Asante Palikuwa na mfalme nchini India, Maharaja na siku yake ya kuzaliwa ilitolewa amri kwamba machifu wote walete zawadi kwa mfalme. Wengine wakaleta hariri bora, wengine wakaleta panga maridadi, wengine dhahabu mwisho wa mstari alikuja akitembea mzee mdogo mwenye makunyanzi ambaye alitembea kutoka kijijini kwake kwa safari ya siku nyingi kando ya bahari. alipokuwa akisogea mwana mfalme akauliza, 'Umemletea zawadi gani Mfalme?' Na mzee yule taratibu sana akakunjua mkono wake kuonyesha kombe la baharini zuri sana, lenye makoa ya zambarau na njano,nyekundu na bluu. Na mwana Mfalme akasema, "Hiyo si zawadi kwa Mfalme! Ni zawadi gani hiyo?" Mzee yule akamwangalia taratibu na kusema "Kutembea mwendo mrefu.. ni sehemu ya zawadi" (Kicheko) Baada ya muda mfupi, Nitawapa zawadi, zawadi niaminiyo ni zawadi inayostahili kuenezwa. Ila kabla ya hayo, ngoja niwachukue kwenye mwendo wangu mrefu. Kama wengi wenu, Nilianza maisha kama mtoto mdogo. Wangapi kati yenu mlianza maisha kama mtoto ? Aliyezaliwa mchanga? Karibia nusu yenu.. Sawa (Kicheko) Na mliobakia, vipi? Mlizaliwa mkiwa watu wazima? Ama kweli, nataka kukutana na mama zenu! Ongelea yasiyowezekana! Nikiwa mtoto mdogo, siku zote nilipendezwa kufanya mambo yasiyowezekana Leo ni siku ambayo nimekuwa nikiitarajia kwa miaka mingi, kwa sababu leo ni siku ambayo nitajaribu kufanya yasiyowezekana mbele ya macho yenu Hapahapa TEDxMaastrich Nitaanza Kwa kuonyesha mwisho wake: Na nitawathibitishia kwamba yasiyowezekana siyo hayawezekani Na nitamalizia kwa kuwapa zawadi yenye kustahili kuieneza: Nitawaonyesha kwamba unaweza kufanya yasiyowezekana maishani mwako. katika kutafuta kufanya yasiyowezekana, nimegundua kuna mambo mawili yanayofanana kati ya watu duniani. Kila mtu ana hofu, na kila mtu ana ndoto. Katika kutafuta kufanya yasiyowezekana nimegundua kuna vitu vitatu ambavyo nimevifanya miaka mingi ambavyo vimenisababishia kufanya yasiyowezekana: Mchezo wa mpira wa kuchenga au "Trefball" Superman, na Mbu Hayo ni maneno yangu matatu makuu. Mmeshajua kwanini nafanya yasiyowezekana maishani mwangu Hivyo nitawachukua katika safari yangu, ya mwendo mrefu kutoka kwenye hofu hadi ndoto kutoka kwenye maneno hadi panga, Kutoka Mpira wa kuchenga hadi Superman hadi kwa Mbu Na ninatumaini kuwaonyesha unawezaje kufanya yasiyo wezekana maishani mwako Oktoba 4, mwaka 2007. Moyo wangu ulienda mbio, magoti yangu yalitetema nilipokuwa napanda jukwaani kwenye ukumbi wa Sanders Chuo cha Harvard kupokea Tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu kwa kushiriki kuandika ikisiri ya utafiti wa kitabibu ulioitwa "Kumeza Upanga... ...na Athari zake" (Kicheko) Ilichapishwa kwenye jarida dogo ambalo sikuwahi kulisoma kabla, Jarida la Kitabibu la Uingereza. Na kwangu, hiyo ilikuwa ndoto isiyowezekana kuwa kweli, ilikuwa ni mshangao usiotegemewa kwa mtu kama mimi, ilikuwa ni heshima ambayo sitaweza kusahau Lakini haikuwa sehemu ya kubwa ya kukumbuka maishani mwangu. Mnamo Oktoba 4, mwaka 1967 kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba aliteseka na hofu kubwa kupita kiasi. Alipojiandaa kupanda jukwaani, moyo wake ulienda mbio, magoti yake yalikuwa yakitetemeka. Alikwenda kufungua kinywa chake kuongea, maneno hayakuweza kutoka. Alisimama akitetemeka na kutoa machozi. Alipooza kwa mshtuko wa ghafla, alipatwa fadhaa kwa hofu. huyu kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba alitesekana na hofu kubwa kupita kiasi. Alikuwa na hofu ya giza, hofu ya vimo virefu, hofu ya buibui na nyoka ... Kuna yeyote anayeogopa buibui na nyoka? Naam, wachache wenu ... Alikuwa na hofu ya maji na papa ... Hofu ya madaktari na manesi na madaktari wa meno, na sindano na kutobolewa na vitu vya ncha kali. Lakini zaidi ya chochote, alikuwa na hofu ya watu Huyo kijana mwoga,mwenye aibu na mwembamba alikuwa mimi. Nilikuwa na hofu ya kushindwa na kukataliwa, kutojithamini, kujiona duni, na kitu ambacho hata hatukujua unaweza kujiandikisha kwa siku hizo: ugonjwa wa hofu ya ukaribu na watu. Kwa sababu nilikuwa na hofu, waonevu walinitania na kunipiga. Walinicheka na kuniita majina, Hawakuniruhusu kucheza nao michezo ya aina yoyote. Ah, kulikuwa na mchezo mmoja walikuwa wakiruhusu kucheza kwenye ... Mpira wa kuchenga - na sikuwa mchengaji nzuri. Waonevu waliita jina langu, na nilipoangalia niliona mipira myekundu ya kukwepa ikivurumishwa usoni wangu kwa kasi kubwa bam, bam, bam! Ninakumbuka siku nyingi nikirudi nyumbani kutoka shule, uso wangu ulikuwa mwekundu ukichonyota, masikio yangu yalikuwa mekundu yakivuma. Macho yangu yalichoma kwa machozi, na maneno yao yalichoma masikioni mwangu. Na yeyote aliyesema, "Fimbo na mawe vyaweza kunivunja mifupa, bali maneno hayatoniumiza kamwe "... Ni uongo. Maneno huweza kukata kama kisu. Maneno huweza kupenya kama upanga. Maneno huwezafanya majeraha yenye kina yasiweze kuonekana. Hivyo nilikuwa na hofu. Na maneno yalikuwa adui yangu mkubwa. Bado ni adui yangu. Lakini pia nilikuwa na ndoto. Nilienda nyumbani na kutorokea kwenye futuhi za Superman na nilisoma futuhi za Superman na niliota kutaka kuwa shujaa mkubwa kama Superman. Nilitaka kupigania kweli na haki, Nilitaka kupambana dhidi ya wahalifu na mahasimu, Nilitaka kupaa duniani kote kufanya vitendo vya ujasiri kuokoa maisha. Nilikuwa pia navutiwa mno na vitu vilivyokuwa kweli. Nilisoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness na kitabu cha Ripley kiitwacho Amini au Usiamini. Yeyote kati yenu amewahi kusoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness au kitabu cha Ripley? Navipenda vitabu hivi! Niliona watu wafanyao ujasiri halisia. Nikasema, Nataka kufanya hivyo. Ikiwa waonevu hawataniruhusu kucheza katika michezo yao yoyote, Nataka kufanya maajabu, ujasiri halisi. Nataka kufanya kitu cha kusifika ambacho hao waonevu hawawezi kufanya. Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, Nataka kujua kuwa maisha yangu yana maana, Nataka kufanya kitu cha kushangaza kubadili ulimwengu; Ninataka kuthibitisha yasiyowezekana sio hayawezekani. Kupeleka mbele miaka 10 - Ilikuwa wiki kabla ya kutimiza miaka 21. Mambo mawili yalitokea kwa siku moja ambayo yangebadilisha maisha yangu milele. Nilikuwa nikiishi Tamil Nadu, India Kusini Nilikuwa mmishonari huko, na mshauri wangu, rafiki yangu aliniuliza, "Je, una Thromu, Daniel?" Na nikasema, "Thromu? Thromu ni nini? " Alisema, "Thromu ni malengo makuu ya maisha. Ni muunganiko wa ndoto na malengo, kama ungeweza kufanya chochote unachotaka, kwenda popote unapotaka kuwa mtu yeyote unayetaka, ungekwenda wapi? Ungefanya nini? Ungekuwa nani? Nikasema, "Siwezi kufanya hivyo! Naogopa sana! Naogopa mengi mno! " Usiku huo nilichukua mkeka wangu wa mchele juu ya paa la ghorofa, nikautandika chini ya nyota, na kuangalia popo wakiwashambulia mbu. Na yote niliyofikiria ilikuwa thromu, na ndoto na malengo, na wale washujaaji wenye mipira ya kuchenga. Masaa machache baadaye niliamka. Moyo wangu ulienda mbio, magoti yangu yakitetemeka. Safari hii haikuwa na hofu. Mwili wangu wote ulitikisika. Na kwa siku tano zilizofuata Nilipoteza na kurudisha fahamu, kitandani nikipigania maisha yangu. Ubongo wangu ulikuwa unawaka na homa ya malaria yenye jotoridi la 105. Na kila fahamu ziliponirudia, nilichowaza ilikuwa kuhusu thromu. Niliwaza "Nataka kufanya nini na maisha yangu?" Hatimaye, usiku kabla sijafikisha miaka 21, katika wakati wa kuelewa, Nilikuja kutambua: Nilitambua kwamba yule mbu mdogo, Anofelesi Stefensi, yule mbu mdogo aliye na uzito chini ya mikrogramu 5 chini ya punje ya chumvi, anaweza kuangusha mtu wa ratili 170, mtu wa kilo 80, Niligundua kwamba alikuwa hasimu wangu. Kisha nikagundua, hapana, hapana, sio mbu, Ni vimelea vidogo ndani ya mbu, Plasmodium Falciparum, ambao huua zaidi ya watu milioni kwa mwaka Kisha nikagundua Hapana, hapana, tena ni ndogo zaidi, lakini kwangu, ilionekana kubwa zaidi. Niligundua, hofu ilikuwa hasimu yangu, vimelea yangu, vilivyonitia ulemavu na kunipooza mimi maisha yangu yote. Unajua, kuna tofauti kati ya hatari na hofu. Hatari ni halisi. Hofu ni hiari. Na nikagundua kuwa nina hiari: Aidha niishi kwa hofu, na kufa katika kushindwa usiku ule, au ningeweza kuua hofu yangu, na ningeweza kufikia ndoto zangu, Ningeweza kuthubutu kuishi maisha. Na unajua, kuna kitu kuhusu kuwa kwenye kitanda cha mauti na kukabiliwa na kifo ambacho haswa kinakufanya utake kweli kuishi maisha. Nikagundua kuwa kila mtu hufa, si kila mtu huishi. Ni katika kufa ndio sisi tunaishi. Unajua, wakati unapojifunza kufa, unajifunza kweli kuishi. Kwa hiyo nikaamua nitaenda kubadilisha hadithi yangu usiku huo. Sikutaka kufa. Hivyo nikafanya sala ndogo, nikasema, "Mungu, ukiniruhusu niishi nifikishe miaka 21, Sitaruhusu hofu itawale maisha yangu tena. Nitaziweka hofu zangu kifoni, Nitaenda kuzifikia ndoto zangu, Ninataka kubadilisha mtazamo wangu, Nataka kufanya kitu cha ajabu na maisha yangu, Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, Ninataka kujua kuwa yasiyowezekana si hayawezekani. " Sitawaambia kama nilinusurika usiku ule; Nitawaacha mfikirie. (Kicheko) Lakini usiku huo niliandika orodha ya Thromu zangu 10 za kwanza: Niliamua nilitaka kutembelea mabara makubwa kutembelea Maajabu 7 ya Dunia kujifunza lugha nyingi, kuishi kwenye kisiwa kitupu, kuishi kwenye meli baharini, kuishi na kabila la Wahindi katika Amazon, kupanda hadi juu ya mlima mrefu kuliko yote Sweden, Nilitaka kuona mawio Mlima Everest, kufanya kazi na biashara ya muziki Nashville, Nilitaka kufanya kazi ya sarakasi, na nilitaka kuruka nje ya ndege. Zaidi ya miaka ishirini iliyofuata, Nilitimiza thromu hizo kwa wingi. Kila wakati niliondoa thromu kwenye orodha yangu, Niliongeza 5 au 10 zaidi kwenye orodha na orodha yangu iliendelea kukua. Kwa miaka saba iliyofuata, niliishi kwenye kisiwa kidogo katika Bahamas kwa karibu miaka saba katika kibanda cha makuti, nikiwinda papa na taa wa kula, nikiwa mtu pekee kwenye kisiwa, nikiwa nimevaa msuli, na nikajifunza kuogelea na papa. Na kutoka huko, nikahamia Mexico, na kisha nikasafiri kwa bonde la Mto Amazon nchini Ecuador, Pujo Pongo Ecuador, niliishi na kabila moja huko, na kidogo kidogo nilianza kuongeza kujiamini kwa thromu zangu tu. Nilihamia biashara ya muziki Nashville, kisha Sweden, nikahamia Stockholm, kufanyakazi katika biashara ya muziki, ambapo nilipanda kilele cha Ml. Kebnekaise juu ya mzunguko wa Arctic. Nilijifunza udamisi, na viinimacho, na kutembea kama ngongoti, kuendesha baiskeli kwa tairi moja, kula moto, kula kioo. Mwaka 1997 nilisikia kuna wameza panga wasiozidi kumi na mbili na nikasema, "Inabidi kufanya hivyo!" Nilikutana na mmeza panga, na nikamwomba vidokezo. Akasema, "Naam, nitakupa vidokezo 2: Namba 1: Ni hatari sana, Watu wamekufa wakifanya hivi. Namba 2: Usijaribu! " (Kicheko) Basi nikaiongeza kwenye orodha ya thromu. Na nikafanya mazoezi mara 10 hadi 12 kwa siku, kila siku kwa miaka minne. Sasa nilipigia hesabu hizo... 4 x 365 [x 12] Ilikuwa karibu 13,000 majaribio yasiyofanikiwa kabla sijatia panga langu wa kwanza chini koo mwaka 2001. Wakati huo nikaweka thromu kuwa mtaalamu wa ulimwengu kwa kumeza panga. Basi nilitafuta kila kitabu, gazeti, makala ya gazeti, kila ripoti ya kitabibu, Nilijifunza fiziolojia, anatomia, Niliongea na madaktari na manesi, niliwakutanisha wameza panga wote pamoja kwenye Shirikisho la Wameza Panga Kimataifa, nikafanya ikisiri miaka 2 ya utafiti kitabibu kuhusu Umezaji wa Panga na athari zake iliyochapishwa katika Jarida la Kitabibu Uingereza. (Kicheko) Asanteni. (Makofi) Na nilijifunza mambo ya kuvutia sana kuhusu umezaji wa panga. Vitu vingine ambavyo haujawahi kufikiria kabla, hutasahau baada ya usiku huu. Wakati utakapoenda nyumbani, na unakata steki yako na kisu chako au panga, au "bestek" zako, utafikiri juu ya hili ... Nilijifunza kwamba umezaji panga ulianzia India - mahali nilipona kwa mara ya kwanza nikiwa kijana wa miaka 20 - karibu miaka 4000 ya kale, karibu 2000 BC. Zaidi ya miaka 150 iliyopita, wameza panga walitumika katika medani za sayansi na kitabibu ili kusaidia kuunda endoskopia imara mwaka 1868 wakiwa na Dk. Adolf Kussmaul wa Freiburg, Ujerumani Mnamo 1906, elektrokadiogramu huko Wales, kujifunza matatizo ya kumeza, na mmeng'enyo wa chakula, aina ya bronkoskopia, . Lakini zaidi ya miaka 150 iliyopita, tunajua mamia ya madhara na vifo kadhaa ... Hii ni endoskopia imara iliyoanzishwa na Dk. Adolph Kussmaul. Lakini tuligundua kuwa kulikuwa na Vifo 29 zaidi ya miaka 150 iliyopita. pamoja na mmezaji panga huko London aliyetoboa moyo wake kwa panga Tulijifunza pia kuwa kuna kesi tatu hadi nane za madhara mkubwa ya umezaji panga kila mwaka. Najua kwa sababu mimi hupata simu. Nilikuwa na wawili, mmoja kutoka Sweden, na kutoka Orlando wiki chache zilizopita, wamezaji panga waliopo hospitalini kutokana na madhara. Kwa hiyo ni hatari sana. Jambo jingine nililojifunza ni kuwa kumeza panga huchukua miaka 2 hadi miaka 10 kujifunza jinsi ya kumeza panga kwa watu wengi. Lakini ugunduzi unaovutia sana Nilijifunza ilikuwa jinsi wameza panga wanavyojifunza kufanya yasiyowezekana. Nami nitawapa siri ndogo: Usizingatie kwenye asilimia 99.9 kuwa haiwezekani. Unazingatia hiyo 1% ambayo inawezekana, na fikiria jinsi ya kufanya iwezeikane Sasa napenda kukupeleka kwenye safari ndani ya akili ya mmeza panga. Ili kumeza panga, inahitaji akili itafakari jambo, uzingativu wa hali ya juu, kuonyesha ufasaha ili kutenganisha viungo vya ndani vya mwili na kushinda vitendo hiari mwilini kupitia njia ya ubongo iliyoimarishwa, kupitia marido ya kumbukumbu ya misuli kwa mazoezi ya makusudi zaidi ya mara 10,000. Sasa ngoja niwasafirishe kidogo ndani ya mwili wa mmeza panga Ili kumeza panga, Lazima niteleze panga juu ya ulimi wangu, nizuie kutaka kutapika kwenye shingo ya umio, zungusha mgeuko wa nyuzi 90 chini ya gegedu ya ulimi, pitia kwenye msuli juu ya kilinda umio, zuia vitendohiari vya tumbo, telezea makali kwenye shimo la kifua kati ya mapafu. Katika hatua hii, Lazma kweli nisukume moyo wangu pembeni. Ikiwa utaangalia kwa makini, unawezaona moyo ukidunda kwa panga langu kwa sababu linaegemea moyo ikitenganishwa na karibu thumuni ya inchi ya tishu ya umio. Hicho sio kitu unaweza kudanganya. Kisha hutelezesha kupita mfupa wa kifua, kupita kilinda umio, chini ndani ya tumbo, zuia vitendohiari ndani ya tumbo njia yote hadi kwenye mbuti. Rahisi sana. (Kicheko) Kama ningetakiwa kwenda zaidi ya hapo, hadi kufikia mirija yangu ya mayai. mirija ya mayai! (Kidachi) Wanaume, mnaweza kuwauliza wake zenu kuhusu hiyo baadaye ... Watu huniuliza, wanasema, "lazima kuchukua ujasiri mwingi ili kuhatarisha maisha yako, kusogeza moyo wako, na kumeza panga ... " Hapana. Kinachofanya ujasiri halisi ni kwa yule kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba kwa kuhatarisha kushindwa na kukataliwa, kufungua moyo wake, na kumeza kiburi chake na kusimama hapa mbele ya kundi la watu asiowafahamu kabisa na kukuambia hadithi yake kuhusu hofu na ndoto zake, kwa hatarisha kumwaga habari zake, vyote kihalisia na kitamathali. Unaona - asante. (Makofi) Unaona, jambo la kustaajabisha sana ni Nimetaka kufanya mambo ya kusifika maishani mwangu na sasa nimesifika. Lakini jambo la kusifika haswa sio kwamba ninaweza kumeza panga 21 kwa mara moja, au futi 20 chini ya maji kwenye tanki la papa 88 na taa kwa kitabu cha Amini au Usiamini, au kuchowa hadi kuwa mwekundu nyuzi 1500 kwa Watu jasiri wa Stan Lee kama "Mtu wa Chuma" na yule jamaa alikuwa moto! Au kuvuta gari kwa upanga kwa Ripley, au Guinness, au kufikia fainali za shindano la vipaji Marekani, au kushinda 2007 tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu. La, hilo sio jambo la kusifika sana. Hivyo ndio watu wanafikiria. La, la, la. Sio hivyo. Jambo la kusifika sana ni Mungu angemchukua kijana, mwoga, mwenye aibu mwembamba aliyehofia vimo virefu, aliyehofia ya maji na papa, na madaktari na manesi na sindano na vyenye ncha kali na kuzungumza na watu na sasa ananifanya nipae duniani kote katika kina cha futi 30,000 kumeza vitu vya ncha chini ya maji ya tanki ya papa, na kuzungumza na madaktari na wauguzi na hadhira kama ninyi duniani Hilo ni jambo la kustaajabu sana kwangu. Nimetaka kufanya mambo yasiyowezekana - Asante. (Makofi) Asante. (Makofi) Sikuzote nilitaka kufanya yasiyowezekana, na sasa nimeweza. Nilitaka kufanya kitu cha kusifika maishani na kubadilisha ulimwengu, na sasa nimeweza. Siku zote nilitaka kupaa duniani kote kufanya vitendo vigumu na kuokoa maisha, sasa nimeweza. Na unajua nini? Bado kuna sehemu ndogo ya ndoto kubwa ya yule mtoto mdogo ndani kabisa. (Kicheko) (Makofi) Na unajua, sikuzote nilitaka kupata kusudi langu na wito wangu, na sasa nimepata. Lakini nadhani nini? Si kwa panga, sio unavyofikiria, si kwa nguvu zangu. Ni kwa udhaifu wangu, maneno yangu. Kusudi langu na wito ni kubadili ulimwengu kwa kukata kupitia hofu, upanga mmoja kwa wakati, neno moja kwa wakati, kisu moja kwa wakati, maisha kwa wakati, kuhamasisha watu kuwa mashujaa na kufanya yasiyowezekana maishani mwao. Kusudi langu ni kusaidia wengine kupata yao. La kwako ni lipi? Nini kusudi lako? Uliwekwa kufanya nini hapa? Naamini sisi wote tumeitwa kuwa mashujaa. Nguvu yako kubwa ni nini? Kati ya idadi ya watu duniani ya watu zaidi ya bilioni 7, kuna wameza upanga wachache sana waliobakia duniani kote leo, lakini kuna wewe mmoja. Wewe ni wa pekee. Hadithi yako ni nini? Nini kinakufanya uwe tofauti? Simulia hadithi yako, hata kama sauti yako ni nyembamba na inatetemeka. Je, thromu zako ni nini? kama ungefanya chochote, kuwa yeyote, kwenda popote - Ungefanya nini? Ungekwenda wapi? Ungefanya nini? Unataka kufanya nini na maisha yako? Nini ndoto zako kubwa? Nini ndoto zako kubwa ulipokuwa mdogo? Fikiria tena Nina uhakika hii haikuwa hivyo, si ndiyo? Nini zilikuwa ndoto zako kuu ulizofikiri zilikuwa ajabu sana na zisizoeleweka? Hakika hii inafanya ndoto zako zisionekane za ajabu tena, sivyo? Upanga wako ni nini? Kila mmoja wenu ana upanga, upanga wa pande mbili wa hofu na ndoto. Meza upanga wako, chochote utachokuwa. Fuata ndoto zako, mabibi na mabwana, Hujachelewa sana kuwa chochote unataka kuwa. Kwa wale waonevu na mipira ya kukwepa, wale watoto waliodhani kuwa sitaweza kufanya yasiyowezekana, Nina kitu kimoja tu cha kuwaambia: Asanteni. Kwa sababu kama si kwa wahalifu, tusingekuwa kuwa na mashujaa. Nipo hapa kuthibitisha yasiyowezekana si hayawezekani. Hii ni hatari sana, Inaweza kuniua. Natumaini mtafurahia. (Kicheko) Nitahitaji msaada wenu kwenye hili. Hadhira:Mbili, tatu. Dan Meyer:La, la, la. Nahitaji msaada wenu kwenye kuhesabu, nyote, sawa? (Vicheko) Kama unajua maneno? Sawa? Hesabu na mimi. Tayari? Moja. Mbili. Tatu. La, hiyo ni 2, lakini mmeelewa Hadhira: Moja. Mbili. Tatu. (Vuta pumzi) (Makofi) DM: Ndiyo! (Makofi) (Kushangilia) Asanteni sana. Asante, asante, asante. Asante kutoka kina cha moyo wangu Kweli, asante kutoka chini ya tumbo langu. Niliwaambia nimekuja hapa kufanya yasiyowezekana, na sasa nimeweza. Ila hii haikuwa isiyowezekana. Ninafanya hivi kila siku. Kitu kisichowezekana ilikuwa yule mwoga, mwenye aibu mwembamba kukabili hofu zake kusimama hapa kwenye jukwaa la [TEDx], na kubadilisha dunia, neno moja kwa wakati, upanga kwa wakati, maisha kwa wakati. kama nimekufanya ufikiri kwa njia mpya, kama nimekufanya uamini yasiyowekana si hayawezekani, ikiwa nimekufanya uelewe kuwa waweza fanya yasiyowezekana maishani mwako, basi kazi yangu imekwisha, na yako ndiyo kwanza imeanza. Usiache kuwa na ndoto. Usiache kuamini. Asanteni kwa kuniamini na asanteni kuwa sehemu ya ndoto yangu. Hii ni zawadi kwenu: Yasiyowezekana si ... Hadhira: Hayawezekani. Mwendo mrefu ni sehemu ya zawadi. (Makofi) Asanteni. (Makofi) (Kushangilia) Mwenyeji: Asante, Dan Meyer, wow!