Je kama unaweza kuchukua kidonge au chanjo na kama ukawa unapona mafua, unaweza kuponya jeraha kwa urahisi? Leo, kama tukiwa na upasuaji au ajali, tunakaa hospitalini kwa wiki, na mara nyingi tunabaki na makovu na madhara ya uchungu kwa uwezo wetu wa kutengeneza au kukuza afya, na viungo visivyo na jeraha. Nafanya kazi kujenga vifaa vinavyofundisha mfumo wetu wa kinga ili utupe alama za kukuza tishu mpya. Kama tu chanjo inavyofundisha mwili wetu kupigana na magonjwa, badala yake tunaweza fundisha mfumo wetu wa kinga kujenga tishu na kuponya majeraha kwa urahisi. Sasa, kukuza sehemu za mwili kutoka popote inaweza kuonekana kama uchawi, lakini kuna viumbe kadhaa vinavyoweza kutimiza mafanikio haya. Baadhi ya mijusi inaweza kukuza mikia yao, yule salamanda mnyenyekevu anaweza kukuza kabisa mkono wake, na hata binadamu tu wanaweza kukuza ini lao baada ya kupoteza zaidi ya nusu ya uzito wao wa awali. Ili kufanya uchawi huu kuwa karibu zaidi na ukweli, nina fanya uchunguzi wa jinsi mwili wetu unaweza kuponya majeraha na kujenga tishu kupitia maelekezo kutoka mfumo wa kinga. Kutoka kwenye mkato wa goti lako mpaka maambukizi ya sinus yanayoboa, mfumo wetu wa kinga unalinda mwili wetu na hatari. Mimi ni immunolojisti na kwa kutumia ninachojua kuhusu mfumo wa ulinzi wa mwili wetu, niliweza kutambua wachezaji wakuu kwenye mapambano ya kujenga mikato na michubuko yetu. Tunapoangalia vifaa vinavyojaribiwa kwa sasa kwa uwezo wao wa kusaidia kukuza misuli, timu yetu imeona kua baada ya kutibu msuli uliojeruhiwa na vifaa hivi, kulikua na idadi kubwa ya seli za kinga ndani ya kifaa na inayozunguka msuli. Hivyo kwa sababu hii, badala ya seli za kinga kukimbilia kwenye maambukizi kupigana na bakteria, zinakimbilia kuelekea kwenye jeraha. Nimegundua aina maalum ya seli za kinga, ni msaidizi T kiini, ilikua inapatikana ndani ya kile kifaa nilichokipanda na ni muhimu kabisa kwa ajili ya uponyaji jeraha. Sasa, kama tu ulivyokua mdogo na ukavunja penseli yako na kujaribu kugundisha kwa pamoja tena, tunaweza kupona, lakini inaweza isiwe njia inayofanya kazi zaidi, na tutapata kovu. Hivyo kama hatuna hizi msaidizi T kiini, badala ya misuli yenye afya, misuli yetu inatengeneza seli za mafuta ndani yake, na kama kuna mafuta kwenye misuli yetu, haina nguvu. Sasa, kutumia mfumo wetu wa kinga, miili yetu inaweza kukua tena bila haya makovu na kuonekana kama ilivyokua kabla hata hatujajeruhiwa. Nina fanya kazi kutengeneza vifaa vinavyotuma alama za kujenga tishu mpya kwa kubadilisha mwitikio wa kinga. Tunajua kua muda wowote kifaa kinapopandwa mwilini mwetu, mfumo wa kinga utaitikia kwake. Hii hutofautiana kwanzia kipima mapigo ya moyo mpaka pampu za insulini mpaka vifaa ambavyo wanatumia wahandisi ili kujaribu kujenga tishu mpya. Hivyo ninapoweka hicho kifaa, au kiguzo, ndani ya mwili, mfumo wa kinga hutengeneza mazingira madogo ya seli na protini ambazo zinaweza badili jinsi seli shina zetu zinavyoishi. Sasa, kama hali ya hewa inavyoathiri shughuli zetu za siku, kama kwenda kukimbia au kukaa ndani na kutazama kipindi kizima cha TV kwenye Netflix, mazingira ya kinga ya kiguzo inaathiri jinsi seli shina zetu zinavyokua na kuendelea. Kama tunakua na ishara za mbovu, tuseme kama ishara za Netflix, tunapata seli za mafuta badala ya misuli. Viguzo hivi vimetengenezwa na aina nyingi tofauti ya vitu, kwanzia plastiki mpaka vitu vinavyopatikana kiasili, nyuzi ndogo zinazotofautiana unene, sifongo ambazo zina matundu makubwa au madogo, jeli zenye ugumu unaotofautiana. Na watafiti wanaweza hata kutengeneza vifaa kutoa ishara tofauti na mda. Hivyo kwa maneno mengine, tunaweza kupanga maonyesho hayaya Broadway ya seli kwa kuzipa jukwaa, sehemu na heshima sahihi inayoweza kubadilishwa kwa tishu tofauti, kama tu mtengenezaji anavyobadilisha jukwaa kwa "Les Mis" dhidi ya "Little Shop of Horrors." Nina changanya aina maalum za ishara ambazo zinaiga jinsi miili yetu inavyojibu maumivu kutusaidia kua wapya. Huko mbeleni, tutaona bandi ya misaada ambayo ni kizuia kovu, kijazo cha msuli kinachofinyangika au hata chanjo inayoponya jeraha. Sasa, hatutaweza kuamka kesho na kuweza kuponywa kama Wolverine. Pengine hata sio Jumanne ijayo pia. Ila na haya maednelelo, na kufanya kazi na mfumo wetu wa kinga kusaidia kuunda tishu na kutibu majeraha, tunaweza kuanza kuona bidhaa kwenye soko zinazofanya kazi na mfumo wa ulinzi mwilini kusaidia kutengeneza upya, na labda siku moja tutaweza kua sambamba na salamander. Asante. (Makofi)