0:00:00.960,0:00:03.016 Nilikuwa na umri wa miaka 14 0:00:03.040,0:00:04.616 nikiwa kwenye jumba la michezo, 0:00:04.640,0:00:06.400 nikiiba kwenye mashine ya mchezo, 0:00:07.200,0:00:08.976 na nilipokuwa nikitoka nje ya jengo 0:00:09.000,0:00:11.380 mlinzi alikamata mkono wangu, [br]hivyo nikakimbia. 0:00:11.760,0:00:14.736 Nilikimbilia mtaani,[br]na nikaruka juu ya uzio. 0:00:14.760,0:00:16.376 Na nilipofika juu, 0:00:16.400,0:00:18.576 uzito wa sarafu 3,000 kwenye mkoba wangu 0:00:18.600,0:00:20.240 ulinielemea na kunivuta chini. 0:00:20.880,0:00:23.936 Niliponyanyuka, mlinzi [br]alikuwa amesima juu yangu, 0:00:23.960,0:00:27.376 na akasema, "Siku nyingine nyinyi vibaka, [br]ibeni vitu mnavyoweza kubeba." 0:00:27.400,0:00:29.416 (Kicheko) 0:00:29.440,0:00:31.576 Nilipelekwa kwenye mahabusu ya watoto 0:00:31.600,0:00:34.160 na nilipoachiliwa [br]chini ya dhamana ya mama yangu, 0:00:35.080,0:00:38.056 maneno ya kwanza mjomba wangu[br]alisema yalikuwa, "Ulikamatwaje?" 0:00:38.080,0:00:40.256 Nikasema, "Mzee, mkoba [br]ulikuwa mzito sana." 0:00:40.280,0:00:42.660 Akasema, "Mzee, [br]hukutakiwa kuchukua sarafu zote." 0:00:42.660,0:00:46.056 Nikasema, "Mzee, zilikuwa ndogo. [br]Ningefanyaje?" 0:00:46.080,0:00:50.976 na dakika 10 baadaye, alinipeleka kuiba [br]kwenye mashine nyingine ya mchezo. 0:00:51.000,0:00:53.020 Tulihitaji pesa ya petroli kufika maskani. 0:00:53.250,0:00:55.290 Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu. 0:00:55.440,0:00:57.296 Nimekulia Oakland, Kalifornia, 0:00:57.320,0:00:59.656 na mama yangu [br]na ndugu wa karibu wa familia 0:00:59.680,0:01:00.920 walevi wa madawa ya kulevya ya kokeini . 0:01:01.560,0:01:06.000 Mazingira yangu yalijumuisha [br]kuishi na familia, marafiki, 0:01:06.960,0:01:08.560 na makazi kwa wasio-na-makazi. 0:01:09.040,0:01:12.720 Mara nyingi, mlo wa jioni tuliupata [br]kwenye foleni za vyakula vya msaada. 0:01:13.440,0:01:15.296 Mjomba aliniambia hivi: 0:01:15.320,0:01:17.296 pesa inatawala dunia 0:01:17.320,0:01:18.536 na kila kitu ndani yake. 0:01:18.560,0:01:20.640 Na katika hii mitaa, pesa ni Mfalme. 0:01:21.320,0:01:22.936 Na ikiwa utafuata pesa, 0:01:22.960,0:01:25.480 itakupeleka kwa mtu mbaya au mtu mzuri. 0:01:26.080,0:01:28.616 Baadaye kidogo,[br]nilifanya uhalifu wangu wa kwanza, 0:01:28.640,0:01:31.616 na ndiyo mara ya kwanza [br]nilipoambiwa kuwa nina kipaji 0:01:31.640,0:01:33.790 na nikajisikia kuwa kuna mtu ananiaminia. 0:01:34.240,0:01:36.946 Hakuna aliyewahi-niambia kuwa[br]ningeweza kuwa mwanasheria, 0:01:36.946,0:01:38.056 daktari au mhandisi. 0:01:38.080,0:01:41.596 Yaani, ningewezaje kufanya hivyo?[br]Sikuweza kusoma, kuandika wala kutahajia. 0:01:41.596,0:01:42.736 Sikuwa mtu aliyesoma. 0:01:42.760,0:01:45.880 Kwahiyo, mara zote nilifikiri[br]uhalifu ndio njia ya kwenda. 0:01:47.480,0:01:49.176 Na kisha siku moja 0:01:49.200,0:01:50.456 Nilikuwa naongea na mtu 0:01:50.480,0:01:54.080 na alikuwa ananiambia juu ya [br]huu wizi ambao tungeweza fanya. 0:01:54.760,0:01:55.960 Na tukaufanya. 0:01:57.080,0:01:58.896 Ukweli ni kwamba nilikuwa nakulia 0:01:58.920,0:02:01.296 kwenye nchi yenye uwezo mkubwa[br]wa kifedha duniani, 0:02:01.296,0:02:03.016 Marekani, 0:02:03.040,0:02:07.120 huku nikiangalia mama yangu, [br]akisimama kwenye foleni ya benki ya damu 0:02:08.680,0:02:12.360 kuuza damu yake kwa Dola 40[br]kujaribu tu kulisha wanae. 0:02:13.320,0:02:16.640 Bado ana alama za sindano [br]mikononi mwake leo kudhihirisha hilo. 0:02:17.480,0:02:19.216 Kwa hiyo sikuijali jumuiya yangu, 0:02:19.240,0:02:20.736 Hawakujali maisha yangu. 0:02:20.760,0:02:24.176 Kila mtu pale alifanya anachotaka fanya kupata alichotaka, 0:02:24.200,0:02:26.376 wauza mihadarati,[br]wezi, benki ya damu. 0:02:26.400,0:02:28.016 Kila mtu alichukua fedha ya damu. 0:02:28.040,0:02:30.196 Hivyo nilipata yangu [br]kwa njia yoyote ile. 0:02:30.196,0:02:31.556 Nilipata yangu. 0:02:31.556,0:02:33.680 Elimu ya fedha[br]kweli ilitawala dunia, 0:02:34.680,0:02:36.656 na nilikuwa mtoto mtumwa kwake 0:02:36.680,0:02:37.920 nikifuata mtu mbaya. 0:02:40.280,0:02:43.456 Nikiwa na miaka 17, [br]nilikamatwa kwa wizi na mauaji 0:02:43.480,0:02:47.456 na punde nikajifunza kuwa fedha jela [br]zinatawala zaidi ya zilivyo mitaani, 0:02:47.480,0:02:48.680 Hivyo nilitaka kuingia. 0:02:49.600,0:02:52.656 Siku moja, nilikurupuka kushika [br]ukurasa wa michezo katika gazeti 0:02:52.680,0:02:54.496 ili mfungwa mwenzangu anisomee, 0:02:54.520,0:02:56.936 na kwa bahati mbaya [br]nikachukua sehemu ya biashara. 0:02:56.960,0:03:00.216 Na huyu mzee akasema,[br]"Hey, kijana, umechukua hisa?" 0:03:00.240,0:03:01.496 Na nikasema, "Ndio nini hicho?" 0:03:01.520,0:03:04.756 Akasema, "Hiyo ndiyo sehemu ambayo[br]watu weupe huweka pesa yao yote." 0:03:04.756,0:03:05.936 (Kicheko) 0:03:05.960,0:03:09.816 Na ilikuwa ndiyo mara ya kwanza [br]nilipata ono fupi la tumaini, 0:03:09.840,0:03:11.336 siku za baadaye. 0:03:11.360,0:03:13.960 Alinipa maelezo mafupi [br]ya hisa zilikuwa ni nini, 0:03:14.800,0:03:16.340 lakini ilikuwa ni muhtasari tu. 0:03:18.360,0:03:20.136 Yaani, ningewezaje kuifanya? 0:03:20.160,0:03:22.210 Sikuweza kusoma, kuandika wala kutahajia. 0:03:22.600,0:03:25.216 Ujuzi niliokuwa nimeukuza [br]kuficha kutokusoma kwangu 0:03:25.240,0:03:27.296 haukufanya kazi tena[br]katika mazingira haya. 0:03:27.296,0:03:30.336 Nilikuwa nimenaswa kwenye kizimba[br]mateka kati ya watekaji, 0:03:30.360,0:03:32.256 nikipigania uhuru ambao sijawahi kuwa nao. 0:03:32.280,0:03:34.456 Nilikuwa nimepotea, nimechoka, 0:03:34.480,0:03:35.840 na sikuwa na machaguzi. 0:03:37.000,0:03:38.776 Kwa hiyo nikiwa na miaka 20, 0:03:38.800,0:03:42.130 nilifanya kitu kigumu kuliko vyote[br]nilivyowahi kufanya maishani mwangu. 0:03:42.160,0:03:43.360 Nilichukua kitabu, 0:03:45.400,0:03:47.880 na ilikuwa ni kipindi kigumu sana [br]maishani mwangu. 0:03:49.320,0:03:51.136 kujaribu kujifunza jinsi ya kusoma, 0:03:51.160,0:03:53.776 kutengana na familia yangu, 0:03:53.800,0:03:55.000 na rafiki zangu. 0:03:56.280,0:03:57.736 Ilikuwa shida, mzee. 0:03:57.760,0:03:59.136 Ilikuwa ni mahangaiko. 0:03:59.160,0:04:00.856 Lakini sikufahamu japo kidogo kuwa 0:04:00.880,0:04:04.296 nilikuwa napata zawadi kubwa kuliko zote[br]nilizowahi kuziota, 0:04:04.320,0:04:05.520 kujithamini, 0:04:06.320,0:04:08.160 maarifa, nidhamu. 0:04:09.000,0:04:12.696 Nilisisimka mno kusoma, kiasi kwamba[br]nilisoma kila kitu nilichokitia mkononi: 0:04:12.720,0:04:16.055 makaratasi ya pipi, nembo za nguo, [br]alama za barabarani, kila kitu. 0:04:16.079,0:04:17.326 Nilikuwa nikisoma tu vitu! 0:04:17.326,0:04:18.336 (Makofi na Vifijo) 0:04:18.360,0:04:19.560 kusoma tu vitu. 0:04:21.360,0:04:24.560 Nilisisimka sana kujua jinsi ya kusoma[br]na kujua jinsi ya kutahajia. 0:04:24.720,0:04:27.006 Rafiki alikuja, akaniuliza,[br]"Mzee, unakula nini?" 0:04:27.006,0:04:28.736 Nikasema, "P-I-P-I, pipi." 0:04:28.760,0:04:31.016 (Kicheko) 0:04:31.040,0:04:33.656 Akasema, "Nipe kidogo."[br]Nikasema, "L-A. La." 0:04:33.656,0:04:34.776 (Kicheko) 0:04:34.800,0:04:36.216 Ilikuwa babukubwa. 0:04:36.240,0:04:39.416 Yaani, sasa naweza, kwa mara ya kwanza[br]katika maisha yangu, kusoma. 0:04:39.440,0:04:41.480 Hisia niliyoipata, ni ya kustaajabu sana. 0:04:43.240,0:04:45.840 Kisha, nikiwa na miaka 22, [br]nikijisikia mwenyewe, 0:04:46.800,0:04:48.536 nikijiamini, 0:04:48.560,0:04:50.400 Nilikumbuka kile yule mzee aliniambia. 0:04:51.760,0:04:55.496 Kwa hiyo nilichukua [br]kurasa za biashara za gazeti. 0:04:55.520,0:04:57.456 Nilitaka kuwatafuta hawa matajiri weupe. 0:04:57.480,0:04:59.080 (Kicheko) 0:05:00.520,0:05:02.440 Kwa hiyo nilitafuta ule muhtasari. 0:05:03.480,0:05:05.096 Nilipokuwa nikijiendeleza kikazi 0:05:05.120,0:05:08.976 nikifundisha wengine namna ya [br]kusimamia fedha na kuwekeza, 0:05:09.000,0:05:12.336 punde nikajifunza kuwa [br]nilihitaji kuwajibika kwa matendo yangu. 0:05:12.360,0:05:15.376 Kweli, [br]nilikulia kwenye mazingira tata sana, 0:05:15.400,0:05:17.336 lakini nilichagua kufanya uhalifu, 0:05:17.360,0:05:19.136 na nilipaswa kukiri hilo. 0:05:19.160,0:05:21.776 Nilipaswa kuwajibika kwa hilo, [br]na nilifanya hivyo. 0:05:21.800,0:05:24.696 Nilikuwa nikiunda mtaala ambao[br]ungeweza kuwafundisha wafungwa 0:05:24.720,0:05:27.110 namna ya kusimamia fedha[br]kupitia ajira za gerezani. 0:05:28.720,0:05:31.896 Kutiisha mtindo wetu wa maisha[br]kungeweza kutoa zana zihamishikazo 0:05:31.920,0:05:35.256 ambazo tunaweza kuzitumia kusimamia fedha[br]tunapoirudi kwenye jamii, 0:05:35.280,0:05:38.536 kama watu wengi walivyofanya[br]ambao hawakufanya uhalifu. 0:05:38.560,0:05:39.760 Kisha niligundua 0:05:40.680,0:05:42.736 kulingana takwimu ya MarketWatch, 0:05:42.760,0:05:45.296 zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa Marekani 0:05:45.320,0:05:47.440 wana chini ya Dola 1,000 katika akiba. 0:05:48.200,0:05:51.416 Michezo ilielezea kwamba zaidi ya asilimia 60 ya wachezaji wa NBA 0:05:51.440,0:05:52.976 na wachezaji wa NFL hufilisika. 0:05:53.000,0:05:56.040 Asilimia 40 ya matatizo ya ndoa[br]hutokana na masuala ya kifedha. 0:05:57.080,0:05:58.296 Balaa gani? 0:05:58.320,0:06:00.456 (Kicheko) 0:06:00.480,0:06:03.176 Unataka kuniambia,[br]watu wamefanya kazi maisha yao yote, 0:06:03.200,0:06:05.776 wakinunua magari, nguo, nyumba[br]na vitu mbalimbali 0:06:05.800,0:06:08.016 lakini walikuwa waliishi hundi kwa hundi? 0:06:08.040,0:06:12.376 Ni namna gani duniani wanajamii [br]wangekwenda kuwasaidia wafungwa 0:06:12.400,0:06:13.616 kurudi kwenye jamii 0:06:13.640,0:06:15.830 ikiwa hawakuweza kusimamia [br]mambo yao wenyewe? 0:06:16.160,0:06:17.416 Tumevurugwa. 0:06:17.440,0:06:19.176 (Kicheko) 0:06:19.200,0:06:20.600 Nahitaji mpango mzuri zaidi. 0:06:22.520,0:06:24.640 Hii haitakwenda kufanya kazi vizuri. 0:06:25.040,0:06:26.240 Hivyo ... 0:06:27.880,0:06:29.080 Nilifikiria. 0:06:31.800,0:06:35.020 Sasa nilikuwa na wajibu kukutana[br]na wale waliokuwa kwenye mkondo huo 0:06:36.360,0:06:37.576 na kuwasaidia, 0:06:37.600,0:06:40.856 na ilikuwa ni ajabu sababu [br]sasa nilijali jumuiya yangu 0:06:40.880,0:06:43.240 Lo, hebu fikiria.[br]Nilijali kuhusu jumuiya yangu. 0:06:44.640,0:06:46.936 Ujinga juu ya Fedha ni ugonjwa 0:06:46.960,0:06:49.976 ambao umedhohofisha wachache[br]na walio chini katika jamii yetu 0:06:50.000,0:06:52.136 kwa vizazi na vizazi, 0:06:52.160,0:06:54.656 na tunapaswa kukasirika juu ya hilo. 0:06:54.680,0:06:56.256 Ebu jiulize: 0:06:56.280,0:06:59.536 Inawezekanaje asilimia 50 [br]ya wakazi wa Marekani 0:06:59.560,0:07:03.520 wasiwe na elimu ya fedha katika nchi[br]inayoendeshwa kwa ustawi wa kifedha? 0:07:05.000,0:07:07.856 Kupatikana kwa haki kwetu, [br]hadhi yetu ya kijamii, 0:07:07.880,0:07:10.896 hali ya maisha, usafirishaji na chakula 0:07:10.920,0:07:13.976 vyote vinategemea fedha[br]ambayo watu wengi hawawezi kuisimamia. 0:07:14.000,0:07:15.576 Ni ajabu! 0:07:15.600,0:07:16.976 Ni janga 0:07:17.000,0:07:20.000 na hatari kubwa kwa usalama wa umma[br]kuliko suala jingine lolote. 0:07:21.720,0:07:24.376 Kadiri ya [br]Kitengo cha Urekebishaji cha Kalifornia, 0:07:24.400,0:07:26.736 zaidi ya asilimia 70 ya wale waliofungwa 0:07:26.760,0:07:30.376 wamefanya au wameshtakiwa kwa uhalifu [br]uhusianao na fedha: 0:07:30.400,0:07:34.920 wizi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba, [br]kutapeli, uporaji, ghusubu -- 0:07:35.720,0:07:37.040 na orodha inaendelea. 0:07:37.920,0:07:39.136 Angalia hii: 0:07:39.160,0:07:42.096 Mfungwa wa kawaida 0:07:42.120,0:07:44.616 huingia katika mfumo wa gereza [br]wa Kalifornia 0:07:44.640,0:07:46.200 pasipo kuwa na elimu ya fedha, 0:07:46.840,0:07:48.816 hupata ujira wa senti 30 kwa saa, 0:07:48.840,0:07:51.056 zaidi ya Dola 800 kwa mwaka, 0:07:51.080,0:07:53.840 bila ya kuwa na matumizi yoyote [br]na kuweka akiba yoyote. 0:07:54.760,0:07:59.096 Anapopewa msamaha, [br]hupewa dola 200 pesa ya geti na kuambiwa, 0:07:59.120,0:08:02.340 "Wee, mafanikio mema, kaa mbali na[br]matatizo. Usirudi gerezani tena." 0:08:02.800,0:08:06.096 Bila kuwa na maandalizi yoyote ya maana[br]au mpango fedha wa muda mrefu, 0:08:06.120,0:08:07.320 anafanyaje ...? 0:08:08.600,0:08:09.800 Akiwa na miaka 60? 0:08:11.120,0:08:12.456 Apate kazi nzuri, 0:08:12.480,0:08:16.400 au arudi kwenye tabia ile ile ya uhalifu [br]iliyompeleka gerezani kwanza? 0:08:17.400,0:08:19.176 Nyinyi walipakodi, chagueni wenyewe. 0:08:19.200,0:08:22.360 Hakika, elimu yake [br]imeshamchagulia, pengine. 0:08:23.120,0:08:25.480 Kwa hiyo, tunatibuje ugonjwa huu? 0:08:26.240,0:08:27.976 Nilishiriki kuanzisha programu 0:08:28.000,0:08:32.576 tuliyoiita Elimu Hisia [br]ya Uwezeshaji wa Kifedha 0:08:32.600,0:08:34.056 tunaiita FEEL 0:08:34.080,0:08:37.256 na inafundisha namna ya kutenganisha[br]maamuzi ya kihisia 0:08:37.280,0:08:39.256 na maamuzi ya kifedha, 0:08:39.280,0:08:42.696 na sheria 4 aushi [br]za utawala fedha binafsi: 0:08:42.720,0:08:44.280 njia sahihi ya kuweka akiba, 0:08:45.560,0:08:47.200 kudhibiti gharama zako za maisha, 0:08:48.320,0:08:50.096 kukopa fedha kwenye ufanisi 0:08:50.120,0:08:53.896 kutawanya fedha yako [br]kuruhusu fedha yako ikufanyie kazi 0:08:53.920,0:08:55.736 badala ya wewe kuifanyia kazi. 0:08:55.760,0:08:59.920 Wafungwa wanahitaji ujuzi huu [br]kabla ya kuingia tena kwenye jamii. 0:09:01.480,0:09:05.376 Hatuwezi kubadilika kuwa na maisha [br]ya kawaida bila ujuzi huu wa maisha. 0:09:05.400,0:09:09.216 Hii dhana kuwa ni Weledi tu[br]wanaweza kuwekeza na kusimamia fedha 0:09:09.240,0:09:11.496 ni ya fedheha kabisa, 0:09:11.520,0:09:13.587 na yeyote aliyewaambia hivyo anadanganya. 0:09:13.627,0:09:18.176 (Makofi na Vifijo) 0:09:18.200,0:09:20.616 Mweledi ni mtu 0:09:20.640,0:09:23.136 anayejua kazi zake kuliko walio wengi, 0:09:23.160,0:09:28.096 na hakuna mtu ajuaye kiasi gani cha fedha[br]wahitaji, unacho, au wataka zaidi ya wewe, 0:09:28.120,0:09:30.080 ikimaanisha kuwa wewe ni mweledi. 0:09:30.880,0:09:35.096 Elimu ya fedha siyo stadi,[br]mabibi na mabwana. 0:09:35.120,0:09:36.320 Ni mtindo wa maisha. 0:09:37.560,0:09:42.056 Uimara wa kifedha ni matokeo ya ziada [br]ya mtindo sahihi wa maisha. 0:09:42.080,0:09:45.880 Mfungwa mwenye elimu nzuri ya kifedha[br]anaweza kuwa mwananchi mlipakodi, 0:09:46.680,0:09:50.176 na mwananchi mlipakodi mwenye elimu[br]nzuri ya kifedha anaweza kubaki hivyo. 0:09:50.200,0:09:54.536 Hii inatuwezesha kuunda daraja [br]kati ya wale watu tunaowashawishi: 0:09:54.560,0:09:57.296 familia, marafiki na wale vijana 0:09:57.320,0:10:00.240 ambao bado wanaamini [br]kuwa uhalifu na pesa vina uhusiano. 0:10:01.720,0:10:04.616 Kwa hiyo tupoteze uwoga na wasiwasi 0:10:04.640,0:10:06.096 wa maneno makubwa ya kifedha 0:10:06.120,0:10:09.696 na ujinga mwingine wote [br]ambao mmekuwa mkisikia huko nje. 0:10:09.720,0:10:13.576 Na tujikite kwenye kiini [br]kilichokuwa kinadhoofisha jamii yetu 0:10:13.600,0:10:17.960 kuanzia kutimiza wajibu wako [br]la kuwa meneja mzuri wa maisha. 0:10:19.000,0:10:22.336 Na tutoe mtaala mwepesi na rahisi kutumia 0:10:22.360,0:10:24.616 ambao utaingia kwenye kiini, kiini 0:10:24.640,0:10:28.576 cha ni nini ukweli wa[br]uwezeshaji wa kifedha na elimu ya hisia. 0:10:28.600,0:10:31.496 Sasa, ikiwa umekaa hapa kwa wasikilizaji [br]na umesema, 0:10:31.520,0:10:33.936 "Ndiyo, kweli, hiyo si mimi [br]na sikubaliani nayo," 0:10:33.960,0:10:35.446 basi njoo uchukue somo langu -- 0:10:35.446,0:10:36.976 (Kicheko) 0:10:37.000,0:10:40.680 ili nikuoneshe ni kiasi gani cha pesa [br]inakugharimu kila unaposhikwa na hisia. 0:10:41.960,0:10:45.120 (Makofi na Vifijo) 0:10:47.600,0:10:49.136 Asanteni sana. Asanteni. 0:10:49.160,0:10:50.320 (Makofi na Vifijo)