Swahili Untertitel

← A Second Chance for the Kamlari Girls of Nepal

Einbettcode generieren
41 Sprachen

Zeige Revision 4 erzeugt am 11/14/2015 von Adams Njagi.

 1. Nilijua wanakuja kunichukua.
 2. Nililia siku nzima,
  nikitumai gari halitakuja.
 3. Lakini likaja.
 4. Sikujua niendako
  wala hao watu walikuwa akina nani.
 5. Wazazi wangu waliniambia
  ni lazima niende na nifanye kazi.
 6. Tulikuwa maskini kupindukia.
 7. Mama yangu alijaribu kunifanya
  nihisi nafuu
 8. kwa kuniambia kuwa nikiwa Kamlari
 9. angalau ndugu zangu watapata chakula cha kukula.
 10. Nilikuwa Kamlari kwa miaka sita.
 11. Niliuzwa nikiwa miaka sita.
 12. Nikawa Kamlari nilipohitimu miaka 13.
 13. Nilitumwa kufanya kazi kama Kamlari nikiwa miaka kumi,
  kama mama yangu kabla mimi.
 14. Siku yangu ilianza saa kumi asubuhi
  wakati mke wa mwenye nyumba aliponiamsha.
 15. Nilifanya kazi mchana kutwa hadi usiku.
 16. Nyumba ile niliyotumwa
  ilikuwa imefungwa na ua,
 17. na sikuruhusiwa kutoka nje.
 18. Japo nilitaka kutoroka, sikuweza.
 19. Wakati wasichana kama mimi
  wanapokuwa Kamlari,
 20. inatulazimu tukumbane na vurugu.
 21. Vita vya kimwili
  na unyanyasaji wa kijinsia.
 22. Nilidhani nitaishi maisha yangu yote
 23. kama Kamlari.
 24. Waliponiambia watanisaidia kurudi shule,
 25. huo ndio ulikuwa wakati
 26. wa furaha zaidi maishani mwangu.
 27. Nikipewa nafasi, nitaendelea
 28. kusoma katika mapumziko ya maisha yangu.
 29. Nataka kuwa mwalimu.
 30. Nataka kuwaweka huru Kamlari wote na
  nihakikishe kuwa wamerudishwa shule.
 31. Wazazi wangu walikuwa makini
 32. na watoto wao wa kiume pekee.
 33. Walisomesha watoto wao wa kiume pekee.
 34. Lakini nilibadilisha hili.
 35. Niliwaambia wazazi wangu,
  "Tuchukulie sote kwa usawa."
 36. "Nichukulie vyenye ungechukulia
  watoto wako wa kiume."
 37. Na taratibu, mama yangu na baba yangu
  walianza kubadilika.