Return to Video

Kama enyi watu wazima hamtaokoa dunia, tutaiokoa sisi.

  • 0:01 - 0:03
    Mpendwa Abuelita,
  • 0:03 - 0:05
    Najua sijakuwepo nyumbani kwa muda.
  • 0:05 - 0:08
    Uko nyumbani kwetu pazuri Mexico,
  • 0:08 - 0:10
    nami niko hapa Marekani,
  • 0:10 - 0:11
    nikipigania maisha
    yetu ya baadaye.
  • 0:12 - 0:14
    Pengine unanyunyuzia ua waridi maji,
  • 0:14 - 0:16
    ukitunza fyulisi
  • 0:16 - 0:19
    na kuhakikisha kua kasa wako wameshiba.
  • 0:19 - 0:22
    Hiyo ni mojawapo ya vitu,
    navikumbuka sana kuhusu nyumbani --
  • 0:22 - 0:24
    kupoteza muda na maua
  • 0:24 - 0:27
    ukinihadithia kuhusu utoto wako
  • 0:28 - 0:32
    Unavyojua,
    tumeishi New York City tangu 2015
  • 0:32 - 0:36
    Lakini maisha yamebadilika mno
    kwa mwaka uliopita.
  • 0:36 - 0:40
    Hapo mwanzoni, New York
    ilikua ni sehemu ya makumbusho
  • 0:40 - 0:41
    na hifadhi
  • 0:41 - 0:42
    na shule na marafiki.
  • 0:43 - 0:45
    Saaa hii ni kama mtandao
  • 0:45 - 0:48
    unaoniunganisha na watu wengine
  • 0:48 - 0:50
    wanaopanga kuokoa dunia.
  • 0:51 - 0:53
    Wajua nilianzaje ?
  • 0:53 - 0:55
    Ni baba na busara zake.
  • 0:56 - 1:00
    Kila kitu ulimfunza,
    alienda akafunza ulimwengu.
  • 1:00 - 1:04
    Maneno yake yote
    kuhusu uwajibikaji tulionao kama binadamu
  • 1:04 - 1:07
    kuishi kwa usawa na asili
  • 1:07 - 1:08
    yalipitishwa kwangu.
  • 1:09 - 1:12
    Nimeona kutokua sawa kwenye ulimwengu wetu
  • 1:12 - 1:15
    na kukumbuka ulichoniambia wakati mmoja:
  • 1:15 - 1:18
    "Acha kila kitu bora kuliko ulivyokikuta."
  • 1:19 - 1:22
    Najua ulikuwa unaongelea kuhusu vyombo,
  • 1:22 - 1:24
    lakini, hiyo inaleta maana kwa ulimwengu pia.
  • 1:25 - 1:27
    Sikujua cha kufanya mwanzoni.
  • 1:27 - 1:29
    Dunia ni kubwa mno,
  • 1:29 - 1:31
    na ina tabia nyingi mbaya.
  • 1:31 - 1:35
    Sikujua vile msichana mwenye miaka 15
    angebadilisha chochote.
  • 1:35 - 1:36
    lakini ilinibidi kujaribu.
  • 1:37 - 1:39
    Ili kuweka hii falsafa katika vitendo,
  • 1:39 - 1:42
    Nilijiunga na klabu ya mazingira shuleni.
  • 1:42 - 1:47
    Lakini niliona wanafunzi wenza
    wakiongelea mchakato wa taka kuna matumizi tena
  • 1:47 - 1:49
    na kutazama filamu zinazohusu bahari.
  • 1:49 - 1:51
    Ulikua mwonekano wa kuzingatia mazingira
  • 1:51 - 1:56
    ulioegemea
    harakati ya kutunza hali ya hewa isiyofaa,
  • 1:56 - 1:59
    na kutupa lawama kwa mtumiaji
    katika janga la kubadiika kwa hali ya hewa
  • 1:59 - 2:02
    na kutangaza joto inaongezeka
  • 2:02 - 2:05
    kwa sababu tulisahau
    kurudisaha mifuko inayoweza tumika tena dukani.
  • 2:06 - 2:09
    Ulinifunza kwamba kutunza ulimwengu
  • 2:09 - 2:12
    inahusu uamuzi tunaochukua kwa pamoja.
  • 2:13 - 2:15
    Nafurahia kukuambia, Abuelita,
  • 2:15 - 2:18
    kwamba nimebadili
    wazo la kila mtu klabuni.
  • 2:18 - 2:21
    Badala ya kuongelea mchakato wa kufanya taka kutumika tena,
  • 2:21 - 2:24
    tumeanza kuandikia wanasiasa wetu barua,
  • 2:24 - 2:26
    kupiga marufuku kabisa plastiki laini.
  • 2:26 - 2:29
    Na kisha, lisilojarajiwa likatokea:
  • 2:30 - 2:32
    tulianza kugoma shuleni.
  • 2:34 - 2:36
    Nafahamu ushatazama kwa habari,
  • 2:36 - 2:38
    au pengine hio si mahususi kwa saa hii.
  • 2:38 - 2:42
    Lakini wakati huo, ilikuwa ni jambo kubwa.
  • 2:42 - 2:46
    Hebu fikiria watoto kutoenda shule
    kisa wanataka watu waokoe dunia.
  • 2:46 - 2:49
    (Video) Umati: Ulimwengu mwingine
    unawezekana ! Hatuzuiliki !
  • 2:49 - 2:51
    XiyeBastide: Kwa mgomo wa
    kwanza kimataifa wa hali ya hewa,
  • 2:51 - 2:53
    ilioandaliwa na Greta Thunberg,
  • 2:53 - 2:57
    Nilishawishi wanafunzi 600 wenzangu
    kutembea nami.
  • 2:58 - 3:00
    Greta Thunberg ni kijana mwanzilishi
    wa migomo
  • 3:00 - 3:01
    Uimara wake ulinihamasisha,
  • 3:01 - 3:02
    na kushtuka na utambuzi huu
  • 3:02 - 3:05
    kua kijana angebadilisha maono ya umaa kwa masuala ya kijamii
  • 3:05 - 3:08
    Harakati zikaanza.
  • 3:08 - 3:12
    (Video) Umati: Nyamazisha !
  • 3:12 - 3:13
    XB: Na nikawa mmoja wa waandalizi wakuu
  • 3:13 - 3:15
    kwa New York, Amerika na ulimwengu
  • 3:15 - 3:17
    (Video) XB: Tunahitaji nini?
    Crowd: Haki ya hali ya hewa!
  • 3:17 - 3:19
    XB: Tunalihitaji lini ?
    Crowd: Sasa !
  • 3:19 - 3:22
    XB: Nilianza kuongelea haki ya hali ya hewa na haki asilia
  • 3:22 - 3:24
    na ushirika miongoni mwa vizazi tofauti.
  • 3:24 - 3:27
    Huu ulikuwa mwazo tu, hata hivyo.
  • 3:27 - 3:29
    Wiki iliyokuwa na shughuli nyingi katika maisha yangu
  • 3:29 - 3:31
    nyakati zote itakuwa ni wiki ya Septemba 20,2019.
  • 3:31 - 3:33
    Mimi na marafiki wangu tulipata watu 300,00 kugoma kwa ajiliya hali ya hewa katika jiji la New York
  • 3:33 - 3:37
    Natamani ungekuwepo.
  • 3:37 - 3:44
    Tuliandamana mitaani ya Wall Street kudai haki ya hali ya hewa.
  • 3:44 - 3:46
    (Video) Umati: Hakuna tena kamwe makaa ya mawe, kamwe tena kwa mafuta, acha kaboni kwenye ardhi !
  • 3:46 - 3:49
    XB: Mwezi huo, nilihudhuria Mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa.
  • 3:49 - 3:52
    Niliongea katika jopo alipokuwepo Al Gore
  • 3:52 - 3:55
    Nikakutana na Jay Inslee na Naomi Klein
    na Bill McKibben
  • 3:55 - 3:57
    na rais wa Umoja wa Mataifa
  • 3:58 - 4:02
    Ilikuwa wiki la kustaajabisha kabisa maishani mwangu,
  • 4:02 - 4:04
    kwa sababu kila mtu ninayemjua walikuja pamoja-
  • 4:05 - 4:07
    walimu wangu, wanafunzi wenzangu wote...
  • 4:07 - 4:10
    Hata maduka niyapendayo yalifungwa kwa ajili ya mgomo wa hali ya hewa.
  • 4:10 - 4:13
    Kama ungeniuiza kwa nini nilifanya haya yote,
  • 4:13 - 4:17
    jibu langu lingekuwa,
  • 4:19 - 4:21
    "Kwanini nishindwe?"
  • 4:21 - 4:23
    Imekua mwaka tangu nianze,
  • 4:23 - 4:25
    na wakati mwingine huchosha.
  • 4:26 - 4:29
    Lakini kama kuna kitu mmoja ulinifunza, ni uthabiti.
  • 4:29 - 4:31
    Nakumbuka ulienda jiji la Mexico kila siku kwa miaka 30
  • 4:32 - 4:35
    ili kupata pesa ya mahitaji ya familia.
  • 4:36 - 4:40
    Na najua Abuelito amekua akitembea nje kwa miaka 20
  • 4:40 - 4:42
    kulinda ardhi takatifu dhidi ya makampuni makubwa yanayataka kuinyakua
  • 4:42 - 4:46
    mwaka moja si lolote
  • 4:46 - 4:50
    kulingana na mapambano familia yetu imepitia.
  • 4:50 - 4:51
    Na kama mapambano yetu yanaboresha dunia,
  • 4:52 - 4:54
    yatatufanya kuwa watu bora.
  • 4:55 - 4:58
    Kumekuwa na matatizo, Abuelita.
  • 4:58 - 5:00
    Ulimwenguni,
  • 5:01 - 5:03
    watu wanatarajia watoto kama sisi kufahamu kila kitu,
  • 5:03 - 5:05
    au angalau wanatarajia tujue,
  • 5:05 - 5:08
    Wanauliza na najibu,
  • 5:08 - 5:10
    na kama najua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi.
  • 5:10 - 5:12
    Wanahitaji matumaini, nasi tunawapa.
  • 5:12 - 5:15
    Nimepanga, kuandika, kuongelea na kusoma kuhusu hali ya hewa na sera
  • 5:15 - 5:17
    karibu kila siku kwa mwaka moja uliopita.
  • 5:19 - 5:24
    Na nina wasiwasi kidogo
  • 5:24 - 5:26
    kwamba sitoweza fanya vya kutosha, Abuelita.
  • 5:27 - 5:29
    Kwangu, kuwa na miaka 18 and kujaribu kuokoa ulimwengu
  • 5:29 - 5:31
    inamanisha kuwa mwanaharakati wa hali ya hewa.
  • 5:32 - 5:36
    Awali, labda ilimanisha kusoma kuwa daktari
  • 5:36 - 5:38
    au mwanasiasa au mtafiti.
  • 5:39 - 5:41
    Lakini siwezi ngojea kuwa mkubwa ili niwe mojawapo ya hayo.
  • 5:41 - 5:43
    Ulimwengu unaumia,
  • 5:44 - 5:47
    na hatuna taanasa ya wakati kamwe.
  • 5:48 - 5:49
    Kuokoa ulimwengu kama kijana unahitaji ueledi wa maneno,
  • 5:49 - 5:52
    kuelewa sayansi inayohusu janga la hali ya hewa
  • 5:53 - 5:57
    kuleta mtazamo wa kipekee kwa suala ibuka
  • 5:57 - 6:00
    na kusahau mambo mengineyo
  • 6:00 - 6:04
    Lakini wakati mwingine, nahisi kuzingatia mambo mengine tena.
  • 6:04 - 6:07
    Nataka kuimba na kucheza na kufanya mazoezi ya viungo vya mwili
  • 6:07 - 6:10
    Kiukweli nahisi ikiwa sisi sote tungelinda ulimwengu
  • 6:10 - 6:14
    kama tabia,
  • 6:14 - 6:18
    kama tamaduni,
  • 6:18 - 6:19
    hakuna mtu angekua mwanaharakati wa hali ya hewa wakati wote
  • 6:19 - 6:21
    Kama biashara zimekua endelevu,
  • 6:21 - 6:25
    kama gridi ya umeme inaendesha kwa nishati mbadala,
  • 6:25 - 6:27
    kama mtaala wa shule unatufundisha
  • 6:27 - 6:31
    kuwa kuzingatia ulimwengu ni moja ya utu wetu
  • 6:31 - 6:34
    labda naweza fanya mazoezi ya sarekasi tena.
  • 6:34 - 6:37
    Au sivyo, Abuelita ?
  • 6:38 - 6:41
    Tunaweza fanya hili.
  • 6:41 - 6:42
    Yote najaribu kufanya na kazi yangu
  • 6:43 - 6:44
    ni kuwapa watu wengine mtazamo chanya wa matumaini.
  • 6:45 - 6:46
    Lakini ni ngumu kidogo.
  • 6:46 - 6:49
    Kuna tamaa,
  • 6:50 - 6:51
    kuna kiburi,
  • 6:52 - 6:53
    kuna pesa,
  • 6:53 - 6:54
    na pia uyakinifu.
  • 6:55 - 6:56
    Hulka ya watu hurahisisha kuongelea haya mambo,
  • 6:56 - 6:57
    lakini napata wakati mgumu kuwafunza.
  • 6:57 - 7:00
    Nataka wajiamini kwa kujitahidi kila wakati.
  • 7:01 - 7:04
    Nawatakia kua na moyo na ujasiri
  • 7:05 - 7:08
    wa kupenda ulimwengu,
  • 7:08 - 7:11
    kamaulivyonifunza.
  • 7:11 - 7:12
    Nimeandika barua hii kukushukuru.
  • 7:13 - 7:15
    Shukrani kwa kunikaribisha kupenda ulimwengu
  • 7:15 - 7:16
    tangu nizaliwe.
  • 7:17 - 7:20
    Shukran kwa kucheka kwa kila kitu.
  • 7:20 - 7:21
    Shukrani kwa kunifunza
  • 7:22 - 7:24
    kua matumaini na matarajio ndizo zana za nguvu tulizo nazo
  • 7:24 - 7:25
    kukumbana na shida yoyote.
  • 7:25 - 7:30
    Nafanya hili kwa kuwa ulinionyesha
  • 7:30 - 7:31
    kwamba uthabiti, upendo na ujuzi
  • 7:32 - 7:35
    vinatosha kuleta mabadiliko.
  • 7:35 - 7:37
    Nataka kurudi Mexico nikutembelee.
  • 7:37 - 7:39
    Nataka kukuonyesha picha ya vitu nilivyofanya.
  • 7:39 - 7:42
    Nataka kukuonyesha sheria ya hali ya hewa
  • 7:42 - 7:45
    tuliyoweza kupitisha.
  • 7:45 - 7:47
    Nataka kunusa maua
  • 7:48 - 7:49
    na kupigania haki ya hali ya hewa pamoja nawe
  • 7:49 - 7:51
    Te quiero mucho.(Nakupenda sana)
  • 7:51 - 7:53
    Nakupenda
  • 7:54 - 7:55
    Xiye.
  • 7:55 - 7:57
    [Te quiero mucho. Xiye.]
Title:
Kama enyi watu wazima hamtaokoa dunia, tutaiokoa sisi.
Speaker:
Xiye Bastida
Description:

Katika barua inalogusa sana kwa bibi yake, Xiye Bastida anawazia chanzo chake kua mwanaharakati wa kutajika kimataifa wa hali ya hewa - kuanzia kuhamasisha wanafunzi wagome mpaka kuzungumuza katika Mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa pamoja na Greta Thunberg - anafuatilia azimio lake, uthabiti na penzi la dhati kwa ulimwengu aliorithi toka kwa nyanya yake.
"Shukran kwa kunikaribisha kupenda ulimwengu tangu nizaliwe," alisema.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
08:37

Swahili subtitles

Revisions