Bibi muongeaji na mhalifu anayezurura
wakizozana katika barabara chafu.
Muuza Biblia anampeleka mwanafalsafa
mwenye mguu mmoja bandani.
Fundi anaesafiri anamfundisha mwanamke
kiziwi neno lake la kwanza shambani.
Kutoka shambani kwake vijijini Georgia,
akizungukwa na kundi la ndege wa kufugwa,
Flannery O'Connor aliandika simulizi
za waliotengwa,
wavamizi na wasioleweka waliunda
dunia aliyoifahamu vizuri:
Marekani Kusini.
Alichapisha riwaya mbili,
lakini anajulikana zaidi
kwa simulizi zake fupi,
ambazo zilichunguza maisha ya mji mdogo kwa
lugha kali, na ucheshi usio wa kawaida,
na mazingira ya kufurahisha yenye karaha.
Kwenye muda wake wa ziada O'Connor
alichora katuni,
na uandishi wake pia
umejaa masihara.
Kwenye simulizi zake, mama na sura
"pana na ya upole kama kabichi",
mwanaume ana nguvu sana kama "dekio la
sakafuni",
na mwili wa mwanamke mmoja
una umbo kama "chombo cha kuzika".
Majina ya wahusika wake yamejawa ujanja.
Chukulia simulizi "Maisha Unayoyaokoa
Yanaweza Kuwa ya Kwako",
ambapo mtembezi mwenye mkono mmoja
Tom Shiftlet anaenda kwenye maisha
ya ajuza mmoja aitwae Lucynell Crater
na binti yake ambaye ni kiziwi na bubu.
Japo mama Carter anajiamini,
nyumba yake iliyojitenga inaanguka.
Mwanzoni, tunaweza kushuku nia za Shiflet
alipojitolea kusaidia kwenye nyumba,
lakini O'Connor anaenda kuonyesha
kuwa yule ajuza ni
mjanja kama mgeni wake asiotarajiwa-
na kutikisa mategemeo ya msomaji
kuhusu nani ana faida zaidi.
Kwa O'Connor, hamna somo lililokuwa
na kizuizi.
Japo alikuwa ni Mkatoliki aliyejitoa,
hakuogopa kufuatilia uwezekano
wa mawazo mema na tabia isiyo njema,
inayokuwepo kwa mtu mmoja.
Kwenye riwaya yake ya Wajeuri
Wanaiondolea Mbali,
mhusika mkuu anatingwa na mawazo
ya kuwa mtu wa Mungu -
lakini pia anawasha moto na kuua.
Kitabu kinaanza na nabii amaesita
akiwa kwenye nafasi yenye utata:
"Mjomba wa Francis Marion Tarwater
alikua amekufa kwa nusu siku tu
pale huyo mvulana alipolewa sana akashindwa
kumalizia kuchimba kaburi lake".
Hii inamuacha mpita njia "kuvuta
mwili kutoka kwenye meza ya chai
ambapo ulikuwa umekaa bado na
kuuzika [...]
na udongo wa kutosha kwa juu
kuzuia mbwa kuufukua".
Japokuwa siasa zake bado ni za kulumbana,
bunilizi ya O'Connor inaweza pia
kulinganishwa na ubaguzi wa Kusini.
Kwenye "Kila Kinachopanda Lazima
Kikutane",
anaelezea mvulana anayechukizwa
na upendeleo wa mama yake.
Lakini simulizi inaelezea kuwa
ana mapungufu yake
na inasema kwamba kuyagundua mabaya tu
haitetei tabia yake kutokuthibitiwa.
Hata O'Connor anavyochunguza
mambo potofu ya ubinadamu,
anaacha mlango wa ukombozi wazi kidogo.
Kwenye "Mwanaume Mzuri ni Mgumu Kupata",
anamkomboa ajuza anayeteseka kwa
kumsamehe mshitakiwa aliyekubuhu,
hata anavyoikaribia familia yake.
Japo tunaweza kushtushwa na malipo
anayolipa huyu mama kusamehewa,
tunalazimika kukabiliana na
yanayoendelea kwenye mda
tunapoweza kuzingatia kuwa
ukatili au ubaya.
Uwezo wa O'Connor wa ajabu
na tafiti zake za kujitenga na
ushirikina wa Kusini
ulimpelekea kutambuliwa kama
mwandishi wa Kigothi wa Kusini.
Lakini kazi yake ilisogea kupita
tabia za kijinga kabisa
na za kutisha zilizohusishwa
na huo mtindo
kuvumbua tofauti na mchanganyiko
wa tabia za binadamu.
Alijua baadhi ya hii tofauti
ilileta karaha,
na kuwa hadithi zake zingekuwa
na ladha inayohitajika -
lakini alisikia raha kuwachanganya
wasomaji wake,
O'Connor alikufa kwa lupus akiwa
na miaka 39,
baada ya ugonjwa kumweka shambani mwake
Georgia kwa miaka kumi na mbili.
Kwenye miaka hiyo,
aliandika kazi zake nyingi
alizokuwa akiwaza.
Uwezo wake wa kuhama kati ya
maudhi na uvumbuzi
unaendelea kuvutia wasomaji kwenye
dunia yake ya kufikirika isiyoisha.
Kama mhusika Tom Shirlet anavyosema,
mwili ni "kama nyumba:
haiendi popote,
lakini roho, mwanamke,
ni kama gari moto:
daima lipo kwenye mwendo".