1 00:00:06,407 --> 00:00:10,697 Bibi muongeaji na mhalifu anayezurura wakizozana katika barabara chafu. 2 00:00:10,697 --> 00:00:14,798 Muuza Biblia anampeleka mwanafalsafa mwenye mguu mmoja bandani. 3 00:00:14,798 --> 00:00:19,641 Fundi anaesafiri anamfundisha mwanamke kiziwi neno lake la kwanza shambani. 4 00:00:20,231 --> 00:00:22,561 Kutoka shambani kwake vijijini Georgia, 5 00:00:22,561 --> 00:00:25,053 akizungukwa na kundi la ndege wa kufugwa, 6 00:00:25,053 --> 00:00:27,533 Flannery O'Connor aliandika simulizi za waliotengwa, 7 00:00:27,533 --> 00:00:31,363 wavamizi na wasioleweka waliunda dunia aliyoifahamu vizuri: 8 00:00:31,753 --> 00:00:33,013 Marekani Kusini. 9 00:00:33,513 --> 00:00:34,962 Alichapisha riwaya mbili, 10 00:00:35,202 --> 00:00:37,652 lakini anajulikana zaidi kwa simulizi zake fupi, 11 00:00:37,852 --> 00:00:42,612 ambazo zilichunguza maisha ya mji mdogo kwa lugha kali, na ucheshi usio wa kawaida, 12 00:00:42,752 --> 00:00:45,152 na mazingira ya kufurahisha yenye karaha. 13 00:00:45,482 --> 00:00:48,538 Kwenye muda wake wa ziada O'Connor alichora katuni, 14 00:00:48,538 --> 00:00:51,088 na uandishi wake pia umejaa masihara. 15 00:00:51,088 --> 00:00:56,088 Kwenye simulizi zake, mama na sura "pana na ya upole kama kabichi", 16 00:00:56,768 --> 00:00:59,858 mwanaume ana nguvu sana kama "dekio la sakafuni", 17 00:01:00,268 --> 00:01:03,217 na mwili wa mwanamke mmoja una umbo kama "chombo cha kuzika". 18 00:01:04,247 --> 00:01:06,787 Majina ya wahusika wake yamejawa ujanja. 19 00:01:07,147 --> 00:01:10,127 Chukulia simulizi "Maisha Unayoyaokoa Yanaweza Kuwa ya Kwako", 20 00:01:10,257 --> 00:01:13,257 ambapo mtembezi mwenye mkono mmoja Tom Shiftlet anaenda kwenye maisha 21 00:01:13,257 --> 00:01:15,767 ya ajuza mmoja aitwae Lucynell Crater 22 00:01:15,767 --> 00:01:17,737 na binti yake ambaye ni kiziwi na bubu. 23 00:01:17,737 --> 00:01:19,767 Japo mama Carter anajiamini, 24 00:01:19,767 --> 00:01:21,967 nyumba yake iliyojitenga inaanguka. 25 00:01:22,197 --> 00:01:25,107 Mwanzoni, tunaweza kushuku nia za Shiflet 26 00:01:25,107 --> 00:01:27,297 alipojitolea kusaidia kwenye nyumba, 27 00:01:27,297 --> 00:01:29,957 lakini O'Connor anaenda kuonyesha kuwa yule ajuza ni 28 00:01:29,957 --> 00:01:32,547 mjanja kama mgeni wake asiotarajiwa- 29 00:01:32,547 --> 00:01:35,697 na kutikisa mategemeo ya msomaji kuhusu nani ana faida zaidi. 30 00:01:35,857 --> 00:01:38,467 Kwa O'Connor, hamna somo lililokuwa na kizuizi. 31 00:01:38,847 --> 00:01:40,637 Japo alikuwa ni Mkatoliki aliyejitoa, 32 00:01:40,637 --> 00:01:42,767 hakuogopa kufuatilia uwezekano 33 00:01:42,767 --> 00:01:45,007 wa mawazo mema na tabia isiyo njema, 34 00:01:45,007 --> 00:01:46,967 inayokuwepo kwa mtu mmoja. 35 00:01:47,027 --> 00:01:49,317 Kwenye riwaya yake ya Wajeuri Wanaiondolea Mbali, 36 00:01:49,317 --> 00:01:52,797 mhusika mkuu anatingwa na mawazo ya kuwa mtu wa Mungu - 37 00:01:52,987 --> 00:01:55,637 lakini pia anawasha moto na kuua. 38 00:01:55,757 --> 00:01:59,907 Kitabu kinaanza na nabii amaesita akiwa kwenye nafasi yenye utata: 39 00:02:00,037 --> 00:02:04,237 "Mjomba wa Francis Marion Tarwater alikua amekufa kwa nusu siku tu 40 00:02:04,287 --> 00:02:07,597 pale huyo mvulana alipolewa sana akashindwa kumalizia kuchimba kaburi lake". 41 00:02:07,597 --> 00:02:11,648 Hii inamuacha mpita njia "kuvuta mwili kutoka kwenye meza ya chai 42 00:02:11,668 --> 00:02:13,728 ambapo ulikuwa umekaa bado na kuuzika [...] 43 00:02:13,728 --> 00:02:16,358 na udongo wa kutosha kwa juu kuzuia mbwa kuufukua". 44 00:02:17,068 --> 00:02:19,108 Japokuwa siasa zake bado ni za kulumbana, 45 00:02:19,108 --> 00:02:22,518 bunilizi ya O'Connor inaweza pia kulinganishwa na ubaguzi wa Kusini. 46 00:02:23,218 --> 00:02:25,768 Kwenye "Kila Kinachopanda Lazima Kikutane", 47 00:02:25,788 --> 00:02:28,508 anaelezea mvulana anayechukizwa na upendeleo wa mama yake. 48 00:02:28,698 --> 00:02:31,598 Lakini simulizi inaelezea kuwa ana mapungufu yake 49 00:02:31,658 --> 00:02:34,048 na inasema kwamba kuyagundua mabaya tu 50 00:02:34,048 --> 00:02:36,598 haitetei tabia yake kutokuthibitiwa. 51 00:02:36,608 --> 00:02:39,857 Hata O'Connor anavyochunguza mambo potofu ya ubinadamu, 52 00:02:39,917 --> 00:02:42,577 anaacha mlango wa ukombozi wazi kidogo. 53 00:02:42,817 --> 00:02:45,007 Kwenye "Mwanaume Mzuri ni Mgumu Kupata", 54 00:02:45,007 --> 00:02:48,897 anamkomboa ajuza anayeteseka kwa kumsamehe mshitakiwa aliyekubuhu, 55 00:02:48,992 --> 00:02:51,232 hata anavyoikaribia familia yake. 56 00:02:51,762 --> 00:02:54,987 Japo tunaweza kushtushwa na malipo anayolipa huyu mama kusamehewa, 57 00:02:54,987 --> 00:02:57,427 tunalazimika kukabiliana na yanayoendelea kwenye mda 58 00:02:57,427 --> 00:03:00,367 tunapoweza kuzingatia kuwa ukatili au ubaya. 59 00:03:00,367 --> 00:03:02,777 Uwezo wa O'Connor wa ajabu 60 00:03:02,777 --> 00:03:06,131 na tafiti zake za kujitenga na ushirikina wa Kusini 61 00:03:06,391 --> 00:03:09,681 ulimpelekea kutambuliwa kama mwandishi wa Kigothi wa Kusini. 62 00:03:09,681 --> 00:03:12,371 Lakini kazi yake ilisogea kupita tabia za kijinga kabisa 63 00:03:12,371 --> 00:03:14,936 na za kutisha zilizohusishwa na huo mtindo 64 00:03:14,936 --> 00:03:18,316 kuvumbua tofauti na mchanganyiko wa tabia za binadamu. 65 00:03:18,336 --> 00:03:20,776 Alijua baadhi ya hii tofauti ilileta karaha, 66 00:03:20,796 --> 00:03:23,286 na kuwa hadithi zake zingekuwa na ladha inayohitajika - 67 00:03:23,286 --> 00:03:25,976 lakini alisikia raha kuwachanganya wasomaji wake, 68 00:03:26,136 --> 00:03:29,136 O'Connor alikufa kwa lupus akiwa na miaka 39, 69 00:03:29,136 --> 00:03:33,396 baada ya ugonjwa kumweka shambani mwake Georgia kwa miaka kumi na mbili. 70 00:03:33,556 --> 00:03:35,036 Kwenye miaka hiyo, 71 00:03:35,036 --> 00:03:37,316 aliandika kazi zake nyingi alizokuwa akiwaza. 72 00:03:37,416 --> 00:03:40,246 Uwezo wake wa kuhama kati ya maudhi na uvumbuzi 73 00:03:40,376 --> 00:03:44,536 unaendelea kuvutia wasomaji kwenye dunia yake ya kufikirika isiyoisha. 74 00:03:44,696 --> 00:03:47,176 Kama mhusika Tom Shirlet anavyosema, 75 00:03:47,436 --> 00:03:49,316 mwili ni "kama nyumba: 76 00:03:49,416 --> 00:03:50,696 haiendi popote, 77 00:03:50,766 --> 00:03:53,750 lakini roho, mwanamke, ni kama gari moto: 78 00:03:53,880 --> 00:03:56,150 daima lipo kwenye mwendo".