YouTube

Teniu un compte YouTube?

New: enable viewer-created translations and captions on your YouTube channel!

Swahili subtítols

← Maajabu ya boksi la Pandora - Iseult Gillespie

Obtén el codi d'incrustació
30 llengües

Showing Revision 3 created 01/28/2019 by Doris Mangalu.

 1. Udadisi:

 2. Baraka au laana?
 3. Utata wa hili fumbo
 4. iliwekewa kwa Wagiriki
 5. kwa umbo la dhana la Pandora.
 6. Wahenga wanasema,
 7. alikuwa mwanamke wa kwanza mfaji,
 8. udadisi wake ulipeleka ugunduzi wa
  mambo mengi kusogea.
 9. Pandora alipewa pumzi na
  Hephaestus, mungu wa moto,

 10. ambae aliomba msaada wa wenzie
  ili amfanye kuwa maridadi
 11. Kutoka kwa Aphrodite alipewa uwezo
  wa hisia za kina;
 12. kwa Hermes akapata
  uwezo wa lugha
 13. Athena akampa zawadi ya usanii bora
  na umakini kwa kila kitu,
 14. Na Hermes akampa jina lake.
 15. Mwishowe, Zeus akampatia
  zawadi mbili Pandora.

 16. Ya kwanza ilikuwa ni zawadi ya udadisi,
 17. iliokaa ndani ya roho yake na kumtuma
  kwa bidii duniani.
 18. Ya pili ilikuwa ni boksi zito,
  lilitengenezwa vizuri, zito kubeba -
 19. na kufungwa kwa nguvu.
 20. Ila yaliyomo, Zeus alimwambia,
  hayakua kwa macho ya mfaji.
 21. Hakutakiwa kufungua boksi
  kwenye hali yeyote ile.
 22. Duniani, Pandora akakutana na kupendana
  na Epimetheus, mtitani mwenye kipaji

 23. ambaye alipewa kazi ya kutengeneza
  dunia ya kawaida na Zeus.
 24. Alifanya kazi hiyo pembeni ya
  kaka yake Prometheus,
 25. aliyeumba binadamu wa kwanza
 26. lakini alipewa adhabu ya milele
  kwa kuwapa moto.
 27. Epimetheus alimkumbuka kaka yake mno,
 28. lakini alivyokuwa na Pandora alipata
  nafsi nyingine machachari ya urafiki.
 29. Pandora alifurahia sana maisha
  ya duniani.

 30. Alipagawa kirahisi pia na kila
  alichokiona na hakuwa mtulivu
 31. kutokana na kiu yake ya maarifa na nia
  ya kujifunza mazingira yake.
 32. Mara nyingi, akili yake iliwaza
  vilivyomo kwenye boksi lililofungwa.
 33. Ni hazina gani kubwa sana mpaka isionekane
  na macho ya binadamu,
 34. na kwanini yeye alipewa alitunze?
 35. Vidole vyake viliwasha kutaka kulifungua.
 36. Kuna muda aliamini alisikia
  sauti zikinong'oneza
 37. na vilivyomo vikitoa sauti kwa ndani,
 38. kama vile vinataka kuwa huru.
 39. Fumbo lake likawa linamtatiza.
 40. Muda ulivyozidi kwenda Pandora alizidi
  kuwa na hamu na boksi.

 41. Ilionekana kulikuwa na nguvu nje ya uwezo
  wake iliyomuita kwenye boksi,
 42. Iliyoita jina lake kwa nguvu zaidi.
 43. Siku moja alishindwa kuvumilia.
 44. Akajificha mbali na Epimetheus,
 45. aliangaza lile boksi la mafumbo.
 46. Angeangalia mara moja ndani,
 47. kisha akili yake itulie na
  asiliwaze tena...
 48. Ila alivyogusa mfuniko mara moja,
  boksi likafunguka kwa nguvu.

 49. Majitu ya kutisha na sauti za ajabu

 50. iktoka na wingu la moshi na kumzunguka
  na sauti za mkwaruzo na kelele.
 51. Akijawa na uwoga,
 52. Pandora alishikilia kwa bidii ile hewa
  akiwarudisha kwenye gereza lao.
 53. Lakini vile viumbe vilifurika nje
  kwenye wingu la kutisha.
 54. Alijisikia hali ya kukataza
  vilivyokuwa vikiondoka.
 55. Zeus alitumia boksi kama chombo
 56. cha mabaya yote na
  mabadhuri aliyotengeneza -
 57. na yakiachiwa,
 58. hayarudi tena.
 59. Pandora akilia,

 60. akasikia sauti ikitoka kwenye boksi,
 61. Hii haikua sauti ya minong'ono
  ya mashetani,
 62. ila mwanga uliovuma ulionekana
  ukipungua hasira yake.
 63. Alipofungua mfuniko na
  kuangalia ndani tena,
 64. mwanga wenye joto zuri ukatoka
  na kuangaza mbali.
 65. Akiutazama ukiwaka kwenye amsho
  la uovu alioachia,

 66. uchungu wa Pandora ukapungua.
 67. Alijua kwamba hatoweza kurekebisha
  kufungua boksi -
 68. lakini pamoja na jitihada, aliweka
  matumaini kubadilisha matokeo.
 69. Leo hii, Boksi la Pandora
  linatufundisha madhara makubwa

 70. ya kuhangaika na tusivyovijua -
 71. lakini hamu ya Pandora ya kujua
  ilidokeza uwili uliopo
 72. kwenye kiini cha uchunguzi wa binadamu.
 73. Je tunatakiwa kuchunguza
  kila tusichokijua,
 74. kuchimbua dunia kwa zaidi -
 75. au kuna baadhi ya maajabu

 76. ambayo ni bora yasitatuliwe?