0:00:00.901,0:00:04.832 Masoko ya Afrika yasiyo rasmi huwekewa kasumba kwa kuonekana 0:00:04.856,0:00:06.703 vile yana kasheshe na goigoi. 0:00:07.234,0:00:09.887 Ubaya wa kusikia neno "yasiyo rasmi" 0:00:09.911,0:00:12.580 hutokana na jumuiya inayojiendesha ya misaada tuliyonayo, 0:00:12.604,0:00:14.230 ambayo ina mitazamo hasi sana, 0:00:14.254,0:00:18.763 na ilikuwa na madhara makubwa katika kuanguka kwa uchumi, 0:00:18.787,0:00:24.273 kuongeza kirahisi -- au kupunguza -- asilimia 40 hadi 60 ya ukomo wa faida 0:00:24.297,0:00:27.133 kwa masoko yasiyo rasmi pekee. 0:00:27.157,0:00:31.459 Ikiwa moja ya jukumu la kuweka ramani ya mzunguko wa biashara zisizo rasmi, 0:00:31.483,0:00:34.016 tumetengeneza machapisho kwa kina 0:00:34.040,0:00:38.991 ya ripoti zote na tafiti kwenye biashara za mipakani katika ukanda wa Afrika Mashariki, 0:00:39.015,0:00:40.826 tukirudi nyuma hadi miaka 20. 0:00:40.850,0:00:45.184 Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutuandaa kwa ajili ya kazi ya kwenda kutathmini tatizo ni nini, 0:00:45.208,0:00:49.370 kipi kilichokuwa kinarudisha nyuma biashara isiyo rasmi katika sekta isiyo rasmi. 0:00:49.990,0:00:53.494 Tulichogundua katika miaka 20 iliyopita ni kwamba, 0:00:53.518,0:00:57.271 hakuna aliyeweza kutofautisha kati ya magendo -- 0:00:57.295,0:01:01.740 ambayo ni sawa na upenyeshaji mali isiyo halali au iliyopigwa marufuku katika sekta isiyo rasmi -- 0:01:01.764,0:01:04.104 na mali halali ambayo haikuwekwa katika kumbukumbu 0:01:04.128,0:01:07.133 kama nyanya, machungwa, matunda. 0:01:07.697,0:01:10.017 Uhalifu huu -- 0:01:10.041,0:01:15.239 ambao kwa kiswahili unafahamika kama "biashara," ambao ni biashara, 0:01:15.263,0:01:18.697 ukilinganisha na "magendo", ambayo upenyeshaji bidhaa usio halali -- 0:01:18.721,0:01:22.242 uhalifu katika sekta isiyo rasmi, 0:01:22.266,0:01:26.135 kwa Kiingereza, bila kutofautisha nyanja hizi, 0:01:26.159,0:01:31.752 kwa urahisi inaweza kugharimu kila uchumi wa Afrika kati ya asilimia 60 hadi 80 ukiongezea 0:01:31.776,0:01:34.544 katika ukuaji wa pato la taifa kwa mwaka, 0:01:34.568,0:01:38.302 kwa sababu hatujambua injini 0:01:38.326,0:01:40.900 inayofanya uchumi kuendelea. 0:01:40.924,0:01:44.401 Sekta isiyo rasmi inaongeza ajira mara nne katika kiasi 0:01:44.425,0:01:46.367 cha uchumi ulio rasmi, 0:01:46.391,0:01:48.948 au uchumi wa "kisasa", kama wengi wauitavyo. 0:01:48.972,0:01:52.438 Hutoa nafasi za ajira na kuweza kujipatia kipato 0:01:52.462,0:01:56.159 kwa wale wengi ambao hawana "ujuzi wa darasani" katika nyanja mbalimbali za taaluma. 0:01:56.183,0:01:59.819 Lakini, je unaweza kutengeneza mashine ya kukaanga chipsi kutokana na gari bovu? 0:02:00.403,0:02:03.864 Kwa hiyo, hili, mabibi na mabwana, 0:02:03.888,0:02:07.104 ni jambo ambalo linatakiwa kutambuliwa kwa shauku kubwa. 0:02:07.128,0:02:11.386 Ambapo mtazamo wa sasa uliopo kuhusu sekta hii ni uhalifu, 0:02:11.410,0:02:12.637 hiki ni kivuli, 0:02:12.661,0:02:14.279 hii si halali, 0:02:14.303,0:02:18.763 hakutakiwa na madhumuni ya kuunganisha mzunguko wa uchumi usio rasmi 0:02:18.787,0:02:21.735 na ule ulio rasmi au hata ule wa kiulimwengu. 0:02:22.968,0:02:25.772 Nitawaeleza hadithi inayomuhusu Teresia, 0:02:25.796,0:02:29.872 mfanyabiashara ambaye anapindua mitazamo yetu yote, 0:02:29.896,0:02:33.246 anatufanya kuhoji kasumba zetu zote tulizokuwa nazo, 0:02:33.270,0:02:36.176 ukihusisha na ripoti ya miaka 20 nyuma. 0:02:37.675,0:02:43.164 Teresia anauza nguo chini ya mti katika mji unaoitwa Malaba, 0:02:43.188,0:02:45.284 katika mpaka wa Uganda na Kenya. 0:02:45.876,0:02:48.045 Unadhani ni rahisi sana, au sivyo? 0:02:48.810,0:02:51.467 Tutakwenda ning'iniza nguo mpya kwenye matawi, 0:02:51.491,0:02:54.423 tutatandika turubai, kisha kuketi chini, kusubiri wateja, 0:02:54.447,0:02:55.792 na hivyo ndivyo inakuwa. 0:02:55.816,0:02:59.201 Alikuwa ni mtu ambaye tuliona anarandana na yale yaliyomo katika ripoti, 0:02:59.225,0:03:00.493 katika tafiti, 0:03:00.517,0:03:04.294 alikuwa ni mama mjane anayefanya biashara, 0:03:04.318,0:03:05.806 akilea watoto wake. 0:03:07.092,0:03:09.702 Ni kipi kilibadili udhanifu wetu? 0:03:09.726,0:03:11.245 Kipi kilitushangaza? 0:03:11.269,0:03:14.991 Kwanza, Teresia analipia kodi ya serikali ya soko la mkoa 0:03:15.015,0:03:16.846 kila siku anayofanya biashara 0:03:16.870,0:03:20.123 kutokana na kuweka biashara chini ya mti wake. 0:03:20.147,0:03:22.198 Amekuwa akifanya hivi kwa miaka saba, 0:03:22.222,0:03:24.144 na amekuwa akipewa risiti. 0:03:24.560,0:03:26.037 Anatunza kumbumkumbu. 0:03:26.061,0:03:29.228 Tunamuona asiye hafifu, 0:03:29.252,0:03:30.599 masikini, 0:03:30.623,0:03:36.439 mwanamke asiye na uwezo anayefanya biashara pembezoni mwa barabara -- hapana. 0:03:36.463,0:03:40.562 Tunamuona mfanyabiashara ambaye anatunza kumbukumbu za mauzo kwa miaka; 0:03:40.586,0:03:46.907 mtu ambaye amekuwa na mzunguko wote wa biashara za rejareja zitokazo Uganda 0:03:46.931,0:03:49.246 hadi orodha ya uchukuaji; 0:03:49.270,0:03:53.132 aliye na mkokoteni unaoleta bidhaa, 0:03:53.156,0:03:56.072 au wakala wa mfumo wa fedha wa simu anayekuja kuchukua pesa taslimu 0:03:56.096,0:03:57.524 kila mwisho wa jioni. 0:03:57.548,0:04:01.956 Unaweza kisia ni kiasi gani Teresia hutumia, kwa wastani, 0:04:01.980,0:04:04.577 kila mwezi katika uorodheshaji bidhaa -- 0:04:04.601,0:04:07.274 shehena ya nguo mpya ambazo anapata kutoka Nairobi? 0:04:07.819,0:04:10.009 Dola za Kimarekani elfu moja na mia tano. 0:04:10.525,0:04:15.965 Ambayo ni takribani dola za Kimarekani 20,000 zilizowekezwa kwenye katika bidhaa za biashara na huduma 0:04:15.989,0:04:17.544 kila mwaka. 0:04:17.568,0:04:19.018 Huyu ni Teresia, 0:04:19.042,0:04:20.439 asiyeonekana, 0:04:20.463,0:04:21.743 aliyefichwa katikati. 0:04:22.442,0:04:26.535 Na huyu ni mtu wa ngazi ya kwanza ya wajasiriamali wadogo, 0:04:26.559,0:04:30.650 biashara ndogo ndogo zinazopatikana katika masoko ya ya miji hii. 0:04:30.674,0:04:35.558 Angalau katika mpaka mkubwa wa Malaba, yupo katika ngazi ya kwanza. 0:04:36.523,0:04:39.159 Watu wa mbele zaidi wanathamini mlolongo huu 0:04:39.183,0:04:42.228 na kwa rahisi wanafanya biashara tatu, 0:04:42.252,0:04:47.343 wakiwekeza dola za Kimarekani kati ya 2500 hadi 3000 kila mwezi. 0:04:47.772,0:04:51.752 Kwa hiyo tatizo lilikuja gundulika kwamba halikuwa uhalifu; 0:04:51.776,0:04:56.421 huwezi kumtuhumu mtu ambaye unamtoza na kumpa risiti. 0:04:56.957,0:05:02.347 Ni ukosefu wa kutambua ujuzi wa kazi zao. 0:05:03.048,0:05:07.044 Mifumo ya kibenki haina njia ya kuwatambua 0:05:07.068,0:05:08.556 kama wafanyabiashara ndogo ndogo. 0:05:08.580,0:05:11.158 pasipo kukataa ukweli, unajua, 0:05:11.182,0:05:13.390 mti wake hauna anuani. 0:05:13.912,0:05:16.238 Kwa hiyo amebanwa katikati. 0:05:16.262,0:05:18.693 Anaangukia katika mpasuko wa dhana zetu. 0:05:18.717,0:05:22.256 Unaijua ile mikopo midogo midogo ya kusaidia wanawake wa Kiafrika ambao ni wafanyabiashara? 0:05:22.646,0:05:25.476 Watampa mkopo wa dola za Kimarekani 50 au 100. 0:05:25.500,0:05:27.106 Atafanyia nini kiasi hiki? 0:05:27.130,0:05:29.472 Anatumia mara 10 ya kiasi hicho kila mwezi 0:05:29.496,0:05:31.098 katika uorodheshaji tu. 0:05:31.122,0:05:33.409 hatuongelei huduma nyingine za ziada 0:05:33.433,0:05:35.267 au mzunguko wote. 0:05:35.864,0:05:39.452 Hawa ni wale ambao hawastahili kuwepo katika kasumba ya sera 0:05:39.476,0:05:41.880 ya walio na ujuzi mdogo au wale duni, 0:05:41.904,0:05:44.775 wala si mwajiriwa, ofisa anayelipwa mshahara 0:05:44.799,0:05:46.660 au mtumishi aliye na pensheni 0:05:46.684,0:05:50.056 ambapo ndipo watu wa kipato cha kati walipo. 0:05:50.080,0:05:54.632 Badala yake, tulichonacho hapa ni mifano ya viwanda vidogo na vya kati 0:05:54.656,0:05:58.451 hizi ni mbegu zilizo na rutuba za biashara na viwanda 0:05:58.475,0:06:00.418 ambazo zinafanya injini iendelee kutembea. 0:06:00.442,0:06:02.177 Vinaleta chakula mezani. 0:06:02.201,0:06:05.274 Hata hapa katika hotel hii, wasioonekana -- 0:06:05.298,0:06:08.750 wachinjaji nyama, watengeneza mikate na watengeneza mishumaa -- 0:06:08.774,0:06:11.167 wanatengeneza mashine ambazo zinatengeneza chipsi 0:06:11.191,0:06:12.417 na wanatengeneza vitanda vyako, 0:06:12.441,0:06:15.846 Hawa ni wanawake ambao hawaonekani wanaofanya biashara mipakani, 0:06:17.037,0:06:19.406 pembezoni mwa barabara, 0:06:19.430,0:06:22.348 hawaonekani kwa watu wanaokusanya taarifa. 0:06:22.704,0:06:26.360 Na wanawekwa pamoja katika sekta kubwa isiyo rasmi 0:06:26.384,0:06:31.457 ambayo haihangaiki kutofautisha watu wanaopenyesha bidhaa na wakwepa kodi 0:06:31.481,0:06:34.089 na wale wanaofanya biashara za magendo, 0:06:34.113,0:06:36.144 na wanawake wanaofanya bashara, 0:06:36.168,0:06:40.313 na wale wanaoleta chakula mezani na kuwasomesha watoto zao hadi chuo kikuu 0:06:40.337,0:06:43.562 Kwa hiyo hili ndilo ninalouliza hapa. 0:06:43.586,0:06:46.421 Hayo ndiyo tunatakiwa kuanza kufanya. 0:06:46.868,0:06:51.477 Je tunaweza kuanza kwa kutambua ujuzi, kazi? 0:06:51.501,0:06:56.125 Tunaweza kubadili uchumi wa sekta isiyo rasmi kwa kuanza na utambuzi huu 0:06:56.149,0:07:00.830 na kisha kutengeneza milango ya wao kupita 0:07:00.854,0:07:03.063 na kushirikiana na sekta iliyo rasmi, 0:07:03.087,0:07:04.391 na ulimwengu, 0:07:04.415,0:07:06.126 na mfumo mzima. 0:07:06.150,0:07:07.714 Asante, mabibi na mabwana. 0:07:07.738,0:07:11.459 (Makofi)