[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:00.92,0:00:06.39,Default,,0000,0000,0000,,Ninataka kuzungumza namna kusoma \Nkunavyoweza kubadilisha maisha yetu Dialogue: 0,0:00:06.42,0:00:08.79,Default,,0000,0000,0000,,na kuhusu mipaka ya mabadiliko hayo Dialogue: 0,0:00:09.75,0:00:14.02,Default,,0000,0000,0000,,Ninataka kuzungumza na wewe namna kusoma\Nkunavyoweza kutupa ulimwengu wa ushirika Dialogue: 0,0:00:14.04,0:00:16.75,Default,,0000,0000,0000,,wa muunganiko wenye nguvu wa kibinadamu Dialogue: 0,0:00:17.83,0:00:21.39,Default,,0000,0000,0000,,pia namna ambavyo muunganiko huo \Nni sehemu tu mara zote Dialogue: 0,0:00:21.42,0:00:26.50,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma mwisho wa siku ni kitendo cha \Nupweke na kisicho cha kawaida. Dialogue: 0,0:00:27.62,0:00:30.48,Default,,0000,0000,0000,,Muandishi aliyebadilisha maisha yangu Dialogue: 0,0:00:30.50,0:00:34.93,Default,,0000,0000,0000,,Ni mmarekani mweusi na mwandishi\Nwa riwaya James Baldwin Dialogue: 0,0:00:34.96,0:00:38.23,Default,,0000,0000,0000,,Wakati ninakuwa katika eneo la\NMagharibi mwa Michigan miaka ya 1980, Dialogue: 0,0:00:38.25,0:00:42.17,Default,,0000,0000,0000,,hakukuwa na wamarekani wenye asili ya asia\Nwengi wanaoandika kuhusu mabadiliko ya kijamii Dialogue: 0,0:00:43.29,0:00:46.52,Default,,0000,0000,0000,,Na ndio maana nilimgeukia James Baldwin Dialogue: 0,0:00:46.54,0:00:50.58,Default,,0000,0000,0000,,kama namna ya kuliziba hili ombwe,\Nkama namna ya kuwamakini na rangi Dialogue: 0,0:00:51.96,0:00:55.93,Default,,0000,0000,0000,,lakini haswa kwa sababu nilifahamu\Nmimi sikuwa mmarekani mweusi, Dialogue: 0,0:00:55.96,0:01:00.48,Default,,0000,0000,0000,,Pia nilisikia kupata changamoto na\Nkuthibitishwa na maneno yake. Dialogue: 0,0:01:00.50,0:01:02.62,Default,,0000,0000,0000,,Hasusani maneno haya: Dialogue: 0,0:01:03.46,0:01:07.06,Default,,0000,0000,0000,,"Ni watu huria walio na mitazamo sahihi, Dialogue: 0,0:01:07.08,0:01:09.04,Default,,0000,0000,0000,,lakini hawana misimamo halisi. Dialogue: 0,0:01:10.08,0:01:14.02,Default,,0000,0000,0000,,pale ambapo vipande vipo chini\Nna unawategemea kuleta matokeo, Dialogue: 0,0:01:14.04,0:01:16.52,Default,,0000,0000,0000,,na huenda hawako hapo kwa namna fulani". Dialogue: 0,0:01:16.54,0:01:19.35,Default,,0000,0000,0000,,Hawako hapo kwa namna fulani. Dialogue: 0,0:01:19.38,0:01:21.73,Default,,0000,0000,0000,,Nikayachukua hayo maneno nikitafakari. Dialogue: 0,0:01:21.75,0:01:23.46,Default,,0000,0000,0000,,Nijiweke wapi? Dialogue: 0,0:01:24.50,0:01:26.52,Default,,0000,0000,0000,,Nilikwenda kwenye delta ya Mississippi, Dialogue: 0,0:01:26.54,0:01:29.68,Default,,0000,0000,0000,,mojawapo ya maeneo masikini sana ya\NMarekani. Dialogue: 0,0:01:29.71,0:01:32.60,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni sehemu ambayo imejengwa\Nna historia yenye nguvu. Dialogue: 0,0:01:32.62,0:01:37.77,Default,,0000,0000,0000,,Katika mwaka wa 1960, Wamarekani weusi\Nwalijitoa maisha yao kupigania Elimu, Dialogue: 0,0:01:37.79,0:01:39.50,Default,,0000,0000,0000,,kupigania haki ya kupiga kura. Dialogue: 0,0:01:40.62,0:01:43.06,Default,,0000,0000,0000,,Nilitaka kuwa sehemu ya badiliko hilo, Dialogue: 0,0:01:43.08,0:01:46.79,Default,,0000,0000,0000,,kuwasaidia vijana wadogo wamalize shule\Nna kujiunga na vyuo. Dialogue: 0,0:01:48.25,0:01:50.98,Default,,0000,0000,0000,,Nilipoenda kwenye Delta ya Mississipi, Dialogue: 0,0:01:51.00,0:01:53.43,Default,,0000,0000,0000,,Palikuwa ni mahali duni bado, Dialogue: 0,0:01:53.46,0:01:55.18,Default,,0000,0000,0000,,bado pametengwa, Dialogue: 0,0:01:55.21,0:01:57.75,Default,,0000,0000,0000,,Bado panahitaji mabadiliko ya kasi. Dialogue: 0,0:01:58.96,0:02:02.39,Default,,0000,0000,0000,,Shule yangu, pale nilipokuwa nasoma, Dialogue: 0,0:02:02.42,0:02:06.73,Default,,0000,0000,0000,,haikuwa na maktaba, hakuna mshauri, Dialogue: 0,0:02:06.75,0:02:09.73,Default,,0000,0000,0000,,lakini ilikuwa na afisa wa polisi. Dialogue: 0,0:02:09.75,0:02:12.31,Default,,0000,0000,0000,,Nusu ya walimu walikuwa ni mbadala Dialogue: 0,0:02:12.33,0:02:14.31,Default,,0000,0000,0000,,na wanafunzi walipoingia kwenye ugomvi, Dialogue: 0,0:02:14.33,0:02:18.21,Default,,0000,0000,0000,,Shule iliwapeleka kwenye jela ya \Nmahali hapo. Dialogue: 0,0:02:20.25,0:02:23.23,Default,,0000,0000,0000,,Hii ndiyo shule nilipokutana na Patrick. Dialogue: 0,0:02:23.25,0:02:28.18,Default,,0000,0000,0000,,Alikuwa na miaka 15 na alikamatwa mara\Nmbili, alikuwa darasa la nane. Dialogue: 0,0:02:28.21,0:02:30.68,Default,,0000,0000,0000,,Alikuwa ni mkimya na mndani, Dialogue: 0,0:02:30.71,0:02:33.52,Default,,0000,0000,0000,,ni kama kila wakati alikuwa mwenye mawazo. Dialogue: 0,0:02:33.54,0:02:36.33,Default,,0000,0000,0000,,Na alichukia kuona wengine wakipigana. Dialogue: 0,0:02:37.50,0:02:41.31,Default,,0000,0000,0000,,Nilimuona mara moja akiruka kati ya \Nmabinti wawili walipokuwa wakipigana Dialogue: 0,0:02:41.33,0:02:44.04,Default,,0000,0000,0000,,Na akajikuta akidondoka na kuanguka chini. Dialogue: 0,0:02:45.38,0:02:47.89,Default,,0000,0000,0000,,Patrick alikuwa na tatizo moja. Dialogue: 0,0:02:47.92,0:02:49.71,Default,,0000,0000,0000,,Hakuwa akifika shuleni. Dialogue: 0,0:02:51.25,0:02:53.73,Default,,0000,0000,0000,,Alisema kuwa shule wakati mwingine humfanya kuwa na msongo Dialogue: 0,0:02:53.75,0:02:56.79,Default,,0000,0000,0000,,Sababu wanafunzi hupigana mara zote na\Nwalimu wanaondoka. Dialogue: 0,0:02:58.04,0:03:03.50,Default,,0000,0000,0000,,Lakini pia, mama yake anafanya kazi mbili\Nna huwa anachoka kuweza kumfanya aje shule. Dialogue: 0,0:03:04.42,0:03:07.18,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo nikafanya iwe kazi yangu\Nkumfanya awe anakuja shule. Dialogue: 0,0:03:07.21,0:03:11.27,Default,,0000,0000,0000,,Na sababu nilikuwa na wazimu na miaka 22\Nna mwenye bidii ya matumaini Dialogue: 0,0:03:11.29,0:03:13.43,Default,,0000,0000,0000,,Njia yangu ilikuwa ni\Nkwenda nyumbani kwao Dialogue: 0,0:03:13.46,0:03:15.58,Default,,0000,0000,0000,,na kusema "Eti, kwanini hauji\Nshuleni?" Dialogue: 0,0:03:16.54,0:03:18.18,Default,,0000,0000,0000,,Na njia hii ilifanya kazi, Dialogue: 0,0:03:18.21,0:03:20.64,Default,,0000,0000,0000,,akaanza kuja shuleni kila siku. Dialogue: 0,0:03:20.67,0:03:23.06,Default,,0000,0000,0000,,Na akaanza kufanikiwa katika darasa langu. Dialogue: 0,0:03:23.08,0:03:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Aliandika mashairi,\Nalisoma vitabu. Dialogue: 0,0:03:26.92,0:03:29.21,Default,,0000,0000,0000,,Alikuja shuleni kila siku. Dialogue: 0,0:03:31.04,0:03:32.52,Default,,0000,0000,0000,,takriban muda ule ule Dialogue: 0,0:03:32.54,0:03:35.23,Default,,0000,0000,0000,,Nilipogundua namna ya kushirikiana\Nna Patrick, Dialogue: 0,0:03:35.25,0:03:37.46,Default,,0000,0000,0000,,Nilikwenda shule ya sheria Harvard. Dialogue: 0,0:03:39.58,0:03:42.93,Default,,0000,0000,0000,,Nilikutana tena na swali hili,\Nnijiweke wapi, Dialogue: 0,0:03:42.96,0:03:44.67,Default,,0000,0000,0000,,niuweke wapi mwili wangu? Dialogue: 0,0:03:45.46,0:03:48.10,Default,,0000,0000,0000,,Na nikawaza mwenyewe Dialogue: 0,0:03:48.12,0:03:51.64,Default,,0000,0000,0000,,Kuwa Mississipi Delta\Nni mahali ambapo watu wenye fedha, Dialogue: 0,0:03:51.67,0:03:53.56,Default,,0000,0000,0000,,watu wenye fursa, Dialogue: 0,0:03:53.58,0:03:54.83,Default,,0000,0000,0000,,watu hao huondoka. Dialogue: 0,0:03:55.88,0:03:57.31,Default,,0000,0000,0000,,Na watu wanaobakia Dialogue: 0,0:03:57.33,0:03:59.83,Default,,0000,0000,0000,,ni watu ambao hawana fursa ya kuondoka. Dialogue: 0,0:04:00.83,0:04:03.10,Default,,0000,0000,0000,,Sikutaka kuwa mtu anayeondoka. Dialogue: 0,0:04:03.12,0:04:05.17,Default,,0000,0000,0000,,Nilitaka kuwa mtu anayebakia. Dialogue: 0,0:04:06.33,0:04:09.27,Default,,0000,0000,0000,,Kwa upande mwingine, nilikuwa mpweke \Nna mchovu. Dialogue: 0,0:04:09.29,0:04:12.75,Default,,0000,0000,0000,,Na hivyo nilijishawishi mwenyewe\Nkuwa ninaweza kufanya mabadiliko Dialogue: 0,0:04:14.12,0:04:17.71,Default,,0000,0000,0000,,Kwa kiasi kikubwa kama ningekuwa\Nna shahada yenye heshima ya sheria. Dialogue: 0,0:04:19.54,0:04:20.79,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo nikaondoka. Dialogue: 0,0:04:22.75,0:04:24.35,Default,,0000,0000,0000,,Miaka mitatu baadaye, Dialogue: 0,0:04:24.38,0:04:26.77,Default,,0000,0000,0000,,Nilipokaribia kuhitimu\Nshule ya sheria, Dialogue: 0,0:04:26.79,0:04:28.52,Default,,0000,0000,0000,,rafiki yangu alinipigia simu Dialogue: 0,0:04:28.54,0:04:33.46,Default,,0000,0000,0000,,na kuniambia kuwa Patrick \Namepigana na kuua mtu. Dialogue: 0,0:04:35.33,0:04:37.39,Default,,0000,0000,0000,,Nilitaharuki. Dialogue: 0,0:04:37.42,0:04:39.85,Default,,0000,0000,0000,,Sehemu ya mimi haikuamini, Dialogue: 0,0:04:39.88,0:04:42.54,Default,,0000,0000,0000,,na sehemu ya mimi pia iliamini kuwa \Nni kweli. Dialogue: 0,0:04:43.58,0:04:45.58,Default,,0000,0000,0000,,Nilisafiri kwenda kumuona Patrick. Dialogue: 0,0:04:46.75,0:04:49.46,Default,,0000,0000,0000,,Nilimtembelea gerezani. Dialogue: 0,0:04:50.54,0:04:54.18,Default,,0000,0000,0000,,Na aliniambia kuwa ilikuwa kweli. Dialogue: 0,0:04:54.21,0:04:56.60,Default,,0000,0000,0000,,Ya kwamba ameua mtu. Dialogue: 0,0:04:56.62,0:04:58.88,Default,,0000,0000,0000,,Na asingependa kuzungumzia suala hilo. Dialogue: 0,0:04:59.83,0:05:01.85,Default,,0000,0000,0000,,Nilimuuliza nini kiliendelea kuhusu shule Dialogue: 0,0:05:01.88,0:05:06.02,Default,,0000,0000,0000,,na akasema aliacha shule mwaka mooja\Nbaada ya mimi kuondoka. Dialogue: 0,0:05:06.04,0:05:08.68,Default,,0000,0000,0000,,Na alitaka kuniambia kuhusu kitu kingine Dialogue: 0,0:05:08.71,0:05:11.98,Default,,0000,0000,0000,,Alitazama chini akasema\Nya kwamba amepata mtoto wa kike Dialogue: 0,0:05:12.00,0:05:13.77,Default,,0000,0000,0000,,ambaye ndiye kwanza amezaliwa. Dialogue: 0,0:05:13.79,0:05:16.38,Default,,0000,0000,0000,,Na anahisi kuwa amemuangusha binti yake. Dialogue: 0,0:05:18.62,0:05:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mazungumzo yetu\Nyalikuwa ya haraka na mabaya. Dialogue: 0,0:05:23.42,0:05:28.48,Default,,0000,0000,0000,,Nilipotoka nje ya gereza,\Nsauti ndani yangu iliniambia, Dialogue: 0,0:05:28.50,0:05:29.77,Default,,0000,0000,0000,,"Rudi. Dialogue: 0,0:05:29.79,0:05:33.08,Default,,0000,0000,0000,,Usiporudi sasa, hutarudi kamwe". Dialogue: 0,0:05:36.29,0:05:39.88,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo nikahitimu shule ya sheria na\Nnikarudi. Dialogue: 0,0:05:40.83,0:05:42.52,Default,,0000,0000,0000,,Nikarudi kumuona Patrick, Dialogue: 0,0:05:42.54,0:05:45.50,Default,,0000,0000,0000,,Nikarudi kuona kama ninaweza kumsaidia\Nna kesi yake ya sheria. Dialogue: 0,0:05:46.92,0:05:50.27,Default,,0000,0000,0000,,Muda huu,\Nnilipomuona kwa mara ya pili, Dialogue: 0,0:05:50.29,0:05:52.56,Default,,0000,0000,0000,,Nilidhani nina hili wazo zuri, \Nnikamwambia, Dialogue: 0,0:05:52.58,0:05:56.18,Default,,0000,0000,0000,,"Hey, Patrick, kwanini usiandike barua\Nkwa binti yako, Dialogue: 0,0:05:56.21,0:05:59.98,Default,,0000,0000,0000,,ili uweze kumuweka katika\Nfikra zako?" Dialogue: 0,0:06:00.00,0:06:03.68,Default,,0000,0000,0000,,Nikampatia kalamu na\Nkipande cha karatasi, Dialogue: 0,0:06:03.71,0:06:05.33,Default,,0000,0000,0000,,na akaanza kuandika. Dialogue: 0,0:06:06.54,0:06:09.35,Default,,0000,0000,0000,,Lakini nilipoiona karatasi aliyonipatia, Dialogue: 0,0:06:09.38,0:06:10.71,Default,,0000,0000,0000,,Nilipigwa na butwaa. Dialogue: 0,0:06:13.00,0:06:15.10,Default,,0000,0000,0000,,Sikuutambua mwandiko wake, Dialogue: 0,0:06:15.12,0:06:17.96,Default,,0000,0000,0000,,alikuwa amefanya makosa\Nmachache ya matamshi. Dialogue: 0,0:06:19.17,0:06:21.85,Default,,0000,0000,0000,,na nikawaza mwenyewe kama mwalimu, Dialogue: 0,0:06:21.88,0:06:25.35,Default,,0000,0000,0000,,Ninafahamu ya kuwa mwanafunzi\Nanaweza kufanya vizuri kwa kasi Dialogue: 0,0:06:25.38,0:06:28.43,Default,,0000,0000,0000,,Kwa muda mfupi sana, Dialogue: 0,0:06:28.46,0:06:32.12,Default,,0000,0000,0000,,lakini sikuwahi kuwaza kuwa mwanafunzi\Nanaweza kurudi nyuma kwa kasi. Dialogue: 0,0:06:34.38,0:06:36.27,Default,,0000,0000,0000,,kilichoniumiza zaidi, Dialogue: 0,0:06:36.29,0:06:39.48,Default,,0000,0000,0000,,ni kuona kile alichokiandika\Nkwa binti yake. Dialogue: 0,0:06:39.50,0:06:40.89,Default,,0000,0000,0000,,aliandika, Dialogue: 0,0:06:40.92,0:06:45.21,Default,,0000,0000,0000,,"Ninasikitika kwa makosa yangu,\Nninasikitika kutokuwa pamoja nawe." Dialogue: 0,0:06:46.46,0:06:49.29,Default,,0000,0000,0000,,Na hiki ndicho alichojisikia\Nanataka kusema naye. Dialogue: 0,0:06:50.25,0:06:54.56,Default,,0000,0000,0000,,Nikajiuliza ni namna gani ninaweza\Nkumshawishi kuwa anaweza kumwambia zaidi, Dialogue: 0,0:06:54.58,0:06:58.00,Default,,0000,0000,0000,,ile sehemu yake ambayo\Nhahitaji kuomba radhi kwayo. Dialogue: 0,0:06:58.96,0:07:00.23,Default,,0000,0000,0000,,Nilitaka yeye ajisikie Dialogue: 0,0:07:00.25,0:07:04.21,Default,,0000,0000,0000,,kuwa anakitu cha thamani\Nkumshirikisha binti yake. Dialogue: 0,0:07:05.92,0:07:09.10,Default,,0000,0000,0000,,Kwa kila siku kwa miezi saba iliyofuatia, Dialogue: 0,0:07:09.12,0:07:11.81,Default,,0000,0000,0000,,Nilimtembelea na kumpelekea vitabu. Dialogue: 0,0:07:11.83,0:07:15.68,Default,,0000,0000,0000,,Mkoba wangu uligeuka kuwa maktaba ndogo. Dialogue: 0,0:07:15.71,0:07:17.77,Default,,0000,0000,0000,,Nilimpelekea James Baldwin, Dialogue: 0,0:07:17.79,0:07:22.68,Default,,0000,0000,0000,,Nilipeleka Walt Whitman, C.S.Lewis. Dialogue: 0,0:07:22.71,0:07:27.52,Default,,0000,0000,0000,,Nilileta vitabu vya mwongozo wa miti, \Nwa ndege, Dialogue: 0,0:07:27.54,0:07:30.75,Default,,0000,0000,0000,,na kitabu alichotokea kukipenda zaidi, \Nkamusi. Dialogue: 0,0:07:31.67,0:07:33.35,Default,,0000,0000,0000,,Kwa baadhi ya siku, Dialogue: 0,0:07:33.38,0:07:37.17,Default,,0000,0000,0000,,tulikaa kimya kwa masaa,\Nwote wawili tukisoma. Dialogue: 0,0:07:38.08,0:07:39.93,Default,,0000,0000,0000,,Na siku nyingine, Dialogue: 0,0:07:39.96,0:07:43.48,Default,,0000,0000,0000,,tulisoma pamoja,\Ntulisoma mashairi. Dialogue: 0,0:07:43.50,0:07:47.39,Default,,0000,0000,0000,,tulianza kwa kusoma haikus,\Nmamia ya haikus, Dialogue: 0,0:07:47.42,0:07:50.31,Default,,0000,0000,0000,,ni kito rahisi na danganyifu. Dialogue: 0,0:07:50.33,0:07:53.14,Default,,0000,0000,0000,,Na ningemuuliza,\N"Nishirikishe haiku zako unazozipenda". Dialogue: 0,0:07:53.17,0:07:56.23,Default,,0000,0000,0000,,Na baadhi yake ni za kufurahisha sana. Dialogue: 0,0:07:56.25,0:07:58.10,Default,,0000,0000,0000,,Kuna hii ya Issa: Dialogue: 0,0:07:58.12,0:08:01.83,Default,,0000,0000,0000,,"Usijali, buibui,\Nninaweka nyumba kikawaida." Dialogue: 0,0:08:02.75,0:08:07.29,Default,,0000,0000,0000,,Na hii: "Nimelala nusu ya siku,\Nna hakuna aliyeniadhibu!" Dialogue: 0,0:08:08.67,0:08:13.10,Default,,0000,0000,0000,,Na hii nyingine ya kuvutia, inayohusu\Nsiku ya kwanza barafu ilipodondoka, Dialogue: 0,0:08:13.12,0:08:17.58,Default,,0000,0000,0000,,"Kulungu wakilamba baridi ya kwanza\Nkutoka kwenye koti la kila mmoja wao." Dialogue: 0,0:08:19.25,0:08:22.27,Default,,0000,0000,0000,,Kuna kitu cha ajabu na cha kuvutia Dialogue: 0,0:08:22.29,0:08:24.93,Default,,0000,0000,0000,,kuhusu namna shairi linavyoonekana. Dialogue: 0,0:08:24.96,0:08:29.58,Default,,0000,0000,0000,,Nafasi ya shairi ni muhimu\Nkama maneno yenyewe. Dialogue: 0,0:08:31.38,0:08:33.89,Default,,0000,0000,0000,,Tunasoma shairi hili lililoandikwa na\NW.S.Merwin, Dialogue: 0,0:08:33.92,0:08:38.14,Default,,0000,0000,0000,,ambalo aliliandika baada ya kumuona\Nmkewe akifanya kazi kwenye bustani Dialogue: 0,0:08:38.17,0:08:42.04,Default,,0000,0000,0000,,na akakumbuka kuwa wataishi maisha\Nyao yote yaliyobaki wakiwa pamoja. Dialogue: 0,0:08:43.17,0:08:45.52,Default,,0000,0000,0000,,"Wacha nifikiri kuwa tutakuja tena Dialogue: 0,0:08:45.54,0:08:48.93,Default,,0000,0000,0000,,tutakapotaka na itakuwa wakati wa masika Dialogue: 0,0:08:48.96,0:08:52.14,Default,,0000,0000,0000,,hatutakuwa na umri mkubwa\Nkuliko tulivyowahi kuwa Dialogue: 0,0:08:52.17,0:08:56.10,Default,,0000,0000,0000,,na majonzi yatakuwa mepesi kama\Nmawingu ya mapema Dialogue: 0,0:08:56.12,0:08:59.89,Default,,0000,0000,0000,,ambayo kwayo asubuhi\Nhuja yenyewe taratibu" Dialogue: 0,0:08:59.92,0:09:03.31,Default,,0000,0000,0000,,Nikamuuliza Patrick mstari alioupenda \Nzaidi ni upi, na akasema Dialogue: 0,0:09:03.33,0:09:06.88,Default,,0000,0000,0000,,"Hatutakuwa na umri mkubwa \Nkuliko tulivyokuwa." Dialogue: 0,0:09:08.38,0:09:12.81,Default,,0000,0000,0000,,Alisema inamkumbusha\Nmahali ambapo muda husimama, Dialogue: 0,0:09:12.83,0:09:15.77,Default,,0000,0000,0000,,pale ambapo muda haumaanishi\Nkitu chochote. Dialogue: 0,0:09:15.79,0:09:17.85,Default,,0000,0000,0000,,Na nikamuuliza kama amewahi kuwa\Nna mahali pa jinsi hiyo. Dialogue: 0,0:09:17.88,0:09:20.27,Default,,0000,0000,0000,,pale ambapo muda hudumu milele. Dialogue: 0,0:09:20.29,0:09:21.96,Default,,0000,0000,0000,,Na akasema, "Mama yangu". Dialogue: 0,0:09:23.88,0:09:28.18,Default,,0000,0000,0000,,Na pale unaposoma shairi \Npamoja na mtu mwingine, Dialogue: 0,0:09:28.21,0:09:30.08,Default,,0000,0000,0000,,shairi hubadilika katika maana. Dialogue: 0,0:09:31.33,0:09:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa sababu huwa la kibinafsi kwa mtu huyo,\Nhuwa la kibinafsi kwako. Dialogue: 0,0:09:37.50,0:09:40.18,Default,,0000,0000,0000,,Halafu tulisoma vitabu,\Ntulisoma vitabu vingi sana, Dialogue: 0,0:09:40.21,0:09:43.35,Default,,0000,0000,0000,,tulisoma kumbukumbu za Frederick Douglass, Dialogue: 0,0:09:43.38,0:09:46.98,Default,,0000,0000,0000,,Mtumwa wa Marekani aliyejifunza mwenyewe\Nkusoma na kuandika Dialogue: 0,0:09:47.00,0:09:50.33,Default,,0000,0000,0000,,na aliyetoroka na kuwa huru\Nsababu ya kuelimika kwake. Dialogue: 0,0:09:51.88,0:09:54.52,Default,,0000,0000,0000,,Nimekua nikimfikiria Frederick Douglass \Nkama shujaa Dialogue: 0,0:09:54.54,0:09:57.75,Default,,0000,0000,0000,,na niliiona hii simulizi kama\Niliyojaa matumaini na yenye kuinua Dialogue: 0,0:09:58.92,0:10:01.75,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kitabu hiki kilimuweka Patrick\Nkatika hofu. Dialogue: 0,0:10:02.88,0:10:07.93,Default,,0000,0000,0000,,Alibakia katika simulizi aliyoielezea \NDouglass jinsi ambavyo, katika Christmas, Dialogue: 0,0:10:07.96,0:10:11.06,Default,,0000,0000,0000,,Mabwana waliwapa watumwa jini(pombe kali) Dialogue: 0,0:10:11.08,0:10:14.56,Default,,0000,0000,0000,,kama namna ya kuwaaminisha kuwa\Nhawawezi kuumudu uhuru. Dialogue: 0,0:10:14.58,0:10:17.38,Default,,0000,0000,0000,,Kwa sababu watumwa waliweweseka\Nkatika mashamba. Dialogue: 0,0:10:19.50,0:10:21.50,Default,,0000,0000,0000,,Patrick alisema anajifananisha na hili. Dialogue: 0,0:10:22.33,0:10:25.81,Default,,0000,0000,0000,,Alisema kuwa kuna watu gerezani ambao,\Nkama watumwa, Dialogue: 0,0:10:25.83,0:10:28.06,Default,,0000,0000,0000,,hawataki kuwaza juu ya hali zao, Dialogue: 0,0:10:28.08,0:10:29.89,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu inawaumiza sana. Dialogue: 0,0:10:29.92,0:10:32.10,Default,,0000,0000,0000,,Inaumiza sana kuwaza mambo ya nyuma, Dialogue: 0,0:10:32.12,0:10:35.46,Default,,0000,0000,0000,,inaumiza sana kuwaza\Nkuhusu umbali gani tunapaswa kwenda. Dialogue: 0,0:10:36.96,0:10:39.85,Default,,0000,0000,0000,,Mstari alioupenda sana ulikuwa huu: Dialogue: 0,0:10:39.88,0:10:43.48,Default,,0000,0000,0000,,"Chochote kile, bila kujali chochote,\Nkujiondoa katika kuwaza! Dialogue: 0,0:10:43.50,0:10:48.54,Default,,0000,0000,0000,,Ilikuwa ni huku kuwaza kusiko koma kuhusu\Nhali yangu ndiko kunako kipa mateso." Dialogue: 0,0:10:49.96,0:10:53.92,Default,,0000,0000,0000,,Patrick alisema Douglass alikuwa jasiri \Nkuandika, ili aendelee kuwaza. Dialogue: 0,0:10:55.08,0:11:00.64,Default,,0000,0000,0000,,Lakini Patrick hakufahamu kuwa alionekana \Nkufanana sana na Douglass kwangu. Dialogue: 0,0:11:00.67,0:11:04.42,Default,,0000,0000,0000,,Namna alivyoendelea kusoma,\Nijapokuwa ilimuweka katika hofu. Dialogue: 0,0:11:05.25,0:11:08.31,Default,,0000,0000,0000,,Alimaliza kitabu kabla yangu, Dialogue: 0,0:11:08.33,0:11:12.04,Default,,0000,0000,0000,,akisoma katika ngazi za \Nzege zisizo na taa. Dialogue: 0,0:11:13.58,0:11:16.31,Default,,0000,0000,0000,,Halafu tukaendelea kusoma mojawapo\Nya vitabu ninavyovipenda, Dialogue: 0,0:11:16.33,0:11:18.52,Default,,0000,0000,0000,,Cha Marilynne Robinson's "Gilead," Dialogue: 0,0:11:18.54,0:11:22.68,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ni barua endelevu kutoka\Nkwa baba kwenda kwa mwanae. Dialogue: 0,0:11:22.71,0:11:25.06,Default,,0000,0000,0000,,Alipenda mstari huu: Dialogue: 0,0:11:25.08,0:11:27.27,Default,,0000,0000,0000,,"Ninaandika hii kwa sehemu kukuambia Dialogue: 0,0:11:27.29,0:11:30.60,Default,,0000,0000,0000,,ya kwamba kama umewahi kujiuliza\Nkile umekifanya katika maisha yako... Dialogue: 0,0:11:30.62,0:11:32.64,Default,,0000,0000,0000,,umekuwa neema ya Mungu kwangu, Dialogue: 0,0:11:32.67,0:11:35.83,Default,,0000,0000,0000,,muujiza, kitu ambacho ni zaidi \Nya muujiza." Dialogue: 0,0:11:37.38,0:11:43.02,Default,,0000,0000,0000,,Kitu kimoja kuhusu hii lugha,\Nupendo wake, subira yake, sauti yake, Dialogue: 0,0:11:43.04,0:11:45.50,Default,,0000,0000,0000,,iliamsha shauku ya Patrick katika kuandika. Dialogue: 0,0:11:46.29,0:11:49.39,Default,,0000,0000,0000,,Na alijaza daftari kwa daftari Dialogue: 0,0:11:49.42,0:11:52.73,Default,,0000,0000,0000,,na barua kwenda kwa binti yake. Dialogue: 0,0:11:52.75,0:11:55.68,Default,,0000,0000,0000,,katika barua hizi nzuri na imara, Dialogue: 0,0:11:55.71,0:12:01.68,Default,,0000,0000,0000,,alijiwazia yeye na binti yake\Nwakipanda mtumbwi katika mto Mississipi Dialogue: 0,0:12:01.71,0:12:04.52,Default,,0000,0000,0000,,Alijiwazia yeye na binti yake\Nwakipata vijito vya milimani Dialogue: 0,0:12:04.54,0:12:06.71,Default,,0000,0000,0000,,vikiwa na maji masafi bila kasoro. Dialogue: 0,0:12:08.04,0:12:10.08,Default,,0000,0000,0000,,Nilipomtazama Patrick akiandika, Dialogue: 0,0:12:11.25,0:12:13.39,Default,,0000,0000,0000,,Nilijiwazia mwenyewe, Dialogue: 0,0:12:13.42,0:12:15.48,Default,,0000,0000,0000,,na sasa ninawaulizeni nyote, Dialogue: 0,0:12:15.50,0:12:20.79,Default,,0000,0000,0000,,ni wangapi wenu mmewahi kuandika barua\Nkwa mtu unayehisi umemwangusha? Dialogue: 0,0:12:22.04,0:12:27.12,Default,,0000,0000,0000,,Ni rahisi sana\Nkuwaweka hao watu nje ya fikra zako. Dialogue: 0,0:12:28.08,0:12:32.73,Default,,0000,0000,0000,,Lakini Patrick alijitokeza kila siku,\Nakimkabili binti yake, Dialogue: 0,0:12:32.75,0:12:35.68,Default,,0000,0000,0000,,akijiwajibisha kwake, Dialogue: 0,0:12:35.71,0:12:39.42,Default,,0000,0000,0000,,neno kwa neno kwa umakini wa hali ya juu. Dialogue: 0,0:12:42.42,0:12:44.96,Default,,0000,0000,0000,,Ningependa katika maisha yangu binafsi Dialogue: 0,0:12:46.04,0:12:49.10,Default,,0000,0000,0000,,kujiweka katika hatari kwa namna hiyo. Dialogue: 0,0:12:49.12,0:12:52.75,Default,,0000,0000,0000,,Kwa sababu hatari hiyo inadhihirisha\Nnguvu za moyo wa mtu. Dialogue: 0,0:12:56.62,0:13:00.68,Default,,0000,0000,0000,,Ngoja nirudi hatua moja nyuma na niulize\Nswali ambalo linaleta wasiwasi. Dialogue: 0,0:13:00.71,0:13:04.42,Default,,0000,0000,0000,,Mimi ni nani kusimulia simulizi hii,\Nhii simulizi ya Patrick? Dialogue: 0,0:13:06.04,0:13:09.02,Default,,0000,0000,0000,,Patrick ndiye aliyeishi kwenye \Nmaumivu haya Dialogue: 0,0:13:09.04,0:13:13.21,Default,,0000,0000,0000,,na mimi sijawahi kukaa na njaa hata \Nkwa siku moja kwenye maisha yangu Dialogue: 0,0:13:15.25,0:13:17.02,Default,,0000,0000,0000,,Ninawaza sana kuhusu swali hili, Dialogue: 0,0:13:17.04,0:13:20.77,Default,,0000,0000,0000,,lakini ninachotaka kusema ni kuwa hii \Nsimulizi sio tu kuhusu Patrick. Dialogue: 0,0:13:20.79,0:13:22.31,Default,,0000,0000,0000,,Inatuhusu sisi, Dialogue: 0,0:13:22.33,0:13:24.83,Default,,0000,0000,0000,,ni kuhusu tofauti kati yetu. Dialogue: 0,0:13:25.67,0:13:27.08,Default,,0000,0000,0000,,Ulimwengu wa vingi Dialogue: 0,0:13:28.38,0:13:32.02,Default,,0000,0000,0000,,ambao Patrick na wazazi wake \Nna mababu zake Dialogue: 0,0:13:32.04,0:13:33.85,Default,,0000,0000,0000,,hawajawahi kuuona. Dialogue: 0,0:13:33.88,0:13:36.96,Default,,0000,0000,0000,,Katika simulizi hii, mimi ninawakilisha\Nhuo ulimwengu wa vingi. Dialogue: 0,0:13:37.79,0:13:41.60,Default,,0000,0000,0000,,Na katika kueleza simulizi hii\Nsikutaka kujificha mwenyewe. Dialogue: 0,0:13:41.62,0:13:44.29,Default,,0000,0000,0000,,Kuficha nguvu ambazo ninazo. Dialogue: 0,0:13:45.33,0:13:48.89,Default,,0000,0000,0000,,Katika kueleza simulizi hii,\Nninataka kuifichua nguvu hiyo Dialogue: 0,0:13:48.92,0:13:51.31,Default,,0000,0000,0000,,halafu kuuliza, Dialogue: 0,0:13:51.33,0:13:54.25,Default,,0000,0000,0000,,tunawezaje kuipunguza\Numbali kati yetu? Dialogue: 0,0:13:56.25,0:13:59.85,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma ni njia mojawapo ya kuipunguza\Nhiyo nafasi. Dialogue: 0,0:13:59.88,0:14:04.31,Default,,0000,0000,0000,,Kunatuma ulimwengu wa ukimya\Nambao tunaweza kuushiriki pamoja, Dialogue: 0,0:14:04.33,0:14:06.58,Default,,0000,0000,0000,,ambao tunaweza kuushiriki kwa usawa. Dialogue: 0,0:14:08.50,0:14:11.60,Default,,0000,0000,0000,,Inawezekana unajiuliza sasa kuwa\Nni nini kilitokea kwa Patrick. Dialogue: 0,0:14:11.62,0:14:13.33,Default,,0000,0000,0000,,Je kusoma kuliokoa maisha yake? Dialogue: 0,0:14:14.58,0:14:16.71,Default,,0000,0000,0000,,Kuliyaokoa na hakukuyaokoa. Dialogue: 0,0:14:17.88,0:14:20.77,Default,,0000,0000,0000,,Patrick alipotoka gerezani, Dialogue: 0,0:14:20.79,0:14:23.12,Default,,0000,0000,0000,,safari yake ilikuwa ya maumivu. Dialogue: 0,0:14:24.29,0:14:27.77,Default,,0000,0000,0000,,Waajiri hawakumkubali kwa sababu\Nya historia yake, Dialogue: 0,0:14:27.79,0:14:30.93,Default,,0000,0000,0000,,rafiki yake mpenzi, mama yake,\Nalifariki katika umri wa miaka 43 Dialogue: 0,0:14:30.96,0:14:33.43,Default,,0000,0000,0000,,kwa ugonjwa wa moyo na kisukari. Dialogue: 0,0:14:33.46,0:14:36.17,Default,,0000,0000,0000,,Alikuwa hana pa kuishi,\Namekuwa hana chakula. Dialogue: 0,0:14:38.25,0:14:42.79,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo watu wanasema mengi kuhusu kusoma\Nambayo kwangu ninahisi wanazidisha chumvi. Dialogue: 0,0:14:43.79,0:14:47.77,Default,,0000,0000,0000,,Uwezo wa kusoma haukumzuia yeye\Nasitengwe na jamii. Dialogue: 0,0:14:47.79,0:14:50.42,Default,,0000,0000,0000,,Hakukumzuia mama yake asifariki. Dialogue: 0,0:14:51.71,0:14:54.08,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo kusoma kunaweza kufanya nini? Dialogue: 0,0:14:55.38,0:14:59.33,Default,,0000,0000,0000,,Nina majibu machache ninapomalizia leo. Dialogue: 0,0:15:00.67,0:15:03.42,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma kulibadili utu wake wa ndani Dialogue: 0,0:15:05.08,0:15:08.14,Default,,0000,0000,0000,,kwa mambo yaliyofichika na uwezo wa\Nkuwaza kwa picha. Dialogue: 0,0:15:08.17,0:15:09.42,Default,,0000,0000,0000,,kwa uzuri. Dialogue: 0,0:15:10.29,0:15:14.62,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma kulimpa taswira zilizompa furaha: Dialogue: 0,0:15:15.42,0:15:20.98,Default,,0000,0000,0000,,milima, bahari, kulungu, theluji. Dialogue: 0,0:15:21.00,0:15:25.12,Default,,0000,0000,0000,,Maneno yenye ladha ya ulimwengu huru\Nna halisi. Dialogue: 0,0:15:27.62,0:15:31.14,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma kulimpa lugha kwa yale aliyopoteza. Dialogue: 0,0:15:31.17,0:15:35.81,Default,,0000,0000,0000,,Ni jinsi gani yalivyo mazuri haya maneno \Nkutoka kwa mshairi Derek Walcott? Dialogue: 0,0:15:35.83,0:15:38.06,Default,,0000,0000,0000,,Patrick alilikariri hili shairi. Dialogue: 0,0:15:38.08,0:15:40.18,Default,,0000,0000,0000,,"Siku ambazo nilizishikilia, Dialogue: 0,0:15:40.21,0:15:42.48,Default,,0000,0000,0000,,siku ambazo nilizipoteza, Dialogue: 0,0:15:42.50,0:15:45.73,Default,,0000,0000,0000,,siku ambazo zinakuwa kupitiliza,\Nkama mabinti, Dialogue: 0,0:15:45.75,0:15:47.58,Default,,0000,0000,0000,,mikono yangu inayoshikilia." Dialogue: 0,0:15:48.67,0:15:51.64,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma kulimfundisha ujasiri wake\Nmwenyewe. Dialogue: 0,0:15:51.67,0:15:54.98,Default,,0000,0000,0000,,Kumbuka kwamba aliendelea kusoma\NFrederick Douglass, Dialogue: 0,0:15:55.00,0:15:57.14,Default,,0000,0000,0000,,ijapokuwa ilikuwa ya kuumiza. Dialogue: 0,0:15:57.17,0:16:00.88,Default,,0000,0000,0000,,Aliendelea kuwa makini,\Nijapokuwa kuwa makini kunauma. Dialogue: 0,0:16:02.21,0:16:04.77,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma ni aina ya kutafakari, Dialogue: 0,0:16:04.79,0:16:08.85,Default,,0000,0000,0000,,ndio maana ni vigumu sana kusoma\Nkwa sababu tunataka kutafakari. Dialogue: 0,0:16:08.88,0:16:13.12,Default,,0000,0000,0000,,Na Patrick alichagua kutafakari,\Nbadala ya kutokutafakari. Dialogue: 0,0:16:16.00,0:16:19.96,Default,,0000,0000,0000,,Na mwishoni, kusoma kulimpa lugha\Nya kuongea na binti yake. Dialogue: 0,0:16:21.38,0:16:24.60,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma kulimpa shauku ya kutaka kuandika. Dialogue: 0,0:16:24.62,0:16:28.77,Default,,0000,0000,0000,,Muunganiko kati ya kusoma na\Nkuandika ni wenye nguvu sana. Dialogue: 0,0:16:28.79,0:16:30.85,Default,,0000,0000,0000,,Tunapoanza kusoma, Dialogue: 0,0:16:30.88,0:16:32.96,Default,,0000,0000,0000,,tunaanza kupata maneno. Dialogue: 0,0:16:33.96,0:16:38.60,Default,,0000,0000,0000,,Na alipata maneno ya kutafakari\Nwao wawili wakiwa pamoja. Dialogue: 0,0:16:38.62,0:16:40.33,Default,,0000,0000,0000,,Alipata maneno Dialogue: 0,0:16:41.96,0:16:44.21,Default,,0000,0000,0000,,ya kumwelezea ni namna gani anampenda. Dialogue: 0,0:16:46.04,0:16:49.98,Default,,0000,0000,0000,,Kusoma pia kulibadilisha\Nmahusiano baina yetu. Dialogue: 0,0:16:50.00,0:16:52.06,Default,,0000,0000,0000,,Kunatupa nyakati za kuwa karibu, Dialogue: 0,0:16:52.08,0:16:54.98,Default,,0000,0000,0000,,kuweza kuona zaidi ya mitazamo yetu. Dialogue: 0,0:16:55.00,0:16:57.68,Default,,0000,0000,0000,,Na kusoma kulichukua mahusiano ya\Nkutokuwa sawa Dialogue: 0,0:16:57.71,0:17:00.38,Default,,0000,0000,0000,,na kulitupa usawa wa muda mfupi. Dialogue: 0,0:17:02.12,0:17:05.06,Default,,0000,0000,0000,,Ukikutana na mtu kama msomaji, Dialogue: 0,0:17:05.08,0:17:07.06,Default,,0000,0000,0000,,unakutana naye kwa mara ya kwanza, Dialogue: 0,0:17:07.08,0:17:08.79,Default,,0000,0000,0000,,kwa upya kabisa. Dialogue: 0,0:17:09.88,0:17:13.08,Default,,0000,0000,0000,,Hakuna namna unaweza kufahamu mstari \Nanaoupenda sana ni upi. Dialogue: 0,0:17:14.46,0:17:17.67,Default,,0000,0000,0000,,Ni kumbukumbu zipi na huzuni zipi za \Nsiri alizonazo. Dialogue: 0,0:17:18.83,0:17:22.83,Default,,0000,0000,0000,,Na unakutana na sitara ya hali ya juu\Nya utu wake wa ndani. Dialogue: 0,0:17:23.67,0:17:27.10,Default,,0000,0000,0000,,Na halafu unaanza kushangaa,\N"Eti,utu wangu wa ndani umejengwa na nini? Dialogue: 0,0:17:27.12,0:17:30.38,Default,,0000,0000,0000,,Ni kitu gani nilichonacho cha thamani\Ncha kumshirikisha mwingine?" Dialogue: 0,0:17:33.00,0:17:34.33,Default,,0000,0000,0000,,Ninataka kufunga Dialogue: 0,0:17:36.21,0:17:40.50,Default,,0000,0000,0000,,kwa mistari yangu ninayoipenda\Nkutoka kwa barua za Patrick kwa bintiye. Dialogue: 0,0:17:41.33,0:17:44.10,Default,,0000,0000,0000,,"Mto una kivuli kwenye baadhi ya maeneo Dialogue: 0,0:17:44.12,0:17:47.39,Default,,0000,0000,0000,,lakini mwanga unaangaza\Nkupitia mianya ya miti... Dialogue: 0,0:17:47.42,0:17:50.98,Default,,0000,0000,0000,,Kwenye baadhi ya matawi\Nmuliberi nyingi zimening'inia. Dialogue: 0,0:17:51.00,0:17:54.46,Default,,0000,0000,0000,,Unanyoosha mkono wako\Nili uweze kuyachukua baadhi". Dialogue: 0,0:17:56.04,0:17:58.48,Default,,0000,0000,0000,,Na barua hii ya upendo, anapoandika, Dialogue: 0,0:17:58.50,0:18:02.85,Default,,0000,0000,0000,,"Fumba macho yako na usikilize\Nsauti ya maneno. Dialogue: 0,0:18:02.88,0:18:05.06,Default,,0000,0000,0000,,Ninafahamu shairi hili kwa moyo Dialogue: 0,0:18:05.08,0:18:07.92,Default,,0000,0000,0000,,na ningependa pia wewe ulifahamu." Dialogue: 0,0:18:09.38,0:18:11.18,Default,,0000,0000,0000,,Ninawashukuruni nyote. Dialogue: 0,0:18:11.21,0:18:14.50,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi)