Siri za maajabu ya Usanifu Majengo ya dunia ya zamani
-
0:01 - 0:04Je unafikiri vitu tunavyojenga leo
-
0:04 - 0:06vitahesabika kama maajabu miaka ijayo?
-
0:07 - 0:09Tafakari kuhusu Stonehenge,
-
0:09 - 0:10Mapiramidi,
-
0:10 - 0:13Machu Picchu na Kisiwa cha Easter
-
0:14 - 0:17Vyote hivi ni tofauti sana
na vile tunavyofanya leo, -
0:18 - 0:20na yale mawe makubwa,
-
0:20 - 0:21yakiwa yamepangwa katika hali ya kiutata
hali ngumu kuelewa -
0:26 - 0:30na mabaki yake yote ya ujenzi
-
0:30 - 0:32yakifutwa,
-
0:32 - 0:34ikiyaacha katika hali ya kutojulikana
-
0:35 - 0:39Inaonekana kama vile watu hawakuweza
kujenga vitu hivi, -
0:41 - 0:42kwa sababu watu hawakujenga.
-
0:43 - 0:47Vilitengenezwa kwa uangalifu na
jamii ya majitu -
0:47 - 0:48yajulikanayo kama Cyclops.
-
0:48 - 0:50(Vicheko)
-
0:50 - 0:52Na nimekuwa nashirikiana na
majitu haya -
0:52 - 0:55ili kujifunza siri zao
za kuhamisha mawe hayo makubwa. -
0:57 - 1:00na ni kwamba,
Cyclops hawana nguvu kivile, -
1:01 - 1:04Ni wajanja sana katika
kufanya vitu kufanya kazi kwa niaba yao. -
1:07 - 1:11Video, ambazo mnaziona nyuma yangu
za vitu vinavyobadilika vikubwa,kama mawe -
1:12 - 1:13ni matokeo ya ushirikiano huu.
-
1:15 - 1:18SAWA, inawezekana Cyclops
vikawa ni viumbe vya kufikirika -
1:19 - 1:22lakini maajabu haya bado ni halisi.
-
1:22 - 1:23Watu waliyajenga.
-
1:24 - 1:26Lakini pia waliunda dhana
kuhusu hayo -
1:28 - 1:31na kuhusu maajabu, kuna kiunganishi
kinene -
1:32 - 1:34kati ya dhana fikirishi na uhalisia.
-
1:35 - 1:37Chukulia mfano wa Kisiwa cha Easter.
-
1:38 - 1:41Pale wavumbuzi wa Kidachi
walipokifikia kwa mara ya kwanza kisiwa hiki, -
1:41 - 1:43Waliwauliza watu wa Rapa Nui
-
1:43 - 1:47Vile mababu zao walivyoweza kuhamisha
sanamu hizi kubwa -
1:48 - 1:50Na watu wa Rapa Nui wakasema,
-
1:50 - 1:53"Mababu zetu hawakuhamisha sanamu hizo,
-
1:54 - 1:56kwa sababu zilitembea zenyewe."
-
1:58 - 2:00Kwa karne kadhaa, hili lilikataliwa,
lakini ni kweli kabisa. -
2:01 - 2:06Sanamu, zijulikanazo kama moai,
zilihamishwa zikiwa zimesimama, -
2:06 - 2:08zikishikiliwa pande moja hadi nyingine.
-
2:10 - 2:11SAWA?
-
2:11 - 2:15Pamoja na uzuri wa moai kwa wageni leo,
-
2:15 - 2:18unahitaji kuwaza kuwa pale wakati ule,
-
2:18 - 2:21na moai makubwa yakitembea
katika kisiwa. -
2:21 - 2:26Kwa sababu kumbukumbu halisi sio
vitu vyenyewe, -
2:26 - 2:30Ilikuwa ni utamaduni
wa kulifanya jiwe liwe hai. -
2:32 - 2:34Kwa hiyo kama msanifu majengo,
nimekuwa nakimbizana na ndoto hiyo. -
2:35 - 2:40Tunawezaje kuhamisha dhana yetu ya ujenzi
ili kutoa nafasi ya dhana hii fikirishi -
2:42 - 2:44Kwa hiyo kile nimekuwa nafanya
ni kujipa changamoto mwenyewe -
2:44 - 2:47kwa kufanya maonyesho kadhaa
-
2:47 - 2:49ya zamani lakini
yaliyo na jukumu la wazi kabisa -
2:50 - 2:54ya kuhamisha na kusimamisha
vitu vikubwa vizito, -
2:54 - 2:57kama vile jiwe hili kubwa
lililosanifiwa kutembea ardhini -
2:58 - 2:59na kusimama wima
-
3:00 - 3:04au jiwe hili kubwa lenye uzito
wa 4,000 linaloibuka likiwa hai -
3:04 - 3:06ili kucheza stejini
-
3:08 - 3:11na nilichojifunza ni kuwa kwa
kuwaza kuhusu usanifu majengo -
3:11 - 3:15si kama bidhaa ya mwisho bali kama onyesho
-
3:15 - 3:18kutoka wazo mpaka kukamilika,
-
3:18 - 3:22tunajikuta tunagundua njia bora sana
za kujenga hivi leo. -
3:23 - 3:26Unajua, sehemu kubwa ya mazungumzo
kuhusu zsiku zetu za baadaye -
3:26 - 3:30yanaangazia zaidi teknolojia,
ufanisi na uharaka. -
3:30 - 3:32Lakini kama nimejifunza chochote kuhusu Cyclops,
-
3:32 - 3:37ni kuwa maajabu yanaweza
kuwa ya kijanja, mazuri sana -
3:37 - 3:38na endelevu --
-
3:38 - 3:41kutokana na uwingi na kutoeleweka kwake.
-
3:42 - 3:46na pamoja na kuwa wanahitaji kujua
jinsi maajabu haya yalivyojengwa, -
3:46 - 3:49Nimekuwa nikiwauliza Cyclops
jinsi ya kuunda sintofahamu hii -
3:49 - 3:51ambayo inawalazimisha watu
kuuuliza swala lenyewe hasa. -
3:52 - 3:54Kwa sababu katika zama
ambazo tunasanifu majengo -
3:54 - 3:57kudumu kwa miaka 30, labda 60,
-
3:58 - 4:01ningependa nijifunze
jinsi ya kutengeneza kitu -
4:01 - 4:02ambacho kinaweza kuburudisha milele.
-
4:03 - 4:04Asante
-
4:04 - 4:09(Makofi)
- Title:
- Siri za maajabu ya Usanifu Majengo ya dunia ya zamani
- Speaker:
- Brandon Clifford
- Description:
-
Jamii za zamani zilihamishaje mawe makubwa kujenga Stonehenge, mapiramidi na sanamu za Kisiwa cha Easter? Katika mazungumzo haya mafupi , TED Fellow Brandon Clifford, anafumbua siri za zamani na kuonyesha jinsi tunavyoweza kutumia njia hizi kujenga kwa ajili ya siku za baadaye. "Katika zama ambazo tunasanifu majengo kudumu kwa miaka 30, au labda 60," he says, " ningependa kujifunza jinsi ya kutengeneza kitu kitachoburudisha milele."
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 04:22
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Architectural secrets of the world's ancient wonders | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Architectural secrets of the world's ancient wonders | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Architectural secrets of the world's ancient wonders | ||
Joyce Nyakale edited Swahili subtitles for Architectural secrets of the world's ancient wonders | ||
Joyce Nyakale edited Swahili subtitles for Architectural secrets of the world's ancient wonders |