Kuna swali tunafaa
kujiuliza:
Kipi hakikwenda sawa?
Si tu kuhusiana na janga
lakini na uraia wetu.
Nini kilichotuletea huu mgawano
na chuki kisiasa ?
Kwa miongo ya karibu,
utengano baina ya washindi na
walioshindwa umezidi,
na kutia sumu siasa yetu,
kututenganisha.
Mgawanyiko huu unahusu udhalimu kwa kiasi fulani.
Lakini pia mtazamo
kuhusu kushinda na kushindwa
ambayo huja nayo.
Walio kileleni
wanaamini ufanisi wao
ni juhudi yao,
kipimo cha ustahili wao,
na walioanguka
hawana wa kulaumu bali nafsi zao.
Mtazamo huu wa mafanikio
unatokana na
kanuni inayovutia,
kwamba kila mtu ana nafasi sawa,
na washindi wanstahili ushindi wao.
Huu ndio kiini cha
wazo la ustahi.
Kwa vitendo,bila shaka, tuna upungufu.
Si kila mtu ana nafasi sawa kuinuka.
Watoto wazaliwao kwa jamii maskini
hukua kwa umaskini,
Wazazi tajiri wana uwezo
kupitisha manufaa kwa wototo wao.
Kwa mfano, katika vyuo bora zaidi,
idadi wengi wametoka
familia tajiri sana
kushinda nusu ya chini ya nchi
ukijumuishwa.
Shida sio tu
kushindwa kufikia
mawazo ya ustahi
tunavyopiga mbiu.
Wazo lenyewe lina kasoro.
Ina dosari.
Ustahi una madhara
kwa manufaa kwa watu wote.
unaleta kiburi kwa washindi
na kufedhehesha waliopeteza.
huchochea washindi
kujiona bora zaidi
na kusahau nasibu na uenyemali
iliyowasaidia kupata mafanikio.
Na kupelekea kuonea
wasiobahatika,
na wasio na wasifi kama wao.
Huu hujalisha kisiasa.
Mojawapo ya chanzo kuu
cha upinzani maarufu
miongoni mwa wafanyikazi
ni dhana ya wasomi kuwadharau.
Ni lawama halali.
Ingawaje utandawazi
umezidi kukosesha usawa
na mshahara usioongezeka,
watetezi wake walishauri
wafanyikazi.
"Kama unataka kushindana na kushinada
karika uchumi wa kimataifa,
enda chuo"
"Mapato yako yanalingana na masomo yako"
"Utafaulu ukijaribu"
Hawa wasomi hawazingatii tusi
fiche kwenye huu ushauri.
Usipoenda chuo,
usiponawiri kwenye huu uchumi mpya,
basi shida ni lako.
Huo ndio sababu.
Si ajabu wafanyikzi wengi
waligeukia ustahi wa wasomi.
Tunafaa tufanye nini ?
Tunafaa kuwazia kipengee tatu
cha uraia wetu.
Nafasi ya chuo,
usharifu wa kazi
na maana ya ufanisi.
Tunafaa kuwazia tena
nafasi ya vyuo
kama suluhishi la fursa.
Kwa watu kama sisi
tunaotangamana na wasomi,
ni rahisi kusahau hakika sahili:
Watu wengi hawana sahada
la miaka minee chuoni.
Kwa hakika, thuluthi mbili
Wamerikani hawana.
Kwa hivyo ni upumbavu kujenga uchumi
inayoshurutisha shahada ya chuo
ili kuwepo na maisha sharifu.
Kuhimiza watu kwenda chuo
ni wazo mzuri.
Upanuzi wa ufikavu
kwa wasiojiweza
ni bora zaidi
Lakini huu si suluhu la kutokuwa na usawe.
Haina faida kuandaa watu
kupambania ustahi
ni kuboresha maisha
tunafaa kuzingatia
kwa watu hawana diploma
lakini wenye mchango muhimu
katika jamii.
Tunafaa kufufua usharifu wa kazi.
na kuiweka kati kwenye siasa zetu
Tunafaa kukumbuaka kazi
sio tu kupata riziki,
ila pia ni kuchangia
uzuri wa pamoja
na kushindania utambuzi wakati huo
Robert F. Kennedy alisema vyema
nusu karne iliyopita
Ushirika,jumuiya, uzalendo shirika
Malengo haya hayaji
kwa ununuzi na ulaji
wa bidhaa pamoja.
Zinatokana na ajira adhama,
kwa mshahara lifaalo.
Ni aina ya ajira
inatuwezesha kusema,
"Nilichangia ujuenzi wa huu nchi.
Mimi ni mshiriki
wa ubia umma zake kubwa"
Huu hisia wa uraia
Haipo pakubwa
katika maisha ya umma siku hizi
Mara mingi tunadhania kipato cha watu
ni kipimo cha mchango wao
kwa mazuri kwa wote
Huu ni kosa.
Martin Luther King Jr alielezea mbona.
Kwa kutafakari mgomo
wa wasafishaji mazingira
uko Memphis, Tennessee,
muda mfupi kabla hajawawa,
King alisema,
"Mtu anyezoa takataka,
kwa uchambuzi wa kina,
ana umuhimu sawa na daktari,
asipofanya kazi yake,
magonjwa yanakithiri.
Kazi zote zina usharifu"
Janga tunao leo unadhihirisha huu.
Unaonyesha tunavyotegemea sana
wafanykazi kunapuuza wakati mwingi.
Wafanyikazi wa upelekaji,
wafanyikazi wa matengenezo,
karani wa duka,
wafanyikazi wa bohari,
madereva wa lori,
wauguzi wasaidizi,
watunza watoto,
wahuduma wa afya nyumbani.
Wafanyikazi hawa kipato
ni duni na wanapuuziliwa.
Lakini sasa, tunawaona muhimu.
Huu ni fursa wa mjadala wa umma
kuhusu kuinua mapato yao na
kuwatambua
kulingana na umuhimu wa
kazi wanayofanya.
Ni wakati wa kubadili
maadili, hata roho,
kuulizia kiburi cha ustahi.
Kimaadili,nastahiki talanta
zinazoniwezesha kunawiri ?
Ni uwezo wangu
kua naishi katika jamii
inayothamini talanta
ninazo ?
Ama ni bahati ?
Kusisitiza ufanisi ni haki yangu
huleta ugumu kujiweka
kwa niaba ya watu wengine.
Kuthamini nafasi ya baraka maishani
yanaweza leta unyenyekevu flani.
Kama si kwa ajali ya uzazi,
ama neema ya mungu
ama fimbo la hatima,
ningekua nani.
Huu moyo wa unyenyekevu
ndio fadhila ya uraia tunahitaji sasa.
Ndio mwanzo wa kurudi
toka maadili makali ya ufanisi
unaotutenganisha.
Inatuelekeza kupita ubabe wa ustahi
hadi maisha ya ukarimu zaidi ya umma