Return to Video

Jinsi ukweli halisi unawabadilisha wanafunzi kuwa wanasayansi

  • 0:01 - 0:02
    kwa jinsi gani uligundua shauku yako
  • 0:02 - 0:04
    ama kupata kazi yako?
  • 0:04 - 0:05
    Je, ulikutana nayo?
  • 0:05 - 0:07
    ama ilikua ni kufanya majaribio na kukosea?
  • 0:07 - 0:10
    Kama mtetezi wa haki za watoto,
    Marian Wright Edelman alisema,
  • 0:11 - 0:13
    ¨Hauwezi ukawa usichokiona.¨
  • 0:14 - 0:16
    Kwa bahati nzuri, sasa tunaishi katika
    wakati
  • 0:16 - 0:20
    ambao teknolojia zinazojitokeza zaweza
    kutusaidia kusuluhisha tatizo hili
  • 0:20 - 0:21
    Kwa miaka miwili iliyopita
  • 0:21 - 0:24
    nimekua nikikuza mpango wa ukweli
    uliopanuliwa
  • 0:24 - 0:27
    unaowezesha wanafunzi wa shule za kati,
    kutoka nchi nzima
  • 0:27 - 0:30
    kuchukua jukumu la mwanasaikolojia wa
    baharini
  • 0:30 - 0:32
    hata kama hawajawahi kuona bahari
  • 0:33 - 0:36
    kama mwanafunzi mmoja wa darasa la saba ambaye hivi
    karibuni amekamilisha programu yetu
  • 0:36 - 0:39
    alisema, ¨Niliweza kujiona ni
    mwanasayansi,
  • 0:39 - 0:41
    kwa sababu nilifurahia mchezo huu.¨
  • 0:41 - 0:43
    Maoni haya yalinisisimua sana
  • 0:43 - 0:47
    kwa sababu wanafunzi wachache sana hujiona
    kama wanasayansi
  • 0:47 - 0:53
    Utafiti wa 2014 ulionyesha kuwa asilimia 57
    ya wanafunzi wa darasa la nane na tisa
  • 0:53 - 0:55
    walisema, ¨Sipendi sayansi¨
  • 0:56 - 0:58
    Vivyo hivyo, pia katika 2014,
  • 0:58 - 1:01
    Nilikutana naye Mandë Holford,
    mtaalamu wa kemia ya baharini
  • 1:01 - 1:04
    na Lindsay Portnoy, mwanasaikolojia wa
    elimu.
  • 1:05 - 1:07
    Sote watatu tulishirikiana shauku
  • 1:07 - 1:10
    ya kuwafanya wanafunzi wavutiwe, na wawe
    na starehe katika sayansi.
  • 1:11 - 1:13
    Tulifikiria juu ya jinsi
    tunaweza kuwapa watoto
  • 1:13 - 1:16
    uzoefu wa kweli zaidi katika taaluma ya
    kisayansi
  • 1:16 - 1:18
    Tulijadili utafiti huo;
  • 1:18 - 1:22
    ulionyesha kuwa wanafunzi walihisi vizuri
    kuwa na uthubutu wakati wa kucheza michezo.
  • 1:23 - 1:26
    Basi sote watatu tulianzisha kampuni ya
    michezo ya kielimu
  • 1:26 - 1:28
    kuipa sayansi uhai
  • 1:29 - 1:33
    Ukweli halisi ulionekana kama njia ya bei
    ya chini ya kuongeza ufikiaji
  • 1:33 - 1:36
    Juu ya hayo, utafiti wa kitaalam
    umeonyesha
  • 1:36 - 1:40
    ukweli halisi unaweza kusababisha
    kuongezeka kwa utunzaji wa kujifunza.
  • 1:40 - 1:43
    Hii ilikuwa kamili kwetu,
    kama tulivyotaka kuwa mashuleni
  • 1:43 - 1:46
    ili tuweze kufikia
    idadi kubwa ya wanafunzi kadiri iwezekanavyo,
  • 1:46 - 1:49
    haswa wanafunzi ambao wana uwakilishi mdogo katika sayansi
  • 1:49 - 1:52
    Kwa hivyo, tukiwa na ufadhili kutoka Mfuko wa Sayansi wa Kitaifa,
  • 1:52 - 1:55
    tulianza kukuza mpango wetu wa ukweli
    uliopanuliwa
  • 1:55 - 1:57
    ulioleta pamoja ukweli halisi
  • 1:57 - 1:59
    na jarida la kibinafsi la kidijitali
  • 2:00 - 2:02
    Tulifanya kazi na waalimu tulipokua
    tukiuendeleza
  • 2:02 - 2:05
    kuhakikisha kuwa utafaa bila shida
    ndani ya mitaala iliyopo
  • 2:06 - 2:10
    na kuwawezesha waalimu kutumia teknolojia
    ya kisasa madarasani mwao.
  • 2:10 - 2:13
    Tulibuni ukweli halisi wa Kadi ya Google,
  • 2:13 - 2:15
    ambao unahitaji simu janja tu
  • 2:15 - 2:19
    na kitazamaji cha VR cha dola 10
    kilichotengenezwa kwa kadibodi.
  • 2:20 - 2:21
    kwa hivi vifaa vya kichwa visivyo ghali,
  • 2:21 - 2:25
    wanafunzi husafirishwa katika msafara
    chini ya maji.
  • 2:25 - 2:27
    Wanafunzi hutumia jarida lao la kidijitali
  • 2:27 - 2:29
    kuandika maelezo yao,
  • 2:29 - 2:30
    kujibu maswali,
  • 2:30 - 2:32
    kujenga mifano
  • 2:32 - 2:33
    na kukuza nadharia.
  • 2:33 - 2:37
    Wanafunzi basi huenda katika ulimwengu wa kweli kujaribu nadharia zao
  • 2:37 - 2:39
    ili waone ikiwa ni sahihi,
  • 2:39 - 2:40
    kadiri wanasayansi waendavyo katika
    nyanja za utafiti
  • 2:40 - 2:42
    katika kazi zao.
  • 2:43 - 2:45
    Wanafunzi wanaporudi kwa jarida lao la
    kidijitali,
  • 2:45 - 2:47
    hushiriki uchunguzi wao, madai,
  • 2:47 - 2:49
    hoja na ushahidi.
  • 2:49 - 2:54
    Majibu ya wanafunzi yaliyoandikwa na
    mwingiliano wa kawaida
  • 2:54 - 2:56
    zote husasishwa moja kwa moja
  • 2:56 - 2:58
    kwenye dashibodi ya tathmini ya mwalimu,
  • 2:58 - 3:00
    ili walimu waweze kufuata maendeleo yao
  • 3:00 - 3:03
    na wawasaidie kama inavyohitajika.
  • 3:03 - 3:05
    Ili kukupa hisia nzuri, nitakuonyesha
  • 3:05 - 3:07
    kidogo ya yale wanafunzi huona.
  • 3:08 - 3:10
    Huu ndio ukweli halisi wanapokuwa chini ya
    maji
  • 3:10 - 3:13
    wakiangalia mimea na wanyama.
  • 3:14 - 3:17
    Hii ni jarida la kidijitali
    ambapo wanaunda mifano yao
  • 3:17 - 3:20
    kulingana na data hii ya kawaida kuonyesha
    wanachotarajia kuona.
  • 3:21 - 3:24
    Hapa, wanaunga mkono hiyo na taarifa za
    ubora.
  • 3:24 - 3:27
    Na hii ndio dashibodi ya ualimu
    inayoonyesha maendeleo
  • 3:27 - 3:31
    na inawezesha [waalimu] kuona majibu ya
    wanafunzi wanapoendelea.
  • 3:33 - 3:35
    Tulipokua tunaunda BioDive,
  • 3:35 - 3:37
    tulitaka sana kuzingatia ufikiaji,
  • 3:37 - 3:41
    kwa hivyo tuliijenga kuhitaji simu moja tu
    kwa kila wanafunzi wanne.
  • 3:41 - 3:45
    Tulijua pia jinsi kazi ya sayansi inavyoshirikisha,
  • 3:45 - 3:47
    kwa hivyo tuliunda uzoefu kutatuliwa tu
  • 3:47 - 3:49
    kupitia kushirikiana
  • 3:49 - 3:53
    kwani kila mwanafunzi ni mtaalam katika
    eneo tofauti la kijiografia.
  • 3:54 - 3:57
    Kwa kuzingatia kwamba akili za watoto hawa
    bado inaendelea kukua,
  • 3:57 - 4:01
    tulipunguza kila uzoefu kudumu kiwango
    kisichozidi dakika mbili.
  • 4:01 - 4:05
    Na mwishowe, kwa sababu tunajua umuhimu
    wa kudhihirishwa mara kwa mara
  • 4:05 - 4:07
    ili kufahamu maarifa
  • 4:07 - 4:11
    tuliunda BioDive ifanyike zaidi ya vipindi
    vya darasa tano.
  • 4:12 - 4:15
    Tulianza majaribio ya BioDive mnamo 2017
  • 4:15 - 4:18
    katika shule 20 huko New York na New Jersey.
  • 4:18 - 4:21
    Tulitaka kuona wanafunzi walipokuwa
    wakitumia teknolojia hii mpya.
  • 4:21 - 4:24
    Mnamo mwaka wa 2019, sasa,
  • 4:24 - 4:28
    tunafanya majaribio katika majimbo 26 kwa
    sasa.
  • 4:28 - 4:31
    Tulichosikia kutoka kwa waalimu
    ambao wamefundisha kwa kutumia programu yetu:
  • 4:31 - 4:34
    "Ilikuwa njia nzuri ya kuonyesha mienendo ya bahari
    bila anasa ya kuwa huko hasa
  • 4:34 - 4:36
    kwa kuwa tupo Ohio. "
  • 4:36 - 4:37
    (Kicheko)
  • 4:37 - 4:38
    "Ni ya kushangaza sana."
  • 4:38 - 4:41
    "Wanafunzi walishiriki kabisa."
  • 4:41 - 4:44
    Lakini kinachotupa tumaini ni tunachosikia
    kutoka kwa wanafunzi
  • 4:45 - 4:47
    "Nilipenda jinsi ilivyoonekana kana kwamba
    nilikuwa pale."
  • 4:47 - 4:49
    "Ina maingiliano na ni njia nzuri ya
    kufurahia unapojifunza."
  • 4:49 - 4:53
    "Ilinipa mifano ya kweli ya jinsi viumbe
    hawa wanavyoonekana. "
  • 4:54 - 4:58
    "Nilijiona kama mwanasayansi
    kwa sababu inaonekana kufurahisha sana. "
  • 4:59 - 5:01
    Maoni yetu hayakuwa mazuri kila wakati.
  • 5:02 - 5:03
    Tulipoanza kukuza,
  • 5:03 - 5:05
    tulianza kwa kuwauliza wanafunzi
  • 5:05 - 5:07
    walichokipenda,
  • 5:07 - 5:08
    kile wasichokipenda
  • 5:08 - 5:10
    na kile walichokipata kinawachanganya.
  • 5:10 - 5:13
    Mwishowe tulianza kuuliza walichokua
    nahamu ya kufanya.
  • 5:14 - 5:17
    Maoni yao yakatupa vitu halisi vya kujenga
    ndani
  • 5:17 - 5:21
    ili kuwa na uhakika kuwa tunajumuisha
    sauti za wanafunzi katika tulichokibuni.
  • 5:22 - 5:26
    Kwa jumla, kile tumejifunza ni kwamba huu
    ni mwanzo wa jukwaa mpya
  • 5:26 - 5:29
    la kuwapa wanafunzi sauti na umiliki
  • 5:29 - 5:32
    katika kuamua jinsi wanataka kuwa na athari
  • 5:32 - 5:33
    katika kazi zao.
  • 5:34 - 5:35
    Tulilenga sayansi,
  • 5:35 - 5:37
    kwa sababu twafahamu kuwa twawahitaji wanasayansi
  • 5:37 - 5:40
    ili kutusaidia kutatua hali yetu ya sasa na
    changamoto za baadaye.
  • 5:41 - 5:45
    Lakini ukweli halisi unaweza kusaidia
    wanafunzi katika eneo lolote.
  • 5:45 - 5:49
    Tunawezaje kuwasaidia wanafunzi katika
    kutafuta tamaa zao zote
  • 5:49 - 5:53
    kwa uzoefu huu wa kufungua jicho na nafasi
    za kujifunza kutoka kwa vyanzo vya msingi?
  • 5:53 - 5:57
    Tunaweza kuunda... VR za vifaa vya kichwa
    visivyo ghali
  • 5:58 - 6:01
    ambazo zinawaruhusu wazame katika fasihi
    ya mdomo
  • 6:01 - 6:03
    au katika wakati mgumu wa historia ya wanadamu?
  • 6:03 - 6:07
    Ukweli uliopanuliwa una uwezo
    wakubadilisha mwelekeo
  • 6:07 - 6:09
    wa maisha ya watoto wetu
  • 6:09 - 6:11
    na uwaongoze kwenye kazi hawakuwahi
    kufikiria
  • 6:12 - 6:15
    kwa kuwapa nafasi ya kuona ni nini
    wanaweza wakawa.
  • 6:15 - 6:16
    Asanteni
  • 6:16 - 6:18
    (Makofi)
Title:
Jinsi ukweli halisi unawabadilisha wanafunzi kuwa wanasayansi
Speaker:
Jessica Ochoa Hendrix
Description:

Kwa kutumia ukweli halisi wa bei ya chini, mwanaharakati wa elimu Jessica Ochoa Hendrix amesaidia kuleta sayansi katika shule kote Amerika. Katika mazungumzo haya ya haraka, anaelezea jinsi uzoefu wa VR alivyokua unawaalika wanafunzi kuchunguza mazingira ya chini ya maji kana kwamba ni biolojia ya baharini - na kujiona katika kazi zingine ambazo labda hawangefikiria.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
06:34

Swahili subtitles

Revisions