialogue: 0,0:12:08.75,0:12:12.98,Default,,0000,0000,0000,,Binamu yangu Polle alifariki \Nsababu hakupata matibabu yanayostahili. Dialogue: 0,0:12:13.00,0:12:15.98,Default,,0000,0000,0000,,Mmoja wa rafiki zangu,Okoloma, \Nalifariki kwenye ajali ya ndege Dialogue: 0,0:12:16.00,0:12:18.98,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu gari zetu za zimamoto \Nhazikuwa na maji. Dialogue: 0,0:12:19.00,0:12:21.98,Default,,0000,0000,0000,,Nimekulia katika serikali ya kijeshi\Nambayo ni kandamizi Dialogue: 0,0:12:22.00,0:12:23.98,Default,,0000,0000,0000,,ambayo haikujali elimu, Dialogue: 0,0:12:24.00,0:12:26.98,Default,,0000,0000,0000,,kwa muda mwingine,\Nwazazi walikuwa hawalipwi mishahara. Dialogue: 0,0:12:27.00,0:12:30.98,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo, kama mtoto, nilianza kuona jamu hakuna mezani wakati wa kupata kifungua kinywa, Dialogue: 0,0:12:31.00,0:12:33.50,Default,,0000,0000,0000,,kisha siagi nayo ikakosekana, Dialogue: 0,0:12:33.52,0:12:35.98,Default,,0000,0000,0000,,kisha mkate ukawa ghali sana, Dialogue: 0,0:12:36.00,0:12:37.87,Default,,0000,0000,0000,,kisha maziwa yakapungua. Dialogue: 0,0:12:39.00,0:12:42.66,Default,,0000,0000,0000,,Na katika yote, hali ya hofu ya kisiasa Dialogue: 0,0:12:42.68,0:12:44.36,Default,,0000,0000,0000,,ikaingilia maisha yetu, Dialogue: 0,0:12:45.82,0:12:47.96,Default,,0000,0000,0000,,Na hadithi zote hizi zimenitengeneza mimi wa leo. Dialogue: 0,0:12:48.46,0:12:51.98,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kusisitiza katika hizi hadithi hasi Dialogue: 0,0:12:52.00,0:12:54.98,Default,,0000,0000,0000,,ni kuongeza uzoefu wangu Dialogue: 0,0:12:55.00,0:12:58.66,Default,,0000,0000,0000,,na kuachana na hadithi nyinginezo nyingi ambazo zimenitengeneza mimi. Dialogue: 0,0:12:59.39,0:13:01.98,Default,,0000,0000,0000,,Hadithi moja hutengeneza tabaka, Dialogue: 0,0:13:02.00,0:13:06.98,Default,,0000,0000,0000,,na tatizo la tabaka \Nsi kwamba hazina kweli, Dialogue: 0,0:13:07.00,0:13:08.98,Default,,0000,0000,0000,,lakini hazijakamilika. Dialogue: 0,0:13:09.36,0:13:11.96,Default,,0000,0000,0000,,Hufanya hadithi moja kuwa hadithi pekee. Dialogue: 0,0:13:13.00,0:13:15.57,Default,,0000,0000,0000,,Hakika, Afrika ni bara \Nambalo limejaa majanga: Dialogue: 0,0:13:15.60,0:13:18.98,Default,,0000,0000,0000,,Kuna majanga yaliyo makubwa,\Nkama ubakaji wa kutisha nchini Congo Dialogue: 0,0:13:19.00,0:13:20.63,Default,,0000,0000,0000,,na wa kudidimiza, Dialogue: 0,0:13:20.65,0:13:25.15,Default,,0000,0000,0000,,kama ukweli kwamba watu 5000 wanaomba \Nnafasi moja ya kazi nchini Nigeria. Dialogue: 0,0:13:26.00,0:13:29.56,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kuna hadithi nyingine \Nambazo hazihusiani na majanga, Dialogue: 0,0:13:29.59,0:13:32.98,Default,,0000,0000,0000,,na ni muhimu sana, ni namna kuziongelea. Dialogue: 0,0:13:33.00,0:13:34.98,Default,,0000,0000,0000,,Wakati wote nimekuwa nikihisi haiwezekani Dialogue: 0,0:13:35.00,0:13:37.98,Default,,0000,0000,0000,,kujiunga kwa utaratibu na sehemu au mtu Dialogue: 0,0:13:38.00,0:13:41.98,Default,,0000,0000,0000,,bila kuhusiana na hadithi zote\Nza mahala pale au mtu huyo. Dialogue: 0,0:13:42.00,0:13:45.58,Default,,0000,0000,0000,,Madhara ya hadithi moja ni kwamba: Dialogue: 0,0:13:45.60,0:13:47.56,Default,,0000,0000,0000,,Hunyang'anya watu wa heshima. Dialogue: 0,0:13:48.33,0:13:51.98,Default,,0000,0000,0000,,Hufanya utambuzi wetu\Nwa usawa wa kibinadamu kuwa mgumu. Dialogue: 0,0:13:52.00,0:13:56.16,Default,,0000,0000,0000,,Husisitiza ni jinsi gani tulivyo tofauti \Nkuliko vile tulivyo sawa. Dialogue: 0,0:13:57.00,0:13:59.49,Default,,0000,0000,0000,,Inakuwaje wakati\Nkabla ya safari yangu ya Mexico, Dialogue: 0,0:13:59.51,0:14:02.98,Default,,0000,0000,0000,,Ningefatilia majadiliano ya uhamiaji \Nkutoka pande zote, Dialogue: 0,0:14:03.00,0:14:04.98,Default,,0000,0000,0000,,upande wa Marekani na wa Mexico? Dialogue: 0,0:14:05.00,0:14:08.98,Default,,0000,0000,0000,,Ingekuwaje kama mama yangu angeniambia \Nfamilia ya Fide ilikuwa masikini Dialogue: 0,0:14:09.00,0:14:10.98,Default,,0000,0000,0000,,na ya wachapakazi? Dialogue: 0,0:14:11.00,0:14:13.10,Default,,0000,0000,0000,,Inakuwaje kama tungekuwa\Nna mtandao wa televisheni wa Kiafrika Dialogue: 0,0:14:13.12,0:14:16.98,Default,,0000,0000,0000,,ambao unarusha vipindi \Nvya hadithi za Afrika duniani kote? Dialogue: 0,0:14:17.00,0:14:21.33,Default,,0000,0000,0000,,Kitu ambacho muandishi wa Kinigeria Chinua Achebe\Nanaita "usawa wa hadithi." Dialogue: 0,0:14:21.36,0:14:25.33,Default,,0000,0000,0000,,Inakuweaje kama mwanafunzi niliyeishi naye chumba kimoja angefahamu kuhusu mchapishaji wangu wa Kinigeria, Dialogue: 0,0:14:25.36,0:14:26.98,Default,,0000,0000,0000,,Muhtar Bakare, Dialogue: 0,0:14:27.00,0:14:29.05,Default,,0000,0000,0000,,mtu wa kipekee ambaye \Naliacha kazi ya benki Dialogue: 0,0:14:29.07,0:14:31.98,Default,,0000,0000,0000,,na kufuata ndoto zake \Nna kuanzisha nyumba ya uchapishaji Dialogue: 0,0:14:32.00,0:14:35.69,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, hekima iliyozoeleka ilikuwa kwamba \NWanigeria huwa hawasomi fasihi. Dialogue: 0,0:14:35.71,0:14:36.97,Default,,0000,0000,0000,,Yeye alikataa. Dialogue: 0,0:14:36.99,0:14:40.08,Default,,0000,0000,0000,,Alihisi kwamba watu \Nambao wanaweza kusoma, wangesoma, Dialogue: 0,0:14:40.10,0:14:43.98,Default,,0000,0000,0000,,kama ungefanya kazi ya fasihi iwe katika bei nafuu na kupatikana kiurahisi. Dialogue: 0,0:14:44.67,0:14:46.98,Default,,0000,0000,0000,,Muda mfupi baada ya kuchapisha\Nriwaya yangu ya kwanza, Dialogue: 0,0:14:47.00,0:14:49.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilikwenda kwenye kituo cha televisheni \Nkilichopo Lagos kwa ajili ya mahojiano, Dialogue: 0,0:14:50.00,0:14:53.19,Default,,0000,0000,0000,,na mwanamke ambaye anafanya kazi pale kama karani alinifata na kusema, Dialogue: 0,0:14:53.22,0:14:55.98,Default,,0000,0000,0000,,"Nimependa sana riwaya yako. \NSijapenda mwishoni mwake. Dialogue: 0,0:14:56.00,0:14:59.24,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, ni lazima uandike muendelezo \Nna hiki ndicho kitatokea ..." Dialogue: 0,0:14:59.26,0:15:01.98,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:15:02.00,0:15:04.98,Default,,0000,0000,0000,,Na alipoendelea kunielezea \Nkipi cha kuandika kwenye muendelezo. Dialogue: 0,0:15:05.56,0:15:07.98,Default,,0000,0000,0000,,Si kwamba nilivutiwa tu, \Nlakini pia nilisisimka. Dialogue: 0,0:15:08.00,0:15:10.98,Default,,0000,0000,0000,,Huyu ni mwanamke, mmoja wa watu wengi \Nwa kawaida waliopo Nigeria, Dialogue: 0,0:15:11.00,0:15:13.00,Default,,0000,0000,0000,,ambao hawakutakiwa kuwa wasomaji. Dialogue: 0,0:15:13.90,0:15:15.52,Default,,0000,0000,0000,,Si kwamba alisoma tu kitabu, Dialogue: 0,0:15:15.55,0:15:17.36,Default,,0000,0000,0000,,lakini pia alikimiliki Dialogue: 0,0:15:17.38,0:15:20.48,Default,,0000,0000,0000,,na aliona ana haki kuaniambia \Nkitu cha kuandika katika muendelezo. Dialogue: 0,0:15:21.58,0:15:24.98,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, ingekuwaje kama mwanafunzi niishiye nae chumba kimoja angejua kuhusu rafiki yangu Funmi Lyanda, Dialogue: 0,0:15:25.00,0:15:27.98,Default,,0000,0000,0000,,mwanamke jasiri ambaye anaongoza \Nkipindi cha televisheni Lagos, Dialogue: 0,0:15:28.00,0:15:31.00,Default,,0000,0000,0000,,na anadhamiria kuelezea hadithi \Nambazo tunapendelea kuzisahau? Dialogue: 0,0:15:31.70,0:15:34.98,Default,,0000,0000,0000,,Inakuwaje kama mwenzangu \Nangetambua kuhusu upasuaji wa moyo Dialogue: 0,0:15:35.00,0:15:37.98,Default,,0000,0000,0000,,ambao ulifanyika wiki iliyopita \Njijini Lagos? Dialogue: 0,0:15:38.00,0:15:41.98,Default,,0000,0000,0000,,Inakuwaje angefahamu \Nkuhusu muziki wa kisasa kwa Kinigeria, Dialogue: 0,0:15:42.00,0:15:44.98,Default,,0000,0000,0000,,watu wenye vipaji wanaoimba \Nkatika lugha za Kiingereza na pijini, Dialogue: 0,0:15:45.00,0:15:46.98,Default,,0000,0000,0000,,na Kiigbo na Kiyoruba na Kiijo, Dialogue: 0,0:15:47.00,0:15:50.98,Default,,0000,0000,0000,,wakichanganya ushawishi \Nkutoka kwa Jay Z hadi kwa Fela Dialogue: 0,0:15:51.00,0:15:53.18,Default,,0000,0000,0000,,kwenda kwa Bob Marley na babu zao. Dialogue: 0,0:15:54.00,0:15:56.24,Default,,0000,0000,0000,,Inakuwaje kama angejua \Nkuhusu wakili mwanamke Dialogue: 0,0:15:56.26,0:15:59.98,Default,,0000,0000,0000,,ambaye hivi karibuni alienda mahakamani nchini Nigeria kuipa changamoto sheria isiyo na maana Dialogue: 0,0:16:00.00,0:16:02.98,Default,,0000,0000,0000,,ambayo inawataka wanawake \Nkupewa ruhusa na waume zao Dialogue: 0,0:16:03.00,0:16:05.98,Default,,0000,0000,0000,,kabla ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria? Dialogue: 0,0:16:06.00,0:16:08.98,Default,,0000,0000,0000,,Inakuwaje kama angefahamu kuhusu Nollywood, Dialogue: 0,0:16:09.00,0:16:13.38,Default,,0000,0000,0000,,iliyojawa na watu wabunifu wanaotengeneza filamu ingawaje kuna changamoto nyingi za kiufundi, Dialogue: 0,0:16:13.40,0:16:14.98,Default,,0000,0000,0000,,filamu ambazo ni maarufu sana Dialogue: 0,0:16:15.00,0:16:19.98,Default,,0000,0000,0000,,ambazo ni mfano mzuri unaoonyesha Wanigeria wanatumia kile wanachotengeneza? Dialogue: 0,0:16:20.00,0:16:23.29,Default,,0000,0000,0000,,Inakuwaje kama angefahamu \Nkuhusu msusi wangu bora kabisa, Dialogue: 0,0:16:23.31,0:16:26.98,Default,,0000,0000,0000,,ambaye ameanza biashara yake mwenyewe \Nakiuza nywele za kuongezea? Dialogue: 0,0:16:27.00,0:16:30.98,Default,,0000,0000,0000,,Au kuhusu mamilioni ya Wanigeria wengine ambao huanza biashara na muda mwingine kuanguka, Dialogue: 0,0:16:31.00,0:16:33.94,Default,,0000,0000,0000,,lakini huendelea kukuza azma yao? Dialogue: 0,0:16:35.00,0:16:36.98,Default,,0000,0000,0000,,Muda wote nikiwa nyumbani hukutana Dialogue: 0,0:16:37.00,0:16:39.98,Default,,0000,0000,0000,,na vyanzo vya kila wakati vya kukwaza \Nkwa Wanigeria wengi: Dialogue: 0,0:16:40.00,0:16:43.44,Default,,0000,0000,0000,,miundombinu yetu mibovu, \Nserikali iliyoanguka, Dialogue: 0,0:16:43.47,0:16:45.52,Default,,0000,0000,0000,,lakini pia kwa ustahimilivu mkubwa Dialogue: 0,0:16:45.55,0:16:48.98,Default,,0000,0000,0000,,wa watu ambao hufanikiwa,\Nbila ya kutegemea serikali, Dialogue: 0,0:16:49.00,0:16:50.26,Default,,0000,0000,0000,,bila yenyewe kabisa. Dialogue: 0,0:16:51.37,0:16:53.98,Default,,0000,0000,0000,,Huwa natoa mafunzo ya uandishi \Nkila kipindi cha joto jijini Lagos, Dialogue: 0,0:16:54.00,0:16:56.98,Default,,0000,0000,0000,,na huwa inanishangaza \Nkwa namna gani watu wengi hujiunga, Dialogue: 0,0:16:57.00,0:16:59.98,Default,,0000,0000,0000,,namna ambavyo watu wengi wana shauku ya kuandika, Dialogue: 0,0:17:00.00,0:17:01.39,Default,,0000,0000,0000,,ili kueleza hadithi. Dialogue: 0,0:17:02.28,0:17:05.30,Default,,0000,0000,0000,,Mimi na mchapishaji wa kitabu changu \Ntumeanzisha taasisi isiyo ya kibiashara Dialogue: 0,0:17:05.32,0:17:06.98,Default,,0000,0000,0000,,inayofahamika kama Farafina Trust, Dialogue: 0,0:17:07.00,0:17:09.98,Default,,0000,0000,0000,,na tuna ndoto kubwa ya kujenga maktaba Dialogue: 0,0:17:10.00,0:17:12.14,Default,,0000,0000,0000,,na kukarabati maktaba ambazo tayari zipo Dialogue: 0,0:17:12.17,0:17:14.98,Default,,0000,0000,0000,,na kutoa vitabu kwa shule za majimboni Dialogue: 0,0:17:15.00,0:17:17.10,Default,,0000,0000,0000,,ambazo hazina vitabu katika maktaba zao, Dialogue: 0,0:17:17.12,0:17:19.50,Default,,0000,0000,0000,,na kuandaa mafunzo mengi mno, Dialogue: 0,0:17:19.52,0:17:20.98,Default,,0000,0000,0000,,katika kuandika na kusoma, Dialogue: 0,0:17:21.00,0:17:24.20,Default,,0000,0000,0000,,kwa watu wote ambao wana shauku \Nya kuelezea hadithi zetu nyingi. Dialogue: 0,0:17:24.33,0:17:25.98,Default,,0000,0000,0000,,Hadithi zina maana. Dialogue: 0,0:17:26.00,0:17:27.98,Default,,0000,0000,0000,,Hadithi nyingi zina maana. Dialogue: 0,0:17:28.00,0:17:31.98,Default,,0000,0000,0000,,Haidithi zimekuwa \Nzikitumika kupokonya na kukejeli, Dialogue: 0,0:17:32.00,0:17:35.98,Default,,0000,0000,0000,,lakini hadithi zinaweza tumika \Nkuhamasisha na kuleta ubinadamu. Dialogue: 0,0:17:36.64,0:17:38.98,Default,,0000,0000,0000,,Hadithi zinaweza kuvunja heshima ya watu, Dialogue: 0,0:17:39.00,0:17:42.70,Default,,0000,0000,0000,,lakini hadithi zinaweza \Nkurudisha heshima iliyopotea. Dialogue: 0,0:17:44.00,0:17:46.05,Default,,0000,0000,0000,,Mwandishi wa Kimarekani \NAlice Walker aliandika Dialogue: 0,0:17:46.07,0:17:49.98,Default,,0000,0000,0000,,kuhusu ndugu zake wanaotokea Kusini\Nambao walihamia Kaskazini. Dialogue: 0,0:17:50.00,0:17:51.98,Default,,0000,0000,0000,,Aliwaonyesha kitabu kuhusu Dialogue: 0,0:17:52.00,0:17:54.07,Default,,0000,0000,0000,,maisha ya Kusini ambayo wameyaacha nyuma. Dialogue: 0,0:17:55.59,0:17:58.98,Default,,0000,0000,0000,,"Walikaa, na wakakisoma kitabu, Dialogue: 0,0:17:59.00,0:18:04.53,Default,,0000,0000,0000,,nisikilize mimi soma kitabu,\Nna raha ya dunia utaipata tena." Dialogue: 0,0:18:05.58,0:18:08.44,Default,,0000,0000,0000,,Ningependelea kumalizia na hili wazo: Dialogue: 0,0:18:08.46,0:18:10.98,Default,,0000,0000,0000,,Kwamba pale tunapokataa hadithi moja, Dialogue: 0,0:18:11.00,0:18:13.98,Default,,0000,0000,0000,,tunapogundua kwamba hakuna hadithi moja Dialogue: 0,0:18:14.00,0:18:16.44,Default,,0000,0000,0000,,kuhusu sehemu yoyote, Dialogue: 0,0:18:16.46,0:18:17.98,Default,,0000,0000,0000,,huwa tunarejesha Furaha. Dialogue: 0,0:18:18.70,0:18:19.82,Default,,0000,0000,0000,,Asante. Dialogue: 0,0:18:19.84,0:18:22.84,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi)