Asante
Palikuwa na mfalme nchini India, Maharaja
na siku yake ya kuzaliwa ilitolewa amri
kwamba machifu wote walete
zawadi kwa mfalme.
Wengine wakaleta hariri bora,
wengine wakaleta panga maridadi,
wengine dhahabu
mwisho wa mstari alikuja akitembea
mzee mdogo mwenye makunyanzi
ambaye alitembea kutoka kijijini kwake
kwa safari ya siku nyingi kando ya bahari.
alipokuwa akisogea mwana mfalme akauliza,
'Umemletea zawadi gani Mfalme?'
Na mzee yule taratibu sana
akakunjua mkono wake kuonyesha
kombe la baharini zuri sana, lenye makoa
ya zambarau na njano,nyekundu na bluu.
Na mwana Mfalme akasema,
"Hiyo si zawadi kwa Mfalme!
Ni zawadi gani hiyo?"
Mzee yule akamwangalia taratibu
na kusema
"Kutembea mwendo mrefu.. ni sehemu
ya zawadi"
(Kicheko)
Baada ya muda mfupi,
Nitawapa zawadi,
zawadi niaminiyo
ni zawadi inayostahili kuenezwa.
Ila kabla ya hayo, ngoja niwachukue
kwenye mwendo wangu mrefu.
Kama wengi wenu,
Nilianza maisha kama mtoto mdogo.
Wangapi kati yenu
mlianza maisha kama mtoto ?
Aliyezaliwa mchanga?
Karibia nusu yenu.. Sawa
(Kicheko)
Na mliobakia, vipi?
Mlizaliwa mkiwa watu wazima?
Ama kweli, nataka kukutana na mama zenu!
Ongelea yasiyowezekana!
Nikiwa mtoto mdogo, siku zote nilipendezwa
kufanya mambo yasiyowezekana
Leo ni siku ambayo nimekuwa nikiitarajia
kwa miaka mingi,
kwa sababu leo ni siku ambayo
nitajaribu
kufanya yasiyowezekana
mbele ya macho yenu
Hapahapa TEDxMaastrich
Nitaanza
Kwa kuonyesha mwisho wake:
Na nitawathibitishia kwamba
yasiyowezekana siyo hayawezekani
Na nitamalizia kwa kuwapa
zawadi yenye kustahili kuieneza:
Nitawaonyesha kwamba unaweza
kufanya yasiyowezekana maishani mwako.
katika kutafuta kufanya yasiyowezekana,
nimegundua kuna
mambo mawili yanayofanana
kati ya watu duniani.
Kila mtu ana hofu,
na kila mtu ana ndoto.
Katika kutafuta kufanya yasiyowezekana
nimegundua kuna vitu vitatu
ambavyo nimevifanya miaka mingi ambavyo
vimenisababishia kufanya yasiyowezekana:
Mchezo wa mpira wa kuchenga au "Trefball"
Superman,
na Mbu
Hayo ni maneno yangu matatu makuu.
Mmeshajua kwanini nafanya
yasiyowezekana maishani mwangu
Hivyo nitawachukua katika safari
yangu, ya mwendo mrefu
kutoka kwenye hofu hadi ndoto
kutoka kwenye maneno hadi panga,
Kutoka Mpira wa kuchenga
hadi Superman
hadi kwa Mbu
Na ninatumaini kuwaonyesha
unawezaje kufanya yasiyo
wezekana maishani mwako
Oktoba 4, mwaka 2007.
Moyo wangu ulienda mbio,
magoti yangu yalitetema
nilipokuwa napanda jukwaani
kwenye ukumbi wa Sanders
Chuo cha Harvard kupokea
Tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu
kwa kushiriki kuandika ikisiri
ya utafiti wa kitabibu
ulioitwa "Kumeza Upanga...
...na Athari zake"
(Kicheko)
Ilichapishwa kwenye jarida dogo
ambalo sikuwahi kulisoma kabla,
Jarida la Kitabibu la Uingereza.
Na kwangu, hiyo ilikuwa ndoto
isiyowezekana kuwa kweli,
ilikuwa ni mshangao usiotegemewa
kwa mtu kama mimi,
ilikuwa ni heshima ambayo sitaweza kusahau
Lakini haikuwa sehemu ya kubwa ya
kukumbuka maishani mwangu.
Mnamo Oktoba 4, mwaka 1967
kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba
aliteseka na hofu kubwa kupita kiasi.
Alipojiandaa kupanda jukwaani,
moyo wake ulienda mbio,
magoti yake yalikuwa yakitetemeka.
Alikwenda kufungua kinywa chake kuongea,
maneno hayakuweza kutoka.
Alisimama akitetemeka na kutoa machozi.
Alipooza kwa mshtuko wa ghafla,
alipatwa fadhaa kwa hofu.
huyu kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba
alitesekana na hofu kubwa kupita kiasi.
Alikuwa na hofu ya giza,
hofu ya vimo virefu,
hofu ya buibui na nyoka ...
Kuna yeyote anayeogopa buibui na nyoka?
Naam, wachache wenu ...
Alikuwa na hofu ya maji na papa ...
Hofu ya madaktari na manesi na madaktari
wa meno,
na sindano na kutobolewa na vitu vya
ncha kali.
Lakini zaidi ya chochote,
alikuwa na hofu ya
watu
Huyo kijana mwoga,mwenye aibu na mwembamba
alikuwa mimi.
Nilikuwa na hofu ya kushindwa na
kukataliwa,
kutojithamini, kujiona duni,
na kitu ambacho hata hatukujua
unaweza kujiandikisha kwa siku hizo:
ugonjwa wa hofu ya ukaribu na watu.
Kwa sababu nilikuwa na hofu, waonevu
walinitania na kunipiga.
Walinicheka na kuniita majina,
Hawakuniruhusu kucheza nao
michezo ya aina yoyote.
Ah, kulikuwa na mchezo mmoja
walikuwa wakiruhusu kucheza kwenye ...
Mpira wa kuchenga -
na sikuwa mchengaji nzuri.
Waonevu waliita jina langu,
na nilipoangalia
niliona mipira myekundu ya kukwepa
ikivurumishwa usoni wangu kwa kasi kubwa
bam, bam, bam!
Ninakumbuka siku nyingi
nikirudi nyumbani kutoka shule,
uso wangu ulikuwa mwekundu ukichonyota,
masikio yangu yalikuwa mekundu yakivuma.
Macho yangu yalichoma kwa machozi,
na maneno yao yalichoma masikioni mwangu.
Na yeyote aliyesema,
"Fimbo na mawe vyaweza kunivunja mifupa,
bali maneno hayatoniumiza kamwe "...
Ni uongo.
Maneno huweza kukata kama kisu.
Maneno huweza kupenya kama upanga.
Maneno huwezafanya majeraha yenye kina
yasiweze kuonekana.
Hivyo nilikuwa na hofu.
Na maneno yalikuwa adui yangu mkubwa.
Bado ni adui yangu.
Lakini pia nilikuwa na ndoto.
Nilienda nyumbani
na kutorokea kwenye futuhi za Superman
na nilisoma futuhi za Superman
na niliota kutaka kuwa shujaa mkubwa
kama Superman.
Nilitaka kupigania kweli na haki,
Nilitaka kupambana dhidi ya
wahalifu na mahasimu,
Nilitaka kupaa duniani kote
kufanya vitendo vya ujasiri kuokoa maisha.
Nilikuwa pia navutiwa mno
na vitu vilivyokuwa kweli.
Nilisoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness
na kitabu cha Ripley kiitwacho Amini au Usiamini.
Yeyote kati yenu amewahi kusoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness au kitabu cha Ripley?
Navipenda vitabu hivi!
Niliona watu wafanyao ujasiri halisia.
Nikasema, Nataka kufanya hivyo.
Ikiwa waonevu hawataniruhusu
kucheza katika michezo yao yoyote,
Nataka kufanya maajabu, ujasiri halisi.
Nataka kufanya kitu cha kusifika
ambacho hao waonevu hawawezi kufanya.
Nataka kupata kusudi langu na wito wangu,
Nataka kujua kuwa maisha yangu yana maana,
Nataka kufanya kitu cha kushangaza
kubadili ulimwengu;
Ninataka kuthibitisha
yasiyowezekana sio hayawezekani.
Kupeleka mbele miaka 10 -
Ilikuwa wiki kabla ya kutimiza miaka 21.
Mambo mawili yalitokea kwa siku moja
ambayo yangebadilisha maisha yangu milele.
Nilikuwa nikiishi Tamil Nadu, India Kusini
Nilikuwa mmishonari huko,
na mshauri wangu, rafiki yangu aliniuliza,
"Je, una Thromu, Daniel?"
Na nikasema, "Thromu?
Thromu ni nini? "
Alisema, "Thromu ni malengo makuu ya
maisha.
Ni muunganiko
wa ndoto na malengo, kama ungeweza
kufanya chochote unachotaka,
kwenda popote unapotaka
kuwa mtu yeyote unayetaka,
ungekwenda wapi?
Ungefanya nini?
Ungekuwa nani?
Nikasema, "Siwezi kufanya hivyo!
Naogopa sana! Naogopa mengi mno! "
Usiku huo nilichukua mkeka wangu wa mchele
juu ya paa la ghorofa,
nikautandika chini ya nyota,
na kuangalia popo wakiwashambulia mbu.
Na yote niliyofikiria ilikuwa thromu,
na ndoto na malengo,
na wale washujaaji wenye mipira ya kuchenga.
Masaa machache baadaye niliamka.
Moyo wangu ulienda mbio,
magoti yangu yakitetemeka.
Safari hii haikuwa na hofu.
Mwili wangu wote ulitikisika.
Na kwa siku tano zilizofuata
Nilipoteza na kurudisha fahamu,
kitandani nikipigania maisha yangu.
Ubongo wangu ulikuwa unawaka
na homa ya malaria yenye jotoridi la 105.
Na kila fahamu ziliponirudia,
nilichowaza ilikuwa kuhusu thromu.
Niliwaza
"Nataka kufanya nini na maisha yangu?"
Hatimaye, usiku kabla
sijafikisha miaka 21,
katika wakati wa kuelewa,
Nilikuja kutambua:
Nilitambua kwamba yule mbu mdogo,
Anofelesi Stefensi,
yule mbu mdogo
aliye na uzito chini ya mikrogramu 5
chini ya punje ya chumvi,
anaweza kuangusha
mtu wa ratili 170, mtu wa kilo 80,
Niligundua kwamba alikuwa hasimu wangu.
Kisha nikagundua,
hapana, hapana, sio mbu,
Ni vimelea vidogo
ndani ya mbu,
Plasmodium Falciparum,
ambao huua zaidi ya watu milioni kwa mwaka
Kisha nikagundua
Hapana, hapana, tena ni ndogo zaidi,
lakini kwangu, ilionekana kubwa zaidi.
Niligundua,
hofu ilikuwa hasimu yangu,
vimelea yangu,
vilivyonitia ulemavu
na kunipooza mimi maisha yangu yote.
Unajua, kuna tofauti
kati ya hatari na hofu.
Hatari ni halisi.
Hofu ni hiari.
Na nikagundua kuwa nina hiari:
Aidha niishi kwa hofu,
na kufa katika kushindwa usiku ule,
au ningeweza kuua hofu yangu,
na ningeweza
kufikia ndoto zangu,
Ningeweza kuthubutu kuishi maisha.
Na unajua, kuna kitu kuhusu
kuwa kwenye kitanda cha mauti
na kukabiliwa na kifo ambacho haswa
kinakufanya utake kweli kuishi maisha.
Nikagundua kuwa kila mtu hufa,
si kila mtu huishi.
Ni katika kufa ndio sisi tunaishi.
Unajua, wakati unapojifunza kufa,
unajifunza kweli kuishi.
Kwa hiyo nikaamua nitaenda kubadilisha
hadithi yangu usiku huo.
Sikutaka kufa.
Hivyo nikafanya sala ndogo, nikasema,
"Mungu, ukiniruhusu niishi
nifikishe miaka 21,
Sitaruhusu hofu
itawale maisha yangu tena.
Nitaziweka hofu zangu kifoni,
Nitaenda kuzifikia ndoto zangu,
Ninataka kubadilisha mtazamo wangu,
Nataka kufanya kitu cha ajabu
na maisha yangu,
Nataka kupata kusudi langu na wito wangu,
Ninataka kujua kuwa yasiyowezekana
si hayawezekani. "
Sitawaambia kama nilinusurika usiku ule;
Nitawaacha mfikirie.
(Kicheko)
Lakini usiku huo niliandika orodha
ya Thromu zangu 10 za kwanza:
Niliamua nilitaka
kutembelea mabara makubwa
kutembelea Maajabu 7 ya Dunia
kujifunza lugha nyingi,
kuishi kwenye kisiwa kitupu,
kuishi kwenye meli baharini,
kuishi na kabila la Wahindi
katika Amazon,
kupanda hadi juu
ya mlima mrefu kuliko yote Sweden,
Nilitaka kuona mawio Mlima Everest,
kufanya kazi na biashara ya muziki
Nashville,
Nilitaka kufanya kazi ya sarakasi,
na nilitaka kuruka nje ya ndege.
Zaidi ya miaka ishirini iliyofuata,
Nilitimiza thromu hizo kwa wingi.
Kila wakati niliondoa
thromu kwenye orodha yangu,
Niliongeza 5 au 10 zaidi kwenye orodha
na orodha yangu iliendelea kukua.
Kwa miaka saba iliyofuata, niliishi
kwenye kisiwa kidogo katika Bahamas
kwa karibu miaka saba
katika kibanda cha makuti,
nikiwinda papa na taa wa kula,
nikiwa mtu pekee kwenye kisiwa,
nikiwa nimevaa msuli,
na nikajifunza kuogelea na papa.
Na kutoka huko, nikahamia Mexico,
na kisha nikasafiri
kwa bonde la Mto Amazon nchini Ecuador,
Pujo Pongo Ecuador,
niliishi na kabila moja huko,
na kidogo kidogo nilianza kuongeza
kujiamini kwa thromu zangu tu.
Nilihamia biashara ya muziki Nashville,
kisha Sweden,
nikahamia Stockholm,
kufanyakazi katika biashara ya muziki,
ambapo nilipanda kilele cha Ml. Kebnekaise
juu ya mzunguko wa Arctic.
Nilijifunza udamisi,
na viinimacho,
na kutembea kama ngongoti,
kuendesha baiskeli kwa tairi moja,
kula moto, kula kioo.
Mwaka 1997 nilisikia kuna
wameza panga wasiozidi kumi na mbili
na nikasema, "Inabidi kufanya hivyo!"
Nilikutana na mmeza panga,
na nikamwomba vidokezo.
Akasema, "Naam, nitakupa vidokezo 2:
Namba 1: Ni hatari sana,
Watu wamekufa wakifanya hivi.
Namba 2:
Usijaribu! "
(Kicheko)
Basi nikaiongeza kwenye orodha ya thromu.
Na nikafanya mazoezi
mara 10 hadi 12 kwa siku, kila siku
kwa miaka minne.
Sasa nilipigia hesabu hizo...
4 x 365 [x 12]
Ilikuwa karibu 13,000
majaribio yasiyofanikiwa
kabla sijatia panga langu wa kwanza
chini koo mwaka 2001.
Wakati huo nikaweka thromu
kuwa mtaalamu wa ulimwengu
kwa kumeza panga.
Basi nilitafuta kila kitabu,
gazeti, makala ya gazeti,
kila ripoti ya kitabibu,
Nilijifunza fiziolojia, anatomia,
Niliongea na madaktari na manesi,
niliwakutanisha wameza panga wote
pamoja
kwenye Shirikisho la Wameza Panga
Kimataifa,
nikafanya ikisiri miaka 2
ya utafiti kitabibu
kuhusu Umezaji wa Panga na athari zake
iliyochapishwa
katika Jarida la Kitabibu Uingereza.
(Kicheko)
Asanteni.
(Makofi)
Na nilijifunza mambo ya kuvutia sana
kuhusu umezaji wa panga.
Vitu vingine ambavyo haujawahi kufikiria
kabla, hutasahau baada ya usiku huu.
Wakati utakapoenda nyumbani, na unakata
steki yako na kisu chako
au panga, au "bestek" zako,
utafikiri juu ya hili ...
Nilijifunza kwamba umezaji panga
ulianzia India -
mahali nilipona kwa mara ya kwanza
nikiwa kijana wa miaka 20 -
karibu miaka 4000 ya kale, karibu 2000 BC.
Zaidi ya miaka 150 iliyopita,
wameza panga walitumika
katika medani za sayansi na kitabibu
ili kusaidia kuunda
endoskopia imara mwaka 1868
wakiwa na Dk. Adolf Kussmaul wa Freiburg, Ujerumani
Mnamo 1906, elektrokadiogramu huko Wales,
kujifunza matatizo ya kumeza,
na mmeng'enyo wa chakula,
aina ya bronkoskopia, .
Lakini zaidi ya miaka 150 iliyopita,
tunajua mamia ya madhara
na vifo kadhaa ...
Hii ni endoskopia imara
iliyoanzishwa na Dk. Adolph Kussmaul.
Lakini tuligundua kuwa kulikuwa na
Vifo 29 zaidi ya miaka 150 iliyopita.
pamoja na mmezaji panga huko London
aliyetoboa moyo wake kwa panga
Tulijifunza pia kuwa kuna kesi tatu hadi nane za
madhara mkubwa ya umezaji panga
kila mwaka.
Najua kwa sababu mimi hupata simu.
Nilikuwa na wawili,
mmoja kutoka Sweden, na kutoka Orlando
wiki chache zilizopita,
wamezaji panga waliopo hospitalini
kutokana na madhara.
Kwa hiyo ni hatari sana.
Jambo jingine nililojifunza ni kuwa
kumeza panga huchukua
miaka 2 hadi miaka 10
kujifunza jinsi ya kumeza panga
kwa watu wengi.
Lakini ugunduzi unaovutia sana
Nilijifunza ilikuwa
jinsi wameza panga wanavyojifunza
kufanya yasiyowezekana.
Nami nitawapa siri ndogo:
Usizingatie kwenye asilimia 99.9
kuwa haiwezekani.
Unazingatia hiyo 1% ambayo inawezekana,
na fikiria jinsi ya kufanya iwezeikane
Sasa napenda kukupeleka kwenye safari
ndani ya akili ya mmeza panga.
Ili kumeza panga,
inahitaji akili itafakari jambo,
uzingativu wa hali ya juu,
kuonyesha ufasaha ili
kutenganisha viungo vya ndani vya mwili
na kushinda vitendo hiari mwilini
kupitia njia ya ubongo iliyoimarishwa,
kupitia marido ya kumbukumbu ya misuli
kwa mazoezi ya makusudi
zaidi ya mara 10,000.
Sasa ngoja niwasafirishe kidogo
ndani ya mwili wa mmeza panga
Ili kumeza panga,
Lazima niteleze panga juu ya ulimi wangu,
nizuie kutaka kutapika
kwenye shingo ya umio,
zungusha mgeuko wa nyuzi 90
chini ya gegedu ya ulimi,
pitia kwenye msuli juu ya kilinda umio,
zuia vitendohiari vya tumbo,
telezea makali kwenye shimo la kifua
kati ya mapafu.
Katika hatua hii,
Lazma kweli nisukume moyo wangu pembeni.
Ikiwa utaangalia kwa makini,
unawezaona moyo ukidunda kwa panga langu
kwa sababu linaegemea moyo
ikitenganishwa na karibu thumuni ya inchi
ya tishu ya umio.
Hicho sio kitu unaweza kudanganya.
Kisha hutelezesha
kupita mfupa wa kifua,
kupita kilinda umio,
chini ndani ya tumbo,
zuia vitendohiari ndani ya tumbo
njia yote hadi kwenye mbuti.
Rahisi sana.
(Kicheko)
Kama ningetakiwa kwenda zaidi ya hapo,
hadi kufikia mirija yangu ya mayai.
mirija ya mayai! (Kidachi)
Wanaume, mnaweza kuwauliza wake zenu
kuhusu hiyo baadaye ...
Watu huniuliza, wanasema,
"lazima kuchukua ujasiri mwingi
ili kuhatarisha maisha yako,
kusogeza moyo wako,
na kumeza panga ... "
Hapana. Kinachofanya ujasiri halisi
ni kwa yule kijana mwoga, mwenye aibu,
mwembamba
kwa kuhatarisha kushindwa na kukataliwa,
kufungua moyo wake,
na kumeza kiburi chake
na kusimama hapa mbele
ya kundi la watu asiowafahamu kabisa
na kukuambia hadithi yake
kuhusu hofu na ndoto zake,
kwa hatarisha kumwaga habari zake,
vyote kihalisia na kitamathali.
Unaona - asante.
(Makofi)
Unaona, jambo la kustaajabisha sana ni
Nimetaka kufanya mambo
ya kusifika maishani mwangu
na sasa nimesifika.
Lakini jambo la kusifika haswa
sio kwamba ninaweza kumeza
panga 21 kwa mara moja,
au futi 20 chini ya maji kwenye tanki
la papa 88 na taa
kwa kitabu cha Amini au Usiamini,
au kuchowa hadi kuwa mwekundu nyuzi 1500
kwa Watu jasiri wa Stan Lee
kama "Mtu wa Chuma"
na yule jamaa alikuwa moto!
Au kuvuta gari kwa upanga kwa Ripley,
au Guinness,
au kufikia fainali za
shindano la vipaji Marekani,
au kushinda 2007
tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu.
La, hilo sio
jambo la kusifika sana.
Hivyo ndio watu wanafikiria.
La, la, la. Sio hivyo.
Jambo la kusifika sana
ni Mungu angemchukua kijana,
mwoga, mwenye aibu mwembamba
aliyehofia vimo virefu,
aliyehofia ya maji na papa,
na madaktari na manesi
na sindano na vyenye ncha kali
na kuzungumza na watu
na sasa ananifanya
nipae duniani kote
katika kina cha futi 30,000
kumeza vitu vya ncha
chini ya maji ya tanki ya papa,
na kuzungumza na madaktari na wauguzi
na hadhira kama ninyi duniani
Hilo ni jambo la kustaajabu sana kwangu.
Nimetaka kufanya mambo yasiyowezekana -
Asante.
(Makofi)
Asante.
(Makofi)
Sikuzote nilitaka kufanya yasiyowezekana,
na sasa nimeweza.
Nilitaka kufanya kitu cha kusifika
maishani na kubadilisha ulimwengu,
na sasa nimeweza.
Siku zote nilitaka kupaa duniani kote
kufanya vitendo vigumu
na kuokoa maisha, sasa nimeweza.
Na unajua nini?
Bado kuna sehemu ndogo
ya ndoto kubwa ya yule mtoto mdogo
ndani kabisa.
(Kicheko) (Makofi)
Na unajua, sikuzote nilitaka kupata
kusudi langu na wito wangu,
na sasa nimepata.
Lakini nadhani nini?
Si kwa panga,
sio unavyofikiria, si kwa nguvu zangu.
Ni kwa udhaifu wangu, maneno yangu.
Kusudi langu na wito
ni kubadili ulimwengu
kwa kukata kupitia hofu,
upanga mmoja kwa wakati, neno moja
kwa wakati,
kisu moja kwa wakati, maisha kwa wakati,
kuhamasisha watu kuwa mashujaa
na kufanya yasiyowezekana maishani mwao.
Kusudi langu ni kusaidia wengine
kupata yao.
La kwako ni lipi?
Nini kusudi lako?
Uliwekwa kufanya nini hapa?
Naamini sisi wote
tumeitwa kuwa mashujaa.
Nguvu yako kubwa ni nini?
Kati ya idadi ya watu duniani
ya watu zaidi ya bilioni 7,
kuna wameza upanga
wachache sana
waliobakia duniani kote leo,
lakini kuna wewe mmoja.
Wewe ni wa pekee.
Hadithi yako ni nini?
Nini kinakufanya uwe tofauti?
Simulia hadithi yako,
hata kama sauti yako ni nyembamba
na inatetemeka.
Je, thromu zako ni nini?
kama ungefanya chochote,
kuwa yeyote, kwenda popote -
Ungefanya nini?
Ungekwenda wapi?
Ungefanya nini?
Unataka kufanya nini na maisha yako?
Nini ndoto zako kubwa?
Nini ndoto zako kubwa ulipokuwa mdogo?
Fikiria tena
Nina uhakika hii haikuwa hivyo, si ndiyo?
Nini zilikuwa ndoto zako
kuu
ulizofikiri zilikuwa ajabu sana
na zisizoeleweka?
Hakika hii inafanya ndoto zako zisionekane
za ajabu tena, sivyo?
Upanga wako ni nini?
Kila mmoja wenu ana upanga,
upanga wa pande mbili wa hofu na ndoto.
Meza upanga wako, chochote utachokuwa.
Fuata ndoto zako, mabibi na mabwana,
Hujachelewa sana kuwa
chochote unataka kuwa.
Kwa wale waonevu na mipira ya kukwepa,
wale watoto waliodhani
kuwa sitaweza kufanya yasiyowezekana,
Nina kitu kimoja tu cha kuwaambia:
Asanteni.
Kwa sababu kama si kwa wahalifu,
tusingekuwa kuwa na mashujaa.
Nipo hapa kuthibitisha
yasiyowezekana si hayawezekani.
Hii ni hatari sana,
Inaweza kuniua.
Natumaini mtafurahia.
(Kicheko)
Nitahitaji msaada wenu kwenye hili.
Hadhira:Mbili, tatu.
Dan Meyer:La, la, la. Nahitaji msaada wenu
kwenye kuhesabu, nyote, sawa?
(Vicheko)
Kama unajua maneno? Sawa?
Hesabu na mimi. Tayari?
Moja.
Mbili.
Tatu.
La, hiyo ni 2, lakini mmeelewa
Hadhira: Moja.
Mbili.
Tatu.
(Vuta pumzi)
(Makofi)
DM: Ndiyo!
(Makofi) (Kushangilia)
Asanteni sana.
Asante, asante, asante.
Asante kutoka kina cha moyo wangu
Kweli, asante
kutoka chini ya tumbo langu.
Niliwaambia nimekuja hapa kufanya
yasiyowezekana, na sasa nimeweza.
Ila hii haikuwa isiyowezekana.
Ninafanya hivi kila siku.
Kitu kisichowezekana ilikuwa yule mwoga,
mwenye aibu mwembamba kukabili hofu zake
kusimama hapa kwenye jukwaa la [TEDx],
na kubadilisha dunia,
neno moja kwa wakati,
upanga kwa wakati, maisha kwa wakati.
kama nimekufanya ufikiri kwa njia mpya,
kama nimekufanya uamini
yasiyowekana si hayawezekani,
ikiwa nimekufanya uelewe kuwa waweza
fanya yasiyowezekana maishani mwako,
basi kazi yangu imekwisha,
na yako ndiyo kwanza imeanza.
Usiache kuwa na ndoto. Usiache kuamini.
Asanteni kwa kuniamini
na asanteni kuwa sehemu
ya ndoto yangu.
Hii ni zawadi kwenu:
Yasiyowezekana si ...
Hadhira: Hayawezekani.
Mwendo mrefu ni sehemu ya zawadi.
(Makofi)
Asanteni.
(Makofi)
(Kushangilia)
Mwenyeji: Asante, Dan Meyer, wow!