Ninataka kuzungumza namna kusoma kunavyoweza kubadilisha maisha yetu na kuhusu mipaka ya mabadiliko hayo Ninataka kuzungumza na wewe namna kusoma kunavyoweza kutupa ulimwengu wa ushirika wa muunganiko wenye nguvu wa kibinadamu pia namna ambavyo muunganiko huo ni sehemu tu mara zote Kusoma mwisho wa siku ni kitendo cha upweke na kisicho cha kawaida. Muandishi aliyebadilisha maisha yangu Ni mmarekani mweusi na mwandishi wa riwaya James Baldwin Wakati ninakuwa katika eneo la Magharibi mwa Michigan miaka ya 1980, hakukuwa na wamarekani wenye asili ya asia wengi wanaoandika kuhusu mabadiliko ya kijamii Na ndio maana nilimgeukia James Baldwin kama namna ya kuliziba hili ombwe, kama namna ya kuwamakini na rangi lakini haswa kwa sababu nilifahamu mimi sikuwa mmarekani mweusi, Pia nilisikia kupata changamoto na kuthibitishwa na maneno yake. Hasusani maneno haya: "Ni watu huria walio na mitazamo sahihi, lakini hawana misimamo halisi. pale ambapo vipande vipo chini na unawategemea kuleta matokeo, na huenda hawako hapo kwa namna fulani". Hawako hapo kwa namna fulani. Nikayachukua hayo maneno nikitafakari. Nijiweke wapi? Nilikwenda kwenye delta ya Mississippi, mojawapo ya maeneo masikini sana ya Marekani. Hii ni sehemu ambayo imejengwa na historia yenye nguvu. Katika mwaka wa 1960, Wamarekani weusi walijitoa maisha yao kupigania Elimu, kupigania haki ya kupiga kura. Nilitaka kuwa sehemu ya badiliko hilo, kuwasaidia vijana wadogo wamalize shule na kujiunga na vyuo. Nilipoenda kwenye Delta ya Mississipi, Palikuwa ni mahali duni bado, bado pametengwa, Bado panahitaji mabadiliko ya kasi. Shule yangu, pale nilipokuwa nasoma, haikuwa na maktaba, hakuna mshauri, lakini ilikuwa na afisa wa polisi. Nusu ya walimu walikuwa ni mbadala na wanafunzi walipoingia kwenye ugomvi, Shule iliwapeleka kwenye jela ya mahali hapo. Hii ndiyo shule nilipokutana na Patrick. Alikuwa na miaka 15 na alikamatwa mara mbili, alikuwa darasa la nane. Alikuwa ni mkimya na mndani, ni kama kila wakati alikuwa mwenye mawazo. Na alichukia kuona wengine wakipigana. Nilimuona mara moja akiruka kati ya mabinti wawili walipokuwa wakipigana Na akajikuta akidondoka na kuanguka chini. Patrick alikuwa na tatizo moja. Hakuwa akifika shuleni. Alisema kuwa shule wakati mwingine humfanya kuwa na msongo Sababu wanafunzi hupigana mara zote na walimu wanaondoka. Lakini pia, mama yake anafanya kazi mbili na huwa anachoka kuweza kumfanya aje shule. Hivyo nikafanya iwe kazi yangu kumfanya awe anakuja shule. Na sababu nilikuwa na wazimu na miaka 22 na mwenye bidii ya matumaini Njia yangu ilikuwa ni kwenda nyumbani kwao na kusema "Eti, kwanini hauji shuleni?" Na njia hii ilifanya kazi, akaanza kuja shuleni kila siku. Na akaanza kufanikiwa katika darasa langu. Aliandika mashairi, alisoma vitabu. Alikuja shuleni kila siku. takriban muda ule ule Nilipogundua namna ya kushirikiana na Patrick, Nilikwenda shule ya sheria Harvard. Nilikutana tena na swali hili, nijiweke wapi, niuweke wapi mwili wangu? Na nikawaza mwenyewe Kuwa Mississipi Delta ni mahali ambapo watu wenye fedha, watu wenye fursa, watu hao huondoka. Na watu wanaobakia ni watu ambao hawana fursa ya kuondoka. Sikutaka kuwa mtu anayeondoka. Nilitaka kuwa mtu anayebakia. Kwa upande mwingine, nilikuwa mpweke na mchovu. Na hivyo nilijishawishi mwenyewe kuwa ninaweza kufanya mabadiliko Kwa kiasi kikubwa kama ningekuwa na shahada yenye heshima ya sheria. Hivyo nikaondoka. Miaka mitatu baadaye, Nilipokaribia kuhitimu shule ya sheria, rafiki yangu alinipigia simu na kuniambia kuwa Patrick amepigana na kuua mtu. Nilitaharuki. Sehemu ya mimi haikuamini, na sehemu ya mimi pia iliamini kuwa ni kweli. Nilisafiri kwenda kumuona Patrick. Nilimtembelea gerezani. Na aliniambia kuwa ilikuwa kweli. Ya kwamba ameua mtu. Na asingependa kuzungumzia suala hilo. Nilimuuliza nini kiliendelea kuhusu shule na akasema aliacha shule mwaka mooja baada ya mimi kuondoka. Na alitaka kuniambia kuhusu kitu kingine Alitazama chini akasema ya kwamba amepata mtoto wa kike ambaye ndiye kwanza amezaliwa. Na anahisi kuwa amemuangusha binti yake. Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mazungumzo yetu yalikuwa ya haraka na mabaya. Nilipotoka nje ya gereza, sauti ndani yangu iliniambia, "Rudi. Usiporudi sasa, hutarudi kamwe". Hivyo nikahitimu shule ya sheria na nikarudi. Nikarudi kumuona Patrick, Nikarudi kuona kama ninaweza kumsaidia na kesi yake ya sheria. Muda huu, nilipomuona kwa mara ya pili, Nilidhani nina hili wazo zuri, nikamwambia, "Hey, Patrick, kwanini usiandike barua kwa binti yako, ili uweze kumuweka katika fikra zako?" Nikampatia kalamu na kipande cha karatasi, na akaanza kuandika. Lakini nilipoiona karatasi aliyonipatia, Nilipigwa na butwaa. Sikuutambua mwandiko wake, alikuwa amefanya makosa machache ya matamshi. na nikawaza mwenyewe kama mwalimu, Ninafahamu ya kuwa mwanafunzi anaweza kufanya vizuri kwa kasi Kwa muda mfupi sana, lakini sikuwahi kuwaza kuwa mwanafunzi anaweza kurudi nyuma kwa kasi. kilichoniumiza zaidi, ni kuona kile alichokiandika kwa binti yake. aliandika, "Ninasikitika kwa makosa yangu, ninasikitika kutokuwa pamoja nawe." Na hiki ndicho alichojisikia anataka kusema naye. Nikajiuliza ni namna gani ninaweza kumshawishi kuwa anaweza kumwambia zaidi, ile sehemu yake ambayo hahitaji kuomba radhi kwayo. Nilitaka yeye ajisikie kuwa anakitu cha thamani kumshirikisha binti yake. Kwa kila siku kwa miezi saba iliyofuatia, Nilimtembelea na kumpelekea vitabu. Mkoba wangu uligeuka kuwa maktaba ndogo. Nilimpelekea James Baldwin, Nilipeleka Walt Whitman, C.S.Lewis. Nilileta vitabu vya mwongozo wa miti, wa ndege, na kitabu alichotokea kukipenda zaidi, kamusi. Kwa baadhi ya siku, tulikaa kimya kwa masaa, wote wawili tukisoma. Na siku nyingine, tulisoma pamoja, tulisoma mashairi. tulianza kwa kusoma haikus, mamia ya haikus, ni kito rahisi na danganyifu. Na ningemuuliza, "Nishirikishe haiku zako unazozipenda". Na baadhi yake ni za kufurahisha sana. Kuna hii ya Issa: "Usijali, buibui, ninaweka nyumba kikawaida." Na hii: "Nimelala nusu ya siku, na hakuna aliyeniadhibu!" Na hii nyingine ya kuvutia, inayohusu siku ya kwanza barafu ilipodondoka, "Kulungu wakilamba baridi ya kwanza kutoka kwenye koti la kila mmoja wao." Kuna kitu cha ajabu na cha kuvutia kuhusu namna shairi linavyoonekana. Nafasi ya shairi ni muhimu kama maneno yenyewe. Tunasoma shairi hili lililoandikwa na W.S.Merwin, ambalo aliliandika baada ya kumuona mkewe akifanya kazi kwenye bustani na akakumbuka kuwa wataishi maisha yao yote yaliyobaki wakiwa pamoja. "Wacha nifikiri kuwa tutakuja tena tutakapotaka na itakuwa wakati wa masika hatutakuwa na umri mkubwa kuliko tulivyowahi kuwa na majonzi yatakuwa mepesi kama mawingu ya mapema ambayo kwayo asubuhi huja yenyewe taratibu" Nikamuuliza Patrick mstari alioupenda zaidi ni upi, na akasema "Hatutakuwa na umri mkubwa kuliko tulivyokuwa." Alisema inamkumbusha mahali ambapo muda husimama, pale ambapo muda haumaanishi kitu chochote. Na nikamuuliza kama amewahi kuwa na mahali pa jinsi hiyo. pale ambapo muda hudumu milele. Na akasema, "Mama yangu". Na pale unaposoma shairi pamoja na mtu mwingine, shairi hubadilika katika maana. Kwa sababu huwa la kibinafsi kwa mtu huyo, huwa la kibinafsi kwako. Halafu tulisoma vitabu, tulisoma vitabu vingi sana, tulisoma kumbukumbu za Frederick Douglass, Mtumwa wa Marekani aliyejifunza mwenyewe kusoma na kuandika na aliyetoroka na kuwa huru sababu ya kuelimika kwake. Nimekua nikimfikiria Frederick Douglass kama shujaa na niliiona hii simulizi kama iliyojaa matumaini na yenye kuinua Lakini kitabu hiki kilimuweka Patrick katika hofu. Alibakia katika simulizi aliyoielezea Douglass jinsi ambavyo, katika Christmas, Mabwana waliwapa watumwa jini(pombe kali) kama namna ya kuwaaminisha kuwa hawawezi kuumudu uhuru. Kwa sababu watumwa waliweweseka katika mashamba. Patrick alisema anajifananisha na hili. Alisema kuwa kuna watu gerezani ambao, kama watumwa, hawataki kuwaza juu ya hali zao, kwa sababu inawaumiza sana. Inaumiza sana kuwaza mambo ya nyuma, inaumiza sana kuwaza kuhusu umbali gani tunapaswa kwenda. Mstari alioupenda sana ulikuwa huu: "Chochote kile, bila kujali chochote, kujiondoa katika kuwaza! Ilikuwa ni huku kuwaza kusiko koma kuhusu hali yangu ndiko kunako kipa mateso." Patrick alisema Douglass alikuwa jasiri kuandika, ili aendelee kuwaza. Lakini Patrick hakufahamu kuwa alionekana kufanana sana na Douglass kwangu. Namna alivyoendelea kusoma, ijapokuwa ilimuweka katika hofu. Alimaliza kitabu kabla yangu, akisoma katika ngazi za zege zisizo na taa. Halafu tukaendelea kusoma mojawapo ya vitabu ninavyovipenda, Cha Marilynne Robinson's "Gilead," ambayo ni barua endelevu kutoka kwa baba kwenda kwa mwanae. Alipenda mstari huu: "Ninaandika hii kwa sehemu kukuambia ya kwamba kama umewahi kujiuliza kile umekifanya katika maisha yako... umekuwa neema ya Mungu kwangu, muujiza, kitu ambacho ni zaidi ya muujiza." Kitu kimoja kuhusu hii lugha, upendo wake, subira yake, sauti yake, iliamsha shauku ya Patrick katika kuandika. Na alijaza daftari kwa daftari na barua kwenda kwa binti yake. katika barua hizi nzuri na imara, alijiwazia yeye na binti yake wakipanda mtumbwi katika mto Mississipi Alijiwazia yeye na binti yake wakipata vijito vya milimani vikiwa na maji masafi bila kasoro. Nilipomtazama Patrick akiandika, Nilijiwazia mwenyewe, na sasa ninawaulizeni nyote, ni wangapi wenu mmewahi kuandika barua kwa mtu unayehisi umemwangusha? Ni rahisi sana kuwaweka hao watu nje ya fikra zako. Lakini Patrick alijitokeza kila siku, akimkabili binti yake, akijiwajibisha kwake, neno kwa neno kwa umakini wa hali ya juu. Ningependa katika maisha yangu binafsi kujiweka katika hatari kwa namna hiyo. Kwa sababu hatari hiyo inadhihirisha nguvu za moyo wa mtu. Ngoja nirudi hatua moja nyuma na niulize swali ambalo linaleta wasiwasi. Mimi ni nani kusimulia simulizi hii, hii simulizi ya Patrick? Patrick ndiye aliyeishi kwenye maumivu haya na mimi sijawahi kukaa na njaa hata kwa siku moja kwenye maisha yangu Ninawaza sana kuhusu swali hili, lakini ninachotaka kusema ni kuwa hii simulizi sio tu kuhusu Patrick. Inatuhusu sisi, ni kuhusu tofauti kati yetu. Ulimwengu wa vingi ambao Patrick na wazazi wake na mababu zake hawajawahi kuuona. Katika simulizi hii, mimi ninawakilisha huo ulimwengu wa vingi. Na katika kueleza simulizi hii sikutaka kujificha mwenyewe. Kuficha nguvu ambazo ninazo. Katika kueleza simulizi hii, ninataka kuifichua nguvu hiyo halafu kuuliza, tunawezaje kuipunguza umbali kati yetu? Kusoma ni njia mojawapo ya kuipunguza hiyo nafasi. Kunatuma ulimwengu wa ukimya ambao tunaweza kuushiriki pamoja, ambao tunaweza kuushiriki kwa usawa. Inawezekana unajiuliza sasa kuwa ni nini kilitokea kwa Patrick. Je kusoma kuliokoa maisha yake? Kuliyaokoa na hakukuyaokoa. Patrick alipotoka gerezani, safari yake ilikuwa ya maumivu. Waajiri hawakumkubali kwa sababu ya historia yake, rafiki yake mpenzi, mama yake, alifariki katika umri wa miaka 43 kwa ugonjwa wa moyo na kisukari. Alikuwa hana pa kuishi, amekuwa hana chakula. Kwa hiyo watu wanasema mengi kuhusu kusoma ambayo kwangu ninahisi wanazidisha chumvi. Uwezo wa kusoma haukumzuia yeye asitengwe na jamii. Hakukumzuia mama yake asifariki. Kwa hiyo kusoma kunaweza kufanya nini? Nina majibu machache ninapomalizia leo. Kusoma kulibadili utu wake wa ndani kwa mambo yaliyofichika na uwezo wa kuwaza kwa picha. kwa uzuri. Kusoma kulimpa taswira zilizompa furaha: milima, bahari, kulungu, theluji. Maneno yenye ladha ya ulimwengu huru na halisi. Kusoma kulimpa lugha kwa yale aliyopoteza. Ni jinsi gani yalivyo mazuri haya maneno kutoka kwa mshairi Derek Walcott? Patrick alilikariri hili shairi. "Siku ambazo nilizishikilia, siku ambazo nilizipoteza, siku ambazo zinakuwa kupitiliza, kama mabinti, mikono yangu inayoshikilia." Kusoma kulimfundisha ujasiri wake mwenyewe. Kumbuka kwamba aliendelea kusoma Frederick Douglass, ijapokuwa ilikuwa ya kuumiza. Aliendelea kuwa makini, ijapokuwa kuwa makini kunauma. Kusoma ni aina ya kutafakari, ndio maana ni vigumu sana kusoma kwa sababu tunataka kutafakari. Na Patrick alichagua kutafakari, badala ya kutokutafakari. Na mwishoni, kusoma kulimpa lugha ya kuongea na binti yake. Kusoma kulimpa shauku ya kutaka kuandika. Muunganiko kati ya kusoma na kuandika ni wenye nguvu sana. Tunapoanza kusoma, tunaanza kupata maneno. Na alipata maneno ya kutafakari wao wawili wakiwa pamoja. Alipata maneno ya kumwelezea ni namna gani anampenda. Kusoma pia kulibadilisha mahusiano baina yetu. Kunatupa nyakati za kuwa karibu, kuweza kuona zaidi ya mitazamo yetu. Na kusoma kulichukua mahusiano ya kutokuwa sawa na kulitupa usawa wa muda mfupi. Ukikutana na mtu kama msomaji, unakutana naye kwa mara ya kwanza, kwa upya kabisa. Hakuna namna unaweza kufahamu mstari anaoupenda sana ni upi. Ni kumbukumbu zipi na huzuni zipi za siri alizonazo. Na unakutana na sitara ya hali ya juu ya utu wake wa ndani. Na halafu unaanza kushangaa, "Eti,utu wangu wa ndani umejengwa na nini? Ni kitu gani nilichonacho cha thamani cha kumshirikisha mwingine?" Ninataka kufunga kwa mistari yangu ninayoipenda kutoka kwa barua za Patrick kwa bintiye. "Mto una kivuli kwenye baadhi ya maeneo lakini mwanga unaangaza kupitia mianya ya miti... Kwenye baadhi ya matawi muliberi nyingi zimening'inia. Unanyoosha mkono wako ili uweze kuyachukua baadhi". Na barua hii ya upendo, anapoandika, "Fumba macho yako na usikilize sauti ya maneno. Ninafahamu shairi hili kwa moyo na ningependa pia wewe ulifahamu." Ninawashukuruni nyote. (Makofi)