WEBVTT 00:00:06.407 --> 00:00:10.697 Bibi muongeaji na mhalifu anayezurura wakizozana katika barabara chafu. 00:00:10.697 --> 00:00:14.798 Muuza Biblia anampeleka mwanafalsafa mwenye mguu mmoja bandani. 00:00:14.798 --> 00:00:19.641 Fundi anaesafiri anamfundisha mwanamke kiziwi neno lake la kwanza shambani. 00:00:20.231 --> 00:00:22.561 Kutoka shambani kwake vijijini Georgia, NOTE Paragraph 00:00:22.561 --> 00:00:25.053 akizungukwa na kundi la ndege wa kufugwa, 00:00:25.053 --> 00:00:27.533 Flannery O'Connor aliandika simulizi za waliotengwa, 00:00:27.533 --> 00:00:31.363 wavamizi na wasioleweka waliunda dunia aliyoifahamu vizuri: 00:00:31.753 --> 00:00:33.013 Marekani Kusini. 00:00:33.513 --> 00:00:34.962 Alichapisha riwaya mbili, 00:00:35.202 --> 00:00:37.652 lakini anajulikana zaidi kwa simulizi zake fupi, 00:00:37.852 --> 00:00:42.612 ambazo zilichunguza maisha ya mji mdogo kwa lugha kali, na ucheshi usio wa kawaida, 00:00:42.752 --> 00:00:45.152 na mazingira ya kufurahisha yenye karaha. 00:00:45.482 --> 00:00:48.538 Kwenye muda wake wa ziada O'Connor alichora katuni, NOTE Paragraph 00:00:48.538 --> 00:00:51.088 na uandishi wake pia umejaa masihara. 00:00:51.088 --> 00:00:56.088 Kwenye simulizi zake, mama na sura "pana na ya upole kama kabichi", 00:00:56.768 --> 00:00:59.858 mwanaume ana nguvu sana kama "dekio la sakafuni", 00:01:00.268 --> 00:01:03.217 na mwili wa mwanamke mmoja una umbo kama "chombo cha kuzika". 00:01:04.247 --> 00:01:06.787 Majina ya wahusika wake yamejawa ujanja. NOTE Paragraph 00:01:07.147 --> 00:01:10.127 Chukulia simulizi "Maisha Unayoyaokoa Yanaweza Kuwa ya Kwako", 00:01:10.257 --> 00:01:13.257 ambapo mtembezi mwenye mkono mmoja Tom Shiftlet anaenda kwenye maisha 00:01:13.257 --> 00:01:15.767 ya ajuza mmoja aitwae Lucynell Crater 00:01:15.767 --> 00:01:17.737 na binti yake ambaye ni kiziwi na bubu. 00:01:17.737 --> 00:01:19.767 Japo mama Carter anajiamini, NOTE Paragraph 00:01:19.767 --> 00:01:21.967 nyumba yake iliyojitenga inaanguka. 00:01:22.197 --> 00:01:25.107 Mwanzoni, tunaweza kushuku nia za Shiflet 00:01:25.107 --> 00:01:27.297 alipojitolea kusaidia kwenye nyumba, 00:01:27.297 --> 00:01:29.957 lakini O'Connor anaenda kuonyesha kuwa yule ajuza ni 00:01:29.957 --> 00:01:32.547 mjanja kama mgeni wake asiotarajiwa- 00:01:32.547 --> 00:01:35.697 na kutikisa mategemeo ya msomaji kuhusu nani ana faida zaidi. 00:01:35.857 --> 00:01:38.467 Kwa O'Connor, hamna somo lililokuwa na kizuizi. NOTE Paragraph 00:01:38.847 --> 00:01:40.637 Japo alikuwa ni Mkatoliki aliyejitoa, 00:01:40.637 --> 00:01:42.767 hakuogopa kufuatilia uwezekano 00:01:42.767 --> 00:01:45.007 wa mawazo mema na tabia isiyo njema, 00:01:45.007 --> 00:01:46.967 inayokuwepo kwa mtu mmoja. 00:01:47.027 --> 00:01:49.317 Kwenye riwaya yake ya Wajeuri Wanaiondolea Mbali, 00:01:49.317 --> 00:01:52.797 mhusika mkuu anatingwa na mawazo ya kuwa mtu wa Mungu - 00:01:52.987 --> 00:01:55.637 lakini pia anawasha moto na kuua. 00:01:55.757 --> 00:01:59.907 Kitabu kinaanza na nabii amaesita akiwa kwenye nafasi yenye utata: 00:02:00.037 --> 00:02:04.237 "Mjomba wa Francis Marion Tarwater alikua amekufa kwa nusu siku tu 00:02:04.287 --> 00:02:07.597 pale huyo mvulana alipolewa sana akashindwa kumalizia kuchimba kaburi lake". 00:02:07.597 --> 00:02:11.648 Hii inamuacha mpita njia "kuvuta mwili kutoka kwenye meza ya chai 00:02:11.668 --> 00:02:13.728 ambapo ulikuwa umekaa bado na kuuzika [...] 00:02:13.728 --> 00:02:16.358 na udongo wa kutosha kwa juu kuzuia mbwa kuufukua". 00:02:17.068 --> 00:02:19.108 Japokuwa siasa zake bado ni za kulumbana, NOTE Paragraph 00:02:19.108 --> 00:02:22.518 bunilizi ya O'Connor inaweza pia kulinganishwa na ubaguzi wa Kusini. 00:02:23.218 --> 00:02:25.768 Kwenye "Kila Kinachopanda Lazima Kikutane", 00:02:25.788 --> 00:02:28.508 anaelezea mvulana anayechukizwa na upendeleo wa mama yake. 00:02:28.698 --> 00:02:31.598 Lakini simulizi inaelezea kuwa ana mapungufu yake 00:02:31.658 --> 00:02:34.048 na inasema kwamba kuyagundua mabaya tu 00:02:34.048 --> 00:02:36.598 haitetei tabia yake kutokuthibitiwa. 00:02:36.608 --> 00:02:39.857 Hata O'Connor anavyochunguza mambo potofu ya ubinadamu, NOTE Paragraph 00:02:39.917 --> 00:02:42.577 anaacha mlango wa ukombozi wazi kidogo. 00:02:42.817 --> 00:02:45.007 Kwenye "Mwanaume Mzuri ni Mgumu Kupata", 00:02:45.007 --> 00:02:48.897 anamkomboa ajuza anayeteseka kwa kumsamehe mshitakiwa aliyekubuhu, 00:02:48.992 --> 00:02:51.232 hata anavyoikaribia familia yake. NOTE Paragraph 00:02:51.762 --> 00:02:54.987 Japo tunaweza kushtushwa na malipo anayolipa huyu mama kusamehewa, 00:02:54.987 --> 00:02:57.427 tunalazimika kukabiliana na yanayoendelea kwenye mda 00:02:57.427 --> 00:03:00.367 tunapoweza kuzingatia kuwa ukatili au ubaya. 00:03:00.367 --> 00:03:02.777 Uwezo wa O'Connor wa ajabu NOTE Paragraph 00:03:02.777 --> 00:03:06.131 na tafiti zake za kujitenga na ushirikina wa Kusini 00:03:06.391 --> 00:03:09.681 ulimpelekea kutambuliwa kama mwandishi wa Kigothi wa Kusini. 00:03:09.681 --> 00:03:12.371 Lakini kazi yake ilisogea kupita tabia za kijinga kabisa 00:03:12.371 --> 00:03:14.936 na za kutisha zilizohusishwa na huo mtindo 00:03:14.936 --> 00:03:18.316 kuvumbua tofauti na mchanganyiko wa tabia za binadamu. 00:03:18.336 --> 00:03:20.776 Alijua baadhi ya hii tofauti ilileta karaha, 00:03:20.796 --> 00:03:23.286 na kuwa hadithi zake zingekuwa na ladha inayohitajika - 00:03:23.286 --> 00:03:25.976 lakini alisikia raha kuwachanganya wasomaji wake, 00:03:26.136 --> 00:03:29.136 O'Connor alikufa kwa lupus akiwa na miaka 39, NOTE Paragraph 00:03:29.136 --> 00:03:33.396 baada ya ugonjwa kumweka shambani mwake Georgia kwa miaka kumi na mbili. 00:03:33.556 --> 00:03:35.036 Kwenye miaka hiyo, 00:03:35.036 --> 00:03:37.316 aliandika kazi zake nyingi alizokuwa akiwaza. 00:03:37.416 --> 00:03:40.246 Uwezo wake wa kuhama kati ya maudhi na uvumbuzi 00:03:40.376 --> 00:03:44.536 unaendelea kuvutia wasomaji kwenye dunia yake ya kufikirika isiyoisha. 00:03:44.696 --> 00:03:47.176 Kama mhusika Tom Shirlet anavyosema, 00:03:47.436 --> 00:03:49.316 mwili ni "kama nyumba: 00:03:49.416 --> 00:03:50.696 haiendi popote, 00:03:50.766 --> 00:03:53.750 lakini roho, mwanamke, ni kama gari moto: 00:03:53.880 --> 00:03:56.150 daima lipo kwenye mwendo".