Udadisi:
Baraka au laana?
Utata wa hili fumbo
iliwekewa kwa Wagiriki
kwa umbo la dhana la Pandora.
Wahenga wanasema,
alikuwa mwanamke wa kwanza mfaji,
udadisi wake ulipeleka ugunduzi wa
mambo mengi kusogea.
Pandora alipewa pumzi na
Hephaestus, mungu wa moto,
ambae aliomba msaada wa wenzie
ili amfanye kuwa maridadi
Kutoka kwa Aphrodite alipewa uwezo
wa hisia za kina;
kwa Hermes akapata
uwezo wa lugha
Athena akampa zawadi ya usanii bora
na umakini kwa kila kitu,
Na Hermes akampa jina lake.
Mwishowe, Zeus akampatia
zawadi mbili Pandora.
Ya kwanza ilikuwa ni zawadi ya udadisi,
iliokaa ndani ya roho yake na kumtuma
kwa bidii duniani.
Ya pili ilikuwa ni boksi zito,
lilitengenezwa vizuri, zito kubeba -
na kufungwa kwa nguvu.
Ila yaliyomo, Zeus alimwambia,
hayakua kwa macho ya mfaji.
Hakutakiwa kufungua boksi
kwenye hali yeyote ile.
Duniani, Pandora akakutana na kupendana
na Epimetheus, mtitani mwenye kipaji
ambaye alipewa kazi ya kutengeneza
dunia ya kawaida na Zeus.
Alifanya kazi hiyo pembeni ya
kaka yake Prometheus,
aliyeumba binadamu wa kwanza
lakini alipewa adhabu ya milele
kwa kuwapa moto.
Epimetheus alimkumbuka kaka yake mno,
lakini alivyokuwa na Pandora alipata
nafsi nyingine machachari ya urafiki.
Pandora alifurahia sana maisha
ya duniani.
Alipagawa kirahisi pia na kila
alichokiona na hakuwa mtulivu
kutokana na kiu yake ya maarifa na nia
ya kujifunza mazingira yake.
Mara nyingi, akili yake iliwaza
vilivyomo kwenye boksi lililofungwa.
Ni hazina gani kubwa sana mpaka isionekane
na macho ya binadamu,
na kwanini yeye alipewa alitunze?
Vidole vyake viliwasha kutaka kulifungua.
Kuna muda aliamini alisikia
sauti zikinong'oneza
na vilivyomo vikitoa sauti kwa ndani,
kama vile vinataka kuwa huru.
Fumbo lake likawa linamtatiza.
Muda ulivyozidi kwenda Pandora alizidi
kuwa na hamu na boksi.
Ilionekana kulikuwa na nguvu nje ya uwezo
wake iliyomuita kwenye boksi,
Iliyoita jina lake kwa nguvu zaidi.
Siku moja alishindwa kuvumilia.
Akajificha mbali na Epimetheus,
aliangaza lile boksi la mafumbo.
Angeangalia mara moja ndani,
kisha akili yake itulie na
asiliwaze tena...
Ila alivyogusa mfuniko mara moja,
boksi likafunguka kwa nguvu.
Majitu ya kutisha na sauti za ajabu
iktoka na wingu la moshi na kumzunguka
na sauti za mkwaruzo na kelele.
Akijawa na uwoga,
Pandora alishikilia kwa bidii ile hewa
akiwarudisha kwenye gereza lao.
Lakini vile viumbe vilifurika nje
kwenye wingu la kutisha.
Alijisikia hali ya kukataza
vilivyokuwa vikiondoka.
Zeus alitumia boksi kama chombo
cha mabaya yote na
mabadhuri aliyotengeneza -
na yakiachiwa,
hayarudi tena.
Pandora akilia,
akasikia sauti ikitoka kwenye boksi,
Hii haikua sauti ya minong'ono
ya mashetani,
ila mwanga uliovuma ulionekana
ukipungua hasira yake.
Alipofungua mfuniko na
kuangalia ndani tena,
mwanga wenye joto zuri ukatoka
na kuangaza mbali.
Akiutazama ukiwaka kwenye amsho
la uovu alioachia,
uchungu wa Pandora ukapungua.
Alijua kwamba hatoweza kurekebisha
kufungua boksi -
lakini pamoja na jitihada, aliweka
matumaini kubadilisha matokeo.
Leo hii, Boksi la Pandora
linatufundisha madhara makubwa
ya kuhangaika na tusivyovijua -
lakini hamu ya Pandora ya kujua
ilidokeza uwili uliopo
kwenye kiini cha uchunguzi wa binadamu.
Je tunatakiwa kuchunguza
kila tusichokijua,
kuchimbua dunia kwa zaidi -
au kuna baadhi ya maajabu
ambayo ni bora yasitatuliwe?