- Kama bado unasumbukana na kibali, fikiria tu badala ya kuanzisha ngono, unawatengezea kikombe cha chai. Unasema: "Hey, ungependa kikombe cha chai?" Na wataenda: "Oh Mungu Wangu, ndio! "Ningependa sana kikombe cha chai! Ahsante!" Kisha unajua wanataka kikombe cha chai. Ukisema, "Ungependa kikombe cha chai?" Na wako kama:"Sina uhakika kikamilifu." Basi unaeza watengezea kikombe cha chai, ama la, lakini uwe mwangalifu; wanaeza kosa kuikunywa. Na wasipoinywa, basi - - na hapa ndipo pahali muhimu - - usiwalazimishe kunywa. Kwa sababu wewe ndio uliyeitengeneza haimaanishi uko na haki ya kuwaona wakiinywa. Na wakisema, "Hapana, ahsante." basi usiwatengezee chai, kabsaa. Usiwategenzee chai. Usiwafanye wakunywe chai, usiwakasirikie kwa kukataa kutaka chai hawataki chai tu, sawa? Wanaeza sema: "Ndio, tafadhali, "Huu ndi ukarimu wako" Na alafu chai itakapo wasili, hawataki chai kabsaa. Kwa ukweli iyo inaudhi kwa sababu umejitolea nguvu ya kutengeneza chai, lakini hawako katika wajibu ya kukunywa chai. Walitaka chai, sahii hawataki. Watu wengine hubadilisha mawazo katika ule muda inachukua birika, kuandaa chai na kuongeza maziwa. na ni sawa kwa watu kubadilisha mawazo. Na bado huna haki ya kuwaona wakiinywa. And kama hawana fahamu, usiwatengezee kahawa. Watu hawana fahamu hawataki chai, na hawawezi jibu hilo swali, "Unataka chai?" kwa sababu hawana famahu. Sawa, labda walikuwa na fahamu wakati uliwauliza kama wanataka chai, na wakasema ndio, lakini katika wakati uliokuchukua kuchemsha birika, kuandaa hio chai na uongeza maziwa , hawana fahamu sahi. Unafaa kueka chai chini, hakikisha huyu Na hii ndio sehemu muhimu tena Usiwalazimishe wanywe kahawa! Walisema ndio angali, lakini watu wasio timamu hawataki chai. Kama mtu alisema ndio atakunywa chai, akanza kuinywa alafu akazimia kabla wamalize kuinywa, usiendelee kumwaga ndani mwa kinywa zao Peleka chai mbali, na uhakikishe ako salama. Kwa sababu watu wasio fahamu hawataki chai, nimamini. Kama kuna mtu alisema ndio kwa chai karibu na nyumba yako siku ya Juma Mosi, hio haimaanishi wanakutaka uwatengenezee chai kila wakati. Hawataki uje karibu na kwao bila kutarajiwa na uwatengezee chai, uwalazimishe kuinywa, ukisema: "Lakini ulisema unahitaji chai wiki iliopita." Ama waamke wapatae unawamwagia chai chini mwa vinywa vyao, ukisema: "Lakini ulisema unahitaji chai jana usiku." Kama unaeza elewa kabsaa namna ya upuzi kulazimisha watu kuchukua chai wakati hawataki kunywa chai, na unaweza kuelewa wakati watu hawataki chai, basi je, ni ugumu upi upo kuelewa inapokuja kwa ngono? Iwapo ni chai ama ngono, kibali ni kila kitu. Na juu ya huo wajibu, ninaenda kujitengezea kikombe cha chai.