1 00:00:00,000 --> 00:00:01,976 Mimi ni msimuliaji wa hadithi 2 00:00:02,000 --> 00:00:04,976 Ningependa kuwasimulia kidogo maisha yangu 3 00:00:05,000 --> 00:00:09,976 juu ya kile ninachopenda kuita "hatari ya simulizi moja" 4 00:00:10,746 --> 00:00:13,976 Nilikulia mazingira ya chuo kikuu magharibi mwa Nigeria 5 00:00:14,158 --> 00:00:17,467 Mama yangu anasema nilianza kusoma nikiwa na miaka miwili 6 00:00:17,491 --> 00:00:20,507 japo nadhani miaka minne ni sahihi zaidi 7 00:00:21,753 --> 00:00:23,564 Niliwahi sana kuanza kusoma 8 00:00:23,588 --> 00:00:26,976 Nilisoma vitabu vya watoto vya Uingereza na Marekani 9 00:00:27,706 --> 00:00:29,976 Pia nilianza kuandika katika umri mdogo 10 00:00:30,000 --> 00:00:33,976 Na nilipoanza kuandika, nikiwa na takriban miaka saba, 11 00:00:34,000 --> 00:00:36,048 hadithi za penseli na michoro ya rangi 12 00:00:36,072 --> 00:00:39,604 ambazo mama yangu alilazimika kuzisoma, 13 00:00:39,628 --> 00:00:43,196 niliandika hadithi sawa na zile nilizokuwa nazisoma: 14 00:00:43,220 --> 00:00:47,976 Wahusika wangu wote walikuwa wazungu na wenye macho ya bluu. 15 00:00:48,000 --> 00:00:50,307 Walicheza katika theluji. 16 00:00:50,331 --> 00:00:52,418 Walikula matofaa 17 00:00:52,442 --> 00:00:53,839 (Kicheko) 18 00:00:54,013 --> 00:00:56,024 Na walizungumza sana kuhusu hali ya hewa, 19 00:00:56,048 --> 00:00:58,176 jinsi ilivyo vizuri kuona jua limechomoza. 20 00:00:58,409 --> 00:01:00,373 (Kicheko) 21 00:01:00,397 --> 00:01:03,531 Yote haya,ingawa niliishi Nigeria. 22 00:01:03,555 --> 00:01:05,333 Nilikuwa sijawahi kwenda nje ya Nigeria. 23 00:01:07,143 --> 00:01:10,404 Hatukuwa na theluji, tulikula maembe. 24 00:01:10,428 --> 00:01:12,276 Na hatukuzungumza kuhusu hali ya hewa, 25 00:01:12,300 --> 00:01:13,976 sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo. 26 00:01:14,269 --> 00:01:16,976 Wahusika wangu pia walikunywa sana bia ya tangawizi 27 00:01:17,000 --> 00:01:19,381 kwa sababu wahusika katika vitabu vya Uingereza 28 00:01:19,405 --> 00:01:20,976 walikunywa bia ya tangawizi. 29 00:01:21,301 --> 00:01:23,976 Ijapokuwa sikuifahamu bia ya tangawizi 30 00:01:24,000 --> 00:01:25,531 (Kicheko) 31 00:01:25,555 --> 00:01:27,005 Na kwa miaka mingi baadaye 32 00:01:27,029 --> 00:01:29,976 nilikuwa na shauku ya kuonja bia ya tangawizi. 33 00:01:30,476 --> 00:01:31,976 Lakini hiyo ni hadithi nyingine. 34 00:01:32,000 --> 00:01:34,483 Ambacho hii inaonyesha,nafikiri 35 00:01:34,507 --> 00:01:37,361 Ni namna tulivyo wajinga na wanyonge 36 00:01:37,385 --> 00:01:38,976 Tunapokabiliana na simulizi 37 00:01:39,000 --> 00:01:40,385 hasa hasa kama watoto 38 00:01:41,639 --> 00:01:45,409 Sababu nilisoma vitabu vyenye wahusika wa kigeni 39 00:01:45,433 --> 00:01:47,552 Nilikuwa nimeaminishwa kwamba vitabu 40 00:01:47,576 --> 00:01:50,746 kwa asili lazima viwe na wahusika wageni 41 00:01:50,770 --> 00:01:54,489 Na vielezo kuhusu mambo ambayo binafsi siyafahamu 42 00:01:55,600 --> 00:01:58,219 Mambo yalibadilika Nilipopata vitabu vya Afrika 43 00:01:59,000 --> 00:02:00,976 havikuwepo kwa wingi 44 00:02:01,000 --> 00:02:03,869 Na haikuwa rahisi kuvipata kama vya kigeni 45 00:02:03,893 --> 00:02:06,976 Lakini sababu ya waandishi kama Chinua Achebe na Camara Laye 46 00:02:07,000 --> 00:02:10,976 Nilipata badiliko la akili ninavyoiona fasihi 47 00:02:11,000 --> 00:02:13,214 Niligundua kwamba watu kama mimi, 48 00:02:13,238 --> 00:02:15,245 wasichana weusi 49 00:02:15,269 --> 00:02:18,531 wenye nywele ngumu 50 00:02:18,555 --> 00:02:20,365 pia wapo katika fasihi. 51 00:02:20,682 --> 00:02:23,976 Nilianza kuandika vitu nilivyovifahamu 52 00:02:24,737 --> 00:02:27,976 Nilikuwa navipenda hivyo vitabu vya Marekani na Uingereza 53 00:02:28,000 --> 00:02:31,976 Viliamsha fikra zangu Vilifunua vitu vipya. 54 00:02:32,000 --> 00:02:33,976 Lakini matokeo yasiyokusudiwa 55 00:02:34,000 --> 00:02:36,048 yalikuwa; sikufahamu kuwa watu kama mimi 56 00:02:36,072 --> 00:02:37,498 waweza kuwepo katika fasihi. 57 00:02:38,451 --> 00:02:41,976 hivyo ufumbuzi wa waandishi Waafrika: 58 00:02:42,000 --> 00:02:45,877 Uliniokoa na mtazamo mmoja juu ya vitabu 59 00:02:47,000 --> 00:02:49,976 Ninatoka kwenye familia ya kawaida 60 00:02:50,000 --> 00:02:51,976 Baba yangu alikuwa mhadhiri 61 00:02:52,385 --> 00:02:54,068 Mama yangu ni afisa wa utawala 62 00:02:55,369 --> 00:02:58,171 Kwa hiyo kama kawaida, tulikuwa na, 63 00:02:58,195 --> 00:03:02,544 mtumishi wa nyumbani anayetoka vijiji vya jirani 64 00:03:03,182 --> 00:03:06,468 Nilipokuwa na miaka nane tulipata mtumishi wa kiume 65 00:03:07,102 --> 00:03:08,356 Jina lake aliitwa Fide 66 00:03:09,658 --> 00:03:13,959 Mama alituambia kuwa familia yake ni masikini sana 67 00:03:15,000 --> 00:03:19,976 Mama alituma magimbi na mchele na nguo zetu za zamani kwa familia yao 68 00:03:20,000 --> 00:03:22,620 Na niliposhindwa kumaliza chakula mama alisema, 69 00:03:22,644 --> 00:03:26,976 "Maliza chakula! kuna watu ambao hawana chochote 70 00:03:27,000 --> 00:03:30,976 Niliwahurumia sana familia ya Fide 71 00:03:31,576 --> 00:03:34,473 Jumamosi moja tukaenda kijijini kwao kutembelea 72 00:03:34,497 --> 00:03:37,976 na mama yake akatuonyesha kikapu kizuri 73 00:03:38,000 --> 00:03:40,976 kilichosukwa kwa ukili uliopakwa rangi na kaka yake Fide 74 00:03:41,000 --> 00:03:42,976 Nilishangaa 75 00:03:43,000 --> 00:03:45,976 Sikudhani kuwa yeyote katika familia yake 76 00:03:46,000 --> 00:03:48,976 angeweza kutengeneza chochote 77 00:03:49,000 --> 00:03:51,976 yote niliyowahi kusikia kuhusu wao ni namna walivyo masikini 78 00:03:52,000 --> 00:03:56,467 Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwangu kuwaona tofauti na umasikini wao 79 00:03:57,143 --> 00:03:59,514 umasikini wao ilikuwa ni simulizi moja kwangu 80 00:04:01,000 --> 00:04:03,524 baadaye niliwaza hili nilipotoka Nigeria 81 00:04:03,548 --> 00:04:06,230 Kwenda Marekani kusoma chuo kikuu 82 00:04:06,341 --> 00:04:07,674 Nilikuwa na miaka 19 83 00:04:08,421 --> 00:04:11,198 Mmarekani niliyekuwa naishi naye chumba kimoja alinishangaa 84 00:04:12,000 --> 00:04:15,586 Aliuliza wapi nimefunza kuzungumza kiingereza vizuri 85 00:04:15,610 --> 00:04:17,698 Alishangaa nilipomwambia kuwa Nigeria 86 00:04:17,722 --> 00:04:20,436 wanatumia kiingereza kama lugha ya taifa 87 00:04:21,753 --> 00:04:25,976 Aliomba kusikiliza "nyimbo za kikabila" 88 00:04:26,000 --> 00:04:27,976 na alipigwa butwaa vile vile 89 00:04:28,000 --> 00:04:29,976 Nilipompa kanda yangu ya Mariah Carey 90 00:04:30,000 --> 00:04:32,976 (kicheko) 91 00:04:33,000 --> 00:04:36,693 Alidhani kuwa sifahamu kutumia jiko la umeme 92 00:04:37,782 --> 00:04:39,038 Kilichonishangaza mimi ni hiki 93 00:04:39,062 --> 00:04:42,137 Alikuwa ananihurimia hata kabla ya kuniona 94 00:04:42,528 --> 00:04:45,976 Mtazamo wake mbovu, kunihusu, kama Mwafrika, 95 00:04:46,000 --> 00:04:49,036 Ulikuwa wa huruma ya kudhalilisha, yenye kujali 96 00:04:50,000 --> 00:04:53,496 Alikuwa na simulizi moja kuhusu Afrika: 97 00:04:53,623 --> 00:04:55,977 Simulizi ya majanga. 98 00:04:56,412 --> 00:04:57,698 Kwenye simulizi hii moja, 99 00:04:57,722 --> 00:05:01,976 Hakukuwa na uwezekano wa Mwafrika kufanana naye kwa namna yeyote, 100 00:05:02,000 --> 00:05:04,976 Hakukuwa na uwezekano wa hisia ngumu zaidi ya huruma, 101 00:05:05,000 --> 00:05:08,976 Hakukuwa na uwezekano wa ushirikiano kama binadamu walio sawa. 102 00:05:09,000 --> 00:05:11,123 Lazima niseme kuwa kabla ya kwenda Marekani, 103 00:05:11,147 --> 00:05:13,428 Sikuwa nikijitambua kwa undani kama Mwafrika. 104 00:05:14,000 --> 00:05:16,976 Lakini Marekani, popote Afrika ilipotajwa, watu walinigeukia. 105 00:05:17,000 --> 00:05:19,746 Bila kujali kuwa sifahamu chochote kuhusu nchi kama Namibia. 106 00:05:21,000 --> 00:05:23,096 Lakini nilikuja kuupokea huu utambulisho mpya, 107 00:05:23,120 --> 00:05:25,976 Na kwa namna nyingi sasa ninajitazama kama Mwafrika. 108 00:05:26,000 --> 00:05:29,976 Ijapokuwa bado ninakasirishwa sana pale Afrika inapoelezewa kama ni nchi 109 00:05:30,000 --> 00:05:33,976 Mfano wa karibu, ni safari yangu ya ndege 110 00:05:34,000 --> 00:05:35,285 Kutoka Lagos hivi juzi, 111 00:05:35,309 --> 00:05:38,191 Ambapo kulikuwa na tangazo 112 00:05:38,215 --> 00:05:42,976 Kuhusu kazi ya kujitolea kule "India, Afika na nchi nyingine" 113 00:05:43,000 --> 00:05:44,317 Kicheko 114 00:05:44,476 --> 00:05:47,976 Baada ya kuishi Marekani kama Mwafrica 115 00:05:48,000 --> 00:05:51,174 Nikaanza kuelewa mwitikio wa niliyekuwa naishi naye chumba kimoja 116 00:05:52,000 --> 00:05:54,025 kama sikukulia Nigeria 117 00:05:54,049 --> 00:05:57,190 Na kama kila nilichofahamu kuhusu Afrika kilitokana na picha maarufu 118 00:05:57,214 --> 00:06:02,386 Mimi pia ningedhani kuwa Africa ni mahali penye mandhari nzuri, 119 00:06:02,410 --> 00:06:03,976 Wanyama wa kupendeza, 120 00:06:04,000 --> 00:06:05,976 na watu wasioeleweka, 121 00:06:06,000 --> 00:06:09,631 wapiganao vita visivyo na maana, wanaokufa na umasikini na UKIMWI 122 00:06:09,655 --> 00:06:11,976 wasioweza kujisemea 123 00:06:12,000 --> 00:06:16,155 wanaosubiri kusaidiwa na mtu mweupe, mgeni mwenye ukarimu 124 00:06:16,928 --> 00:06:19,097 Ningewaona waafrika kwa namna ile ambayo mimi, 125 00:06:19,121 --> 00:06:21,824 nilipokuwa mtoto, niliiona familia ya Fide 126 00:06:23,000 --> 00:06:26,976 Hii simulizi moja kuhusu Afrika nadhani inatokana na fasihi za magharibi 127 00:06:27,000 --> 00:06:31,976 Sasa, huu ni msemo kutoka katika uandishi wa mfanyabiashara wa London aitwaye John Lok, 128 00:06:32,000 --> 00:06:34,976 aliyesafiri kwa maji kuelekea Afrika magharibi mwaka 1561 129 00:06:35,000 --> 00:06:38,663 na aliweka hazina ya kuvutia kutokana na safari yake. 130 00:06:40,203 --> 00:06:43,976 Baada ya kuwaita Waafrika weusi kama " hayawani wasio na nyumba," 131 00:06:44,000 --> 00:06:47,976 aliandika,"Pia kuna watu wasio na vichwa, 132 00:06:48,000 --> 00:06:51,968 midomo na macho yao yapo katika vifua vyao." 133 00:06:53,000 --> 00:06:55,096 Sasa, nilicheka kila nikisoma haya maneno. 134 00:06:55,120 --> 00:06:58,500 Na lazima mtu atakubaliana na fikira za John Lok. 135 00:06:59,373 --> 00:07:01,239 Lakini kipi ni muhimu kuhusu uandishi wake 136 00:07:01,263 --> 00:07:02,976 ni kwamba inawakilisha mwanzo 137 00:07:03,000 --> 00:07:05,976 wa utamaduni wa kuelezea hadithi za Afrika kwa Magharibi: 138 00:07:06,000 --> 00:07:09,367 Utamaduni wa kusini mwa jangwa la Sahara kama sehemu isiyofaa, 139 00:07:09,479 --> 00:07:11,634 yenye utofauti, yenye kiza, 140 00:07:11,658 --> 00:07:16,976 ya watu ambao, kutokana na maneno ya mshairi bora aitwaye Rudyard Kipling, 141 00:07:17,000 --> 00:07:18,941 ni "nusu shetani, nusu watoto." 142 00:07:20,211 --> 00:07:22,976 Hivyo, nilianza kuelewa kwamba mwanafunzi Mmarekani ninayeshirikiana nae chumba 143 00:07:23,000 --> 00:07:24,976 lazima katika maisha yake 144 00:07:25,000 --> 00:07:28,976 atakuwa ameona na kusikia namna mbalimbali za hii hadithi moja, 145 00:07:29,000 --> 00:07:30,976 kama ilivyo kwa profesa, 146 00:07:31,000 --> 00:07:34,766 ambaye aliwahi niambia kuwa riwaya yangu haikuwa "na uhalisia wa Kiafrika," 147 00:07:35,869 --> 00:07:37,560 Sasa, nilikubaliana na kuchanganua 148 00:07:37,584 --> 00:07:40,679 kwamba kulikuwa na baadhi ya vitu ambavyo si sawa katika riwaya hii, 149 00:07:40,703 --> 00:07:43,976 na kuwa nilifeli katika maeneo mbalimbali, 150 00:07:44,000 --> 00:07:46,239 lakini sikufiria kwamba ilifeli 151 00:07:46,263 --> 00:07:48,976 katika kutekeleza uhalisia wake wa Kiafrika. 152 00:07:49,000 --> 00:07:52,706 Kiukweli, sikufahamu uhalisia wa Kiafrika ni upi. 153 00:07:54,000 --> 00:07:58,396 Profesa alinielezza kwamba wahusika kwenye riwaya walikuwa wanafanana mno kama yeye, 154 00:07:58,420 --> 00:08:00,396 msomi aliye katika maisha ya kati. 155 00:08:00,420 --> 00:08:02,522 Wahusika wangu waliendesha magari. 156 00:08:02,546 --> 00:08:04,976 Hawakuwa wanashinda na njaa. 157 00:08:05,000 --> 00:08:07,927 Kwa hiyo hawakuwa Waafrika halisi. 158 00:08:09,000 --> 00:08:11,976 Lakini niongeze haraka-haraka kwamba najisikia hatia 159 00:08:12,000 --> 00:08:14,070 katika swali la la hadithi iliyo moja. 160 00:08:15,000 --> 00:08:17,991 Miaka michache iliyopita, nilitembelea Mexico nikitokea Marekani. 161 00:08:19,000 --> 00:08:21,667 Hali ya kisiasa nchini Marekani wakati huo ilikuwa tete, 162 00:08:21,691 --> 00:08:24,976 kulikuwa na majadiliano yanayoendelea kuhusu uhamiaji. 163 00:08:25,000 --> 00:08:26,976 Na, mara kwa mara hutokea Marekani, 164 00:08:27,000 --> 00:08:29,976 neno uhamiaji likaja kuwa linahusishwa na watu wenye asili ya Mexico. 165 00:08:30,698 --> 00:08:32,631 Kulikuwa na hadithi ndefu kuhusu Wamexico 166 00:08:32,655 --> 00:08:35,976 kama watu wanaonyonya mfumo wa afya, 167 00:08:36,000 --> 00:08:37,976 wanajipenyeza kwenye mipaka, 168 00:08:38,000 --> 00:08:40,465 wanakamatwa kwenye mipaka, vitu kama hivyo. 169 00:08:42,163 --> 00:08:45,976 Nakumbuka siku ya kwanza nilipokuwa natembea eneo liitwalo Guadalajara, 170 00:08:46,000 --> 00:08:47,976 nikiwaangalia watu wakielekea makazini, 171 00:08:48,000 --> 00:08:49,976 wakitengeneza tortilla maeneo ya sokoni, 172 00:08:50,000 --> 00:08:51,973 wakivuta sigara, wakicheka. 173 00:08:53,195 --> 00:08:55,976 Nakumbuka kwa mara ya kwanza nilipatwa na mshangao kidogo. 174 00:08:56,000 --> 00:08:58,976 Kisha, nikagubikwa na aibu. 175 00:08:59,341 --> 00:09:03,976 Nikatambua ya kwamba nimezama sana katika habari zinazoelezea watu wa Mexico 176 00:09:04,000 --> 00:09:06,000 ambao wamekuwa jambo katika akili yangu, 177 00:09:06,024 --> 00:09:07,849 wahamiaji duni, 178 00:09:08,769 --> 00:09:11,191 nilidanganyika katika hadithi moja ya watu wa Mexico 179 00:09:11,215 --> 00:09:13,722 na sikuweza kujisikia aibu zaidi. 180 00:09:14,071 --> 00:09:16,618 Kwa hiyo hiyo ndiyo namna ya kutengeneza hadithi moja. 181 00:09:16,642 --> 00:09:18,976 kuwaeleza watu kama jambo moja, 182 00:09:19,000 --> 00:09:20,976 kama jambo moja tu, 183 00:09:21,000 --> 00:09:22,976 tena na tena, 184 00:09:23,000 --> 00:09:24,515 na hivyo ndivyo watakavyokuwa. 185 00:09:25,793 --> 00:09:28,239 Haiwezekani kuongelea kuhusu hadithi moja 186 00:09:28,263 --> 00:09:29,952 bila kuongelea kuhusu uwezo ya mamlaka. 187 00:09:31,496 --> 00:09:33,244 Kuna neno, neno la lugha ya Igbo, 188 00:09:33,268 --> 00:09:36,919 ambalo huwa naliwaza kila nikifikiria mfumo wa mamlaka wa dunia, 189 00:09:36,943 --> 00:09:38,133 na hili "nkali". 190 00:09:38,332 --> 00:09:42,976 Ni nomino ambayo inatafsiriwa kama "kuwa juu zaidi ya mwigine." 191 00:09:43,554 --> 00:09:46,482 Kama ulivyo ulimwengu wa kiuchumi na kisiasa, 192 00:09:46,506 --> 00:09:50,976 hadithi pia huelezwa kwa kanuni ya nkali: 193 00:09:51,000 --> 00:09:52,976 Zinaelezwaje, nani anaelezea, 194 00:09:53,000 --> 00:09:56,237 wakati gani zilielezwa, hadithi ngapi zinaelezwa, 195 00:09:56,261 --> 00:09:58,468 haya yote yanategemea sana nguvu ya mamlaka. 196 00:10:00,000 --> 00:10:03,143 Mamlaka ni uwezo sio tu wa kueleza hadithi ya kuhusu mtu mwingine, 197 00:10:03,167 --> 00:10:06,976 lakini kuifanya iwe hadithi mahususi kuhusu mtu huyo. 198 00:10:07,000 --> 00:10:09,096 Mshairi wa Kipalestina Mourid Barghouti aliandika 199 00:10:09,120 --> 00:10:11,976 kwamba kama unataka kuwaondoa watu, 200 00:10:12,000 --> 00:10:14,976 njia rahisi ya kufanya hivyo ni kuelezea hadithi yao 201 00:10:15,000 --> 00:10:17,230 na kuanza na, "pili." 202 00:10:18,484 --> 00:10:22,382 Anza hadithi na mishale ya waliokuwa wakazi halisi wa Amerika, 203 00:10:22,406 --> 00:10:24,976 na sio baada ya kufika kwa Waingereza, 204 00:10:25,000 --> 00:10:27,977 na utakuwa na hadithi tofauti nyingine kabisa. 205 00:10:28,001 --> 00:10:32,433 Anza na hadithi kuhusu kuanguka kwa dola za Kiafrika, 206 00:10:32,457 --> 00:10:35,976 na sio dola za Kiafrika zilizotokana na ukoloni, 207 00:10:36,000 --> 00:10:38,742 na utakuwa na hadithi tofauti kabisa. 208 00:10:40,000 --> 00:10:41,976 Hivi karibun nilitoa hotuba katika chuo 209 00:10:42,000 --> 00:10:45,785 ambapo mwanafunzi aliniambia kwamba ilikuwa ni aibu 210 00:10:45,809 --> 00:10:48,928 kwamba wanaume wa Kinigeria walikuwa wanyanyasaji 211 00:10:48,952 --> 00:10:50,896 kama alivyo muhusika ambaye ni baba katika riwaya yangu. 212 00:10:52,000 --> 00:10:55,976 Nikamwambia nimesoma riwaya iitwayo "Mwendawazimu wa Kiamerika" -- 213 00:10:56,000 --> 00:10:57,976 (Kicheko) 214 00:10:58,000 --> 00:10:59,976 -- na kwamba ilikuwa aibu 215 00:11:00,000 --> 00:11:02,976 kwamba vijana wadogo wa Kiamerika walikuwa wauaji waliokubuhu. 216 00:11:03,000 --> 00:11:06,976 (Kicheko) 217 00:11:07,000 --> 00:11:12,976 (Makofi) 218 00:11:13,000 --> 00:11:15,976 Sasa, kiukweli nilisema hili kutokana na kukerwa. 219 00:11:16,000 --> 00:11:17,976 (Kicheko) 220 00:11:18,000 --> 00:11:20,191 Lakini isingeweza kutokea kwangu kuwaza 221 00:11:20,215 --> 00:11:23,976 kwamba kwa sababu nimesoma riwaya ambayo muhusika ni muuaji wa kufululiza 222 00:11:24,000 --> 00:11:27,976 kwamba kwa kiasi fulani wanawakilisha Wamarekani wote. 223 00:11:28,000 --> 00:11:30,976 Hii si kwamba mimi ni mtu bora kuliko yule mwanafunzi, 224 00:11:31,000 --> 00:11:33,976 lakini kwa sababu ya utamaduni na nguvu ya uchumi wa Marekani, 225 00:11:34,000 --> 00:11:35,976 Nilikuwa nina hadithi nyingi za Marekani. 226 00:11:36,000 --> 00:11:39,976 Nilisoma Tyler na Updike na Steinbeck na Gaitskill. 227 00:11:40,000 --> 00:11:42,560 Sikuwa na hadithi moja ya Marekani. 228 00:11:43,671 --> 00:11:45,377 Nilipojifunza, miaka kadhaa iliyopita, 229 00:11:45,401 --> 00:11:49,742 kwamba waandishi wanategemewa kuwa na maisha ya utotoni ambayo siyo ya furaha 230 00:11:49,766 --> 00:11:51,976 ili kuja kufanikiwa baadaye, 231 00:11:52,000 --> 00:11:56,000 Nilianza kuwaza ni namna gani naweza buni vitu vibaya ambavyo wazazi wangu walinifanyia. 232 00:11:56,024 --> 00:11:57,976 (Kicheko) 233 00:11:58,000 --> 00:12:01,976 Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na maisha ya utoto ambayo yalikuwa ya furaha sana, 234 00:12:02,000 --> 00:12:04,976 yaliyojaa vicheko na upendo, katika familia iliyo na ukaribu sana. 235 00:12:05,000 --> 00:12:08,211 Lakini pia nilikuwa na mababu waliofia kwenye kambi za wakimbizi. 236 00:12:08,750 --> 00:12:12,976 Binamu yangu Polle alifariki sababu hakupata matibabu yanayostahili. 237 00:12:13,000 --> 00:12:15,976 Mmoja wa rafiki zangu,Okoloma, alifariki kwenye ajali ya ndege 238 00:12:16,000 --> 00:12:18,976 kwa sababu gari zetu za zimamoto hazikuwa na maji. 239 00:12:19,000 --> 00:12:21,976 Nimekulia katika serikali ya kijeshi ambayo ni kandamizi 240 00:12:22,000 --> 00:12:23,976 ambayo haikujali elimu, 241 00:12:24,000 --> 00:12:26,976 kwa muda mwingine, wazazi walikuwa hawalipwi mishahara. 242 00:12:27,000 --> 00:12:30,977 Hivyo, kama mtoto, nilianza kuona jamu hakuna mezani wakati wa kupata kifungua kinywa, 243 00:12:31,001 --> 00:12:33,498 kisha siagi nayo ikakosekana, 244 00:12:33,522 --> 00:12:35,976 kisha mkate ukawa ghali sana, 245 00:12:36,000 --> 00:12:37,871 kisha maziwa yakapungua. 246 00:12:39,000 --> 00:12:42,657 Na katika yote, hali ya hofu ya kisiasa 247 00:12:42,681 --> 00:12:44,363 ikaingilia maisha yetu, 248 00:12:45,823 --> 00:12:47,960 Na hadithi zote hizi zimenitengeneza mimi wa leo. 249 00:12:48,457 --> 00:12:51,976 Lakini kusisitiza katika hizi hadithi hasi 250 00:12:52,000 --> 00:12:54,976 ni kuongeza uzoefu wangu 251 00:12:55,000 --> 00:12:58,664 na kuachana na hadithi nyinginezo nyingi ambazo zimenitengeneza mimi. 252 00:12:59,394 --> 00:13:01,976 Hadithi moja hutengeneza tabaka, 253 00:13:02,000 --> 00:13:06,976 na tatizo la tabaka si kwamba hazina kweli, 254 00:13:07,000 --> 00:13:08,976 lakini hazijakamilika. 255 00:13:09,357 --> 00:13:11,960 Hufanya hadithi moja kuwa hadithi pekee. 256 00:13:13,000 --> 00:13:15,572 Hakika, Afrika ni bara ambalo limejaa majanga: 257 00:13:15,596 --> 00:13:18,976 Kuna majanga yaliyo makubwa, kama ubakaji wa kutisha nchini Congo 258 00:13:19,000 --> 00:13:20,626 na wa kudidimiza, 259 00:13:20,650 --> 00:13:25,150 kama ukweli kwamba watu 5000 wanaomba nafasi moja ya kazi nchini Nigeria. 260 00:13:26,000 --> 00:13:29,563 Lakini kuna hadithi nyingine ambazo hazihusiani na majanga, 261 00:13:29,587 --> 00:13:32,976 na ni muhimu sana, ni namna kuziongelea. 262 00:13:33,000 --> 00:13:34,976 Wakati wote nimekuwa nikihisi haiwezekani 263 00:13:35,000 --> 00:13:37,976 kujiunga kwa utaratibu na sehemu au mtu 264 00:13:38,000 --> 00:13:41,976 bila kuhusiana na hadithi zote za mahala pale au mtu huyo. 265 00:13:42,000 --> 00:13:45,580 Madhara ya hadithi moja ni kwamba: 266 00:13:45,604 --> 00:13:47,561 Hunyang'anya watu wa heshima. 267 00:13:48,332 --> 00:13:51,976 Hufanya utambuzi wetu wa usawa wa kibinadamu kuwa mgumu. 268 00:13:52,000 --> 00:13:56,164 Husisitiza ni jinsi gani tulivyo tofauti kuliko vile tulivyo sawa. 269 00:13:57,000 --> 00:13:59,489 Inakuwaje wakati kabla ya safari yangu ya Mexico, 270 00:13:59,513 --> 00:14:02,976 Ningefatilia majadiliano ya uhamiaji kutoka pande zote, 271 00:14:03,000 --> 00:14:04,976 upande wa Marekani na wa Mexico? 272 00:14:05,000 --> 00:14:08,976 Ingekuwaje kama mama yangu angeniambia familia ya Fide ilikuwa masikini 273 00:14:09,000 --> 00:14:10,976 na ya wachapakazi? 274 00:14:11,000 --> 00:14:13,096 Inakuwaje kama tungekuwa na mtandao wa televisheni wa Kiafrika 275 00:14:13,120 --> 00:14:16,976 ambao unarusha vipindi vya hadithi za Afrika duniani kote? 276 00:14:17,000 --> 00:14:21,331 Kitu ambacho muandishi wa Kinigeria Chinua Achebe anaita "usawa wa hadithi." 277 00:14:21,355 --> 00:14:25,331 Inakuweaje kama mwanafunzi niliyeishi naye chumba kimoja angefahamu kuhusu mchapishaji wangu wa Kinigeria, 278 00:14:25,355 --> 00:14:26,976 Muhtar Bakare, 279 00:14:27,000 --> 00:14:29,048 mtu wa kipekee ambaye aliacha kazi ya benki 280 00:14:29,072 --> 00:14:31,977 na kufuata ndoto zake na kuanzisha nyumba ya uchapishaji 281 00:14:32,001 --> 00:14:35,688 Sasa, hekima iliyozoeleka ilikuwa kwamba Wanigeria huwa hawasomi fasihi. 282 00:14:35,712 --> 00:14:36,966 Yeye alikataa. 283 00:14:36,990 --> 00:14:40,076 Alihisi kwamba watu ambao wanaweza kusoma, wangesoma, 284 00:14:40,100 --> 00:14:43,976 kama ungefanya kazi ya fasihi iwe katika bei nafuu na kupatikana kiurahisi. 285 00:14:44,666 --> 00:14:46,976 Muda mfupi baada ya kuchapisha riwaya yangu ya kwanza, 286 00:14:47,000 --> 00:14:49,976 Nilikwenda kwenye kituo cha televisheni kilichopo Lagos kwa ajili ya mahojiano, 287 00:14:50,000 --> 00:14:53,191 na mwanamke ambaye anafanya kazi pale kama karani alinifata na kusema, 288 00:14:53,215 --> 00:14:55,976 "Nimependa sana riwaya yako. Sijapenda mwishoni mwake. 289 00:14:56,000 --> 00:14:59,239 Sasa, ni lazima uandike muendelezo na hiki ndicho kitatokea ..." 290 00:14:59,263 --> 00:15:01,977 (Kicheko) 291 00:15:02,001 --> 00:15:04,977 Na alipoendelea kunielezea kipi cha kuandika kwenye muendelezo. 292 00:15:05,564 --> 00:15:07,976 Si kwamba nilivutiwa tu, lakini pia nilisisimka. 293 00:15:08,000 --> 00:15:10,976 Huyu ni mwanamke, mmoja wa watu wengi wa kawaida waliopo Nigeria, 294 00:15:11,000 --> 00:15:13,003 ambao hawakutakiwa kuwa wasomaji. 295 00:15:13,901 --> 00:15:15,525 Si kwamba alisoma tu kitabu, 296 00:15:15,549 --> 00:15:17,358 lakini pia alikimiliki 297 00:15:17,382 --> 00:15:20,485 na aliona ana haki kuaniambia kitu cha kuandika katika muendelezo. 298 00:15:21,580 --> 00:15:24,976 Sasa, ingekuwaje kama mwanafunzi niishiye nae chumba kimoja angejua kuhusu rafiki yangu Funmi Lyanda, 299 00:15:25,000 --> 00:15:27,976 mwanamke jasiri ambaye anaongoza kipindi cha televisheni Lagos, 300 00:15:28,000 --> 00:15:31,000 na anadhamiria kuelezea hadithi ambazo tunapendelea kuzisahau? 301 00:15:31,695 --> 00:15:34,976 Inakuwaje kama mwenzangu angetambua kuhusu upasuaji wa moyo 302 00:15:35,000 --> 00:15:37,976 ambao ulifanyika wiki iliyopita jijini Lagos? 303 00:15:38,000 --> 00:15:41,976 Inakuwaje angefahamu kuhusu muziki wa kisasa kwa Kinigeria, 304 00:15:42,000 --> 00:15:44,976 watu wenye vipaji wanaoimba katika lugha za Kiingereza na pijini, 305 00:15:45,000 --> 00:15:46,976 na Kiigbo na Kiyoruba na Kiijo, 306 00:15:47,000 --> 00:15:50,976 wakichanganya ushawishi kutoka kwa Jay Z hadi kwa Fela 307 00:15:51,000 --> 00:15:53,182 kwenda kwa Bob Marley na babu zao. 308 00:15:54,000 --> 00:15:56,239 Inakuwaje kama angejua kuhusu wakili mwanamke 309 00:15:56,263 --> 00:15:59,976 ambaye hivi karibuni alienda mahakamani nchini Nigeria kuipa changamoto sheria isiyo na maana 310 00:16:00,000 --> 00:16:02,976 ambayo inawataka wanawake kupewa ruhusa na waume zao 311 00:16:03,000 --> 00:16:05,976 kabla ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria? 312 00:16:06,000 --> 00:16:08,976 Inakuwaje kama angefahamu kuhusu Nollywood, 313 00:16:09,000 --> 00:16:13,380 iliyojawa na watu wabunifu wanaotengeneza filamu ingawaje kuna changamoto nyingi za kiufundi, 314 00:16:13,404 --> 00:16:14,976 filamu ambazo ni maarufu sana 315 00:16:15,000 --> 00:16:19,976 ambazo ni mfano mzuri unaoonyesha Wanigeria wanatumia kile wanachotengeneza? 316 00:16:20,000 --> 00:16:23,286 Inakuwaje kama angefahamu kuhusu msusi wangu bora kabisa, 317 00:16:23,310 --> 00:16:26,976 ambaye ameanza biashara yake mwenyewe akiuza nywele za kuongezea? 318 00:16:27,000 --> 00:16:30,976 Au kuhusu mamilioni ya Wanigeria wengine ambao huanza biashara na muda mwingine kuanguka, 319 00:16:31,000 --> 00:16:33,938 lakini huendelea kukuza azma yao? 320 00:16:35,000 --> 00:16:36,976 Muda wote nikiwa nyumbani hukutana 321 00:16:37,000 --> 00:16:39,976 na vyanzo vya kila wakati vya kukwaza kwa Wanigeria wengi: 322 00:16:40,000 --> 00:16:43,444 miundombinu yetu mibovu, serikali iliyoanguka, 323 00:16:43,468 --> 00:16:45,523 lakini pia kwa ustahimilivu mkubwa 324 00:16:45,547 --> 00:16:48,976 wa watu ambao hufanikiwa, bila ya kutegemea serikali, 325 00:16:49,000 --> 00:16:50,261 bila yenyewe kabisa. 326 00:16:51,373 --> 00:16:53,976 Huwa natoa mafunzo ya uandishi kila kipindi cha joto jijini Lagos, 327 00:16:54,000 --> 00:16:56,976 na huwa inanishangaza kwa namna gani watu wengi hujiunga, 328 00:16:57,000 --> 00:16:59,976 namna ambavyo watu wengi wana shauku ya kuandika, 329 00:17:00,000 --> 00:17:01,386 ili kueleza hadithi. 330 00:17:02,275 --> 00:17:05,298 Mimi na mchapishaji wa kitabu changu tumeanzisha taasisi isiyo ya kibiashara 331 00:17:05,322 --> 00:17:06,976 inayofahamika kama Farafina Trust, 332 00:17:07,000 --> 00:17:09,976 na tuna ndoto kubwa ya kujenga maktaba 333 00:17:10,000 --> 00:17:12,143 na kukarabati maktaba ambazo tayari zipo 334 00:17:12,167 --> 00:17:14,976 na kutoa vitabu kwa shule za majimboni 335 00:17:15,000 --> 00:17:17,096 ambazo hazina vitabu katika maktaba zao, 336 00:17:17,120 --> 00:17:19,501 na kuandaa mafunzo mengi mno, 337 00:17:19,525 --> 00:17:20,976 katika kuandika na kusoma, 338 00:17:21,000 --> 00:17:24,199 kwa watu wote ambao wana shauku ya kuelezea hadithi zetu nyingi. 339 00:17:24,326 --> 00:17:25,976 Hadithi zina maana. 340 00:17:26,000 --> 00:17:27,976 Hadithi nyingi zina maana. 341 00:17:28,000 --> 00:17:31,976 Haidithi zimekuwa zikitumika kupokonya na kukejeli, 342 00:17:32,000 --> 00:17:35,976 lakini hadithi zinaweza tumika kuhamasisha na kuleta ubinadamu. 343 00:17:36,642 --> 00:17:38,976 Hadithi zinaweza kuvunja heshima ya watu, 344 00:17:39,000 --> 00:17:42,703 lakini hadithi zinaweza kurudisha heshima iliyopotea. 345 00:17:44,000 --> 00:17:46,048 Mwandishi wa Kimarekani Alice Walker aliandika 346 00:17:46,072 --> 00:17:49,976 kuhusu ndugu zake wanaotokea Kusini ambao walihamia Kaskazini. 347 00:17:50,000 --> 00:17:51,976 Aliwaonyesha kitabu kuhusu 348 00:17:52,000 --> 00:17:54,068 maisha ya Kusini ambayo wameyaacha nyuma. 349 00:17:55,592 --> 00:17:58,976 "Walikaa, na wakakisoma kitabu, 350 00:17:59,000 --> 00:18:04,528 nisikilize mimi soma kitabu, na raha ya dunia utaipata tena." 351 00:18:05,579 --> 00:18:08,441 Ningependelea kumalizia na hili wazo: 352 00:18:08,465 --> 00:18:10,976 Kwamba pale tunapokataa hadithi moja, 353 00:18:11,000 --> 00:18:13,976 tunapogundua kwamba hakuna hadithi moja 354 00:18:14,000 --> 00:18:16,441 kuhusu sehemu yoyote, 355 00:18:16,465 --> 00:18:17,976 huwa tunarejesha Furaha. 356 00:18:18,695 --> 00:18:19,817 Asante. 357 00:18:19,841 --> 00:18:22,841 (Makofi)