-
Sitasahau kamwe jinsi nilihisi nilipoona bahari
-
na kuingia mashuani kwa mara ya kwanza.
-
Kwa mtoto wa umri wa miaka minne,
-
ilikuwa hisia kuu ya uhuru ambayo ningeweza dhania.
-
Nilihisi, wajua, kutokea umri huo,
-
Ningependa sana kwa njia moja au nyingine, kuenda kwa matanga kote duniani.
-
Unapong'oa nanga kuanzisha safari hizi,
-
wajua, unabeba kila kitu unachohitaji kusalimika.
-
Ulichonacho ndicho chote unacho.
-
lazima utumie vizuri ulicho nacho
-
hadi tone la mwisho la mafuta ya diseli, kifurushi cha mwisho cha chakula.
-
Ni muhimu sana, au hautafanikiwa.
-
Na ghafla nikagundua, "mbona ulimwengu wetu ni tofauti?'
-
Unajua tuna raslimali chache,
-
vinavyopatikana mara moja katika historia ya binadamu.
-
Wajua, vyuma, plastiki na mbolea.
-
Tunachimba vitu hivi vyote ardhini na kuvimaliza.
-
Inawezekanaje kwa muda mrefu?
-
Hakika kuna njia tofauti tungeweza kutumia raslimali kimataifa
-
bila kuzimaliza.
-
Hilo ndilo swali nililolitia maanani,
-
na ikachukua muda mrefu kufika mahali
-
ambapo niligundua kuwa kuna njia mbadala ya kuendesha uchumi,
-
kuna njia mbadala tunaweza kutumia vitu, kutumia vifaa.
-
Na hiyo inaweza kuwa uchumi mzunguko.
-
Jinsi uchumi inavyoendeshwa sana leo hii ni kwa kutoa.
-
Ni finyu.
-
Tunatoa kitu chini ya ardhi, tunatengeneza kitu kwayo,
-
hatimaye mwishoni mwa utumizi ya bidhaa ile, tunaitupa.
-
Haijalishi upo na ufanisi upi
-
na vifaa unavyoleta mfumoni,
-
hata kama umetengeneza hiyo bidhaa
-
kutumia nishati kidogo au vifaa chache,
-
mwishowe utapungukiwa.
-
Ukigeuza hiyo na kuangalia mfano mzunguko,
-
pale ambapo unapobuni bidhaa,
-
unachukua kifaa chini ya ardhi, au kifaa kilicho tengezwa upya,
-
kimsingi, unaingiza hicho ndani ya bidhaa,
-
lakini unabuni bidhaa
-
ndio uweze kurejesha kifaa kwa kubuni, tangia mwanzo.
-
Unabuni kukabiliana na taka na uchafuzi wa mazingira.
-
Kwa nini uunde mojawapo ya haya kwa ulimwengu wa raslimali finyu?
-
Ni kuhusu maelezo fupi ya kubuni.
-
Leo hii ukinunua mashine ya kufulia nguo
-
unalipa ushuru ukinunua, na kumiliki vifaa vyake vyote,
-
na inapoharibika, na lazima ziharibike,
-
unalipa ushuru tena, ushuru wa taka.
-
Katika mfumo mzunguko, hayo yote yanabadilika.
-
Haumiliki mashine yako, unalipa kila unapofua.
-
Itachukuzwa na watengenezaji wa mashine,
-
na watahakikisha
-
mara mashine ile inapofika hatima yake,
-
wanaichukua, wanajua kilicho ndani yake,
-
na wanaweza rudisha vifaa kutoka kwayo.
-
kwa hivyo unabakia kubuni mfumo mzunguko.
-
Tumetafiti kwa upana takwimu zake,
-
wajua, hisabati,
-
na ni wa bei nafuu zaidi.
-
Ni senti 12 za Marekani kinyume na senti 27 za Marekani kwa kila mwosho
-
kwa mashine mzunguko.
-
Tungeishi ndani ya mfumo unaofanya kazi.
-
Hatungekuwa tunazalisha taka.
-
Tungekuwa na huduma bora.
-
Tungepata teknolojia kwa njia rahisi.
-
Kutokana na utafiti wote tuliofanya,
-
kwa sababu hao watengenezaji hawanunui bidhaa zote,
-
waendelea wanaziuza,
-
tungeweza kupata bei bora,
-
kwa sababu wangehakikishiwa mpito wa vifaa
-
kurudi kwa mfumo.
-
Ni na matumaini makubwa
-
kwa sababu unapotizama takwimu,
-
unapotizama hesabu,
-
ina maana kubadili na kutumia uchumi mzunguko.
-
Kuna thamani kubwa kwa uchumi mzunguko kuliko uchumi finyu.
-
Hakika kuna gharama kwa mpito kwa mashirika kubwa,
-
lakini pengine unafaa kujiuliza :
-
Ni nini athari ya mfumo finyu?
-
Kwa sababu kwangu ni rahisi,
-
Kuna athari kubwa kwa mfumo finyu.
-
Haiwezi kuwa kesho, kulingana na uchumi safi.
-
Kwa hivyo, ni wapi unawekeza wakati wako?
-
Ni wapi unawekeza juhudi zako?
-
Wacha tushughulikie ni nini uchumi mzunguko
-
na ujaribu kuchora aina ya mzunguko huo unavyoweza
-
manukuu ni na Mauricio Kakuei Tanaka,
-
Uhakiki na Jenny Lam-Chowdhury
¶
-
tamati