Mpendwa Abuelita, Najua sijakuwepo nyumbani kwa muda. Uko nyumbani kwetu pazuri Mexico, nami niko hapa Marekani, nikipigania maisha yetu ya baadaye. Pengine unanyunyuzia ua waridi maji, ukitunza fyulisi na kuhakikisha kua kasa wako wameshiba. Hiyo ni mojawapo ya vitu, navikumbuka sana kuhusu nyumbani -- kupoteza muda na maua ukinihadithia kuhusu utoto wako Unavyojua, tumeishi New York City tangu 2015 Lakini maisha yamebadilika mno kwa mwaka uliopita. Hapo mwanzoni, New York ilikua ni sehemu ya makumbusho na hifadhi na shule na marafiki. Saaa hii ni kama mtandao unaoniunganisha na watu wengine wanaopanga kuokoa dunia. Wajua nilianzaje ? Ni baba na busara zake. Kila kitu ulimfunza, alienda akafunza ulimwengu. Maneno yake yote kuhusu uwajibikaji tulionao kama binadamu kuishi kwa usawa na asili yalipitishwa kwangu. Nimeona kutokua sawa kwenye ulimwengu wetu na kukumbuka ulichoniambia wakati mmoja: "Acha kila kitu bora kuliko ulivyokikuta." Najua ulikuwa unaongelea kuhusu vyombo, lakini, hiyo inaleta maana kwa ulimwengu pia. Sikujua cha kufanya mwanzoni. Dunia ni kubwa mno, na ina tabia nyingi mbaya. Sikujua vile msichana mwenye miaka 15 angebadilisha chochote. lakini ilinibidi kujaribu. Ili kuweka hii falsafa katika vitendo, Nilijiunga na klabu ya mazingira shuleni. Lakini niliona wanafunzi wenza wakiongelea mchakato wa taka kuna matumizi tena na kutazama filamu zinazohusu bahari. Ulikua mwonekano wa kuzingatia mazingira ulioegemea harakati ya kutunza hali ya hewa isiyofaa, na kutupa lawama kwa mtumiaji katika janga la kubadiika kwa hali ya hewa na kutangaza joto inaongezeka kwa sababu tulisahau kurudisaha mifuko inayoweza tumika tena dukani. Ulinifunza kwamba kutunza ulimwengu inahusu uamuzi tunaochukua kwa pamoja. Nafurahia kukuambia, Abuelita, kwamba nimebadili wazo la kila mtu klabuni. Badala ya kuongelea mchakato wa kufanya taka kutumika tena, tumeanza kuandikia wanasiasa wetu barua, kupiga marufuku kabisa plastiki laini. Na kisha, lisilojarajiwa likatokea: tulianza kugoma shuleni. Nafahamu ushatazama kwa habari, au pengine hio si mahususi kwa saa hii. Lakini wakati huo, ilikuwa ni jambo kubwa. Hebu fikiria watoto kutoenda shule kisa wanataka watu waokoe dunia. (Video) Umati: Ulimwengu mwingine unawezekana ! Hatuzuiliki ! XiyeBastide: Kwa mgomo wa kwanza kimataifa wa hali ya hewa, ilioandaliwa na Greta Thunberg, Nilishawishi wanafunzi 600 wenzangu kutembea nami. Greta Thunberg ni kijana mwanzilishi wa migomo Uimara wake ulinihamasisha, na kushtuka na utambuzi huu kua kijana angebadilisha maono ya umaa kwa masuala ya kijamii Harakati zikaanza. (Video) Umati: Nyamazisha ! XB: Na nikawa mmoja wa waandalizi wakuu kwa New York, Amerika na ulimwengu (Video) XB: Tunahitaji nini? Crowd: Haki ya hali ya hewa! XB: Tunalihitaji lini ? Crowd: Sasa ! XB: Nilianza kuongelea haki ya hali ya hewa na haki asilia na ushirika miongoni mwa vizazi tofauti. Huu ulikuwa mwazo tu, hata hivyo. Wiki iliyokuwa na shughuli nyingi katika maisha yangu nyakati zote itakuwa ni wiki ya Septemba 20,2019. Mimi na marafiki wangu tulipata watu 300,00 kugoma kwa ajiliya hali ya hewa katika jiji la New York Natamani ungekuwepo. Tuliandamana mitaani ya Wall Street kudai haki ya hali ya hewa. (Video) Umati: Hakuna tena kamwe makaa ya mawe, kamwe tena kwa mafuta, acha kaboni kwenye ardhi ! XB: Mwezi huo, nilihudhuria Mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa. Niliongea katika jopo alipokuwepo Al Gore Nikakutana na Jay Inslee na Naomi Klein na Bill McKibben na rais wa Umoja wa Mataifa Ilikuwa wiki la kustaajabisha kabisa maishani mwangu, kwa sababu kila mtu ninayemjua walikuja pamoja- walimu wangu, wanafunzi wenzangu wote... Hata maduka niyapendayo yalifungwa kwa ajili ya mgomo wa hali ya hewa. Kama ungeniuiza kwa nini nilifanya haya yote, jibu langu lingekuwa, "Kwanini nishindwe?" Imekua mwaka tangu nianze, na wakati mwingine huchosha. Lakini kama kuna kitu mmoja ulinifunza, ni uthabiti. Nakumbuka ulienda jiji la Mexico kila siku kwa miaka 30 ili kupata pesa ya mahitaji ya familia. Na najua Abuelito amekua akitembea nje kwa miaka 20 kulinda ardhi takatifu dhidi ya makampuni makubwa yanayataka kuinyakua mwaka moja si lolote kulingana na mapambano familia yetu imepitia. Na kama mapambano yetu yanaboresha dunia, yatatufanya kuwa watu bora. Kumekuwa na matatizo, Abuelita. Ulimwenguni, watu wanatarajia watoto kama sisi kufahamu kila kitu, au angalau wanatarajia tujue, Wanauliza na najibu, na kama najua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi. Wanahitaji matumaini, nasi tunawapa. Nimepanga, kuandika, kuongelea na kusoma kuhusu hali ya hewa na sera karibu kila siku kwa mwaka moja uliopita. Na nina wasiwasi kidogo kwamba sitoweza fanya vya kutosha, Abuelita. Kwangu, kuwa na miaka 18 and kujaribu kuokoa ulimwengu inamanisha kuwa mwanaharakati wa hali ya hewa. Awali, labda ilimanisha kusoma kuwa daktari au mwanasiasa au mtafiti. Lakini siwezi ngojea kuwa mkubwa ili niwe mojawapo ya hayo. Ulimwengu unaumia, na hatuna taanasa ya wakati kamwe. Kuokoa ulimwengu kama kijana unahitaji ueledi wa maneno, kuelewa sayansi inayohusu janga la hali ya hewa kuleta mtazamo wa kipekee kwa suala ibuka na kusahau mambo mengineyo Lakini wakati mwingine, nahisi kuzingatia mambo mengine tena. Nataka kuimba na kucheza na kufanya mazoezi ya viungo vya mwili Kiukweli nahisi ikiwa sisi sote tungelinda ulimwengu kama tabia, kama tamaduni, hakuna mtu angekua mwanaharakati wa hali ya hewa wakati wote Kama biashara zimekua endelevu, kama gridi ya umeme inaendesha kwa nishati mbadala, kama mtaala wa shule unatufundisha kuwa kuzingatia ulimwengu ni moja ya utu wetu labda naweza fanya mazoezi ya sarekasi tena. Au sivyo, Abuelita ? Tunaweza fanya hili. Yote najaribu kufanya na kazi yangu ni kuwapa watu wengine mtazamo chanya wa matumaini. Lakini ni ngumu kidogo. Kuna tamaa, kuna kiburi, kuna pesa, na pia uyakinifu. Hulka ya watu hurahisisha kuongelea haya mambo, lakini napata wakati mgumu kuwafunza. Nataka wajiamini kwa kujitahidi kila wakati. Nawatakia kua na moyo na ujasiri wa kupenda ulimwengu, kamaulivyonifunza. Nimeandika barua hii kukushukuru. Shukrani kwa kunikaribisha kupenda ulimwengu tangu nizaliwe. Shukran kwa kucheka kwa kila kitu. Shukrani kwa kunifunza kua matumaini na matarajio ndizo zana za nguvu tulizo nazo kukumbana na shida yoyote. Nafanya hili kwa kuwa ulinionyesha kwamba uthabiti, upendo na ujuzi vinatosha kuleta mabadiliko. Nataka kurudi Mexico nikutembelee. Nataka kukuonyesha picha ya vitu nilivyofanya. Nataka kukuonyesha sheria ya hali ya hewa tuliyoweza kupitisha. Nataka kunusa maua na kupigania haki ya hali ya hewa pamoja nawe Te quiero mucho.(Nakupenda sana) Nakupenda Xiye. [Te quiero mucho. Xiye.]