Saida Aden Said: Bado nina taswira hii mbaya katika kumbukumbu zangu. ningeweza ona watu wakianguka chini, milio ya risasi. Niliogopa sana. Kwa kweli, nililia sana. Mtu aliyewajua baba na mama yangu akanishika mkono, akisema, "Twenda! Twende! Twende!" Nikawa nasema," Mamangu yuwapi? Mama yangu? Mama yangu?" Noria Dambrine Dusabireme: Usiku tungesikia milio ya risasi, tulisikia bunduki, Uchaguzi ulitakiwa kufanyika. Vijana walienda barabarani, walikuwa na migomo. Na vijana wengi walifariki SAS: Tulipanda gari. Lilikuwa limejaa sana Watu walikimbia kunusuru maisha yao, Hivi ndivyo nilivyochipuruka Somalia. Mama yangu alinimisi sana. Hakuna yeyote aliyemweleza nilikokwenda. NDD:Ukweli ni kwamba, hatukusoma, Hatukuweza kwenda sokoni, tulibaki nyumbani tu ikanifanya nijue kuwa ningepata nafasi ya kuchagua kitu kizuri, ningeweza kukichagua na kuwa na maisha bora mbeleni. (Muziki) Ignazio Matteini: Duniani, idadi wa watu walio uhamishoni imekuwa ikiongezeka Sasa takriban watu Millioni 60 wako uhamishoni duniani Na kwa bahati mbaya, haipungui. Chrystina Russell:Nafikiri jamii ya misaada kibinadamu inaanza kugundua kutokana na utafiti na uhakika tunaongelea tatizo la kudumu zaidi Baylie Damtie Yeshita: Wanafunzi hawa, wanahitaji elimu ya juu, shahada wanayoweza kuitumia. Ikiwa wanafunzi wanaishi Rwanda sasa, Ikiwa watahama, bado wataendelea na masomo yao. Bado, shahada yao itakuwa na maana, kokote wako CR: Mradi wetu wa kijasiri ulikuwa ni kwa ajili ya kupima Vuguvugu la Elimu Ulimwenguni la Chuo cha New Hampshire ya Kusini uwezo wa kukuza shahada za kwanza na mifumo ya kupata ajira kufikia wahamiaji na wale ambao wasingeweza kufikia elimu ya juu SAS: Kama mhamiaji, ni changamani kujiendeleza kielimu na kitaaluma. Jina langu ni Saida Aden Said, Na ninatokea Somalia, Nilikuwa na miaka tisa, nilipokuja Kakuma, na nikaanza shule nikiwa na miaka 17 Kwa sasa nafanya shahada yangu ya kwanza na SNHU. NDD: My name is Noria Dambrine Dusabireme. Ninasomea shahada ya kwanza ya sanaa katika mawasiliano nikijikita katika masuala ya biashara. CR:Tunahudumia wanafunzi kutoka nchi tano tofauti: Lebanon, Kenya, Malawi, Rwanda na Afrika ya Kusini. Tunafurahia wahitimu wa kiwango cha AA 800 na zaidi ya 400 wa shahada ya kwanza na karibu wanafunzi 1000 walioandikisha kwa sasa. la ajabu, tunaangazia maisha ya wakimbizi kama yalivyo. Hakuna ubaguzi kitabaka Hakuna mihadhara. Hakuna tarehe za mwisho Hakuna mitihani ya mwisho. shahada hili linapima uwezo na haujafungwa na muda. Unachagua muda wa kuanza mradi wako. Unachagua utakavyoikabili NDD:Unapofungua jukwaa, ndipo unapoweza kuona malengo. Kwenye kila lengo, tunaweza kupata miradi. Unapofungua mradi, unakutana na uweza ambao unatakiwa kumudu, uelekeo na muhtasari wa mradi, CR: Kiungo muhimu cha SNHU ni kujumuisha usomaji kwa kuangalia uwezo pamoja na usomaji wa pamoja na washirika ili kuwa na msaada pande zote Hii ni pamoja na ufundishaji kitaaluma. Inamaanisha msaada saikolojia-jamii, msaada wa kimatibabu, na pia ni ule msaada wa mlango wa nyuma wa ajira ndiyo inasababisha hitimu kwa asilimia 95, na asilimia 88 kuajiriwa, NDD: mimi mzoezi wa vitendo ya kuratibu mitandao ya kijamii. Inahusiana na shahada ya mawasiliano ninayoifanya. Nimejifunza mambo mengi katika mradi huu na dunia halisi. CR: Mazoezi ya vitendo yanayoongozwa ni nafasi kwa wanafunzi kufanyia mazoezi ujuzi wao kwa sisi kutengeneza daraja katika mazoezi kwa vitendo na upatikanaji wa nafasi za kazi baadae. (Muziki) Hii ni modeli ambayo inazuia kuweka muda na sera za chuo kikuu na utaratibu kipao mbele na badala yake unamweka mwanafunzi kileleni IM: Modeli ya SNHU ni njia kubwa ya kutikisa mti. Kubwa ni mtikisiko mkubwa kwenye njia ya asili ya elimu ya juu hapa BDY:inaweza badilisha maisha ya wanafunzi kutoka katika hali ya mashaka na ukimbizi NDD: nikipata shahada naweza rudi na kufanya kazi popote nitakapo Ninaweza kufanya shahada ya pili kwa ujasiri katika Kiingereza, kitu nisingewazia hapo awali Na nina ujasiri na ujuzi unaohitajika kwenda na kupambana katika mazingira ya kazi bila kujali kuwa nitaweza. SAS: Nilitaka kufanya kazi na jamii. Nataka kuanzisha shirika isiyo ya faida Tunahimiza elimu ya wanawake. Ninataka kuwa mtu ambaye ni kama balozi na kuwashawishi kusoma na kuwaambia hawajachelewa. Ni ndoto