1 00:00:01,324 --> 00:00:04,602 Je kama unaweza kuchukua kidonge au chanjo 2 00:00:04,730 --> 00:00:06,670 na kama ukawa unapona mafua, 3 00:00:06,780 --> 00:00:08,785 unaweza kuponya jeraha kwa urahisi? 4 00:00:08,899 --> 00:00:12,051 Leo, kama tukiwa na upasuaji au ajali, 5 00:00:12,355 --> 00:00:13,976 tunakaa hospitalini kwa wiki, 6 00:00:14,000 --> 00:00:16,626 na mara nyingi tunabaki na makovu na madhara ya uchungu 7 00:00:16,650 --> 00:00:21,785 kwa uwezo wetu wa kutengeneza au kukuza afya, na viungo visivyo na jeraha. 8 00:00:22,436 --> 00:00:24,462 Nafanya kazi kujenga vifaa 9 00:00:24,486 --> 00:00:28,689 vinavyofundisha mfumo wetu wa kinga ili utupe alama za kukuza tishu mpya. 10 00:00:29,497 --> 00:00:32,571 Kama tu chanjo inavyofundisha mwili wetu kupigana na magonjwa, 11 00:00:32,595 --> 00:00:35,323 badala yake tunaweza fundisha mfumo wetu wa kinga 12 00:00:35,347 --> 00:00:38,211 kujenga tishu na kuponya majeraha kwa urahisi. 13 00:00:38,886 --> 00:00:42,664 Sasa, kukuza sehemu za mwili kutoka popote inaweza kuonekana kama uchawi, 14 00:00:42,688 --> 00:00:45,879 lakini kuna viumbe kadhaa vinavyoweza kutimiza mafanikio haya. 15 00:00:45,903 --> 00:00:48,346 Baadhi ya mijusi inaweza kukuza mikia yao, 16 00:00:48,370 --> 00:00:52,315 yule salamanda mnyenyekevu anaweza kukuza kabisa mkono wake, 17 00:00:52,339 --> 00:00:55,228 na hata binadamu tu wanaweza kukuza ini lao 18 00:00:55,252 --> 00:00:58,343 baada ya kupoteza zaidi ya nusu ya uzito wao wa awali. 19 00:00:58,615 --> 00:01:01,250 Ili kufanya uchawi huu kuwa karibu zaidi na ukweli, 20 00:01:01,274 --> 00:01:05,369 nina fanya uchunguzi wa jinsi mwili wetu unaweza kuponya majeraha na kujenga tishu 21 00:01:05,393 --> 00:01:07,522 kupitia maelekezo kutoka mfumo wa kinga. 22 00:01:08,387 --> 00:01:11,912 Kutoka kwenye mkato wa goti lako mpaka maambukizi ya sinus yanayoboa, 23 00:01:11,936 --> 00:01:14,617 mfumo wetu wa kinga unalinda mwili wetu na hatari. 24 00:01:15,199 --> 00:01:16,660 Mimi ni immunolojisti 25 00:01:16,684 --> 00:01:19,714 na kwa kutumia ninachojua kuhusu mfumo wa ulinzi wa mwili wetu, 26 00:01:19,738 --> 00:01:21,914 niliweza kutambua wachezaji wakuu 27 00:01:21,938 --> 00:01:24,626 kwenye mapambano ya kujenga mikato na michubuko yetu. 28 00:01:25,436 --> 00:01:28,105 Tunapoangalia vifaa vinavyojaribiwa kwa sasa 29 00:01:28,129 --> 00:01:30,327 kwa uwezo wao wa kusaidia kukuza misuli, 30 00:01:30,351 --> 00:01:34,510 timu yetu imeona kua baada ya kutibu msuli uliojeruhiwa na vifaa hivi, 31 00:01:34,534 --> 00:01:36,857 kulikua na idadi kubwa ya seli za kinga 32 00:01:36,881 --> 00:01:39,438 ndani ya kifaa na inayozunguka msuli. 33 00:01:40,010 --> 00:01:41,168 Hivyo kwa sababu hii, 34 00:01:41,192 --> 00:01:45,406 badala ya seli za kinga kukimbilia kwenye maambukizi kupigana na bakteria, 35 00:01:45,430 --> 00:01:47,517 zinakimbilia kuelekea kwenye jeraha. 36 00:01:47,922 --> 00:01:50,755 Nimegundua aina maalum ya seli za kinga, 37 00:01:50,779 --> 00:01:52,073 ni msaidizi T kiini, 38 00:01:52,097 --> 00:01:54,826 ilikua inapatikana ndani ya kile kifaa nilichokipanda 39 00:01:54,850 --> 00:01:57,767 na ni muhimu kabisa kwa ajili ya uponyaji jeraha. 40 00:01:58,325 --> 00:02:01,767 Sasa, kama tu ulivyokua mdogo na ukavunja penseli yako 41 00:02:01,791 --> 00:02:04,329 na kujaribu kugundisha kwa pamoja tena, 42 00:02:04,353 --> 00:02:05,507 tunaweza kupona, 43 00:02:05,531 --> 00:02:07,776 lakini inaweza isiwe njia inayofanya kazi zaidi, 44 00:02:07,800 --> 00:02:09,173 na tutapata kovu. 45 00:02:09,515 --> 00:02:12,499 Hivyo kama hatuna hizi msaidizi T kiini, 46 00:02:12,523 --> 00:02:14,110 badala ya misuli yenye afya, 47 00:02:14,134 --> 00:02:16,745 misuli yetu inatengeneza seli za mafuta ndani yake, 48 00:02:16,769 --> 00:02:19,646 na kama kuna mafuta kwenye misuli yetu, haina nguvu. 49 00:02:20,033 --> 00:02:22,433 Sasa, kutumia mfumo wetu wa kinga, 50 00:02:22,457 --> 00:02:24,954 miili yetu inaweza kukua tena bila haya makovu 51 00:02:24,978 --> 00:02:28,380 na kuonekana kama ilivyokua kabla hata hatujajeruhiwa. 52 00:02:29,128 --> 00:02:31,688 Nina fanya kazi kutengeneza vifaa 53 00:02:31,712 --> 00:02:33,991 vinavyotuma alama za kujenga tishu mpya 54 00:02:34,015 --> 00:02:36,305 kwa kubadilisha mwitikio wa kinga. 55 00:02:36,840 --> 00:02:41,055 Tunajua kua muda wowote kifaa kinapopandwa mwilini mwetu, 56 00:02:41,079 --> 00:02:43,134 mfumo wa kinga utaitikia kwake. 57 00:02:43,158 --> 00:02:47,667 Hii hutofautiana kwanzia kipima mapigo ya moyo mpaka pampu za insulini 58 00:02:47,691 --> 00:02:51,617 mpaka vifaa ambavyo wanatumia wahandisi ili kujaribu kujenga tishu mpya. 59 00:02:51,932 --> 00:02:55,997 Hivyo ninapoweka hicho kifaa, au kiguzo, ndani ya mwili, 60 00:02:56,021 --> 00:03:00,426 mfumo wa kinga hutengeneza mazingira madogo ya seli na protini 61 00:03:00,450 --> 00:03:03,322 ambazo zinaweza badili jinsi seli shina zetu zinavyoishi. 62 00:03:03,817 --> 00:03:07,715 Sasa, kama hali ya hewa inavyoathiri shughuli zetu za siku, 63 00:03:07,739 --> 00:03:09,064 kama kwenda kukimbia 64 00:03:09,088 --> 00:03:13,573 au kukaa ndani na kutazama kipindi kizima cha TV kwenye Netflix, 65 00:03:13,597 --> 00:03:15,565 mazingira ya kinga ya kiguzo 66 00:03:15,589 --> 00:03:18,644 inaathiri jinsi seli shina zetu zinavyokua na kuendelea. 67 00:03:18,883 --> 00:03:20,899 Kama tunakua na ishara za mbovu, 68 00:03:20,923 --> 00:03:22,598 tuseme kama ishara za Netflix, 69 00:03:22,622 --> 00:03:25,746 tunapata seli za mafuta badala ya misuli. 70 00:03:26,790 --> 00:03:29,917 Viguzo hivi vimetengenezwa na aina nyingi tofauti ya vitu, 71 00:03:29,941 --> 00:03:33,306 kwanzia plastiki mpaka vitu vinavyopatikana kiasili, 72 00:03:33,330 --> 00:03:36,081 nyuzi ndogo zinazotofautiana unene, 73 00:03:36,105 --> 00:03:38,518 sifongo ambazo zina matundu makubwa au madogo, 74 00:03:38,542 --> 00:03:40,661 jeli zenye ugumu unaotofautiana. 75 00:03:40,685 --> 00:03:42,795 Na watafiti wanaweza hata kutengeneza vifaa 76 00:03:42,819 --> 00:03:44,858 kutoa ishara tofauti na mda. 77 00:03:45,473 --> 00:03:50,719 Hivyo kwa maneno mengine, tunaweza kupanga maonyesho hayaya Broadway ya seli 78 00:03:50,743 --> 00:03:54,601 kwa kuzipa jukwaa, sehemu na heshima sahihi 79 00:03:54,625 --> 00:03:56,846 inayoweza kubadilishwa kwa tishu tofauti, 80 00:03:56,870 --> 00:03:59,066 kama tu mtengenezaji anavyobadilisha jukwaa 81 00:03:59,090 --> 00:04:02,013 kwa "Les Mis" dhidi ya "Little Shop of Horrors." 82 00:04:02,398 --> 00:04:05,082 Nina changanya aina maalum za ishara 83 00:04:05,106 --> 00:04:09,814 ambazo zinaiga jinsi miili yetu inavyojibu maumivu kutusaidia kua wapya. 84 00:04:10,283 --> 00:04:13,811 Huko mbeleni, tutaona bandi ya misaada ambayo ni kizuia kovu, 85 00:04:13,835 --> 00:04:17,813 kijazo cha msuli kinachofinyangika au hata chanjo inayoponya jeraha. 86 00:04:17,837 --> 00:04:21,414 Sasa, hatutaweza kuamka kesho na kuweza kuponywa kama Wolverine. 87 00:04:21,438 --> 00:04:23,304 Pengine hata sio Jumanne ijayo pia. 88 00:04:23,328 --> 00:04:24,512 Ila na haya maednelelo, 89 00:04:24,536 --> 00:04:28,741 na kufanya kazi na mfumo wetu wa kinga kusaidia kuunda tishu na kutibu majeraha, 90 00:04:28,765 --> 00:04:30,994 tunaweza kuanza kuona bidhaa kwenye soko 91 00:04:31,018 --> 00:04:34,884 zinazofanya kazi na mfumo wa ulinzi mwilini kusaidia kutengeneza upya, 92 00:04:34,908 --> 00:04:38,963 na labda siku moja tutaweza kua sambamba na salamander. 93 00:04:39,876 --> 00:04:41,027 Asante. 94 00:04:41,051 --> 00:04:44,690 (Makofi)