1 00:00:08,380 --> 00:00:09,561 Asante 2 00:00:16,270 --> 00:00:21,200 Palikuwa na mfalme nchini India, Maharaja na siku yake ya kuzaliwa ilitolewa amri 3 00:00:21,200 --> 00:00:24,200 kwamba machifu wote walete zawadi kwa mfalme. 4 00:00:24,400 --> 00:00:28,370 Wengine wakaleta hariri bora, wengine wakaleta panga maridadi, 5 00:00:28,370 --> 00:00:29,490 wengine dhahabu 6 00:00:29,490 --> 00:00:32,659 mwisho wa mstari alikuja akitembea mzee mdogo mwenye makunyanzi 7 00:00:32,659 --> 00:00:36,630 ambaye alitembea kutoka kijijini kwake kwa safari ya siku nyingi kando ya bahari. 8 00:00:36,630 --> 00:00:41,150 alipokuwa akisogea mwana mfalme akauliza, 'Umemletea zawadi gani Mfalme?' 9 00:00:41,457 --> 00:00:44,750 Na mzee yule taratibu sana akakunjua mkono wake kuonyesha 10 00:00:44,750 --> 00:00:49,600 kombe la baharini zuri sana, lenye makoa ya zambarau na njano,nyekundu na bluu. 11 00:00:50,160 --> 00:00:51,380 Na mwana Mfalme akasema, 12 00:00:51,460 --> 00:00:54,400 "Hiyo si zawadi kwa Mfalme! Ni zawadi gani hiyo?" 13 00:00:54,600 --> 00:00:57,400 Mzee yule akamwangalia taratibu na kusema 14 00:00:57,590 --> 00:01:00,750 "Kutembea mwendo mrefu.. ni sehemu ya zawadi" 15 00:01:01,060 --> 00:01:02,560 (Kicheko) 16 00:01:02,900 --> 00:01:05,970 Baada ya muda mfupi, Nitawapa zawadi, 17 00:01:05,970 --> 00:01:08,270 zawadi niaminiyo ni zawadi inayostahili kuenezwa. 18 00:01:08,290 --> 00:01:10,050 Ila kabla ya hayo, ngoja niwachukue 19 00:01:10,050 --> 00:01:11,960 kwenye mwendo wangu mrefu. 20 00:01:12,160 --> 00:01:13,740 Kama wengi wenu, 21 00:01:13,740 --> 00:01:15,320 Nilianza maisha kama mtoto mdogo. 22 00:01:15,320 --> 00:01:17,460 Wangapi kati yenu mlianza maisha kama mtoto ? 23 00:01:17,460 --> 00:01:18,510 Aliyezaliwa mchanga? 24 00:01:18,740 --> 00:01:20,500 Karibia nusu yenu.. Sawa 25 00:01:20,570 --> 00:01:21,590 (Kicheko) 26 00:01:21,820 --> 00:01:24,910 Na mliobakia, vipi? Mlizaliwa mkiwa watu wazima? 27 00:01:25,060 --> 00:01:27,640 Ama kweli, nataka kukutana na mama zenu! 28 00:01:27,820 --> 00:01:29,460 Ongelea yasiyowezekana! 29 00:01:30,560 --> 00:01:34,740 Nikiwa mtoto mdogo, siku zote nilipendezwa kufanya mambo yasiyowezekana 30 00:01:35,620 --> 00:01:38,880 Leo ni siku ambayo nimekuwa nikiitarajia kwa miaka mingi, 31 00:01:38,880 --> 00:01:41,000 kwa sababu leo ni siku ambayo nitajaribu 32 00:01:41,020 --> 00:01:43,620 kufanya yasiyowezekana mbele ya macho yenu 33 00:01:43,620 --> 00:01:45,460 Hapahapa TEDxMaastrich 34 00:01:45,800 --> 00:01:48,160 Nitaanza 35 00:01:48,760 --> 00:01:50,880 Kwa kuonyesha mwisho wake: 36 00:01:51,220 --> 00:01:52,640 Na nitawathibitishia kwamba 37 00:01:52,640 --> 00:01:54,940 yasiyowezekana siyo hayawezekani 38 00:01:55,300 --> 00:01:58,210 Na nitamalizia kwa kuwapa zawadi yenye kustahili kuieneza: 39 00:01:58,210 --> 00:02:01,350 Nitawaonyesha kwamba unaweza kufanya yasiyowezekana maishani mwako. 40 00:02:02,660 --> 00:02:05,420 katika kutafuta kufanya yasiyowezekana, nimegundua kuna 41 00:02:05,420 --> 00:02:08,230 mambo mawili yanayofanana kati ya watu duniani. 42 00:02:08,230 --> 00:02:09,870 Kila mtu ana hofu, 43 00:02:09,870 --> 00:02:11,640 na kila mtu ana ndoto. 44 00:02:12,900 --> 00:02:17,560 Katika kutafuta kufanya yasiyowezekana nimegundua kuna vitu vitatu 45 00:02:17,560 --> 00:02:20,100 ambavyo nimevifanya miaka mingi ambavyo 46 00:02:20,110 --> 00:02:23,290 vimenisababishia kufanya yasiyowezekana: 47 00:02:24,200 --> 00:02:26,900 Mchezo wa mpira wa kuchenga au "Trefball" 48 00:02:27,290 --> 00:02:28,360 Superman, 49 00:02:28,460 --> 00:02:29,460 na Mbu 50 00:02:29,460 --> 00:02:30,810 Hayo ni maneno yangu matatu makuu. 51 00:02:30,810 --> 00:02:33,500 Mmeshajua kwanini nafanya yasiyowezekana maishani mwangu 52 00:02:33,610 --> 00:02:36,220 Hivyo nitawachukua katika safari yangu, ya mwendo mrefu 53 00:02:36,320 --> 00:02:38,680 kutoka kwenye hofu hadi ndoto 54 00:02:38,740 --> 00:02:40,980 kutoka kwenye maneno hadi panga, 55 00:02:41,160 --> 00:02:42,740 Kutoka Mpira wa kuchenga 56 00:02:42,850 --> 00:02:44,020 hadi Superman 57 00:02:44,020 --> 00:02:45,340 hadi kwa Mbu 58 00:02:45,800 --> 00:02:47,360 Na ninatumaini kuwaonyesha 59 00:02:47,360 --> 00:02:49,900 unawezaje kufanya yasiyo wezekana maishani mwako 60 00:02:52,480 --> 00:02:54,934 Oktoba 4, mwaka 2007. 61 00:02:55,840 --> 00:02:58,120 Moyo wangu ulienda mbio, magoti yangu yalitetema 62 00:02:58,120 --> 00:02:59,340 nilipokuwa napanda jukwaani 63 00:02:59,340 --> 00:03:00,930 kwenye ukumbi wa Sanders 64 00:03:01,040 --> 00:03:03,240 Chuo cha Harvard kupokea 65 00:03:03,240 --> 00:03:06,160 Tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu 66 00:03:06,160 --> 00:03:08,660 kwa kushiriki kuandika ikisiri ya utafiti wa kitabibu 67 00:03:08,660 --> 00:03:10,270 ulioitwa "Kumeza Upanga... 68 00:03:10,420 --> 00:03:11,740 ...na Athari zake" 69 00:03:11,870 --> 00:03:13,275 (Kicheko) 70 00:03:13,840 --> 00:03:17,880 Ilichapishwa kwenye jarida dogo ambalo sikuwahi kulisoma kabla, 71 00:03:18,460 --> 00:03:20,419 Jarida la Kitabibu la Uingereza. 72 00:03:21,360 --> 00:03:24,740 Na kwangu, hiyo ilikuwa ndoto isiyowezekana kuwa kweli, 73 00:03:24,900 --> 00:03:28,120 ilikuwa ni mshangao usiotegemewa kwa mtu kama mimi, 74 00:03:28,130 --> 00:03:31,459 ilikuwa ni heshima ambayo sitaweza kusahau 75 00:03:31,459 --> 00:03:34,539 Lakini haikuwa sehemu ya kubwa ya kukumbuka maishani mwangu. 76 00:03:35,540 --> 00:03:37,640 Mnamo Oktoba 4, mwaka 1967 77 00:03:38,020 --> 00:03:40,260 kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 78 00:03:41,100 --> 00:03:43,120 aliteseka na hofu kubwa kupita kiasi. 79 00:03:43,460 --> 00:03:45,579 Alipojiandaa kupanda jukwaani, 80 00:03:45,579 --> 00:03:47,234 moyo wake ulienda mbio, 81 00:03:47,500 --> 00:03:49,162 magoti yake yalikuwa yakitetemeka. 82 00:03:49,780 --> 00:03:52,120 Alikwenda kufungua kinywa chake kuongea, 83 00:03:56,490 --> 00:03:58,130 maneno hayakuweza kutoka. 84 00:03:58,130 --> 00:04:00,040 Alisimama akitetemeka na kutoa machozi. 85 00:04:00,630 --> 00:04:02,360 Alipooza kwa mshtuko wa ghafla, 86 00:04:02,360 --> 00:04:03,760 alipatwa fadhaa kwa hofu. 87 00:04:03,960 --> 00:04:06,130 huyu kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 88 00:04:06,130 --> 00:04:08,142 alitesekana na hofu kubwa kupita kiasi. 89 00:04:08,649 --> 00:04:10,330 Alikuwa na hofu ya giza, 90 00:04:10,520 --> 00:04:11,640 hofu ya vimo virefu, 91 00:04:11,640 --> 00:04:13,040 hofu ya buibui na nyoka ... 92 00:04:13,040 --> 00:04:15,140 Kuna yeyote anayeogopa buibui na nyoka? 93 00:04:15,280 --> 00:04:16,660 Naam, wachache wenu ... 94 00:04:16,660 --> 00:04:19,079 Alikuwa na hofu ya maji na papa ... 95 00:04:19,079 --> 00:04:21,939 Hofu ya madaktari na manesi na madaktari wa meno, 96 00:04:21,939 --> 00:04:24,680 na sindano na kutobolewa na vitu vya ncha kali. 97 00:04:24,680 --> 00:04:27,380 Lakini zaidi ya chochote, alikuwa na hofu ya 98 00:04:27,470 --> 00:04:28,470 watu 99 00:04:29,380 --> 00:04:31,530 Huyo kijana mwoga,mwenye aibu na mwembamba 100 00:04:31,540 --> 00:04:32,570 alikuwa mimi. 101 00:04:33,320 --> 00:04:35,997 Nilikuwa na hofu ya kushindwa na kukataliwa, 102 00:04:37,300 --> 00:04:39,520 kutojithamini, kujiona duni, 103 00:04:39,520 --> 00:04:42,840 na kitu ambacho hata hatukujua unaweza kujiandikisha kwa siku hizo: 104 00:04:42,840 --> 00:04:44,660 ugonjwa wa hofu ya ukaribu na watu. 105 00:04:44,955 --> 00:04:48,610 Kwa sababu nilikuwa na hofu, waonevu walinitania na kunipiga. 106 00:04:48,610 --> 00:04:52,240 Walinicheka na kuniita majina, Hawakuniruhusu kucheza nao 107 00:04:52,300 --> 00:04:54,260 michezo ya aina yoyote. 108 00:04:55,020 --> 00:04:58,056 Ah, kulikuwa na mchezo mmoja walikuwa wakiruhusu kucheza kwenye ... 109 00:04:58,100 --> 00:04:59,427 Mpira wa kuchenga - 110 00:04:59,500 --> 00:05:01,443 na sikuwa mchengaji nzuri. 111 00:05:01,760 --> 00:05:03,500 Waonevu waliita jina langu, 112 00:05:03,500 --> 00:05:05,970 na nilipoangalia niliona mipira myekundu ya kukwepa 113 00:05:05,970 --> 00:05:08,200 ikivurumishwa usoni wangu kwa kasi kubwa 114 00:05:08,210 --> 00:05:09,950 bam, bam, bam! 115 00:05:10,580 --> 00:05:13,220 Ninakumbuka siku nyingi nikirudi nyumbani kutoka shule, 116 00:05:13,300 --> 00:05:18,180 uso wangu ulikuwa mwekundu ukichonyota, masikio yangu yalikuwa mekundu yakivuma. 117 00:05:18,180 --> 00:05:21,140 Macho yangu yalichoma kwa machozi, 118 00:05:21,180 --> 00:05:23,515 na maneno yao yalichoma masikioni mwangu. 119 00:05:23,740 --> 00:05:25,000 Na yeyote aliyesema, 120 00:05:25,020 --> 00:05:28,660 "Fimbo na mawe vyaweza kunivunja mifupa, bali maneno hayatoniumiza kamwe "... 121 00:05:28,880 --> 00:05:30,131 Ni uongo. 122 00:05:30,310 --> 00:05:31,980 Maneno huweza kukata kama kisu. 123 00:05:31,980 --> 00:05:34,030 Maneno huweza kupenya kama upanga. 124 00:05:34,210 --> 00:05:36,040 Maneno huwezafanya majeraha yenye kina 125 00:05:36,040 --> 00:05:37,780 yasiweze kuonekana. 126 00:05:38,150 --> 00:05:41,070 Hivyo nilikuwa na hofu. Na maneno yalikuwa adui yangu mkubwa. 127 00:05:41,260 --> 00:05:42,491 Bado ni adui yangu. 128 00:05:43,355 --> 00:05:45,300 Lakini pia nilikuwa na ndoto. 129 00:05:45,300 --> 00:05:47,980 Nilienda nyumbani na kutorokea kwenye futuhi za Superman 130 00:05:47,980 --> 00:05:49,774 na nilisoma futuhi za Superman 131 00:05:49,774 --> 00:05:53,440 na niliota kutaka kuwa shujaa mkubwa kama Superman. 132 00:05:53,480 --> 00:05:56,240 Nilitaka kupigania kweli na haki, 133 00:05:56,240 --> 00:05:58,680 Nilitaka kupambana dhidi ya wahalifu na mahasimu, 134 00:05:58,680 --> 00:06:02,895 Nilitaka kupaa duniani kote kufanya vitendo vya ujasiri kuokoa maisha. 135 00:06:03,400 --> 00:06:05,850 Nilikuwa pia navutiwa mno na vitu vilivyokuwa kweli. 136 00:06:05,860 --> 00:06:09,460 Nilisoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness na kitabu cha Ripley kiitwacho Amini au Usiamini. 137 00:06:09,460 --> 00:06:13,080 Yeyote kati yenu amewahi kusoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness au kitabu cha Ripley? 138 00:06:13,100 --> 00:06:14,390 Navipenda vitabu hivi! 139 00:06:14,390 --> 00:06:16,270 Niliona watu wafanyao ujasiri halisia. 140 00:06:16,270 --> 00:06:17,790 Nikasema, Nataka kufanya hivyo. 141 00:06:17,790 --> 00:06:19,330 Ikiwa waonevu hawataniruhusu 142 00:06:19,330 --> 00:06:21,030 kucheza katika michezo yao yoyote, 143 00:06:21,030 --> 00:06:23,335 Nataka kufanya maajabu, ujasiri halisi. 144 00:06:23,335 --> 00:06:26,659 Nataka kufanya kitu cha kusifika ambacho hao waonevu hawawezi kufanya. 145 00:06:26,659 --> 00:06:28,609 Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, 146 00:06:28,609 --> 00:06:30,729 Nataka kujua kuwa maisha yangu yana maana, 147 00:06:30,729 --> 00:06:33,320 Nataka kufanya kitu cha kushangaza kubadili ulimwengu; 148 00:06:33,320 --> 00:06:36,960 Ninataka kuthibitisha yasiyowezekana sio hayawezekani. 149 00:06:38,340 --> 00:06:40,240 Kupeleka mbele miaka 10 - 150 00:06:40,240 --> 00:06:42,706 Ilikuwa wiki kabla ya kutimiza miaka 21. 151 00:06:42,819 --> 00:06:46,799 Mambo mawili yalitokea kwa siku moja ambayo yangebadilisha maisha yangu milele. 152 00:06:47,040 --> 00:06:49,391 Nilikuwa nikiishi Tamil Nadu, India Kusini 153 00:06:49,540 --> 00:06:51,020 Nilikuwa mmishonari huko, 154 00:06:51,020 --> 00:06:53,090 na mshauri wangu, rafiki yangu aliniuliza, 155 00:06:53,090 --> 00:06:54,720 "Je, una Thromu, Daniel?" 156 00:06:54,720 --> 00:06:57,440 Na nikasema, "Thromu? Thromu ni nini? " 157 00:06:57,440 --> 00:07:00,490 Alisema, "Thromu ni malengo makuu ya maisha. 158 00:07:00,490 --> 00:07:04,630 Ni muunganiko wa ndoto na malengo, kama ungeweza 159 00:07:04,630 --> 00:07:07,240 kufanya chochote unachotaka, kwenda popote unapotaka 160 00:07:07,240 --> 00:07:08,479 kuwa mtu yeyote unayetaka, 161 00:07:08,479 --> 00:07:10,356 ungekwenda wapi? Ungefanya nini? 162 00:07:10,356 --> 00:07:11,280 Ungekuwa nani? 163 00:07:11,280 --> 00:07:14,500 Nikasema, "Siwezi kufanya hivyo! Naogopa sana! Naogopa mengi mno! " 164 00:07:14,500 --> 00:07:17,800 Usiku huo nilichukua mkeka wangu wa mchele juu ya paa la ghorofa, 165 00:07:17,810 --> 00:07:19,259 nikautandika chini ya nyota, 166 00:07:19,259 --> 00:07:21,869 na kuangalia popo wakiwashambulia mbu. 167 00:07:21,869 --> 00:07:26,200 Na yote niliyofikiria ilikuwa thromu, na ndoto na malengo, 168 00:07:26,200 --> 00:07:28,360 na wale washujaaji wenye mipira ya kuchenga. 169 00:07:28,760 --> 00:07:30,730 Masaa machache baadaye niliamka. 170 00:07:31,220 --> 00:07:33,940 Moyo wangu ulienda mbio, magoti yangu yakitetemeka. 171 00:07:34,080 --> 00:07:36,020 Safari hii haikuwa na hofu. 172 00:07:36,420 --> 00:07:38,395 Mwili wangu wote ulitikisika. 173 00:07:38,500 --> 00:07:40,180 Na kwa siku tano zilizofuata 174 00:07:40,330 --> 00:07:44,199 Nilipoteza na kurudisha fahamu, kitandani nikipigania maisha yangu. 175 00:07:44,199 --> 00:07:48,239 Ubongo wangu ulikuwa unawaka na homa ya malaria yenye jotoridi la 105. 176 00:07:48,390 --> 00:07:51,600 Na kila fahamu ziliponirudia, nilichowaza ilikuwa kuhusu thromu. 177 00:07:51,600 --> 00:07:53,820 Niliwaza "Nataka kufanya nini na maisha yangu?" 178 00:07:53,950 --> 00:07:56,380 Hatimaye, usiku kabla sijafikisha miaka 21, 179 00:07:56,380 --> 00:07:58,030 katika wakati wa kuelewa, 180 00:07:58,030 --> 00:07:59,639 Nilikuja kutambua: 181 00:07:59,639 --> 00:08:02,100 Nilitambua kwamba yule mbu mdogo, 182 00:08:02,620 --> 00:08:05,020 Anofelesi Stefensi, 183 00:08:05,280 --> 00:08:06,610 yule mbu mdogo 184 00:08:06,610 --> 00:08:08,390 aliye na uzito chini ya mikrogramu 5 185 00:08:08,390 --> 00:08:09,810 chini ya punje ya chumvi, 186 00:08:09,810 --> 00:08:12,780 anaweza kuangusha mtu wa ratili 170, mtu wa kilo 80, 187 00:08:12,780 --> 00:08:14,860 Niligundua kwamba alikuwa hasimu wangu. 188 00:08:14,860 --> 00:08:17,150 Kisha nikagundua, hapana, hapana, sio mbu, 189 00:08:17,150 --> 00:08:19,480 Ni vimelea vidogo ndani ya mbu, 190 00:08:19,480 --> 00:08:23,160 Plasmodium Falciparum, ambao huua zaidi ya watu milioni kwa mwaka 191 00:08:23,509 --> 00:08:25,999 Kisha nikagundua Hapana, hapana, tena ni ndogo zaidi, 192 00:08:25,999 --> 00:08:28,550 lakini kwangu, ilionekana kubwa zaidi. 193 00:08:28,550 --> 00:08:29,640 Niligundua, 194 00:08:29,640 --> 00:08:31,270 hofu ilikuwa hasimu yangu, 195 00:08:31,270 --> 00:08:32,140 vimelea yangu, 196 00:08:32,140 --> 00:08:34,990 vilivyonitia ulemavu na kunipooza mimi maisha yangu yote. 197 00:08:35,200 --> 00:08:38,080 Unajua, kuna tofauti kati ya hatari na hofu. 198 00:08:38,109 --> 00:08:39,699 Hatari ni halisi. 199 00:08:39,990 --> 00:08:42,010 Hofu ni hiari. 200 00:08:42,080 --> 00:08:44,309 Na nikagundua kuwa nina hiari: 201 00:08:44,309 --> 00:08:48,180 Aidha niishi kwa hofu, na kufa katika kushindwa usiku ule, 202 00:08:49,070 --> 00:08:52,080 au ningeweza kuua hofu yangu, na ningeweza 203 00:08:52,080 --> 00:08:56,060 kufikia ndoto zangu, Ningeweza kuthubutu kuishi maisha. 204 00:08:56,680 --> 00:08:59,560 Na unajua, kuna kitu kuhusu kuwa kwenye kitanda cha mauti 205 00:08:59,560 --> 00:09:04,080 na kukabiliwa na kifo ambacho haswa kinakufanya utake kweli kuishi maisha. 206 00:09:04,180 --> 00:09:07,140 Nikagundua kuwa kila mtu hufa, si kila mtu huishi. 207 00:09:08,040 --> 00:09:09,890 Ni katika kufa ndio sisi tunaishi. 208 00:09:09,890 --> 00:09:11,580 Unajua, wakati unapojifunza kufa, 209 00:09:11,580 --> 00:09:13,070 unajifunza kweli kuishi. 210 00:09:13,070 --> 00:09:15,140 Kwa hiyo nikaamua nitaenda kubadilisha 211 00:09:15,140 --> 00:09:16,420 hadithi yangu usiku huo. 212 00:09:16,915 --> 00:09:18,230 Sikutaka kufa. 213 00:09:18,230 --> 00:09:20,010 Hivyo nikafanya sala ndogo, nikasema, 214 00:09:20,010 --> 00:09:22,230 "Mungu, ukiniruhusu niishi nifikishe miaka 21, 215 00:09:22,230 --> 00:09:24,544 Sitaruhusu hofu itawale maisha yangu tena. 216 00:09:24,670 --> 00:09:26,520 Nitaziweka hofu zangu kifoni, 217 00:09:26,520 --> 00:09:29,530 Nitaenda kuzifikia ndoto zangu, 218 00:09:29,530 --> 00:09:31,270 Ninataka kubadilisha mtazamo wangu, 219 00:09:31,270 --> 00:09:33,540 Nataka kufanya kitu cha ajabu na maisha yangu, 220 00:09:33,540 --> 00:09:35,550 Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, 221 00:09:35,550 --> 00:09:38,632 Ninataka kujua kuwa yasiyowezekana si hayawezekani. " 222 00:09:38,780 --> 00:09:42,820 Sitawaambia kama nilinusurika usiku ule; Nitawaacha mfikirie. 223 00:09:42,850 --> 00:09:43,978 (Kicheko) 224 00:09:43,978 --> 00:09:47,100 Lakini usiku huo niliandika orodha ya Thromu zangu 10 za kwanza: 225 00:09:47,100 --> 00:09:50,210 Niliamua nilitaka kutembelea mabara makubwa 226 00:09:50,210 --> 00:09:51,820 kutembelea Maajabu 7 ya Dunia 227 00:09:51,820 --> 00:09:53,410 kujifunza lugha nyingi, 228 00:09:53,410 --> 00:09:54,940 kuishi kwenye kisiwa kitupu, 229 00:09:54,940 --> 00:09:56,480 kuishi kwenye meli baharini, 230 00:09:56,480 --> 00:09:58,650 kuishi na kabila la Wahindi katika Amazon, 231 00:09:58,650 --> 00:10:01,210 kupanda hadi juu ya mlima mrefu kuliko yote Sweden, 232 00:10:01,210 --> 00:10:03,180 Nilitaka kuona mawio Mlima Everest, 233 00:10:03,190 --> 00:10:05,390 kufanya kazi na biashara ya muziki Nashville, 234 00:10:05,400 --> 00:10:07,060 Nilitaka kufanya kazi ya sarakasi, 235 00:10:07,080 --> 00:10:09,120 na nilitaka kuruka nje ya ndege. 236 00:10:09,120 --> 00:10:12,380 Zaidi ya miaka ishirini iliyofuata, Nilitimiza thromu hizo kwa wingi. 237 00:10:12,410 --> 00:10:14,650 Kila wakati niliondoa thromu kwenye orodha yangu, 238 00:10:14,650 --> 00:10:18,190 Niliongeza 5 au 10 zaidi kwenye orodha na orodha yangu iliendelea kukua. 239 00:10:18,800 --> 00:10:23,280 Kwa miaka saba iliyofuata, niliishi kwenye kisiwa kidogo katika Bahamas 240 00:10:23,320 --> 00:10:25,360 kwa karibu miaka saba 241 00:10:25,370 --> 00:10:27,274 katika kibanda cha makuti, 242 00:10:29,480 --> 00:10:33,820 nikiwinda papa na taa wa kula, nikiwa mtu pekee kwenye kisiwa, 243 00:10:33,820 --> 00:10:36,249 nikiwa nimevaa msuli, 244 00:10:36,680 --> 00:10:39,160 na nikajifunza kuogelea na papa. 245 00:10:39,160 --> 00:10:40,980 Na kutoka huko, nikahamia Mexico, 246 00:10:40,980 --> 00:10:45,000 na kisha nikasafiri kwa bonde la Mto Amazon nchini Ecuador, 247 00:10:45,241 --> 00:10:48,100 Pujo Pongo Ecuador, niliishi na kabila moja huko, 248 00:10:48,100 --> 00:10:52,180 na kidogo kidogo nilianza kuongeza kujiamini kwa thromu zangu tu. 249 00:10:52,180 --> 00:10:55,100 Nilihamia biashara ya muziki Nashville, kisha Sweden, 250 00:10:55,110 --> 00:10:57,870 nikahamia Stockholm, kufanyakazi katika biashara ya muziki, 251 00:10:57,870 --> 00:11:01,920 ambapo nilipanda kilele cha Ml. Kebnekaise juu ya mzunguko wa Arctic. 252 00:11:03,300 --> 00:11:04,750 Nilijifunza udamisi, 253 00:11:04,750 --> 00:11:05,860 na viinimacho, 254 00:11:05,860 --> 00:11:07,480 na kutembea kama ngongoti, 255 00:11:07,480 --> 00:11:10,440 kuendesha baiskeli kwa tairi moja, kula moto, kula kioo. 256 00:11:10,450 --> 00:11:13,620 Mwaka 1997 nilisikia kuna wameza panga wasiozidi kumi na mbili 257 00:11:13,620 --> 00:11:15,410 na nikasema, "Inabidi kufanya hivyo!" 258 00:11:15,420 --> 00:11:18,290 Nilikutana na mmeza panga, na nikamwomba vidokezo. 259 00:11:18,290 --> 00:11:20,190 Akasema, "Naam, nitakupa vidokezo 2: 260 00:11:20,190 --> 00:11:21,926 Namba 1: Ni hatari sana, 261 00:11:21,926 --> 00:11:23,948 Watu wamekufa wakifanya hivi. 262 00:11:23,948 --> 00:11:24,953 Namba 2: 263 00:11:24,953 --> 00:11:26,206 Usijaribu! " 264 00:11:26,206 --> 00:11:27,520 (Kicheko) 265 00:11:27,540 --> 00:11:29,540 Basi nikaiongeza kwenye orodha ya thromu. 266 00:11:30,440 --> 00:11:33,320 Na nikafanya mazoezi mara 10 hadi 12 kwa siku, kila siku 267 00:11:33,660 --> 00:11:35,160 kwa miaka minne. 268 00:11:35,209 --> 00:11:36,709 Sasa nilipigia hesabu hizo... 269 00:11:36,709 --> 00:11:40,020 4 x 365 [x 12] 270 00:11:40,020 --> 00:11:42,660 Ilikuwa karibu 13,000 majaribio yasiyofanikiwa 271 00:11:42,660 --> 00:11:45,420 kabla sijatia panga langu wa kwanza chini koo mwaka 2001. 272 00:11:46,002 --> 00:11:47,630 Wakati huo nikaweka thromu 273 00:11:47,630 --> 00:11:50,940 kuwa mtaalamu wa ulimwengu kwa kumeza panga. 274 00:11:50,970 --> 00:11:53,820 Basi nilitafuta kila kitabu, gazeti, makala ya gazeti, 275 00:11:53,820 --> 00:11:57,670 kila ripoti ya kitabibu, Nilijifunza fiziolojia, anatomia, 276 00:11:57,676 --> 00:11:59,719 Niliongea na madaktari na manesi, 277 00:11:59,719 --> 00:12:01,760 niliwakutanisha wameza panga wote pamoja 278 00:12:01,760 --> 00:12:04,250 kwenye Shirikisho la Wameza Panga Kimataifa, 279 00:12:04,250 --> 00:12:06,450 nikafanya ikisiri miaka 2 ya utafiti kitabibu 280 00:12:06,450 --> 00:12:08,580 kuhusu Umezaji wa Panga na athari zake 281 00:12:08,580 --> 00:12:10,980 iliyochapishwa katika Jarida la Kitabibu Uingereza. 282 00:12:10,980 --> 00:12:11,840 (Kicheko) 283 00:12:11,840 --> 00:12:12,940 Asanteni. 284 00:12:12,960 --> 00:12:17,748 (Makofi) 285 00:12:18,200 --> 00:12:21,570 Na nilijifunza mambo ya kuvutia sana kuhusu umezaji wa panga. 286 00:12:21,571 --> 00:12:25,260 Vitu vingine ambavyo haujawahi kufikiria kabla, hutasahau baada ya usiku huu. 287 00:12:25,260 --> 00:12:28,550 Wakati utakapoenda nyumbani, na unakata steki yako na kisu chako 288 00:12:28,550 --> 00:12:31,759 au panga, au "bestek" zako, utafikiri juu ya hili ... 289 00:12:34,257 --> 00:12:36,589 Nilijifunza kwamba umezaji panga ulianzia India - 290 00:12:36,589 --> 00:12:39,889 mahali nilipona kwa mara ya kwanza nikiwa kijana wa miaka 20 - 291 00:12:39,889 --> 00:12:42,290 karibu miaka 4000 ya kale, karibu 2000 BC. 292 00:12:42,290 --> 00:12:45,580 Zaidi ya miaka 150 iliyopita, wameza panga walitumika 293 00:12:45,590 --> 00:12:47,400 katika medani za sayansi na kitabibu 294 00:12:47,480 --> 00:12:51,160 ili kusaidia kuunda endoskopia imara mwaka 1868 295 00:12:51,160 --> 00:12:53,820 wakiwa na Dk. Adolf Kussmaul wa Freiburg, Ujerumani 296 00:12:53,880 --> 00:12:56,639 Mnamo 1906, elektrokadiogramu huko Wales, 297 00:12:56,639 --> 00:13:00,240 kujifunza matatizo ya kumeza, na mmeng'enyo wa chakula, 298 00:13:00,240 --> 00:13:01,860 aina ya bronkoskopia, . 299 00:13:01,860 --> 00:13:03,840 Lakini zaidi ya miaka 150 iliyopita, 300 00:13:03,840 --> 00:13:07,860 tunajua mamia ya madhara na vifo kadhaa ... 301 00:13:07,880 --> 00:13:14,560 Hii ni endoskopia imara iliyoanzishwa na Dk. Adolph Kussmaul. 302 00:13:14,740 --> 00:13:18,679 Lakini tuligundua kuwa kulikuwa na Vifo 29 zaidi ya miaka 150 iliyopita. 303 00:13:18,679 --> 00:13:22,462 pamoja na mmezaji panga huko London aliyetoboa moyo wake kwa panga 304 00:13:23,142 --> 00:13:25,340 Tulijifunza pia kuwa kuna kesi tatu hadi nane za 305 00:13:25,340 --> 00:13:27,780 madhara mkubwa ya umezaji panga kila mwaka. 306 00:13:27,780 --> 00:13:29,880 Najua kwa sababu mimi hupata simu. 307 00:13:29,880 --> 00:13:31,150 Nilikuwa na wawili, 308 00:13:31,150 --> 00:13:34,320 mmoja kutoka Sweden, na kutoka Orlando wiki chache zilizopita, 309 00:13:34,320 --> 00:13:37,019 wamezaji panga waliopo hospitalini kutokana na madhara. 310 00:13:37,019 --> 00:13:38,769 Kwa hiyo ni hatari sana. 311 00:13:38,769 --> 00:13:41,629 Jambo jingine nililojifunza ni kuwa kumeza panga huchukua 312 00:13:41,629 --> 00:13:44,320 miaka 2 hadi miaka 10 kujifunza jinsi ya kumeza panga 313 00:13:44,320 --> 00:13:45,610 kwa watu wengi. 314 00:13:45,610 --> 00:13:48,020 Lakini ugunduzi unaovutia sana Nilijifunza ilikuwa 315 00:13:48,020 --> 00:13:51,360 jinsi wameza panga wanavyojifunza kufanya yasiyowezekana. 316 00:13:51,460 --> 00:13:53,460 Nami nitawapa siri ndogo: 317 00:13:53,520 --> 00:13:57,580 Usizingatie kwenye asilimia 99.9 kuwa haiwezekani. 318 00:13:57,580 --> 00:14:02,030 Unazingatia hiyo 1% ambayo inawezekana, na fikiria jinsi ya kufanya iwezeikane 319 00:14:02,817 --> 00:14:06,140 Sasa napenda kukupeleka kwenye safari ndani ya akili ya mmeza panga. 320 00:14:06,140 --> 00:14:09,479 Ili kumeza panga, inahitaji akili itafakari jambo, 321 00:14:09,479 --> 00:14:12,270 uzingativu wa hali ya juu, kuonyesha ufasaha ili 322 00:14:12,270 --> 00:14:15,670 kutenganisha viungo vya ndani vya mwili na kushinda vitendo hiari mwilini 323 00:14:15,710 --> 00:14:20,370 kupitia njia ya ubongo iliyoimarishwa, kupitia marido ya kumbukumbu ya misuli 324 00:14:20,450 --> 00:14:23,720 kwa mazoezi ya makusudi zaidi ya mara 10,000. 325 00:14:24,020 --> 00:14:28,090 Sasa ngoja niwasafirishe kidogo ndani ya mwili wa mmeza panga 326 00:14:28,310 --> 00:14:30,130 Ili kumeza panga, 327 00:14:30,130 --> 00:14:32,250 Lazima niteleze panga juu ya ulimi wangu, 328 00:14:32,250 --> 00:14:34,780 nizuie kutaka kutapika kwenye shingo ya umio, 329 00:14:34,780 --> 00:14:37,740 zungusha mgeuko wa nyuzi 90 chini ya gegedu ya ulimi, 330 00:14:38,240 --> 00:14:41,040 pitia kwenye msuli juu ya kilinda umio, 331 00:14:41,060 --> 00:14:42,600 zuia vitendohiari vya tumbo, 332 00:14:42,600 --> 00:14:44,380 telezea makali kwenye shimo la kifua 333 00:14:44,380 --> 00:14:45,960 kati ya mapafu. 334 00:14:46,080 --> 00:14:48,349 Katika hatua hii, 335 00:14:48,399 --> 00:14:50,389 Lazma kweli nisukume moyo wangu pembeni. 336 00:14:50,389 --> 00:14:51,720 Ikiwa utaangalia kwa makini, 337 00:14:51,720 --> 00:14:53,860 unawezaona moyo ukidunda kwa panga langu 338 00:14:53,860 --> 00:14:55,859 kwa sababu linaegemea moyo 339 00:14:55,859 --> 00:14:58,809 ikitenganishwa na karibu thumuni ya inchi ya tishu ya umio. 340 00:14:58,809 --> 00:15:00,580 Hicho sio kitu unaweza kudanganya. 341 00:15:00,580 --> 00:15:02,710 Kisha hutelezesha kupita mfupa wa kifua, 342 00:15:02,710 --> 00:15:05,540 kupita kilinda umio, chini ndani ya tumbo, 343 00:15:05,540 --> 00:15:09,020 zuia vitendohiari ndani ya tumbo njia yote hadi kwenye mbuti. 344 00:15:09,020 --> 00:15:09,750 Rahisi sana. 345 00:15:09,750 --> 00:15:10,930 (Kicheko) 346 00:15:10,930 --> 00:15:12,880 Kama ningetakiwa kwenda zaidi ya hapo, 347 00:15:12,880 --> 00:15:17,720 hadi kufikia mirija yangu ya mayai. mirija ya mayai! (Kidachi) 348 00:15:17,720 --> 00:15:20,980 Wanaume, mnaweza kuwauliza wake zenu kuhusu hiyo baadaye ... 349 00:15:22,160 --> 00:15:23,900 Watu huniuliza, wanasema, 350 00:15:23,900 --> 00:15:26,740 "lazima kuchukua ujasiri mwingi ili kuhatarisha maisha yako, 351 00:15:26,740 --> 00:15:28,800 kusogeza moyo wako, na kumeza panga ... " 352 00:15:28,800 --> 00:15:30,500 Hapana. Kinachofanya ujasiri halisi 353 00:15:30,500 --> 00:15:33,020 ni kwa yule kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 354 00:15:33,080 --> 00:15:35,620 kwa kuhatarisha kushindwa na kukataliwa, 355 00:15:35,620 --> 00:15:37,040 kufungua moyo wake, 356 00:15:37,040 --> 00:15:38,240 na kumeza kiburi chake 357 00:15:38,240 --> 00:15:41,060 na kusimama hapa mbele ya kundi la watu asiowafahamu kabisa 358 00:15:41,060 --> 00:15:43,670 na kukuambia hadithi yake kuhusu hofu na ndoto zake, 359 00:15:43,680 --> 00:15:47,580 kwa hatarisha kumwaga habari zake, vyote kihalisia na kitamathali. 360 00:15:48,280 --> 00:15:49,450 Unaona - asante. 361 00:15:49,450 --> 00:15:53,720 (Makofi) 362 00:15:53,850 --> 00:15:56,250 Unaona, jambo la kustaajabisha sana ni 363 00:15:56,250 --> 00:15:58,650 Nimetaka kufanya mambo ya kusifika maishani mwangu 364 00:15:58,650 --> 00:15:59,780 na sasa nimesifika. 365 00:15:59,780 --> 00:16:02,880 Lakini jambo la kusifika haswa sio kwamba ninaweza kumeza 366 00:16:02,880 --> 00:16:05,170 panga 21 kwa mara moja, 367 00:16:07,640 --> 00:16:10,500 au futi 20 chini ya maji kwenye tanki la papa 88 na taa 368 00:16:10,500 --> 00:16:12,307 kwa kitabu cha Amini au Usiamini, 369 00:16:13,840 --> 00:16:17,600 au kuchowa hadi kuwa mwekundu nyuzi 1500 kwa Watu jasiri wa Stan Lee 370 00:16:17,610 --> 00:16:19,470 kama "Mtu wa Chuma" 371 00:16:19,520 --> 00:16:21,574 na yule jamaa alikuwa moto! 372 00:16:22,460 --> 00:16:24,920 Au kuvuta gari kwa upanga kwa Ripley, 373 00:16:24,930 --> 00:16:26,290 au Guinness, 374 00:16:26,290 --> 00:16:28,760 au kufikia fainali za shindano la vipaji Marekani, 375 00:16:28,820 --> 00:16:31,540 au kushinda 2007 tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu. 376 00:16:31,550 --> 00:16:33,900 La, hilo sio jambo la kusifika sana. 377 00:16:33,900 --> 00:16:36,350 Hivyo ndio watu wanafikiria. La, la, la. Sio hivyo. 378 00:16:36,350 --> 00:16:37,800 Jambo la kusifika sana 379 00:16:37,800 --> 00:16:40,660 ni Mungu angemchukua kijana, mwoga, mwenye aibu mwembamba 380 00:16:40,660 --> 00:16:42,200 aliyehofia vimo virefu, 381 00:16:42,200 --> 00:16:43,890 aliyehofia ya maji na papa, 382 00:16:43,890 --> 00:16:46,370 na madaktari na manesi na sindano na vyenye ncha kali 383 00:16:46,370 --> 00:16:47,640 na kuzungumza na watu 384 00:16:47,640 --> 00:16:49,800 na sasa ananifanya nipae duniani kote 385 00:16:49,800 --> 00:16:51,320 katika kina cha futi 30,000 386 00:16:51,320 --> 00:16:53,900 kumeza vitu vya ncha chini ya maji ya tanki ya papa, 387 00:16:53,900 --> 00:16:57,430 na kuzungumza na madaktari na wauguzi na hadhira kama ninyi duniani 388 00:16:57,430 --> 00:16:59,580 Hilo ni jambo la kustaajabu sana kwangu. 389 00:16:59,580 --> 00:17:01,450 Nimetaka kufanya mambo yasiyowezekana - 390 00:17:01,450 --> 00:17:02,380 Asante. 391 00:17:02,380 --> 00:17:03,760 (Makofi) 392 00:17:03,760 --> 00:17:05,220 Asante. 393 00:17:05,660 --> 00:17:09,040 (Makofi) 394 00:17:09,700 --> 00:17:12,569 Sikuzote nilitaka kufanya yasiyowezekana, na sasa nimeweza. 395 00:17:12,569 --> 00:17:15,858 Nilitaka kufanya kitu cha kusifika maishani na kubadilisha ulimwengu, 396 00:17:15,858 --> 00:17:16,899 na sasa nimeweza. 397 00:17:16,899 --> 00:17:19,819 Siku zote nilitaka kupaa duniani kote kufanya vitendo vigumu 398 00:17:19,819 --> 00:17:21,379 na kuokoa maisha, sasa nimeweza. 399 00:17:21,379 --> 00:17:22,720 Na unajua nini? 400 00:17:22,720 --> 00:17:25,569 Bado kuna sehemu ndogo ya ndoto kubwa ya yule mtoto mdogo 401 00:17:25,569 --> 00:17:27,291 ndani kabisa. 402 00:17:30,320 --> 00:17:36,197 (Kicheko) (Makofi) 403 00:17:37,000 --> 00:17:40,240 Na unajua, sikuzote nilitaka kupata kusudi langu na wito wangu, 404 00:17:40,270 --> 00:17:41,530 na sasa nimepata. 405 00:17:41,540 --> 00:17:42,920 Lakini nadhani nini? 406 00:17:42,920 --> 00:17:46,230 Si kwa panga, sio unavyofikiria, si kwa nguvu zangu. 407 00:17:46,230 --> 00:17:48,510 Ni kwa udhaifu wangu, maneno yangu. 408 00:17:48,510 --> 00:17:51,090 Kusudi langu na wito ni kubadili ulimwengu 409 00:17:51,090 --> 00:17:52,390 kwa kukata kupitia hofu, 410 00:17:52,390 --> 00:17:54,910 upanga mmoja kwa wakati, neno moja kwa wakati, 411 00:17:55,070 --> 00:17:57,450 kisu moja kwa wakati, maisha kwa wakati, 412 00:17:57,540 --> 00:17:59,700 kuhamasisha watu kuwa mashujaa 413 00:17:59,700 --> 00:18:01,860 na kufanya yasiyowezekana maishani mwao. 414 00:18:02,060 --> 00:18:04,680 Kusudi langu ni kusaidia wengine kupata yao. 415 00:18:04,680 --> 00:18:05,680 La kwako ni lipi? 416 00:18:05,680 --> 00:18:06,960 Nini kusudi lako? 417 00:18:06,960 --> 00:18:08,960 Uliwekwa kufanya nini hapa? 418 00:18:09,260 --> 00:18:11,590 Naamini sisi wote tumeitwa kuwa mashujaa. 419 00:18:12,160 --> 00:18:14,260 Nguvu yako kubwa ni nini? 420 00:18:14,560 --> 00:18:17,990 Kati ya idadi ya watu duniani ya watu zaidi ya bilioni 7, 421 00:18:17,990 --> 00:18:20,250 kuna wameza upanga wachache sana 422 00:18:20,250 --> 00:18:21,661 waliobakia duniani kote leo, 423 00:18:21,661 --> 00:18:22,940 lakini kuna wewe mmoja. 424 00:18:22,940 --> 00:18:24,070 Wewe ni wa pekee. 425 00:18:24,070 --> 00:18:25,540 Hadithi yako ni nini? 426 00:18:25,540 --> 00:18:27,760 Nini kinakufanya uwe tofauti? 427 00:18:27,760 --> 00:18:29,180 Simulia hadithi yako, 428 00:18:29,180 --> 00:18:31,721 hata kama sauti yako ni nyembamba na inatetemeka. 429 00:18:31,900 --> 00:18:33,340 Je, thromu zako ni nini? 430 00:18:33,340 --> 00:18:35,850 kama ungefanya chochote, kuwa yeyote, kwenda popote - 431 00:18:35,850 --> 00:18:37,430 Ungefanya nini? Ungekwenda wapi? 432 00:18:37,430 --> 00:18:38,480 Ungefanya nini? 433 00:18:38,480 --> 00:18:40,340 Unataka kufanya nini na maisha yako? 434 00:18:40,340 --> 00:18:41,760 Nini ndoto zako kubwa? 435 00:18:41,760 --> 00:18:44,450 Nini ndoto zako kubwa ulipokuwa mdogo? Fikiria tena 436 00:18:44,450 --> 00:18:46,240 Nina uhakika hii haikuwa hivyo, si ndiyo? 437 00:18:46,483 --> 00:18:47,880 Nini zilikuwa ndoto zako kuu 438 00:18:47,880 --> 00:18:50,450 ulizofikiri zilikuwa ajabu sana na zisizoeleweka? 439 00:18:50,450 --> 00:18:54,040 Hakika hii inafanya ndoto zako zisionekane za ajabu tena, sivyo? 440 00:18:55,370 --> 00:18:57,050 Upanga wako ni nini? 441 00:18:57,050 --> 00:18:58,650 Kila mmoja wenu ana upanga, 442 00:18:58,650 --> 00:19:00,600 upanga wa pande mbili wa hofu na ndoto. 443 00:19:00,600 --> 00:19:03,520 Meza upanga wako, chochote utachokuwa. 444 00:19:03,890 --> 00:19:05,870 Fuata ndoto zako, mabibi na mabwana, 445 00:19:05,870 --> 00:19:08,900 Hujachelewa sana kuwa chochote unataka kuwa. 446 00:19:09,720 --> 00:19:12,920 Kwa wale waonevu na mipira ya kukwepa, wale watoto waliodhani 447 00:19:12,920 --> 00:19:14,916 kuwa sitaweza kufanya yasiyowezekana, 448 00:19:15,060 --> 00:19:17,645 Nina kitu kimoja tu cha kuwaambia: 449 00:19:17,645 --> 00:19:18,841 Asanteni. 450 00:19:18,940 --> 00:19:22,220 Kwa sababu kama si kwa wahalifu, tusingekuwa kuwa na mashujaa. 451 00:19:23,020 --> 00:19:27,237 Nipo hapa kuthibitisha yasiyowezekana si hayawezekani. 452 00:19:28,300 --> 00:19:32,310 Hii ni hatari sana, Inaweza kuniua. 453 00:19:32,340 --> 00:19:33,720 Natumaini mtafurahia. 454 00:19:33,720 --> 00:19:35,260 (Kicheko) 455 00:19:36,350 --> 00:19:38,700 Nitahitaji msaada wenu kwenye hili. 456 00:19:46,731 --> 00:19:48,405 Hadhira:Mbili, tatu. 457 00:19:48,405 --> 00:19:52,100 Dan Meyer:La, la, la. Nahitaji msaada wenu kwenye kuhesabu, nyote, sawa? 458 00:19:52,100 --> 00:19:53,210 (Vicheko) 459 00:19:53,210 --> 00:19:55,840 Kama unajua maneno? Sawa? Hesabu na mimi. Tayari? 460 00:19:55,870 --> 00:19:56,964 Moja. 461 00:19:56,964 --> 00:19:58,150 Mbili. 462 00:19:58,170 --> 00:19:58,980 Tatu. 463 00:19:58,980 --> 00:20:00,920 La, hiyo ni 2, lakini mmeelewa 464 00:20:06,760 --> 00:20:07,780 Hadhira: Moja. 465 00:20:07,840 --> 00:20:08,750 Mbili. 466 00:20:08,800 --> 00:20:10,010 Tatu. 467 00:20:11,260 --> 00:20:13,280 (Vuta pumzi) 468 00:20:14,360 --> 00:20:15,940 (Makofi) 469 00:20:16,251 --> 00:20:17,450 DM: Ndiyo! 470 00:20:17,450 --> 00:20:23,100 (Makofi) (Kushangilia) 471 00:20:23,100 --> 00:20:24,820 Asanteni sana. 472 00:20:25,450 --> 00:20:28,800 Asante, asante, asante. Asante kutoka kina cha moyo wangu 473 00:20:28,800 --> 00:20:31,290 Kweli, asante kutoka chini ya tumbo langu. 474 00:20:31,880 --> 00:20:35,020 Niliwaambia nimekuja hapa kufanya yasiyowezekana, na sasa nimeweza. 475 00:20:35,030 --> 00:20:37,730 Ila hii haikuwa isiyowezekana. Ninafanya hivi kila siku. 476 00:20:37,800 --> 00:20:42,800 Kitu kisichowezekana ilikuwa yule mwoga, mwenye aibu mwembamba kukabili hofu zake 477 00:20:42,840 --> 00:20:44,600 kusimama hapa kwenye jukwaa la [TEDx], 478 00:20:44,600 --> 00:20:47,100 na kubadilisha dunia, neno moja kwa wakati, 479 00:20:47,100 --> 00:20:49,080 upanga kwa wakati, maisha kwa wakati. 480 00:20:49,080 --> 00:20:52,060 kama nimekufanya ufikiri kwa njia mpya, kama nimekufanya uamini 481 00:20:52,060 --> 00:20:54,460 yasiyowekana si hayawezekani, 482 00:20:54,460 --> 00:20:57,960 ikiwa nimekufanya uelewe kuwa waweza fanya yasiyowezekana maishani mwako, 483 00:20:58,120 --> 00:21:01,020 basi kazi yangu imekwisha, na yako ndiyo kwanza imeanza. 484 00:21:01,020 --> 00:21:04,100 Usiache kuwa na ndoto. Usiache kuamini. 485 00:21:04,820 --> 00:21:06,350 Asanteni kwa kuniamini 486 00:21:06,350 --> 00:21:08,250 na asanteni kuwa sehemu ya ndoto yangu. 487 00:21:08,250 --> 00:21:09,550 Hii ni zawadi kwenu: 488 00:21:09,550 --> 00:21:11,486 Yasiyowezekana si ... 489 00:21:11,486 --> 00:21:12,920 Hadhira: Hayawezekani. 490 00:21:12,920 --> 00:21:14,920 Mwendo mrefu ni sehemu ya zawadi. 491 00:21:15,100 --> 00:21:19,560 (Makofi) 492 00:21:19,560 --> 00:21:21,020 Asanteni. 493 00:21:21,060 --> 00:21:25,360 (Makofi) 494 00:21:25,580 --> 00:21:27,560 (Kushangilia) 495 00:21:27,750 --> 00:21:30,570 Mwenyeji: Asante, Dan Meyer, wow!