1 00:00:00,917 --> 00:00:06,393 Ninataka kuzungumza namna kusoma kunavyoweza kubadilisha maisha yetu 2 00:00:06,417 --> 00:00:08,792 na kuhusu mipaka ya mabadiliko hayo 3 00:00:09,750 --> 00:00:14,018 Ninataka kuzungumza na wewe namna kusoma kunavyoweza kutupa ulimwengu wa ushirika 4 00:00:14,042 --> 00:00:16,750 wa muunganiko wenye nguvu wa kibinadamu 5 00:00:17,833 --> 00:00:21,393 pia namna ambavyo muunganiko huo ni sehemu tu mara zote 6 00:00:21,417 --> 00:00:26,500 Kusoma mwisho wa siku ni kitendo cha upweke na kisicho cha kawaida. 7 00:00:27,625 --> 00:00:30,476 Muandishi aliyebadilisha maisha yangu 8 00:00:30,500 --> 00:00:34,934 Ni mmarekani mweusi na mwandishi wa riwaya James Baldwin 9 00:00:34,958 --> 00:00:38,226 Wakati ninakuwa katika eneo la Magharibi mwa Michigan miaka ya 1980, 10 00:00:38,250 --> 00:00:42,167 hakukuwa na wamarekani wenye asili ya asia wengi wanaoandika kuhusu mabadiliko ya kijamii 11 00:00:43,292 --> 00:00:46,518 Na ndio maana nilimgeukia James Baldwin 12 00:00:46,542 --> 00:00:50,583 kama namna ya kuliziba hili ombwe, kama namna ya kuwamakini na rangi 13 00:00:51,958 --> 00:00:55,934 lakini haswa kwa sababu nilifahamu mimi sikuwa mmarekani mweusi, 14 00:00:55,958 --> 00:01:00,476 Pia nilisikia kupata changamoto na kuthibitishwa na maneno yake. 15 00:01:00,500 --> 00:01:02,625 Hasusani maneno haya: 16 00:01:03,458 --> 00:01:07,059 "Ni watu huria walio na mitazamo sahihi, 17 00:01:07,083 --> 00:01:09,042 lakini hawana misimamo halisi. 18 00:01:10,083 --> 00:01:14,018 pale ambapo vipande vipo chini na unawategemea kuleta matokeo, 19 00:01:14,042 --> 00:01:16,518 na huenda hawako hapo kwa namna fulani". 20 00:01:16,542 --> 00:01:19,351 Hawako hapo kwa namna fulani. 21 00:01:19,375 --> 00:01:21,726 Nikayachukua hayo maneno nikitafakari. 22 00:01:21,750 --> 00:01:23,458 Nijiweke wapi? 23 00:01:24,500 --> 00:01:26,518 Nilikwenda kwenye delta ya Mississippi, 24 00:01:26,542 --> 00:01:29,684 mojawapo ya maeneo masikini sana ya Marekani. 25 00:01:29,708 --> 00:01:32,601 Hii ni sehemu ambayo imejengwa na historia yenye nguvu. 26 00:01:32,625 --> 00:01:37,768 Katika mwaka wa 1960, Wamarekani weusi walijitoa maisha yao kupigania Elimu, 27 00:01:37,792 --> 00:01:39,500 kupigania haki ya kupiga kura. 28 00:01:40,625 --> 00:01:43,059 Nilitaka kuwa sehemu ya badiliko hilo, 29 00:01:43,083 --> 00:01:46,792 kuwasaidia vijana wadogo wamalize shule na kujiunga na vyuo. 30 00:01:48,250 --> 00:01:50,976 Nilipoenda kwenye Delta ya Mississipi, 31 00:01:51,000 --> 00:01:53,434 Palikuwa ni mahali duni bado, 32 00:01:53,458 --> 00:01:55,184 bado pametengwa, 33 00:01:55,208 --> 00:01:57,750 Bado panahitaji mabadiliko ya kasi. 34 00:01:58,958 --> 00:02:02,393 Shule yangu, pale nilipokuwa nasoma, 35 00:02:02,417 --> 00:02:06,726 haikuwa na maktaba, hakuna mshauri, 36 00:02:06,750 --> 00:02:09,726 lakini ilikuwa na afisa wa polisi. 37 00:02:09,750 --> 00:02:12,309 Nusu ya walimu walikuwa ni mbadala 38 00:02:12,333 --> 00:02:14,309 na wanafunzi walipoingia kwenye ugomvi, 39 00:02:14,333 --> 00:02:18,208 Shule iliwapeleka kwenye jela ya mahali hapo. 40 00:02:20,250 --> 00:02:23,226 Hii ndiyo shule nilipokutana na Patrick. 41 00:02:23,250 --> 00:02:28,184 Alikuwa na miaka 15 na alikamatwa mara mbili, alikuwa darasa la nane. 42 00:02:28,208 --> 00:02:30,684 Alikuwa ni mkimya na mndani, 43 00:02:30,708 --> 00:02:33,518 ni kama kila wakati alikuwa mwenye mawazo. 44 00:02:33,542 --> 00:02:36,333 Na alichukia kuona wengine wakipigana. 45 00:02:37,500 --> 00:02:41,309 Nilimuona mara moja akiruka kati ya mabinti wawili walipokuwa wakipigana 46 00:02:41,333 --> 00:02:44,042 Na akajikuta akidondoka na kuanguka chini. 47 00:02:45,375 --> 00:02:47,893 Patrick alikuwa na tatizo moja. 48 00:02:47,917 --> 00:02:49,708 Hakuwa akifika shuleni. 49 00:02:51,249 --> 00:02:53,726 Alisema kuwa shule wakati mwingine humfanya kuwa na msongo 50 00:02:53,750 --> 00:02:56,792 Sababu wanafunzi hupigana mara zote na walimu wanaondoka. 51 00:02:58,042 --> 00:03:03,500 Lakini pia, mama yake anafanya kazi mbili na huwa anachoka kuweza kumfanya aje shule. 52 00:03:04,417 --> 00:03:07,184 Hivyo nikafanya iwe kazi yangu kumfanya awe anakuja shule. 53 00:03:07,208 --> 00:03:11,268 Na sababu nilikuwa na wazimu na miaka 22 na mwenye bidii ya matumaini 54 00:03:11,292 --> 00:03:13,434 Njia yangu ilikuwa ni kwenda nyumbani kwao 55 00:03:13,458 --> 00:03:15,583 na kusema "Eti, kwanini hauji shuleni?" 56 00:03:16,542 --> 00:03:18,184 Na njia hii ilifanya kazi, 57 00:03:18,208 --> 00:03:20,643 akaanza kuja shuleni kila siku. 58 00:03:20,667 --> 00:03:23,059 Na akaanza kufanikiwa katika darasa langu. 59 00:03:23,083 --> 00:03:26,000 Aliandika mashairi, alisoma vitabu. 60 00:03:26,917 --> 00:03:29,208 Alikuja shuleni kila siku. 61 00:03:31,042 --> 00:03:32,518 takriban muda ule ule 62 00:03:32,542 --> 00:03:35,226 Nilipogundua namna ya kushirikiana na Patrick, 63 00:03:35,250 --> 00:03:37,458 Nilikwenda shule ya sheria Harvard. 64 00:03:39,583 --> 00:03:42,934 Nilikutana tena na swali hili, nijiweke wapi, 65 00:03:42,958 --> 00:03:44,667 niuweke wapi mwili wangu? 66 00:03:45,458 --> 00:03:48,101 Na nikawaza mwenyewe 67 00:03:48,125 --> 00:03:51,643 Kuwa Mississipi Delta ni mahali ambapo watu wenye fedha, 68 00:03:51,667 --> 00:03:53,559 watu wenye fursa, 69 00:03:53,583 --> 00:03:54,833 watu hao huondoka. 70 00:03:55,875 --> 00:03:57,309 Na watu wanaobakia 71 00:03:57,333 --> 00:03:59,833 ni watu ambao hawana fursa ya kuondoka. 72 00:04:00,833 --> 00:04:03,101 Sikutaka kuwa mtu anayeondoka. 73 00:04:03,125 --> 00:04:05,167 Nilitaka kuwa mtu anayebakia. 74 00:04:06,333 --> 00:04:09,268 Kwa upande mwingine, nilikuwa mpweke na mchovu. 75 00:04:09,292 --> 00:04:12,750 Na hivyo nilijishawishi mwenyewe kuwa ninaweza kufanya mabadiliko 76 00:04:14,125 --> 00:04:17,708 Kwa kiasi kikubwa kama ningekuwa na shahada yenye heshima ya sheria. 77 00:04:19,541 --> 00:04:20,791 Hivyo nikaondoka. 78 00:04:22,750 --> 00:04:24,351 Miaka mitatu baadaye, 79 00:04:24,375 --> 00:04:26,768 Nilipokaribia kuhitimu shule ya sheria, 80 00:04:26,792 --> 00:04:28,518 rafiki yangu alinipigia simu 81 00:04:28,542 --> 00:04:33,458 na kuniambia kuwa Patrick amepigana na kuua mtu. 82 00:04:35,333 --> 00:04:37,393 Nilitaharuki. 83 00:04:37,417 --> 00:04:39,851 Sehemu ya mimi haikuamini, 84 00:04:39,875 --> 00:04:42,542 na sehemu ya mimi pia iliamini kuwa ni kweli. 85 00:04:43,583 --> 00:04:45,583 Nilisafiri kwenda kumuona Patrick. 86 00:04:46,750 --> 00:04:49,458 Nilimtembelea gerezani. 87 00:04:50,542 --> 00:04:54,184 Na aliniambia kuwa ilikuwa kweli. 88 00:04:54,208 --> 00:04:56,601 Ya kwamba ameua mtu. 89 00:04:56,625 --> 00:04:58,875 Na asingependa kuzungumzia suala hilo. 90 00:04:59,833 --> 00:05:01,851 Nilimuuliza nini kiliendelea kuhusu shule 91 00:05:01,875 --> 00:05:06,018 na akasema aliacha shule mwaka mooja baada ya mimi kuondoka. 92 00:05:06,042 --> 00:05:08,684 Na alitaka kuniambia kuhusu kitu kingine 93 00:05:08,708 --> 00:05:11,976 Alitazama chini akasema ya kwamba amepata mtoto wa kike 94 00:05:12,000 --> 00:05:13,768 ambaye ndiye kwanza amezaliwa. 95 00:05:13,792 --> 00:05:16,375 Na anahisi kuwa amemuangusha binti yake. 96 00:05:18,625 --> 00:05:22,000 Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mazungumzo yetu yalikuwa ya haraka na mabaya. 97 00:05:23,417 --> 00:05:28,476 Nilipotoka nje ya gereza, sauti ndani yangu iliniambia, 98 00:05:28,500 --> 00:05:29,768 "Rudi. 99 00:05:29,792 --> 00:05:33,083 Usiporudi sasa, hutarudi kamwe". 100 00:05:36,292 --> 00:05:39,875 Hivyo nikahitimu shule ya sheria na nikarudi. 101 00:05:40,833 --> 00:05:42,518 Nikarudi kumuona Patrick, 102 00:05:42,542 --> 00:05:45,500 Nikarudi kuona kama ninaweza kumsaidia na kesi yake ya sheria. 103 00:05:46,917 --> 00:05:50,268 Muda huu, nilipomuona kwa mara ya pili, 104 00:05:50,292 --> 00:05:52,559 Nilidhani nina hili wazo zuri, nikamwambia, 105 00:05:52,583 --> 00:05:56,184 "Hey, Patrick, kwanini usiandike barua kwa binti yako, 106 00:05:56,208 --> 00:05:59,976 ili uweze kumuweka katika fikra zako?" 107 00:06:00,000 --> 00:06:03,684 Nikampatia kalamu na kipande cha karatasi, 108 00:06:03,708 --> 00:06:05,333 na akaanza kuandika. 109 00:06:06,542 --> 00:06:09,351 Lakini nilipoiona karatasi aliyonipatia, 110 00:06:09,375 --> 00:06:10,708 Nilipigwa na butwaa. 111 00:06:13,000 --> 00:06:15,101 Sikuutambua mwandiko wake, 112 00:06:15,125 --> 00:06:17,958 alikuwa amefanya makosa machache ya matamshi. 113 00:06:19,167 --> 00:06:21,851 na nikawaza mwenyewe kama mwalimu, 114 00:06:21,875 --> 00:06:25,351 Ninafahamu ya kuwa mwanafunzi anaweza kufanya vizuri kwa kasi 115 00:06:25,375 --> 00:06:28,434 Kwa muda mfupi sana, 116 00:06:28,458 --> 00:06:32,125 lakini sikuwahi kuwaza kuwa mwanafunzi anaweza kurudi nyuma kwa kasi. 117 00:06:34,375 --> 00:06:36,268 kilichoniumiza zaidi, 118 00:06:36,292 --> 00:06:39,476 ni kuona kile alichokiandika kwa binti yake. 119 00:06:39,500 --> 00:06:40,893 aliandika, 120 00:06:40,917 --> 00:06:45,208 "Ninasikitika kwa makosa yangu, ninasikitika kutokuwa pamoja nawe." 121 00:06:46,458 --> 00:06:49,292 Na hiki ndicho alichojisikia anataka kusema naye. 122 00:06:50,250 --> 00:06:54,559 Nikajiuliza ni namna gani ninaweza kumshawishi kuwa anaweza kumwambia zaidi, 123 00:06:54,583 --> 00:06:58,000 ile sehemu yake ambayo hahitaji kuomba radhi kwayo. 124 00:06:58,958 --> 00:07:00,226 Nilitaka yeye ajisikie 125 00:07:00,250 --> 00:07:04,208 kuwa anakitu cha thamani kumshirikisha binti yake. 126 00:07:05,917 --> 00:07:09,101 Kwa kila siku kwa miezi saba iliyofuatia, 127 00:07:09,125 --> 00:07:11,809 Nilimtembelea na kumpelekea vitabu. 128 00:07:11,833 --> 00:07:15,684 Mkoba wangu uligeuka kuwa maktaba ndogo. 129 00:07:15,708 --> 00:07:17,768 Nilimpelekea James Baldwin, 130 00:07:17,792 --> 00:07:22,684 Nilipeleka Walt Whitman, C.S.Lewis. 131 00:07:22,708 --> 00:07:27,518 Nilileta vitabu vya mwongozo wa miti, wa ndege, 132 00:07:27,542 --> 00:07:30,750 na kitabu alichotokea kukipenda zaidi, kamusi. 133 00:07:31,667 --> 00:07:33,351 Kwa baadhi ya siku, 134 00:07:33,375 --> 00:07:37,167 tulikaa kimya kwa masaa, wote wawili tukisoma. 135 00:07:38,083 --> 00:07:39,934 Na siku nyingine, 136 00:07:39,958 --> 00:07:43,476 tulisoma pamoja, tulisoma mashairi. 137 00:07:43,500 --> 00:07:47,393 tulianza kwa kusoma haikus, mamia ya haikus, 138 00:07:47,417 --> 00:07:50,309 ni kito rahisi na danganyifu. 139 00:07:50,333 --> 00:07:53,143 Na ningemuuliza, "Nishirikishe haiku zako unazozipenda". 140 00:07:53,167 --> 00:07:56,226 Na baadhi yake ni za kufurahisha sana. 141 00:07:56,250 --> 00:07:58,101 Kuna hii ya Issa: 142 00:07:58,125 --> 00:08:01,833 "Usijali, buibui, ninaweka nyumba kikawaida." 143 00:08:02,750 --> 00:08:07,292 Na hii: "Nimelala nusu ya siku, na hakuna aliyeniadhibu!" 144 00:08:08,667 --> 00:08:13,101 Na hii nyingine ya kuvutia, inayohusu siku ya kwanza barafu ilipodondoka, 145 00:08:13,125 --> 00:08:17,583 "Kulungu wakilamba baridi ya kwanza kutoka kwenye koti la kila mmoja wao." 146 00:08:19,250 --> 00:08:22,268 Kuna kitu cha ajabu na cha kuvutia 147 00:08:22,292 --> 00:08:24,934 kuhusu namna shairi linavyoonekana. 148 00:08:24,958 --> 00:08:29,583 Nafasi ya shairi ni muhimu kama maneno yenyewe. 149 00:08:31,375 --> 00:08:33,893 Tunasoma shairi hili lililoandikwa na W.S.Merwin, 150 00:08:33,917 --> 00:08:38,143 ambalo aliliandika baada ya kumuona mkewe akifanya kazi kwenye bustani 151 00:08:38,167 --> 00:08:42,042 na akakumbuka kuwa wataishi maisha yao yote yaliyobaki wakiwa pamoja. 152 00:08:43,167 --> 00:08:45,518 "Wacha nifikiri kuwa tutakuja tena 153 00:08:45,542 --> 00:08:48,934 tutakapotaka na itakuwa wakati wa masika 154 00:08:48,958 --> 00:08:52,143 hatutakuwa na umri mkubwa kuliko tulivyowahi kuwa 155 00:08:52,167 --> 00:08:56,101 na majonzi yatakuwa mepesi kama mawingu ya mapema 156 00:08:56,125 --> 00:08:59,893 ambayo kwayo asubuhi huja yenyewe taratibu" 157 00:08:59,917 --> 00:09:03,309 Nikamuuliza Patrick mstari alioupenda zaidi ni upi, na akasema 158 00:09:03,333 --> 00:09:06,875 "Hatutakuwa na umri mkubwa kuliko tulivyokuwa." 159 00:09:08,375 --> 00:09:12,809 Alisema inamkumbusha mahali ambapo muda husimama, 160 00:09:12,833 --> 00:09:15,768 pale ambapo muda haumaanishi kitu chochote. 161 00:09:15,792 --> 00:09:17,851 Na nikamuuliza kama amewahi kuwa na mahali pa jinsi hiyo. 162 00:09:17,875 --> 00:09:20,268 pale ambapo muda hudumu milele. 163 00:09:20,292 --> 00:09:21,958 Na akasema, "Mama yangu". 164 00:09:23,875 --> 00:09:28,184 Na pale unaposoma shairi pamoja na mtu mwingine, 165 00:09:28,208 --> 00:09:30,083 shairi hubadilika katika maana. 166 00:09:31,333 --> 00:09:36,000 Kwa sababu huwa la kibinafsi kwa mtu huyo, huwa la kibinafsi kwako. 167 00:09:37,500 --> 00:09:40,184 Halafu tulisoma vitabu, tulisoma vitabu vingi sana, 168 00:09:40,208 --> 00:09:43,351 tulisoma kumbukumbu za Frederick Douglass, 169 00:09:43,375 --> 00:09:46,976 Mtumwa wa Marekani aliyejifunza mwenyewe kusoma na kuandika 170 00:09:47,000 --> 00:09:50,333 na aliyetoroka na kuwa huru sababu ya kuelimika kwake. 171 00:09:51,875 --> 00:09:54,518 Nimekua nikimfikiria Frederick Douglass kama shujaa 172 00:09:54,542 --> 00:09:57,750 na niliiona hii simulizi kama iliyojaa matumaini na yenye kuinua 173 00:09:58,917 --> 00:10:01,750 Lakini kitabu hiki kilimuweka Patrick katika hofu. 174 00:10:02,875 --> 00:10:07,934 Alibakia katika simulizi aliyoielezea Douglass jinsi ambavyo, katika Christmas, 175 00:10:07,958 --> 00:10:11,059 Mabwana waliwapa watumwa jini(pombe kali) 176 00:10:11,083 --> 00:10:14,559 kama namna ya kuwaaminisha kuwa hawawezi kuumudu uhuru. 177 00:10:14,583 --> 00:10:17,375 Kwa sababu watumwa waliweweseka katika mashamba. 178 00:10:19,500 --> 00:10:21,500 Patrick alisema anajifananisha na hili. 179 00:10:22,333 --> 00:10:25,809 Alisema kuwa kuna watu gerezani ambao, kama watumwa, 180 00:10:25,833 --> 00:10:28,059 hawataki kuwaza juu ya hali zao, 181 00:10:28,083 --> 00:10:29,893 kwa sababu inawaumiza sana. 182 00:10:29,917 --> 00:10:32,101 Inaumiza sana kuwaza mambo ya nyuma, 183 00:10:32,125 --> 00:10:35,458 inaumiza sana kuwaza kuhusu umbali gani tunapaswa kwenda. 184 00:10:36,958 --> 00:10:39,851 Mstari alioupenda sana ulikuwa huu: 185 00:10:39,875 --> 00:10:43,476 "Chochote kile, bila kujali chochote, kujiondoa katika kuwaza! 186 00:10:43,500 --> 00:10:48,542 Ilikuwa ni huku kuwaza kusiko koma kuhusu hali yangu ndiko kunako kipa mateso." 187 00:10:49,958 --> 00:10:53,917 Patrick alisema Douglass alikuwa jasiri kuandika, ili aendelee kuwaza. 188 00:10:55,083 --> 00:11:00,643 Lakini Patrick hakufahamu kuwa alionekana kufanana sana na Douglass kwangu. 189 00:11:00,667 --> 00:11:04,417 Namna alivyoendelea kusoma, ijapokuwa ilimuweka katika hofu. 190 00:11:05,250 --> 00:11:08,309 Alimaliza kitabu kabla yangu, 191 00:11:08,333 --> 00:11:12,042 akisoma katika ngazi za zege zisizo na taa. 192 00:11:13,583 --> 00:11:16,309 Halafu tukaendelea kusoma mojawapo ya vitabu ninavyovipenda, 193 00:11:16,333 --> 00:11:18,518 Cha Marilynne Robinson's "Gilead," 194 00:11:18,542 --> 00:11:22,684 ambayo ni barua endelevu kutoka kwa baba kwenda kwa mwanae. 195 00:11:22,708 --> 00:11:25,059 Alipenda mstari huu: 196 00:11:25,083 --> 00:11:27,268 "Ninaandika hii kwa sehemu kukuambia 197 00:11:27,292 --> 00:11:30,601 ya kwamba kama umewahi kujiuliza kile umekifanya katika maisha yako... 198 00:11:30,625 --> 00:11:32,643 umekuwa neema ya Mungu kwangu, 199 00:11:32,667 --> 00:11:35,833 muujiza, kitu ambacho ni zaidi ya muujiza." 200 00:11:37,375 --> 00:11:43,018 Kitu kimoja kuhusu hii lugha, upendo wake, subira yake, sauti yake, 201 00:11:43,042 --> 00:11:45,500 iliamsha shauku ya Patrick katika kuandika. 202 00:11:46,292 --> 00:11:49,393 Na alijaza daftari kwa daftari 203 00:11:49,417 --> 00:11:52,726 na barua kwenda kwa binti yake. 204 00:11:52,750 --> 00:11:55,684 katika barua hizi nzuri na imara, 205 00:11:55,708 --> 00:12:01,684 alijiwazia yeye na binti yake wakipanda mtumbwi katika mto Mississipi 206 00:12:01,708 --> 00:12:04,518 Alijiwazia yeye na binti yake wakipata vijito vya milimani 207 00:12:04,542 --> 00:12:06,708 vikiwa na maji masafi bila kasoro. 208 00:12:08,042 --> 00:12:10,083 Nilipomtazama Patrick akiandika, 209 00:12:11,250 --> 00:12:13,393 Nilijiwazia mwenyewe, 210 00:12:13,417 --> 00:12:15,476 na sasa ninawaulizeni nyote, 211 00:12:15,500 --> 00:12:20,792 ni wangapi wenu mmewahi kuandika barua kwa mtu unayehisi umemwangusha? 212 00:12:22,042 --> 00:12:27,125 Ni rahisi sana kuwaweka hao watu nje ya fikra zako. 213 00:12:28,083 --> 00:12:32,726 Lakini Patrick alijitokeza kila siku, akimkabili binti yake, 214 00:12:32,750 --> 00:12:35,684 akijiwajibisha kwake, 215 00:12:35,708 --> 00:12:39,417 neno kwa neno kwa umakini wa hali ya juu. 216 00:12:42,417 --> 00:12:44,958 Ningependa katika maisha yangu binafsi 217 00:12:46,042 --> 00:12:49,101 kujiweka katika hatari kwa namna hiyo. 218 00:12:49,125 --> 00:12:52,750 Kwa sababu hatari hiyo inadhihirisha nguvu za moyo wa mtu. 219 00:12:56,625 --> 00:13:00,684 Ngoja nirudi hatua moja nyuma na niulize swali ambalo linaleta wasiwasi. 220 00:13:00,708 --> 00:13:04,417 Mimi ni nani kusimulia simulizi hii, hii simulizi ya Patrick? 221 00:13:06,042 --> 00:13:09,018 Patrick ndiye aliyeishi kwenye maumivu haya 222 00:13:09,042 --> 00:13:13,208 na mimi sijawahi kukaa na njaa hata kwa siku moja kwenye maisha yangu 223 00:13:15,250 --> 00:13:17,018 Ninawaza sana kuhusu swali hili, 224 00:13:17,042 --> 00:13:20,768 lakini ninachotaka kusema ni kuwa hii simulizi sio tu kuhusu Patrick. 225 00:13:20,792 --> 00:13:22,309 Inatuhusu sisi, 226 00:13:22,333 --> 00:13:24,833 ni kuhusu tofauti kati yetu. 227 00:13:25,667 --> 00:13:27,083 Ulimwengu wa vingi 228 00:13:28,375 --> 00:13:32,018 ambao Patrick na wazazi wake na mababu zake 229 00:13:32,042 --> 00:13:33,851 hawajawahi kuuona. 230 00:13:33,875 --> 00:13:36,958 Katika simulizi hii, mimi ninawakilisha huo ulimwengu wa vingi. 231 00:13:37,792 --> 00:13:41,601 Na katika kueleza simulizi hii sikutaka kujificha mwenyewe. 232 00:13:41,625 --> 00:13:44,292 Kuficha nguvu ambazo ninazo. 233 00:13:45,333 --> 00:13:48,893 Katika kueleza simulizi hii, ninataka kuifichua nguvu hiyo 234 00:13:48,917 --> 00:13:51,309 halafu kuuliza, 235 00:13:51,333 --> 00:13:54,250 tunawezaje kuipunguza umbali kati yetu? 236 00:13:56,250 --> 00:13:59,851 Kusoma ni njia mojawapo ya kuipunguza hiyo nafasi. 237 00:13:59,875 --> 00:14:04,309 Kunatuma ulimwengu wa ukimya ambao tunaweza kuushiriki pamoja, 238 00:14:04,333 --> 00:14:06,583 ambao tunaweza kuushiriki kwa usawa. 239 00:14:08,500 --> 00:14:11,601 Inawezekana unajiuliza sasa kuwa ni nini kilitokea kwa Patrick. 240 00:14:11,625 --> 00:14:13,333 Je kusoma kuliokoa maisha yake? 241 00:14:14,583 --> 00:14:16,708 Kuliyaokoa na hakukuyaokoa. 242 00:14:17,875 --> 00:14:20,768 Patrick alipotoka gerezani, 243 00:14:20,792 --> 00:14:23,125 safari yake ilikuwa ya maumivu. 244 00:14:24,292 --> 00:14:27,768 Waajiri hawakumkubali kwa sababu ya historia yake, 245 00:14:27,792 --> 00:14:30,934 rafiki yake mpenzi, mama yake, alifariki katika umri wa miaka 43 246 00:14:30,958 --> 00:14:33,434 kwa ugonjwa wa moyo na kisukari. 247 00:14:33,458 --> 00:14:36,167 Alikuwa hana pa kuishi, amekuwa hana chakula. 248 00:14:38,250 --> 00:14:42,792 Kwa hiyo watu wanasema mengi kuhusu kusoma ambayo kwangu ninahisi wanazidisha chumvi. 249 00:14:43,792 --> 00:14:47,768 Uwezo wa kusoma haukumzuia yeye asitengwe na jamii. 250 00:14:47,792 --> 00:14:50,417 Hakukumzuia mama yake asifariki. 251 00:14:51,708 --> 00:14:54,083 Kwa hiyo kusoma kunaweza kufanya nini? 252 00:14:55,375 --> 00:14:59,333 Nina majibu machache ninapomalizia leo. 253 00:15:00,667 --> 00:15:03,417 Kusoma kulibadili utu wake wa ndani 254 00:15:05,083 --> 00:15:08,143 kwa mambo yaliyofichika na uwezo wa kuwaza kwa picha. 255 00:15:08,167 --> 00:15:09,417 kwa uzuri. 256 00:15:10,292 --> 00:15:14,625 Kusoma kulimpa taswira zilizompa furaha: 257 00:15:15,417 --> 00:15:20,976 milima, bahari, kulungu, theluji. 258 00:15:21,000 --> 00:15:25,125 Maneno yenye ladha ya ulimwengu huru na halisi. 259 00:15:27,625 --> 00:15:31,143 Kusoma kulimpa lugha kwa yale aliyopoteza. 260 00:15:31,167 --> 00:15:35,809 Ni jinsi gani yalivyo mazuri haya maneno kutoka kwa mshairi Derek Walcott? 261 00:15:35,833 --> 00:15:38,059 Patrick alilikariri hili shairi. 262 00:15:38,083 --> 00:15:40,184 "Siku ambazo nilizishikilia, 263 00:15:40,208 --> 00:15:42,476 siku ambazo nilizipoteza, 264 00:15:42,500 --> 00:15:45,726 siku ambazo zinakuwa kupitiliza, kama mabinti, 265 00:15:45,750 --> 00:15:47,583 mikono yangu inayoshikilia." 266 00:15:48,667 --> 00:15:51,643 Kusoma kulimfundisha ujasiri wake mwenyewe. 267 00:15:51,667 --> 00:15:54,976 Kumbuka kwamba aliendelea kusoma Frederick Douglass, 268 00:15:55,000 --> 00:15:57,143 ijapokuwa ilikuwa ya kuumiza. 269 00:15:57,167 --> 00:16:00,875 Aliendelea kuwa makini, ijapokuwa kuwa makini kunauma. 270 00:16:02,208 --> 00:16:04,768 Kusoma ni aina ya kutafakari, 271 00:16:04,792 --> 00:16:08,851 ndio maana ni vigumu sana kusoma kwa sababu tunataka kutafakari. 272 00:16:08,875 --> 00:16:13,125 Na Patrick alichagua kutafakari, badala ya kutokutafakari. 273 00:16:16,000 --> 00:16:19,958 Na mwishoni, kusoma kulimpa lugha ya kuongea na binti yake. 274 00:16:21,375 --> 00:16:24,601 Kusoma kulimpa shauku ya kutaka kuandika. 275 00:16:24,625 --> 00:16:28,768 Muunganiko kati ya kusoma na kuandika ni wenye nguvu sana. 276 00:16:28,792 --> 00:16:30,851 Tunapoanza kusoma, 277 00:16:30,875 --> 00:16:32,958 tunaanza kupata maneno. 278 00:16:33,958 --> 00:16:38,601 Na alipata maneno ya kutafakari wao wawili wakiwa pamoja. 279 00:16:38,625 --> 00:16:40,333 Alipata maneno 280 00:16:41,958 --> 00:16:44,208 ya kumwelezea ni namna gani anampenda. 281 00:16:46,042 --> 00:16:49,976 Kusoma pia kulibadilisha mahusiano baina yetu. 282 00:16:50,000 --> 00:16:52,059 Kunatupa nyakati za kuwa karibu, 283 00:16:52,083 --> 00:16:54,976 kuweza kuona zaidi ya mitazamo yetu. 284 00:16:55,000 --> 00:16:57,684 Na kusoma kulichukua mahusiano ya kutokuwa sawa 285 00:16:57,708 --> 00:17:00,375 na kulitupa usawa wa muda mfupi. 286 00:17:02,125 --> 00:17:05,059 Ukikutana na mtu kama msomaji, 287 00:17:05,083 --> 00:17:07,059 unakutana naye kwa mara ya kwanza, 288 00:17:07,083 --> 00:17:08,791 kwa upya kabisa. 289 00:17:09,875 --> 00:17:13,083 Hakuna namna unaweza kufahamu mstari anaoupenda sana ni upi. 290 00:17:14,458 --> 00:17:17,666 Ni kumbukumbu zipi na huzuni zipi za siri alizonazo. 291 00:17:18,833 --> 00:17:22,833 Na unakutana na sitara ya hali ya juu ya utu wake wa ndani. 292 00:17:23,666 --> 00:17:27,101 Na halafu unaanza kushangaa, "Eti,utu wangu wa ndani umejengwa na nini? 293 00:17:27,125 --> 00:17:30,375 Ni kitu gani nilichonacho cha thamani cha kumshirikisha mwingine?" 294 00:17:33,000 --> 00:17:34,333 Ninataka kufunga 295 00:17:36,208 --> 00:17:40,500 kwa mistari yangu ninayoipenda kutoka kwa barua za Patrick kwa bintiye. 296 00:17:41,333 --> 00:17:44,101 "Mto una kivuli kwenye baadhi ya maeneo 297 00:17:44,125 --> 00:17:47,393 lakini mwanga unaangaza kupitia mianya ya miti... 298 00:17:47,417 --> 00:17:50,976 Kwenye baadhi ya matawi muliberi nyingi zimening'inia. 299 00:17:51,000 --> 00:17:54,458 Unanyoosha mkono wako ili uweze kuyachukua baadhi". 300 00:17:56,042 --> 00:17:58,476 Na barua hii ya upendo, anapoandika, 301 00:17:58,500 --> 00:18:02,851 "Fumba macho yako na usikilize sauti ya maneno. 302 00:18:02,875 --> 00:18:05,059 Ninafahamu shairi hili kwa moyo 303 00:18:05,083 --> 00:18:07,917 na ningependa pia wewe ulifahamu." 304 00:18:09,375 --> 00:18:11,184 Ninawashukuruni nyote. 305 00:18:11,208 --> 00:18:14,500 (Makofi)