Ambieni ma binti wenu kuhusu mwaka huu
jinsi tulivyo amka tukihitaji kahawa
ila tukapata pindi imemwagwa,
kati ya magazeti ya asubuhi
faksi za dada, mke/mume, watoto wadogo
zilizojaa maji
Mwambie mwana wako kuhusu huu mwaka
atakapo kuuliza, anavyofaa kukuuliza,
mwambie ili kuwa imechelewa kuja
Kubali kuwahata ule mwaka tulikodisha
uhuru,hatuku umiliki moja kwa moja
Bado kulikuwa na sheria jinsi
tunavyotumia sehemu zetu za siri.
ilhali wakivuruga upole wetu
wakatunyakua bila kujali ridhaa
Hamna sheria ziliundiwa wanaume
walioitekeleza
Tulifunzwa ku hepa,
kungoja, kuhofia, na kujifunika
kungoja zaidi, na bado kungoja.
Tuliambiwa tuwe kimya
Ila ambia ma binti wako
kuhusu muda huu wa vita
mwaka uliotanguliwa na matokeo sawa,
kama miongo miwili iliyopita
tuliyapangusa macho yetu
ma jeneza yakafunikwa na bendera
kuondoa eneo la uhalifu wa Klabu,
kwaruza kuomboleza mitaani,
tukailaza mili yetu kwenye sakafu
ya saruji tukiegemea walioanguka,
tukalia, "Bila shaka tuna umuhimu,"
tukawaimbia waliopotea.
Wanawake walilia huu mwaka.
Walilia.
Mwaka huo huo, tulikuwa tayari.
Mwaka tuliopoteza uoga
na kusonga kwa ujasiri
huu pia ndio mwaka
tulioyangalia chini mapipa
tukaimba korongo angani,
tuka hepa na kupangua,
kashika dhahabu kwa hijab,
tukapokea vitisho vya kifo,
tulijifahamu kama wazalendo,
kasema, "tuko 35 sasa, mda wa kutulia na
kumtafuta mgombea mwenza,"
tukakuza ramani ya furaha mpya ya kitoto,
kutokua na aibu ila ya hofu,
tukajiita wanene na kumaanisha,
bila shaka,
safi kabisa
Mwaka huu, tulikuwa wanawake,
sio bibi harusi au kishaufu,
sio jinsia duni,
sio mawaidha, ila wanawake.
Wafunze watoto wako.
Wakumbushe kua mwaka wa kuwa
watulivu au wadogo umepita.
Wale kati yetu waliosema ni
wanawake kwa mara ya kwanza,
kachukua kiapo hiki cha umoja kwa umahiri
Kuna wale walizaa watoto na
wale hawakuzaa,
na hamna miongoni mwetu
aliuliza ilitufanyawakweli
au sahihi au kweli.
Anapokuuliza juu ya mwaka huu,
binti wako, iwapo mwanawe au
mrithi wa ushindi wako,
toka pande ya faraja yake historia,
kiyumba kuelekea wanawake,
atashangaa na kuuliza kwa lafua,
licha yake kutoweza kuelewa kafara yako,
ataiweka ukadiri wako takatifu,
jambo la ajabu atadadisi,"Ulikuwa wapi?
Ulipigana?
Ulikuwa na hofu au ulihofisha?
Nini ilikupa majuto?
Ulifanyia nini wanawake
katika mwaka uliowasili
Njia hii ulio nitengezea,
mifupa ipi ilibidii ivunjwe?
Ulifanya ya kutosha, na je uko sawa, mama?
Na je wewe ni shujaa?
Atauliza yale maswali magumu.
Hatajali
juu ya mikunjo ya uso wako,
uzito wa ufumbata wako.
Hatakuuliza kuhusu kutajwa kwako.
Binti wako, uliyembebea mengi,
anataka kujua
ulimletea nini, zawadi ipi,
ulizuia nuru ipi kutokomea
Walipowakujia waathirika usiku,
ulilala au uliamshwa?
Bei ya kuwa macho ilikuwa nini?
Nini, kwa mwaka tuisema saa imefika,
ulifanyia nini upendeleo wako?
Uliyanywa umaskini wa wengine?
Uliangalia kando au uliuangalia moto?
Uliujua ujuzi wako au
uliutunza kama dhima?
Je ulidanganywa na matusi ya
"gonjwa" au "ndogo kuliko"?
Je ulifunza na moyo mkunjufu
au ngumu iliyokazwa?
Ulikuwa wapi?
Mwambie ukweli. Ifanye iwe maisha yako.
Ithibitishe. Sema,"Binti, nilisimama pale
kwa muda,
uliochorwa kwa uso wangu kama sime
na kuirusha ilipotoka
kukata nafasi kwa'jili yako."
Mwambie ukweli, vile ulivyoishi
licha ya tabia mbaya
Mwambie ulikuwa jasiri
na daima, daima ukaungana na ujasiri,
sana sana zile siku,
ulikuwa wewe mwenyewe,
Mwambie alizaliwa jinsi wewe ulivyo,
kama kina mama wako mbeleni,
na kina dada kando yao,
Katika muda wa wazalendo, kama kawaida.
Mwambie alizaliwa kwa muda uliyofaa,
kwa muda uliyofaa
kuongoza.
(Vigelegele)