-
Asante Mwenyekiti Alexander, Seneta Murray,
-
na wanachama mashuhuri wa kamati
-
kwa nafasi hii kuongea leo.
-
Habari ya asubuhi kwa kila mtu.
-
Nilivyosema awali, naitwa Ethan Lindenberger,
-
na nipo mwaka wangu wa mwisho katika shule ya upili ya Norwalk,
-
na mamangu ni mwanaharakati wa kupinga chanjo
-
anayeamini kuwa chanjo zinasababisha usonji na uharibifu wa ubongo,
-
na hazina manufaa kwa afya na usalama wa jamii
-
licha ya kuwa maoni kama hayo yamefutiliwa mbali mara nyingi
-
na jamii ya wanasayansi.
-
Nimekuwa bila chanjo nyingi
-
dhidi ya magonjwa kama surua, tetekuwanga au ugonjwa wa kupooza.
-
Hata hivyo, kuanzia Desemba 2018,
-
nilianza kupata chanjo ambazo nilikosa
-
licha ya kuguna kwa mamangu,
-
hatima yake hadithi na kuweza kuongea hapa leo
-
na nimefurahia hayo sana, kwa hivyo asante.
-
Sasa kuelewa kwa nini nimekuja hapa na ni nini haswa nataka kuongelea,
-
Itabidi niwapashe maelezo fulani kuhusu maisha ya kwetu, malezi yangu.
-
Nilikuwa nikielewa imani ya mamangu
-
kuwa chanjo ni hatari,
-
na angeongea wazi kuhusu maoni haya.
-
Mtandaoni na pia moja kwa moja,
-
angeeleza wasiwasi wake,
-
na imani hii kosolewa vikali.
-
Maishani mwangu, nilianza kutia shaka
-
na kuuliza maswali
-
kwa sababu ya pingamizi aliopokea mamangu.
-
Baada ya muda, hayo hayakufikia popote.
-
Sasa ni muhimu kuelewa
-
kuwa nilipoelekea shule ya upili
-
na kuanza kujifikiria kwa kina,
-
niliona kuwa taarifa ya kuunga mkono chanjo
-
ilizidi wasiwasi hizo.
-
nilianza kuongoza vilabu vya mijadala shuleni mwangu
-
na kuandama ukweli kuliko chochote
-
na niligundua ubora fulani katika mijadala
-
na midahalo kwa jumla
-
inapofika katika majadiliano tata
-
ambayo ni kuwa yaonekana kuwa na pande mbili za mjadala.
-
Kila mara kuna madai ya kupinga au kukataa
-
na kitu cha kujibu kulingana na mjadala.
-
Ingawa haya yanaonekana kuwa kweli kimsingi,
-
haya si kweli kuhusu mjadala wa chanjo,
-
na nilimkabili mamangu na wasiwasi hii
-
kuwa hakuwa sahihi.
-
Nilimkabili mamangu mara nyingi,
-
kujaribu kueleza kuwa chanjo ni salama, na kuwa nafaa kuchanjwa.
-
kumweleza na majarida kutoka CDC
-
inayodai kwa upana kuwa maoni kuwa chanjo zinasababisha usonji
-
na matokeo mengineo hatari sana
-
siyo ya sahihi.
-
Mojawapo ya wakati nilipomkabili mamangu
-
na taarifa kutoka CDC inayodai kuwa chanjo haisababishi usonji,
-
alijibu kuwa hivyo ndivyo wanavyotaka ufikiri.
-
Kutoamini na kuwa na wasiwasi kulichukua kipaumbele katika taarifa.
-
Mazungumzi kama haya yalinithibitishia
-
kuwa ushahidi kuunga mkono chanjo
-
ilikuwa angalau kwa kiwango kisichoaminika,
-
kwa kiwango kikubwa kuliko taarifa iliyokita mizizi
-
ambayo mamangu aliathiriana nayo,
-
na hiyo ndiyo nataka kulenga leo.
-
Kukabiliana na milipuko ya magonjwa yanayoweza kukingwa,
-
taarifa ni, kwa fahamu zangu, ya kipaumbele.
-
Mamangu angegeukia makundi yanayopinga chanjo kwa mitandao ya kijamii
-
kutafuta ushahidi na utetezi wake
-
badala ya maafisa wa afya na vyanzo vinavyoaminika.
-
Hii inaweza onekana kama uhabithi
-
kwa sababu ya hatari ambazo kutochanja huweka.
-
lakini hii sio hali.
-
Mamangu alikuwa na hisia ya kupenda watoto wake
-
na kuwa na wasiwasi.
-
Taarifa hii potofu inaenea,
-
na huyo sio sababu ya uhalali.
-
Lakini nafahamu kuwa
-
ni kwa heshima na upendo kuwa sikukubaliana na mamangu.
-
na taarifa aliyopeana,
-
Naendelea kujaribu kueleza kuwa ilikuwa potofu.
-
maoni kuwa chanjo zinaweza sababisha usonji, uharibifu wa ubongo
-
na pia mlipuko wa surua
-
si ya kuhusu jamii na Marekani,
-
ambapo maoni haya yalisisitizwa na vyanzo vyake.
-
Na kwa watu fulani binafsi na mashirika
-
ambazo zinaeneza taarifa hii potofu,
-
wanatia hofu kwa umma kwa ajili ya faida yao binafsi
-
na wanafanya hivyo wakijua kuwa taarifa hiyo ni potofu.
-
Kwa mamangu, mapenzi yake na kujali kama mzazi
-
ilitumiwa kupitisha ajenda ya dhiki ya uwongo,
-
na waarifu hawa ambao husambaza taarifa potofu
-
wanafaa kuwa wasiwasi ya msingi kwa Wamarekani.
-
Ingawa mabadiliko yapo, mengi yanaweza fanywa,
-
takriban watu asilimia 80 kulingana na kituo cha utafiti cha Pew,
-
hugeukia mtandao wa intaneti kutatua maswala yanayohusiana na afya.
-
Nilieleza zaidi takwimu na ushahidi katika ushuhuda wangu ulioandikwa.
-
Sasa kwa suala la ninachotaka kutoka nalo leo
-
na kumaliza nalo.
-
Ingawa mamangu angegeukia waarifu wasio halali
-
ambao hawakuwa na taarifa yenye ushahidi wenye uhakiki linganishi,
-
ningeweza kuona vizuri kuwa ushahidi na madai
-
hazikuwa sahihi,
-
na kwa sababu hiyo,
-
na wataalam wa huduma za kiafya ambao niliweza kuongea nao,
-
na taarifa niliopewa,
-
niliweza kufanya uamuzi fika na wa kisayansi.
-
Kukabiliana na suala hili kwa kuzingatia elimu
-
na kushughulikia taarifa potofu kikamilifu
-
inaweza sababisha mabadiliko kama ilivyonifanyia.
-
Ingawa mjadala kuhusu chanjo
-
hauna misingi katika taarifa na kujali afya na usalama,
-
hii ndio maana elimu ni muhimu na pia taarifa potofu ni hatari sana.
-
Manukuu na uhakiki na Mauricio Kakuei Tanaka na Jenny Lam-Chowdhury