Karibu tena. Wakanada wengi hawatahitaji kushawishiwa kuwa chanjo ya UVIKO inastahili, pindi ifikapo. Lakini jinsi ulivyosikia, Wakanada wengi wapo na maswali. Kwa hivyo kujibu baadhi, Dkt. Cora Constantinescu, mtaalam wa magonjwa ya kuambukizwa anayehudumu katika kliniki ya kuchunguza mienendo ya kusita kuchanjwa katika hospitali ya watoto ya Alberta iliyoko Caligary. Na daktari, sikujua sehemu kama yako ipo Ni nani hasa huletwa kwako? Tumeifanya kuwa mchakato nyoofu na tumefikia jamii ya matabibu na kuwaambia kuwa tuko hapa kuwaunga mkono wanapotuletea wagonjwa. Unaona kushawishi watu kuchanjwa kuwa kazi yako? Naona kuwa ni kazi yangu kuwasaidia watu wanapofanya uamuzi kuchanja. Mdahalo huo huwa vipi? Unaanzia wapi? Ninaanza kwa kujikumbusha kila wakati kuwa katika kiini cha kila miadi ya kusita kuchanjwa ni mzazi anayejaribu uamuzi mwafaka kwao na familia yao. Na inahitaji ukakamavu mwingi kuja kwa sababu wanapambana na uoga mwingi na habari potofu, na kwa ujumla ukosefu wa uaminifu. Kwa hivyo tunatumia muda mwingi kujenga uhusiano na uaminifu na kila familia, kuwaelewa ilituweze kubinafsisha mawasiliano na ujumbe tunaowapa kuhusu chanjo. Halafu tunahushisha afya ya umma kwa karibu kisha wanafululiza na kupeana chanjo. Na inashangaza kuwa unasema kuwa kuna huu ukosefu wa uaminifu. Unawezaje kuanza kushauri serikali ya mkoani, serikali ya mtaa, ama serikali ya jumuiya kuiunda? Nafikiri kuwa tunapofikiria kuhusu uaminifu, lazima tufikirie kwa kiwango cha ubinafsi na kwa kiwango cha umma. na kwa kiwango binafsi, inarejelea hii wazo ya kuweka kwa taswira na kuelewa ni nini manufaa ya chanjo na hatari ya ugonjwa kwa kila mmoja wetu. Kwa hivyo ikija kwa UVIKO kwa mfano, Ningependa kuhimiza kila mkanada kufikiria kile hili janga, limewamelifanyia, na kile limewanyanganya. Kwa hivyo, inaweza kuwa wengine wamepoteza wapendwa wao, wengine wamepoteza kutangamana kwao, uwezekano wa watoto kwenda shule. Kuna gharama kwa kila mmoja wetu na kwa hivyo, kuna manufaa kwa kila mmoja wetu. Halafu, itabidi sote twende kuchanjwa ili tuonyeshe kuwa tuko kwa hili pamoja. Halafu tunapozidi kwenda kiwango cha umma, Ni muhimu sana kuanza kujenga uhusiano huu. Na ni kazi ngumu kutekeleza, kwa sababu inabidi umezingatia utata wa tabia za binadamu, hususan kuhusu UVIKO-19. Na taasisi zetu za afya haziwezi fanya hii pekee yao. Sitaki hii kutokezea kama swali ya kijinga, lakini ni vipi unajua unachofanya kimefaulu? Kwa sababu sio wewe unayepeana chanjo, sawa? Unafuatilia viwango vya mafanikio? Kulingana na jinsi tunavyoitazama ni uwezekano wa takriban asilimia 50 mpaka 60. kuwa wagonjwa watafululiza kupokea chanjo. baada ya kuhudhuria kliniki yetu. na katika ulimwengu wa kusita kuchanjwa hayo ni mafanikio. Huu umekuwa mdahalo wa kusisimua. Dkt. Constantinescu, asante sana kwa muda wako. nimefurahia kuwa hapa, asante kwa kunialika.