Mwaka 2019, ubinadamu ulipata tahadhari: 30 ya wanasayansi mashuhuri duniani walipeana majibu ya utafiti wa miaka mitatu ya kilimo cha kimataifa na kutangaza kuwa uzalishaji wa nyama unaathiri sayari yetu na kuhatarisha afya ya dunia. Mwandishi mmoja wa utafiti alinena ya kuwa "ubinadamu ni hatarisho kwa utulivu wa sayari ... [Hii inahitaji] sio chini ya uvumbuzi mpya wa kilimo wa kimataifa." Kama mtu ambaye ametumia miongo miwili kutetea kuhama uzalishaji wa nyama kwa viwanda, nilitaka kuamini kuwa wito huu ulikuwa unaenda kuleta mabadiliko. Jambo ni kuwa nimeona hili mara kwa mara kwa miongo. Hii hapa 2018 kutoka kwa jarida "Nature," 2017 kutoka "Bioscience Journal," 2016 kutoka Chuo cha Taifa cha Sayansi. Lengo kuu la utafiti hizi huwa ni mabadiliko ya hewa. Lakini upinzani wa kiuavijasumu ni tishio kubwa. Tunawapa mifugo vipimo kubwa vya viuavijasumu. Viuavijasumu kisha hubadilika na kuwa wadudu wenye nguvu wanaotishia kufanya kiuavijasumu kuwa bila kazi katika maisha yetu. Unataka kitisho? Tafuta: "mwisho wa kazi wa kiuavijasumu." Naenda kuweka bayana jambo moja: Siko hapa kueleza mtu anachopaswa kula. Hatua ya kibinafsi ni sawa, lakini upinzani wa kiuavijasumu na mabadiliko ya hewa -- yanahitaji zaidi. Kando na hayo, kusadikisha ulimwengu kupunguza kula nyama haijafaulu. Kwa miaka 50, wanaharakati wa mazingira, wataalamu wa afya wa duniani na wanaharakati wa wanyama, wamesihi umma kula nyama kiasi. Na bado, wastani wa ulaji nyama umekuwa juu kihistoria. Mkazi wastani wa Amerika Kaskazini alikula pauni 200 ya nyama mwaka jana. Na sikula ata. (Kicheko) Inamaanisha kuna mtu huko nje alikula pauni 400 ya nyama. (Kicheko) Kwa njia tunayoelekea, tunaenda kuhitaji kuzalisha asilimia 70 hadi 100 zaidi ya nyama ifikapo 2050. Hili linahitaji suluhisho la duniani pote. Tunachohitaji ni kuzalisha nyama ambayo watu watapenda, lakini tuizalishe kwa njia mpya. Nina mawazo kadhaa. Wazo la kwanza: tukuze nyama kutoka kwa mimea. Badala ya kukuza mimea, kuyalisha kwa wanyama, na hayo yote yasiyofaa, tukuze mimea hiyo, tuikuze na nyama, tuifanye iwe na nyama. Wazo la pili: kwa nyama halisi ya wanyama, tuikuze kwa chembe moja kwa moja. Badala ya kukuza wanyama waliohai, tukuze chembe moja kwa moja, Inachukua wiki sita kulea kuku afike kimo cha kuchinjwa. Kuza chembe moja kwa moja, na utapata matokea sawia kwa siku sita. Hivi ndivyo itakuwa katika skeli. Ni ujirani wa kirafiki wa kiwanda cha nyama. (Kicheko) Nitataja mambo mawili kuhusu hili. Jambo la kwanza, tunasadiki tunaweza. Miaka iliyopita, makampuni mengine yamekuwa yakikuza nyama kutoka kwa mimea na walaji hawawezi tofautisha na nyama halisi, na sasa kuna makampuni mbalimbali yanayokuza nyama halisi ya wanyama moja kwa moja kutoka kwa chembe. Nyama hii ya mimea na ya chembe inawapa walaji vyote wanavyopenda kuhusu nyama -- ladha, umbile na kadhalika -- lakini bila hitaji ya viuavijasumu na sehemu ya madhara kwa hali ya hewa. Na kwa sababu teknolojia hizi mbili ni bora zaidi, kwa ukuzaji bidhaa hizi zitakuwa za bei ya chini. Jambo moja kuhusu hilo -- haitakuwa rahisi. Makampuni haya yanayotumia mimea yametumia misandali kidogo kwa baga zao, na chembe ya nyama bado haijazinduliwa kibiashara. Kwa hivyo tutahitaji ushirikiano wa wote ili kufanya hili liwe kiwanda cha nyama duniani. Mwanzo, tunahiaji sekta ya nyama ya sasa. Hatutaki kuvuruga sekta ya nyama, tunataka kuibadilisha. Tunahitaji dhana yake ya uchumi, msururu wake wa ugavi, utaalam wake wa uuzaji na wateja wake. Tunahitaji pia serikali. Serikali hutumia mabilioni ya madola kila mwaka kwa utafiti na maendeleo unaozingatia afya duniani na mazingira. Yanafaa kuwekeza sehemu ya fedha hizo katika sadifisha na kuboresha uzalishaji wa mimea na nyama iliyokuzwa na chembe ya mimea. Tazama, kumi ya maelfu ya watu walikufa kutoka kwa usugu wa viuavijasumu Amerika Kaskazini mwaka jana. Ifikapo 2050, tarakimu hiyo itakuwa milioni 10 kwa mwaka duniani. Mabadiliko ya hewa pia ni athari iliyopo kwa sehemu kubwa ya familia yetu duniani, wakiwemo watu maskini zaidi hapa duniani. Mabadiliko ya hewa, kinga ya viuavijasumu-- hizi ni dharura duniani. Uzalishaji wa nyama unazidi dharura hizi kwa kipimo duniani. Lakini hatuendi kupunduza ulaji nyama hadi tuwape walaji bidhaa mbadala zitakazo gharimu sawa au chini na ladha iwe sawia au bora. Tuko na jawabu. Tutengeneze nyama kutoka kwa mimea. Tuikuze moja kwa moja kutoka kwa chembe. Tayari tumechelewa kutumia raslimali tulizonazo kutengeneza mapinduzi ya kilimo mapya. Asanteni. (Makofi)