Ambieni ma binti wenu kuhusu mwaka huu jinsi tulivyo amka tukihitaji kahawa ila tukapata pindi imemwagwa, kati ya magazeti ya asubuhi faksi za dada, mke/mume, watoto wadogo zilizojaa maji Mwambie mwana wako kuhusu huu mwaka atakapo kuuliza, anavyofaa kukuuliza, mwambie ili kuwa imechelewa kuja Kubali kuwahata ule mwaka tulikodisha uhuru,hatuku umiliki moja kwa moja Bado kulikuwa na sheria jinsi tunavyotumia sehemu zetu za siri. ilhali wakivuruga upole wetu wakatunyakua bila kujali ridhaa Hamna sheria ziliundiwa wanaume walioitekeleza Tulifunzwa ku hepa, kungoja, kuhofia, na kujifunika kungoja zaidi, na bado kungoja. Tuliambiwa tuwe kimya Ila ambia ma binti wako kuhusu muda huu wa vita mwaka uliotanguliwa na matokeo sawa, kama miongo miwili iliyopita tuliyapangusa macho yetu ma jeneza yakafunikwa na bendera kuondoa eneo la uhalifu wa Klabu, kwaruza kuomboleza mitaani, tukailaza mili yetu kwenye sakafu ya saruji tukiegemea walioanguka, tukalia, "Bila shaka tuna umuhimu," tukawaimbia waliopotea. Wanawake walilia huu mwaka. Walilia. Mwaka huo huo, tulikuwa tayari. Mwaka tuliopoteza uoga na kusonga kwa ujasiri huu pia ndio mwaka tulioyangalia chini mapipa tukaimba korongo angani, tuka hepa na kupangua, kashika dhahabu kwa hijab, tukapokea vitisho vya kifo, tulijifahamu kama wazalendo, kasema, "tuko 35 sasa, mda wa kutulia na kumtafuta mgombea mwenza," tukakuza ramani ya furaha mpya ya kitoto, kutokua na aibu ila ya hofu, tukajiita wanene na kumaanisha, bila shaka, safi kabisa Mwaka huu, tulikuwa wanawake, sio bibi harusi au kishaufu, sio jinsia duni, sio mawaidha, ila wanawake. Wafunze watoto wako. Wakumbushe kua mwaka wa kuwa watulivu au wadogo umepita. Wale kati yetu waliosema ni wanawake kwa mara ya kwanza, kachukua kiapo hiki cha umoja kwa umahiri Kuna wale walizaa watoto na wale hawakuzaa, na hamna miongoni mwetu aliuliza ilitufanyawakweli au sahihi au kweli. Anapokuuliza juu ya mwaka huu, binti wako, iwapo mwanawe au mrithi wa ushindi wako, toka pande ya faraja yake historia, kiyumba kuelekea wanawake, atashangaa na kuuliza kwa lafua, licha yake kutoweza kuelewa kafara yako, ataiweka ukadiri wako takatifu, jambo la ajabu atadadisi,"Ulikuwa wapi? Ulipigana? Ulikuwa na hofu au ulihofisha? Nini ilikupa majuto? Ulifanyia nini wanawake katika mwaka uliowasili Njia hii ulio nitengezea, mifupa ipi ilibidii ivunjwe? Ulifanya ya kutosha, na je uko sawa, mama? Na je wewe ni shujaa? Atauliza yale maswali magumu. Hatajali juu ya mikunjo ya uso wako, uzito wa ufumbata wako. Hatakuuliza kuhusu kutajwa kwako. Binti wako, uliyembebea mengi, anataka kujua ulimletea nini, zawadi ipi, ulizuia nuru ipi kutokomea Walipowakujia waathirika usiku, ulilala au uliamshwa? Bei ya kuwa macho ilikuwa nini? Nini, kwa mwaka tuisema saa imefika, ulifanyia nini upendeleo wako? Uliyanywa umaskini wa wengine? Uliangalia kando au uliuangalia moto? Uliujua ujuzi wako au uliutunza kama dhima? Je ulidanganywa na matusi ya "gonjwa" au "ndogo kuliko"? Je ulifunza na moyo mkunjufu au ngumu iliyokazwa? Ulikuwa wapi? Mwambie ukweli. Ifanye iwe maisha yako. Ithibitishe. Sema,"Binti, nilisimama pale kwa muda, uliochorwa kwa uso wangu kama sime na kuirusha ilipotoka kukata nafasi kwa'jili yako." Mwambie ukweli, vile ulivyoishi licha ya tabia mbaya Mwambie ulikuwa jasiri na daima, daima ukaungana na ujasiri, sana sana zile siku, ulikuwa wewe mwenyewe, Mwambie alizaliwa jinsi wewe ulivyo, kama kina mama wako mbeleni, na kina dada kando yao, Katika muda wa wazalendo, kama kawaida. Mwambie alizaliwa kwa muda uliyofaa, kwa muda uliyofaa kuongoza. (Vigelegele)