Bibi muongeaji na mhalifu anayezurura wakizozana katika barabara chafu. Muuza Biblia anampeleka mwanafalsafa mwenye mguu mmoja bandani. Fundi anaesafiri anamfundisha mwanamke kiziwi neno lake la kwanza shambani. Kutoka shambani kwake vijijini Georgia, akizungukwa na kundi la ndege wa kufugwa, Flannery O'Connor aliandika simulizi za waliotengwa, wavamizi na wasioleweka waliunda dunia aliyoifahamu vizuri: Marekani Kusini. Alichapisha riwaya mbili, lakini anajulikana zaidi kwa simulizi zake fupi, ambazo zilichunguza maisha ya mji mdogo kwa lugha kali, na ucheshi usio wa kawaida, na mazingira ya kufurahisha yenye karaha. Kwenye muda wake wa ziada O'Connor alichora katuni, na uandishi wake pia umejaa masihara. Kwenye simulizi zake, mama na sura "pana na ya upole kama kabichi", mwanaume ana nguvu sana kama "dekio la sakafuni", na mwili wa mwanamke mmoja una umbo kama "chombo cha kuzika". Majina ya wahusika wake yamejawa ujanja. Chukulia simulizi "Maisha Unayoyaokoa Yanaweza Kuwa ya Kwako", ambapo mtembezi mwenye mkono mmoja Tom Shiftlet anaenda kwenye maisha ya ajuza mmoja aitwae Lucynell Crater na binti yake ambaye ni kiziwi na bubu. Japo mama Carter anajiamini, nyumba yake iliyojitenga inaanguka. Mwanzoni, tunaweza kushuku nia za Shiflet alipojitolea kusaidia kwenye nyumba, lakini O'Connor anaenda kuonyesha kuwa yule ajuza ni mjanja kama mgeni wake asiotarajiwa- na kutikisa mategemeo ya msomaji kuhusu nani ana faida zaidi. Kwa O'Connor, hamna somo lililokuwa na kizuizi. Japo alikuwa ni Mkatoliki aliyejitoa, hakuogopa kufuatilia uwezekano wa mawazo mema na tabia isiyo njema, inayokuwepo kwa mtu mmoja. Kwenye riwaya yake ya Wajeuri Wanaiondolea Mbali, mhusika mkuu anatingwa na mawazo ya kuwa mtu wa Mungu - lakini pia anawasha moto na kuua. Kitabu kinaanza na nabii amaesita akiwa kwenye nafasi yenye utata: "Mjomba wa Francis Marion Tarwater alikua amekufa kwa nusu siku tu pale huyo mvulana alipolewa sana akashindwa kumalizia kuchimba kaburi lake". Hii inamuacha mpita njia "kuvuta mwili kutoka kwenye meza ya chai ambapo ulikuwa umekaa bado na kuuzika [...] na udongo wa kutosha kwa juu kuzuia mbwa kuufukua". Japokuwa siasa zake bado ni za kulumbana, bunilizi ya O'Connor inaweza pia kulinganishwa na ubaguzi wa Kusini. Kwenye "Kila Kinachopanda Lazima Kikutane", anaelezea mvulana anayechukizwa na upendeleo wa mama yake. Lakini simulizi inaelezea kuwa ana mapungufu yake na inasema kwamba kuyagundua mabaya tu haitetei tabia yake kutokuthibitiwa. Hata O'Connor anavyochunguza mambo potofu ya ubinadamu, anaacha mlango wa ukombozi wazi kidogo. Kwenye "Mwanaume Mzuri ni Mgumu Kupata", anamkomboa ajuza anayeteseka kwa kumsamehe mshitakiwa aliyekubuhu, hata anavyoikaribia familia yake. Japo tunaweza kushtushwa na malipo anayolipa huyu mama kusamehewa, tunalazimika kukabiliana na yanayoendelea kwenye mda tunapoweza kuzingatia kuwa ukatili au ubaya. Uwezo wa O'Connor wa ajabu na tafiti zake za kujitenga na ushirikina wa Kusini ulimpelekea kutambuliwa kama mwandishi wa Kigothi wa Kusini. Lakini kazi yake ilisogea kupita tabia za kijinga kabisa na za kutisha zilizohusishwa na huo mtindo kuvumbua tofauti na mchanganyiko wa tabia za binadamu. Alijua baadhi ya hii tofauti ilileta karaha, na kuwa hadithi zake zingekuwa na ladha inayohitajika - lakini alisikia raha kuwachanganya wasomaji wake, O'Connor alikufa kwa lupus akiwa na miaka 39, baada ya ugonjwa kumweka shambani mwake Georgia kwa miaka kumi na mbili. Kwenye miaka hiyo, aliandika kazi zake nyingi alizokuwa akiwaza. Uwezo wake wa kuhama kati ya maudhi na uvumbuzi unaendelea kuvutia wasomaji kwenye dunia yake ya kufikirika isiyoisha. Kama mhusika Tom Shirlet anavyosema, mwili ni "kama nyumba: haiendi popote, lakini roho, mwanamke, ni kama gari moto: daima lipo kwenye mwendo".