WEBVTT 00:00:06.795 --> 00:00:08.055 Udadisi: 00:00:08.055 --> 00:00:09.863 Baraka au laana? 00:00:09.863 --> 00:00:11.603 Utata wa hili fumbo 00:00:11.603 --> 00:00:13.553 iliwekewa kwa Wagiriki 00:00:13.553 --> 00:00:15.913 kwa umbo la dhana la Pandora. 00:00:15.913 --> 00:00:17.033 Wahenga wanasema, 00:00:17.033 --> 00:00:18.743 alikuwa mwanamke wa kwanza mfaji, 00:00:18.743 --> 00:00:23.413 udadisi wake ulipeleka ugunduzi wa mambo mengi kusogea. NOTE Paragraph 00:00:23.413 --> 00:00:27.076 Pandora alipewa pumzi na Hephaestus, mungu wa moto, 00:00:27.076 --> 00:00:31.266 ambae aliomba msaada wa wenzie ili amfanye kuwa maridadi 00:00:31.266 --> 00:00:34.626 Kutoka kwa Aphrodite alipewa uwezo wa hisia za kina; 00:00:34.626 --> 00:00:37.386 kwa Hermes akapata uwezo wa lugha 00:00:37.386 --> 00:00:41.826 Athena akampa zawadi ya usanii bora na umakini kwa kila kitu, 00:00:41.826 --> 00:00:44.506 Na Hermes akampa jina lake. NOTE Paragraph 00:00:44.506 --> 00:00:48.006 Mwishowe, Zeus akampatia zawadi mbili Pandora. 00:00:48.006 --> 00:00:50.376 Ya kwanza ilikuwa ni zawadi ya udadisi, 00:00:50.376 --> 00:00:54.546 iliokaa ndani ya roho yake na kumtuma kwa bidii duniani. 00:00:54.546 --> 00:00:58.926 Ya pili ilikuwa ni boksi zito, lilitengenezwa vizuri, zito kubeba - 00:00:58.926 --> 00:01:00.792 na kufungwa kwa nguvu. 00:01:00.792 --> 00:01:04.802 Ila yaliyomo, Zeus alimwambia, hayakua kwa macho ya mfaji. 00:01:04.802 --> 00:01:08.592 Hakutakiwa kufungua boksi kwenye hali yeyote ile. NOTE Paragraph 00:01:08.592 --> 00:01:13.313 Duniani, Pandora akakutana na kupendana na Epimetheus, mtitani mwenye kipaji 00:01:13.313 --> 00:01:17.093 ambaye alipewa kazi ya kutengeneza dunia ya kawaida na Zeus. 00:01:17.093 --> 00:01:19.763 Alifanya kazi hiyo pembeni ya kaka yake Prometheus, 00:01:19.763 --> 00:01:21.503 aliyeumba binadamu wa kwanza 00:01:21.503 --> 00:01:24.603 lakini alipewa adhabu ya milele kwa kuwapa moto. 00:01:24.603 --> 00:01:27.103 Epimetheus alimkumbuka kaka yake mno, 00:01:27.103 --> 00:01:31.773 lakini alivyokuwa na Pandora alipata nafsi nyingine machachari ya urafiki. NOTE Paragraph 00:01:31.773 --> 00:01:34.403 Pandora alifurahia sana maisha ya duniani. 00:01:34.403 --> 00:01:37.743 Alipagawa kirahisi pia na kila alichokiona na hakuwa mtulivu 00:01:37.743 --> 00:01:42.073 kutokana na kiu yake ya maarifa na nia ya kujifunza mazingira yake. 00:01:42.073 --> 00:01:45.568 Mara nyingi, akili yake iliwaza vilivyomo kwenye boksi lililofungwa. 00:01:45.568 --> 00:01:49.784 Ni hazina gani kubwa sana mpaka isionekane na macho ya binadamu, 00:01:49.784 --> 00:01:51.864 na kwanini yeye alipewa alitunze? 00:01:51.864 --> 00:01:54.244 Vidole vyake viliwasha kutaka kulifungua. 00:01:54.244 --> 00:01:57.234 Kuna muda aliamini alisikia sauti zikinong'oneza 00:01:57.234 --> 00:01:59.334 na vilivyomo vikitoa sauti kwa ndani, 00:01:59.334 --> 00:02:00.944 kama vile vinataka kuwa huru. 00:02:00.944 --> 00:02:04.674 Fumbo lake likawa linamtatiza. NOTE Paragraph 00:02:04.674 --> 00:02:08.736 Muda ulivyozidi kwenda Pandora alizidi kuwa na hamu na boksi. 00:02:08.736 --> 00:02:12.396 Ilionekana kulikuwa na nguvu nje ya uwezo wake iliyomuita kwenye boksi, 00:02:12.396 --> 00:02:15.516 Iliyoita jina lake kwa nguvu zaidi. 00:02:15.516 --> 00:02:17.817 Siku moja alishindwa kuvumilia. 00:02:17.817 --> 00:02:19.437 Akajificha mbali na Epimetheus, 00:02:19.437 --> 00:02:21.697 aliangaza lile boksi la mafumbo. 00:02:21.697 --> 00:02:23.830 Angeangalia mara moja ndani, 00:02:23.830 --> 00:02:27.091 kisha akili yake itulie na asiliwaze tena... NOTE Paragraph 00:02:27.091 --> 00:02:30.339 Ila alivyogusa mfuniko mara moja, boksi likafunguka kwa nguvu. NOTE Paragraph 00:02:30.339 --> 00:02:32.309 Majitu ya kutisha na sauti za ajabu 00:02:32.309 --> 00:02:36.639 iktoka na wingu la moshi na kumzunguka na sauti za mkwaruzo na kelele. 00:02:36.639 --> 00:02:37.629 Akijawa na uwoga, 00:02:37.629 --> 00:02:42.309 Pandora alishikilia kwa bidii ile hewa akiwarudisha kwenye gereza lao. 00:02:42.309 --> 00:02:46.222 Lakini vile viumbe vilifurika nje kwenye wingu la kutisha. 00:02:46.226 --> 00:02:49.806 Alijisikia hali ya kukataza vilivyokuwa vikiondoka. 00:02:49.806 --> 00:02:51.826 Zeus alitumia boksi kama chombo 00:02:51.826 --> 00:02:55.176 cha mabaya yote na mabadhuri aliyotengeneza - 00:02:55.176 --> 00:02:56.276 na yakiachiwa, 00:02:56.276 --> 00:02:58.196 hayarudi tena. NOTE Paragraph 00:02:58.196 --> 00:02:59.296 Pandora akilia, 00:02:59.296 --> 00:03:03.266 akasikia sauti ikitoka kwenye boksi, 00:03:03.266 --> 00:03:05.954 Hii haikua sauti ya minong'ono ya mashetani, 00:03:05.954 --> 00:03:09.264 ila mwanga uliovuma ulionekana ukipungua hasira yake. 00:03:09.264 --> 00:03:11.914 Alipofungua mfuniko na kuangalia ndani tena, 00:03:11.914 --> 00:03:15.914 mwanga wenye joto zuri ukatoka na kuangaza mbali. NOTE Paragraph 00:03:15.914 --> 00:03:19.089 Akiutazama ukiwaka kwenye amsho la uovu alioachia, 00:03:19.624 --> 00:03:21.934 uchungu wa Pandora ukapungua. 00:03:21.934 --> 00:03:24.594 Alijua kwamba hatoweza kurekebisha kufungua boksi - 00:03:24.594 --> 00:03:29.464 lakini pamoja na jitihada, aliweka matumaini kubadilisha matokeo. NOTE Paragraph 00:03:29.464 --> 00:03:32.894 Leo hii, Boksi la Pandora linatufundisha madhara makubwa 00:03:32.894 --> 00:03:34.992 ya kuhangaika na tusivyovijua - 00:03:34.992 --> 00:03:38.822 lakini hamu ya Pandora ya kujua ilidokeza uwili uliopo 00:03:38.822 --> 00:03:40.752 kwenye kiini cha uchunguzi wa binadamu. 00:03:40.752 --> 00:03:43.492 Je tunatakiwa kuchunguza kila tusichokijua, 00:03:43.492 --> 00:03:45.542 kuchimbua dunia kwa zaidi - NOTE Paragraph 00:03:45.542 --> 00:03:47.082 au kuna baadhi ya maajabu 00:03:47.082 --> 00:03:48.852 ambayo ni bora yasitatuliwe?