WEBVTT 00:00:01.912 --> 00:00:03.237 Hauwajui. 00:00:04.150 --> 00:00:05.436 Hauwaoni. 00:00:06.405 --> 00:00:08.408 Lakini daima wapo wanazunguka, 00:00:09.404 --> 00:00:11.084 wananong'oneza, 00:00:11.108 --> 00:00:12.922 wakitengeneza mipango ya siri, 00:00:13.700 --> 00:00:17.382 wakijenga jeshi la mamilioni ya wanajeshi. 00:00:18.826 --> 00:00:20.617 Na wanapoamua kushambulia, 00:00:21.435 --> 00:00:23.697 wanashambulia kwa wakati mmoja. 00:00:27.130 --> 00:00:28.909 Ninaongelea kuhusu bakteria. NOTE Paragraph 00:00:28.933 --> 00:00:30.258 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:00:30.282 --> 00:00:32.517 Mlidhani ninaongelea kuhusu nani? NOTE Paragraph 00:00:34.401 --> 00:00:37.595 Bakteria wanaishi kwenye jamii kama tu binadamu. 00:00:37.619 --> 00:00:38.892 Wana familia, 00:00:38.916 --> 00:00:40.067 wanaongea, 00:00:40.091 --> 00:00:41.933 na wanapanga shughuli zao. 00:00:41.957 --> 00:00:44.614 Na kama tu binadamu, wanahila, waongo, 00:00:44.638 --> 00:00:46.772 na wengine hata wanadanganyana wenyewe. 00:00:48.127 --> 00:00:51.974 Je kama nikikuambia kua tunaweza kusikiliza mazungumzo ya bakteria 00:00:51.998 --> 00:00:55.572 na kutafsiri taarifa zao za siri kuwa lugha ya binadamu? 00:00:56.255 --> 00:01:01.053 Na kama je nikiwaambia kuwa kutafsiri mazungumzo ya bakteria kutaokoa maisha? 00:01:02.519 --> 00:01:04.290 Nina PhD ya nanofizikia, 00:01:04.314 --> 00:01:08.690 na nimetumia teknolojia ya nano kuunda chombo cha kutafsiri cha muda halisi 00:01:08.714 --> 00:01:11.033 kinachoweza kupeleleza kwenye jamii za bakteria 00:01:11.057 --> 00:01:13.973 na kutupa rekodi za nini bakteria wanafanya. NOTE Paragraph 00:01:16.123 --> 00:01:17.719 Bakteria wanaishi kila sehemu. 00:01:17.743 --> 00:01:20.072 Wako kwenye udongo, kwenye samani zetu 00:01:20.096 --> 00:01:21.407 na ndani ya miili yetu. 00:01:22.083 --> 00:01:26.622 Ki ukweli, asilimia 90 ya seli zote hai kwenye huu ukumbi ni bakteria. 00:01:27.685 --> 00:01:29.514 Baadhi ya bakteria ni wazuri kwetu; 00:01:29.538 --> 00:01:32.750 wanatusaidia kumeng'enya chakula au kutengeneza dawa. 00:01:32.774 --> 00:01:34.866 Na baadhi ya bakteria na wabaya kwetu: 00:01:34.890 --> 00:01:36.784 wanasababisha magonjwa na kifo. 00:01:37.794 --> 00:01:40.210 Kushirikisha kazi zote bakteria walizonazo, 00:01:40.234 --> 00:01:42.306 wanatakiwa wawe na uwezo wa kupanga, 00:01:42.330 --> 00:01:44.371 na wanafanya hivyo kama tu sisi binadamu -- 00:01:44.395 --> 00:01:45.554 kwa mawasiliano. 00:01:46.751 --> 00:01:48.226 Lakini badala ya kutumia maneno, 00:01:48.250 --> 00:01:51.192 wanatumia molekuli za ishara kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe. 00:01:51.903 --> 00:01:53.340 Bakteria wanapokuwa wachche, 00:01:53.364 --> 00:01:56.107 molekuli za ishara zinatiririka nje, 00:01:56.131 --> 00:01:58.636 kama kelele za mtu peke yake jangwani. 00:01:59.518 --> 00:02:03.510 Lakini kukiwa na bakteria wengi, molekuli za ishara zinajikusanya, 00:02:03.534 --> 00:02:06.526 na bakteria wanaanza kuhisi kuwa hawapo peke yao. 00:02:07.309 --> 00:02:08.643 Wanasikilizana wenyewe. 00:02:09.459 --> 00:02:12.275 Kwa njia hii, wanapima wako wangapi 00:02:12.299 --> 00:02:15.620 na wanapokuwa wengi wa kutosha kuanzisha hatua mpya. 00:02:16.575 --> 00:02:20.432 Na pale molekuli za ishara zinafika kizingiti flani, 00:02:20.456 --> 00:02:23.577 bakteria wote wanahisi kwa mara moja kua wanahitaji kutenda 00:02:23.601 --> 00:02:24.919 kwa tendo hilo hilo. NOTE Paragraph 00:02:25.967 --> 00:02:30.293 Hivyo mazungumzo ya bakteria yanakuwa na mwanzo na jibu, 00:02:30.317 --> 00:02:33.389 uzalishaji wa molekuli na majibu yake. 00:02:35.094 --> 00:02:38.434 Kwenye utafiti wangu, nimelenga kupeleleza kwenye jamii za bakteria 00:02:38.458 --> 00:02:39.861 ndani ya mwili wa binadamu. 00:02:40.343 --> 00:02:41.588 Inafanyaje kazi? 00:02:42.385 --> 00:02:44.300 Tunasampuli kutoka kwa mgonjwa. 00:02:44.324 --> 00:02:46.862 Inaweza kuwa ni sampuli ya damu au mate. 00:02:47.304 --> 00:02:49.841 Tunapiga elektroni ndani ya sampuli, 00:02:49.865 --> 00:02:53.785 elektroni zitaingilia na molekuli zozote za mazungumzo zilizopo, 00:02:53.809 --> 00:02:56.190 na huu muingiliano utatupa taarifa 00:02:56.214 --> 00:02:58.105 ya aina ya bakteria, 00:02:58.129 --> 00:02:59.800 aina ya mawasiliano 00:02:59.824 --> 00:03:02.117 na kiasi gani bakteria wanazungumza. NOTE Paragraph 00:03:04.269 --> 00:03:06.590 Lakini inakuaje pale bakteria wakizungumza? 00:03:07.747 --> 00:03:11.507 Kabla sijaunda chombo cha kutafsiri, 00:03:11.531 --> 00:03:15.377 dhana yangu ya kwanza ilikua bakteria watakua na lugha ya halisi, 00:03:15.401 --> 00:03:18.579 kama vichanga ambao bado hawajaunda maneno na sentensi. 00:03:19.208 --> 00:03:22.129 Wanapocheka, wanafuraha; wanapolia, wanahuzuni. 00:03:22.153 --> 00:03:23.303 Rahisi kama hivyo. 00:03:24.008 --> 00:03:28.123 Lakini bakteria walionekana kutokuwa karibu na halisi kama nilivyodhani. 00:03:28.615 --> 00:03:30.855 Molekuli sio tu molekuli. 00:03:30.879 --> 00:03:33.633 Inaweza kumaanisha vitu tofauti kulingana na muktadha, 00:03:34.404 --> 00:03:37.346 kama tu vilio vya watoto vinavyomaanisha vitu tofauti: 00:03:37.370 --> 00:03:39.140 saa nyingine mtoto ana njaa, 00:03:39.164 --> 00:03:40.358 saa nyingine amelowa, 00:03:40.382 --> 00:03:42.401 saa nyingine ameumia au anaogopa. 00:03:42.425 --> 00:03:44.775 Wazazi wanajua jinsi ya kusoma hivi vilio. 00:03:45.624 --> 00:03:47.506 Na kua chombo kizuri cha kutafsiri, 00:03:47.530 --> 00:03:50.503 kinatakiwa kiwe na uwezo wa kusoma molekuli za ishara 00:03:50.527 --> 00:03:54.588 na kuzitafsiri kulingana na muktadha. 00:03:55.497 --> 00:03:56.648 Na nani anajua? 00:03:56.672 --> 00:03:58.833 Labda Tafsiri ya Google inaweza kuiptisha hii. NOTE Paragraph 00:03:58.857 --> 00:04:01.226 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:02.386 --> 00:04:04.104 Hebu niwape mfano. 00:04:04.128 --> 00:04:07.717 Nimeleta baadhi ya taarifa za bakteria zinazoweza kuwa ngumu kuelewa 00:04:07.741 --> 00:04:08.892 kama hauna mafunzo, 00:04:08.916 --> 00:04:10.261 lakini jaribu kuangalia. NOTE Paragraph 00:04:11.548 --> 00:04:13.467 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:14.959 --> 00:04:18.436 Hii ni familia ya bakteria yeye furaha ambayo imemshambulia mgonjwa. 00:04:20.261 --> 00:04:22.294 Wacha tuwaite familia ya Montague. 00:04:23.920 --> 00:04:27.381 Wanatumia wote rasilimali, wanazaliana, wanakua. 00:04:28.294 --> 00:04:30.273 Siku moja, wanapata mgeni mpya, 00:04:32.746 --> 00:04:34.513 familia ya bakteria Capulet. NOTE Paragraph 00:04:34.537 --> 00:04:35.687 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:36.157 --> 00:04:38.947 Kila kitu ni sawa, alimradi wanafanya kazi kwa pamoja. 00:04:40.377 --> 00:04:43.383 Lakini kitu kisichopangwa kinatokea. 00:04:44.449 --> 00:04:48.667 Romeo wa Montague anakua na mahusiano na Juliet wa Capulet. NOTE Paragraph 00:04:48.691 --> 00:04:49.841 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:50.978 --> 00:04:53.873 Na ndio, wanagawiana chembe za urithi. NOTE Paragraph 00:04:53.897 --> 00:04:56.006 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:58.260 --> 00:05:01.381 Sasa, uhamisho wa kinasaba unaweza kuwa hatari kwa wakina Montague 00:05:01.405 --> 00:05:05.365 waliokuwa na matarajio ya kuwa familia pekee kwenye mgonjwa waliomshambulia, 00:05:05.365 --> 00:05:06.999 kugawana chembe za urithi kunachangia 00:05:06.999 --> 00:05:09.777 kwa wakina Capulet kutengeneza kinga kwa dawa. 00:05:11.747 --> 00:05:16.392 Hivyo wakina Montague wanaanza kuongea kwa ndani kuondoa hii familia nyingine 00:05:16.416 --> 00:05:18.138 kwa kutoa molekuli hii. NOTE Paragraph 00:05:18.688 --> 00:05:19.838 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:05:20.700 --> 00:05:22.062 Na kwa maelezo: NOTE Paragraph 00:05:22.372 --> 00:05:23.978 [Hebu turatibu shambulizi.] NOTE Paragraph 00:05:24.002 --> 00:05:25.293 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:05:25.639 --> 00:05:27.430 Hebu turatibu shambulizi. 00:05:29.148 --> 00:05:32.248 Na kila mtu mara moja akaitikia 00:05:32.272 --> 00:05:36.595 kwa kutoa sumu itakayoua ile familia nyingine. NOTE Paragraph 00:05:36.619 --> 00:05:38.387 [Ondoa!] NOTE Paragraph 00:05:40.129 --> 00:05:42.261 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:05:43.338 --> 00:05:47.731 Wakina Capulet wakajibu kwa kuita shambulizi la kujibu. NOTE Paragraph 00:05:47.755 --> 00:05:48.911 [Shambulia!] NOTE Paragraph 00:05:48.935 --> 00:05:50.360 Na wakawa na vita. NOTE Paragraph 00:05:52.090 --> 00:05:56.708 Hii ni video ya bakteria wa ukweli wakipigana na viumbe kama upanga, 00:05:56.732 --> 00:05:58.345 ambapo wanajaribu kuuana 00:05:58.369 --> 00:06:01.207 kwa kuchomana kihalisi na kupasuana wenyewe. 00:06:02.784 --> 00:06:06.745 Familia ya yeyote atakayeshinda hii vita anakuwa bakteria mkuu. NOTE Paragraph 00:06:08.360 --> 00:06:11.633 Hivyo ninachoweza kufanya ni kuchunguza mazungumzo ya bakteria 00:06:11.633 --> 00:06:13.725 yanayopelekea tabia tofauti za kwa pamoja 00:06:13.725 --> 00:06:15.154 kama ugomvi mliyouona. 00:06:15.633 --> 00:06:18.550 Na nilichofanya ni kupeleleza kwenye jamii za bakteria 00:06:18.574 --> 00:06:20.617 ndani ya mwili wa binadamu 00:06:20.641 --> 00:06:22.357 kwenye wagonjwa hospitalini. 00:06:22.737 --> 00:06:25.207 Nilifuatilia wagonjwa 62 kwenye jaribio, 00:06:25.231 --> 00:06:28.979 ambapo nilipima sampuli ya mgonjwa kwa aina moja ya shambulizi, 00:06:29.003 --> 00:06:32.332 bila kujua majibu ya vipimo vya kawaida. NOTE Paragraph 00:06:32.356 --> 00:06:36.576 Basi, kwenye upimaji wa bakteria, 00:06:36.600 --> 00:06:38.581 sampuli inasambazwa kwenye kisahani, 00:06:38.605 --> 00:06:41.729 na kama bakteria watakua ndani ya siku tano, 00:06:41.753 --> 00:06:44.117 mgonjwa anagunduliwa kama ameathirika. 00:06:45.842 --> 00:06:48.661 Nilipomaliza utafiti na kulinganisha majibu ya chombo 00:06:48.685 --> 00:06:51.923 na vipimo vya kawaida na vipimo vya kuhakikisha, 00:06:51.947 --> 00:06:53.347 nilishtuka. 00:06:53.371 --> 00:06:57.082 Ilikua inashangaza zaidi kuliko nilivyowahi kutarajia. NOTE Paragraph 00:06:58.011 --> 00:07:00.150 Ila kabla sijawaambia nini chombo kilionyesha, 00:07:00.174 --> 00:07:03.168 ningependa kuwaambia kuhusu mgonjwa mahsusi niliomfuatilia, 00:07:03.192 --> 00:07:04.359 binti mdogo. 00:07:04.803 --> 00:07:06.253 Alikua na cystic fibrosis, 00:07:06.277 --> 00:07:10.017 ugonjwa wa kurithi uliofanya mapafu yake kuathiriwa kirahisi na bakteria. 00:07:10.837 --> 00:07:13.233 Huyu binti hakua sehemu ya majaribio. 00:07:13.257 --> 00:07:16.084 Nilimfuatilia kwa sababu nilijua kutoka kwenye taarifa zake 00:07:16.108 --> 00:07:18.208 kua hakuwahi kupata mashambulizi kabla. 00:07:19.243 --> 00:07:21.558 Mara moja kwa mwezi, huyu binti alienda hospitali 00:07:21.582 --> 00:07:24.236 kuweka sampuli ya kohozi ambayo alitemea kwenye kikombe. 00:07:24.916 --> 00:07:28.042 Hii sampuli ilisafirishwa kwa uchunguzi wa bakteria 00:07:28.066 --> 00:07:29.996 huko maabara kuu 00:07:30.020 --> 00:07:33.486 ili madaktari watende haraka iwapi wangekuta shambulizi. 00:07:34.099 --> 00:07:36.973 Iliniruhusu mimi kupima chombo changu kwa sampuli zake pia. NOTE Paragraph 00:07:37.355 --> 00:07:40.767 Miezi miwili ya mwanzo nilipima sampuli zake, hakukua na kitu. 00:07:41.794 --> 00:07:42.961 Lakini mwezi wa tatu, 00:07:42.985 --> 00:07:45.641 Niligundua mazungumzo ya bakteria kwenye sampuli yake. 00:07:46.473 --> 00:07:49.585 Bakteria walikua wanashirikiana kuharibu tishu ya pafu lake. 00:07:50.534 --> 00:07:54.545 Lakini vipimo vya kawaida havikuonyesha bakteria kabisa. 00:07:55.711 --> 00:07:57.630 Nilipima tena mwezi ujao, 00:07:57.654 --> 00:08:01.282 na niliona kua yale mazungumzo ya bakteria yamekua makali zaidi. 00:08:02.167 --> 00:08:04.919 Bado, vipimo vya kawaida havikuonyesha chochote. 00:08:06.456 --> 00:08:10.100 Utafiti wangu ukaisha, lakini nusu mwaka baadae, nikafuatilia hali yake 00:08:10.124 --> 00:08:13.365 kuona kama bakteria niliowajua pekee walipotea 00:08:13.389 --> 00:08:15.404 bila muingilio wa tiba. 00:08:16.350 --> 00:08:17.500 Hawakupotea. 00:08:18.020 --> 00:08:20.853 Yule binti sasa alikua amegundulika na mashambulio makali 00:08:20.877 --> 00:08:22.195 ya bakteria wabaya. 00:08:23.511 --> 00:08:27.589 Walikua ni wale wale bakteria chombo changu kiligundua kabla. 00:08:28.537 --> 00:08:31.033 Na licha ya ukali wa dawa za kutibu, 00:08:31.057 --> 00:08:33.586 ilikua inashindikana kuondoa mashambulizi. 00:08:34.816 --> 00:08:37.898 Madaktari waliona kua asingeweza kufikia miaka ya 20. NOTE Paragraph 00:08:40.404 --> 00:08:42.509 Nilipopima kwenye sampuli ya binti huyu, 00:08:42.533 --> 00:08:44.732 kifaa changu kilikua kwenye hatua za mwanzo. 00:08:44.756 --> 00:08:47.455 Sikujua hata kama njia yangu ilifanya kazi kabisa, 00:08:47.479 --> 00:08:49.626 hivyo nikawa na makubaliano na madaktari 00:08:49.650 --> 00:08:51.511 kutowaambia chombo changu kilichoonyesha 00:08:51.535 --> 00:08:53.675 ili kutokuharibu matibabu yao. 00:08:53.861 --> 00:08:56.914 Hivyo nilipoona haya majibu ambayo hata hayakuwa yamehakikishwa, 00:08:56.938 --> 00:08:58.290 sikudhubutu kusema 00:08:58.314 --> 00:09:01.121 ka sababu kutibu mgonjwa bila mashambulizi halisi 00:09:01.145 --> 00:09:03.755 pia ina matokeo mabaya kwa mgonjwa. 00:09:05.092 --> 00:09:06.714 Lakini sasa tunajua bora, 00:09:06.738 --> 00:09:10.137 na kuna wavulana na wasichana wadogo wengi bado wanaweza kuokolewa 00:09:11.172 --> 00:09:14.596 kwa sababu, bahati mbaya, hii hali inatokea mara nyingi. 00:09:14.620 --> 00:09:16.163 Wagonjwa wanaathirika, 00:09:16.187 --> 00:09:19.664 bakteria kwa namna flani hawaonekani kwenye vipimo vya kawaida, 00:09:19.688 --> 00:09:23.540 na ghafla, maambukizi yanatokea ndani ya mgojwa na dalili kali. 00:09:23.564 --> 00:09:25.722 Na kwenye mda huo, tayari tumechelewa. NOTE Paragraph 00:09:27.219 --> 00:09:30.773 Majibu ya kushangaza ya wagonjwa 62 niliowafuatilia 00:09:30.797 --> 00:09:33.340 yalikua chombo changu kilishika mazungumzo ya bakteria 00:09:33.364 --> 00:09:35.580 kwa zaidi ya nusu ya sampuli za wagonjwa 00:09:35.604 --> 00:09:38.875 ambao walikua wamegundulika bila kitu kwa njia za upimaji za kawaida. 00:09:39.381 --> 00:09:43.055 Kwa maneno mengine, zaidi ya nusu ya hawa wagonjwa walirudi nyumbani wakiwaza 00:09:43.079 --> 00:09:44.764 kua wako huru na maambukizi, 00:09:44.788 --> 00:09:47.536 japokuwa kihalisi walibeba bakteria hatari. 00:09:49.257 --> 00:09:51.554 Ndani ya wagonjwa waliopimwa vibaya, 00:09:51.578 --> 00:09:54.598 bakteria walikuwa wanaandaa shambulizi la kuambatanishwa. 00:09:55.530 --> 00:09:57.218 Walikua wananong'onezana. 00:09:57.892 --> 00:09:59.523 Ninachoita "mnong'ono wa bakteria" 00:09:59.547 --> 00:10:02.551 ni bakteria ambao njia za kawaida za upimjai haziwezi kuona. 00:10:03.383 --> 00:10:07.326 Mpaka sasa, ni chombo cha kutafsiri tu kinachoweza kudaka hao wanong'onezaji. 00:10:08.364 --> 00:10:11.767 Ninaamini kua mda uliopo ambao bakteria bado wananong'onezana 00:10:11.791 --> 00:10:14.778 ni nafasi nzuri ya matibabu ya malengo. 00:10:15.608 --> 00:10:18.741 Kama yule binti angekua ametibiwwa kwenye kuu mda wenye nafasi, 00:10:18.765 --> 00:10:21.266 ingekua inawezekana kuua bakteria 00:10:21.290 --> 00:10:22.755 kwenye hatua yao ya mwanzo, 00:10:22.779 --> 00:10:24.885 kabla maambukizi kuwa nje ya uwezo. NOTE Paragraph 00:10:27.131 --> 00:10:31.102 Nilichopitia na huyu binti mdogo kumenifanya niamue kufanya ninachoweza 00:10:31.126 --> 00:10:33.331 kusukuma hii teknolojia kwenye hospitali. 00:10:34.212 --> 00:10:35.363 Pamoja na madaktari, 00:10:35.387 --> 00:10:38.356 tayari ninafanya kazi kutumia hiki kifaa kwenye kliniki 00:10:38.380 --> 00:10:40.202 kutambua maambukizi ya kwanza. NOTE Paragraph 00:10:41.319 --> 00:10:44.563 Japo bado haijajulikana jinsi madaktari watatibu wagonjwa 00:10:44.587 --> 00:10:46.400 kwenye kipindi cha mnong'ono, 00:10:46.424 --> 00:10:50.127 hiki kifaa kinaweza kusaidia madaktari kuwa makini na wagonjwa kwenye hatari. 00:10:50.548 --> 00:10:53.830 Kinaweza kuwasaidia kuhakikisha kama tiba imefanya kazi au la, 00:10:53.854 --> 00:10:56.618 na inaweza kusaidia kujibu maswali rahisi: 00:10:56.642 --> 00:10:58.372 Mgonjwa ana mashambulizi? 00:10:58.396 --> 00:11:00.206 Na bakteria wako wanapanga nini? NOTE Paragraph 00:11:00.958 --> 00:11:02.745 Bakteria wanaongea, 00:11:02.769 --> 00:11:04.795 wanatengeneza mipango ya siri, 00:11:04.819 --> 00:11:07.642 na wanatumiana taarifa za siri. 00:11:08.253 --> 00:11:10.932 Lakini sio tu kuawaangalia wenyewe wakinong'onezana, 00:11:10.956 --> 00:11:13.423 sisi sote tunaweza kujifunza lugha ya siri 00:11:13.447 --> 00:11:16.326 na kua wenyewe wanong'onezi wa bakteria. 00:11:16.973 --> 00:11:18.687 Na, kama bakteria wangesema, 00:11:19.656 --> 00:11:22.754 "3-oxo-C12-aniline." NOTE Paragraph 00:11:23.763 --> 00:11:24.931 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:11:24.955 --> 00:11:26.040 (Makofi) NOTE Paragraph 00:11:26.064 --> 00:11:27.248 Asanteni.